Chenge anaweza kuwa mmoja wa majambazi wasomi wa kitanzania.
Ana mwanasheria wa kumlinda kutoka Cleveland, Ohio.
Aulizwe anamlipaje?
Bandari ya Elizabeth Marina, Jersey.
Andrew Chenge hatimae amejiuzuru na sasa hivi anapanga mikakati ya kuhakikisha anapona kufikishwa mahakamani na asizijibu tuhuma mbalimbali ambazo anakabaliwa nazo ikiwemo ya kuhifadhi fwedha za mlungula za rada, katika kisiwa cha Jersey ambacho kwa namna moja ama ingine hakiwajibiki sana na sheria yoyoye ile kutaka kuibana endapo kuna matatizo kama ya Chenge.
Lakini nimefanza utafiti kidogo kujua zaidi kuhusu kisiwa hiki maarufu kwa watu wote wenye makusudio ya kuficha na kuhifadhi mali za wizi ama wa aina ya Chenge au watu engine.
Jersey ni moja ya visiwa vinavoizunguka nchi ya Uingereza pamoja na vingine vya Isle of Man ambavyo vinaitwa kwa jina la pamoja la Channel Island.
Visiwa hivi viko mbali ya pwani za kusini mwa Uingereza na kaskazini mwa Ufaransa na ni visiwa maarufu kwa watalii ambao hupenda kwenda huko ama kununua nyumba za mapumziko au meli ndogo zenye mazingira ya kuishi kama nyumba.
Lakini cha msingi kisiwa cha Jersey hakipo katika umoja wa Ulaya wala si sehemu ya Uingereza kwa kusingatia masuala ya kuwa chini ya Malkia au sheria za Uingereza.
Lakini kabla ya kuelezea kuhusu uhuni uliofanzwa na bwana Chenge na genge lake, ni vizuri nikagusia kidogo kuhusu mambo matatu kuhusu Jersey ambayo yanahusu fwedha au uchumi , ulipaji kodi na uhusiano na nchi zingine.
Uchumi wa Jersey umelowea katika shughuli za kibenki na huduma zake na asilimia sitini ya uchumi wa kisiwa hiki inapatikana katika shughuli hizi.
Lakini katika sheria za Uingereza kama benki yoyote ile ina tawi katika kisiwa cha Jersey, basi mamlaka ya Ushuru ya Uingereza inaweza kudai taarifa ya akaunti ya mteja yoyote yule ambae anasadikiwa kufanza shughuli za uhalifu.
Ila kwa kesi ya Chenge bado haifahamiki kama ana akaunti katika benki yoyote ilio katika Jumuiya ya Ulaya ambapo wachunguzi wa kiingreza wanaweza kutafuta kwa kumuuliza bwana Chenge ambae wanasema ni "valuable witness" katika uchunguzi wao.
Suala la ulipaji kodi ni jambo lingine ambalo linaitisha vimulimuli ukizingatia kwamba bwana Chenge ameamua kuwekeza pesa yake kisiwani Jersey huku akipata faida na riba ambapo kwa upande wa Tanzania angelazimika kulipa kodo kutokana na kufanza hivo.
Na sula lingine ni uhusiano wa kisiwa hiki na nchi zingine.Kisiwa hiki kinajetegema chenyewe kama nchi kamili, tofauti na Uingereza. pia kisiwa hiki hakiwezi kushughulikia mambo yoyote yale yenye utata kama yanaingiliana na Uingereza na kwa kesi ya Chenge mambo yanaweza kuchukua miaka kuyatatua.
Jambo la msingi kuelewa hapa ni kwamba Andrew Chenge alikuwa anafahamu hii ni softicated, well documented case ambayo ilibidi amuajiri mwanasheria kutoka Cleveland Ohio,bwana J Lewis Madorsky.
Mambo haya ni magumu na natabiri kuwepo kwa utata katika kuyatatua katika siku zijazo.