The Radar Scandal: Investigation & Progress

Kwanza nianze kwa haya:
Hapa ni mjadala wa wazi..wazi kabisa. Yeyote apendaye huwezi kutoa hoja ama maoni yake, hivyo basi unaweza kuwasilisha hoja yenye kubeba maana kubwa na ukweli, lakini wana JF wakakupinga . Hapo jifunze kitu kimoja: panga vizuri hoja zako – wana JF huwa wanapenda kuchimba ndani kabisa ya hoja. Jukwaaani hapa si mahali pa ndio mzee!

Kuhusu thread yako Mkuu Njowepo:
Siku ya kusaini mkataba huwa ni ceremonial tu, sio siku ambayo mkataba unaandaliwa!
Siku ya kusaini wanasaini kilichokubalika kabla.......

Hii haijakaa sawa, tafadhali Mkuu rudi mezani kafikirie kingine cha kuandika!
 
Siku ya kusaini mkataba huwa ni ceremonial tu, sio siku ambayo mkataba unaandaliwa!
Siku ya kusaini wanasaini kilichokubalika kabla.......

Hii haijakaa sawa, tafadhali Mkuu rudi mezani kafikirie kingine cha kuandika!
sio afikirire,aje hapa akanushe huu udaku wake,ole toa udaku huu mapema
 


Kama ni kweli umesainiwa mwenye Kaya kakoroma hapa Gembe unabisha nini ?Nani wa kuharibiwa jina ? CCM huwa wanajiharibia wenyewe .
 
kama tukitaka kila mmoja awajibike nani atabaki.

Mkulu kumbe wakati mwingine unakubali kuwa CCM wote wameoza ndo maana kutakuwa hakuna mtu wa kubaki, lakini sio wa kwanza kulisema hili maana hata EL alilisema. unajicontradict mwenyewe kwenye posting zako mara CCM wote wasihusishwe na ufisadi mara wote wakiwajibika nani atabaki. We dont care nani anabaki undeni serikali ya mseto kama mnaona mambo magumu kiasi cha kukosa watu wa kujaza nafasi muhimu.
 
mi ninachomuonea huruma JK ni kuwa yeye bado anaufuatisha ule msemo wa wahenga kuwa "mtoto akiunyea mkono huukati ila unausafisha kisha maisha yanaendelea" na ndo hichi anachokifanya kwenye uongozi wake kuwa uozo wooote unaofanywa na mawaziri wake ye anausafisha tu...
 
Hii habari yenyewe inajichanganya sana. Inaanza kufabnya reference ya mawaziri wawili waandalmizi hata kabla hawajatajwa majina yao! Imeandikwa na gazeti gani kwa sbaabu kuna sehemu nimesoma kwa mujibu wa taarifa zilizofikishwa kwenye gazeti hilo wakati hatuambiwi ni gazeti gani.
Halafu hivi mwenye kosa ni aliyesaini mkataba ay aliyeuandaa?
 

mi napingana na wewe kidogo mpita njia, mi kwa upeo wangu nahisi kama kabla ya kusaini hiyo mikataba ukiomba upewe ili uupitie sidhani kama utanyimwa.
na kwa mtu yeyote mwenye kulitakia taifa mema ni lazma aupiitie huo mkataba hata kama hajauandaa yeye au la.
ila kwa mtu hopeless akifika tu mezani anaulizia peni iko wapi kisha anasaini na matokeo yake ndo tunakuta mikataba imeingiwa kwa miaka 50 na watalipa kodi hiyo hiyo wanayolipa sasa kwa kipindi chote watakachokuwa wanapokezana.
sasa hii ni akili au matope?
 

Mpita Njia naona badi hujajua style ya JF .Unataka link ? Sisi ndiy huwa tunatengeneza news na wao wana kuja ku copya hapa .Tumeanza nalo hilo kaa huamini kaa pembeni wacha watu walete nyeti na ukweli utauona .Kumbuka hii imetokea China na JK kasemea uvunguni na yamefika hapa .Alijua akibwatuka yataandikwa na hapo itakuwa balaa lakin haya hivyo yamefika .Chanzo ni JF na ngojea utasikia zaidi .
 

Sibishi kuwa JF imekuwa chanzo kikubwa cha habari nyeti. Ninachosema, ukiisoma ile habari mwanzo wa thread, inaonyesha kuwa imeshaandika kwenye gazeti fulani. Angalia utaona sehemu zimeandikwa kwa mfano ' wakizungumza na gazeti kwa sharti la kutotajwa jina'. Ndo nilikuwa naomba nijue kuwa ni gazeti gani hilo lililozungumza na hao watoa habari ambao hawakutaka kutajwa majina.
 
Nimegundua kuna watu humu JF wanachangia mada hasa kuisupport kwa kuangalia majina.
You need to be situational na mchangie mada fairly.
JK huyu huyu aliwai kabidhi cheki toka Exim yenye kutofautiana kati ya tarakimu na maandishi.
Ndani ya CCM hayo yote yawezekana.
Source ya Habari ni KLH News-22nd of April(By Changamoto0
 
hii habari mbona haieleweki .....tunaomba sorce na muandishi aandike ili ieleweke, asitupe habari kama anatoa kitandawilki vile
 
kila mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe, kama Rais aliwateuwa yeye mwenyewe acha afaidi matunda yake, anajua wanafaa kumsaidia.
 
Waziri aliyeachia madaraka asema hakuzaliwa ili awe waziri

SAA chache baada ya kutangaza kujiuzulu, Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge amesema hakuzaliwa kuwa waziri hivyo, uamuzi aliochukua ni wa kawaida.

Akizungumza na gazeti hili juzi usiku muda mfupi baada ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kuthibitisha kujiuzulu kwake, Chenge alisema anashangaa watu wanaompa pole.

"Baadhi ya watu wananipa pole, pole ya nini, huu ni utaratibu wa kawaida wa utendaji kazi za umma," alisema Chenge na kuongeza:,

"Mimi sikuzaliwa kuwa waziri, mtu anaponipa pole ana maana mimi nilazaliwa kuwa waziri, mimi sikuzaliwa kuwa waziri bwana," alisisitiza.

Chenge alifafanua kwamba, uamuzi wake wa kujiuzulu umeangalia maslahi ya taifa kutokana na kuona suala lake limechukua sura tofauti.

Waziri huyo wa zamani wa Miundombinu ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), alisema suala lake lilikuwa limeanza kumsumbua Rais Jakaya Kikwete.

Alisema kwamba, ameona si vema Rais ajikute katika wakati mgumu kutokana na suala lake kutafsiriwa katika misingi tofuati na ukweli ndiyo maana ameamua kujiuzulu.

"Pia nimeona ni vema nijiuzulu kutokana na kuona watu wanataka kumsumbua Rais, ukilala ukiamka wanasema hivi, sasa si vema Rais asisumbuliwe," alisisitiza.

Chenge aliweka bayana kwamba, yeye hajawajibika bali amejiuzulu kulinda maslahi ya taifa.

Alisema si wakati wa kuzungumza mambo mengi, lakini amejiuzulu kwani kama ni kuwajibika kwa suala analochunguzwa atakuwa amethibitisha amekula rushwa kitu ambacho si kweli kwani uchunguzi unaendelea.
 
Sizitaki mbichi hizi, mbona alishasema hawezi kujiuzuru mpaka uchunguzi ukamilike, alikurupushwa na nani, mbona alikuwa anangangania, kwanini hakujiuzuru tangia watu waliposema hafai kuwa waziri au na yeye alikuwa hajajua kuwa anavijisenti kwenye offshore account.
Kama akuzaliwa kuwa waziri alitakiwa kujiuzuru mapema sana kwani alichelewa kufanya hivyo.
 
Hebu pata picha
Baba amefumaniwa akizini na hausigeli tena anafumaniwa mbele ya mke, wakwe, watoto na nduguze. Unafikiri atapata akili njema ya kuongea neno la HEKIMA?????

At least ameonesha ushujaa wake wa kuguguma maana alipaswa akae japo mwezi ndipo aibuke na kusema atakavyo..
 
Chenge alifafanua kwamba, uamuzi wake wa kujiuzulu umeangalia maslahi ya taifa kutokana na kuona suala lake limechukua sura tofauti.

Huu ndio mchosho sasa,yaani anajidai anajali maslahi ya taifa sasa hivi??
Sasa na yale maslahi ya taifa mengine kwenye account zake atayajali kivyake sio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…