MwanaHabari
JF-Expert Member
- Nov 9, 2006
- 442
- 13
Hapa dawa ni nguvu ya kura, ninamatumaini kwamba wananchi wanaanza kutenganisha nani fisadi nani siyo. Tuache wamalizane maana ni wakina Rostam walio-leak hii ku-divert attention, wameanza kukanyagana, tusubiri hii splinter group ya mafisadi itatoa info gani... hapa inaanza kuwa Chenge-Mkapa vs Rostam-Lowassa wataanza kurushiana mawe,
Chenge hajiuzulu hivi hivi, also he wont be arrested.
ACHA KUCHANGANYA HABARI HAPA FALASI WEWE.EBU TAJA UFISADI WA KAMALA,TAJA UFISADI WA MATHAYO AU TAJA UFISADI WA NCHIMBI.JIFUNZENI KUJENGA HOJA ILI WANANCHI WAWAELEWE.Kikwete hana credibility hata kidogo kucheka cheka tu utadhani mwana si ridh...., akitaka rudisha imani kwa wananchi ajiuzulu uitishwe uchaguzi mpya, ataachisha kazi wangapi? Serikali yote imeoza, wakuu wa wilaya aligawa kishikaji, wakuu wa Mikoa hivyo hivyo, idara nyeti za serikali pia, mawaziri mchezo ule ule akimtoa Chenge wafuate akina Mkullo, Kapuya, Nchimbi, Matayo, Kamara, Msolla, nadhani wote ni mafisadi waende zao wamefilisi nchi yetu...
ni kweli kwamba kijiwe hiki cha jamboforum kinatumika na watu kurushiana mawe na madongo
...naomba mjiulize data za akaunti ya chenge zilitolewa na nani? gazeti litapataje data nyeti hivi mpaka akaunt namba? lakini mambo yakianza kuwekwa hadharani na maakaunti ya nje ya akina rostamu na wenzake tanzania hapatatosha...
badala ya kushangilia hapa, mngeanza kujiuliza nani ametoa data kwa malengo gani.
Data zimetolewa na Serious Fraud Office, sio gazeti wala sio 'madongo' ya JF. Uwezo iliyokuwa nao SFO kuingia kwenye akaunti za watu wakati wa uchunguzi ni sheria zao wenyewe, na haihusiani na Rostam.
Wakuu,
Hivi hawa watu ni akina nani?
Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.
Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.
Hapa kuna ndoa za watu zitaota mchanga. Mtu unaweza kufikiri mama anajituma, anakuja na mlo safi, kumbe ni mafisadi yamekuingilia hata nyumbani kwako.
Nina uhakika hakutaja hayo mamilioni wakati alipoambia ataje mali zake!!!! hapo ndipo tutakapomshika!!!Nilisema ajieleze kwa misingi gani? Hawezi kuongea mpaka uchunguzi wa SFO uishe. Baada ya hapo hawezi kuongea mpaka uchunguzi wa PCCB uishe. PCCB wakimaliza aidha ana kesi ya kujibu - kwa hiyo hawezi kuongea kwa sababu ana kesi -, au hana kesi ya kujibu - kwa hiyo hana la kuongea, ni msafi, na mambo yalienda safi kama walivyosema dili la EPA. Angalia mchezo utakavyo enda.
Ninachoweza kukwambia tu ni kwamba haya mambo yote yanayotokea nchini mwetu ni sisi tu wachache ndio tunaona athari zake na kuzikemea kila kukicha. Mimi sitoshangaa Jambazi Jakaya Kikwete na wenzake wote ndani ya Chama Cha Majambazi (CCM) wataposhinda tena kwenye chaguzi mbalimbali hapo 2010. I am sorry to say this lakini asilimia kubwa ya Watanzania ni WAPUMBAVU, WAJINGA NA MAGOIGOI WA KIFIKRA. ... Jamani hivi tutasubiri mpaka lini huku hawa viongozi wanawafanya wananchi wote mazoba na wajinga kiasi hiki... Inaniumaga sana kuona baadhi ya watu kwenye picha za mikutano ya CCM, WENGI WAO SURA ZAO ZIKIWA ZINAONYESHA UFUKARA MKUBWA NA UMASIKINI ULIOKITHIRI lakini ndio hao hao wanaoongoza kuimba zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM na hawaishi kupiga vigelegele kuwashangilia hawa Majambazi.
... Leo asilimia kubwa ya watu vijijini na hata mijini hawana hata yale mahitaji muhimu ambayo taifa lolote linatakiwa kumsaidia mwananchi wake lakini Jambazi Andrew Chenge amezificha pesa zetu ambazo zinajenga uchumi wa nchi nyingine za Ulaya. Halafu unakuta hao hao wananchi wanakipigia tena kura Chama Cha Majambazi (CCM).
Mkuu hilo halinishangazi, hata balali alisemaga hivo hivo....
Kwa vile anachunguzwa ingekuwa vizuri zaidi ajiuzulu ili apishe uchunguzi huru. Kwani kuna ulazima gani wa yeye kuendelea na uwaziri!!!??? mwambieni asing'ang'nie madaraka, watu hawamtaki na hawampendi. Nasikia eti kijiwe chake ni kwenye bar moja maarufu ndani ya Movenpick.
ACHA KUCHANGANYA HABARI HAPA FALASI WEWE.EBU TAJA UFISADI WA KAMALA,TAJA UFISADI WA MATHAYO AU TAJA UFISADI WA NCHIMBI.JIFUNZENI KUJENGA HOJA ILI WANANCHI WAWAELEWE.
Kwi kwi kwi kwi!
Kibri.
Yeye ana kibri kumshinda Ibilisi?
Tusha muwahi kwa upupu na pilipili kichaa makalioni.
Safari hii atasema tu, kama hasemi chozi litamtoka kwa joto la mseto nilio utaja.