1.
Hivi kweli mnaamini kwamba viongozi wetu ni wasafi?... Nani kati yao mwenye wadhifa hana account nje!..
lakini hizi mbona ni pesa kidogo sana,au watu wanatishika na hilo neno us dollar au pound sterling.
Mkuu Bob,
Heshima mbele mkuu, sikweli kuwa viongozi wote ni wachafu, kama ambavyo sio wananchi wote tumelala usingizi kama wanaowachagua, na si kweli kuwa viongozi wote wana account nje, maana kuna ambao hata hawajawahi kutoka nje ya nchi,
However, baadhi ya viongozi wetu ni wachafu, tena sana, tuziruhusu facts zijiseme kama zinavyoanza kujisema zenyewe, kwenye hili la Chenge, kwa kweli ni aibu tena sana, huyu Chenge, amewahi kushika nafasi gani huko nje mpaka kuwa na hela kiasi hiki?
Mkuu wangu Katibu Tarafa, hebu soma gazeti la Forbes, uone ni wa-Marekani, wangapi kati millioni 245 wanazo hizo amount, tena bank zimekaa tu as a hard cash? Maana hata hao walionazo utakuwa robo tatu yake ziko in shares za stock, lakini sio hard cash, I mean something is not right na our political and legal system,
All and all, ni kwamba baadhi ya viongozi wetu ni wakatili kama sio makafiri, maana unawezaje kuwa na hela zote hizo bank USA, huku ukiona wananchi tena wa jimbo lako wanateseka kwa matatizo ambayo yanaweza kuwa solved na just dola 10,000 tu? Kwa wale manaofanya kazi bank au kwenye markets, hebu tuambieni hizi hela ambazo lazima Chenge, amezifunga kwenye CD, zinatoa interest kiasi gani kwa mwaka?
Halafu bado niko curious kama ni Chenge mwenyewe, aliyewaambia hao wachunguzi kuwa anzo hizo hela, au walimua-ambush? Najua kuna utaratibu wa uwt kumpa rais faili la any Tanzanian in advance ambaye anafikiriwa kupewa madaraka makubwa kitaifa, sasa how did they miss this Chenge's mega account?
Somebody need to answer haya maswali, unajua kuan viongozi kama watatu waliowahi kumwambia muungwana usoni, kabla ya uchaguzi kuwa asahau haitakuja kutokea yeye kuwa rais wa bongo, Nyang'anyi, Sarakikya, na huyu Chenge, wengine wamepigwa chini lakini yeye amesimama WHY?