THE MODERN WAR: Simulizi ya kijasusi mapenzi na upelelezi

THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..............22
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

22-(Kikosi cha Kunguru weusi)
ILIPOISHIA...
Vita kali inaibuka ndani na nje ya boti iliyokuwa ikienda kwa kasi, ni vita kati ya Tino anayemzuia Jasusi Shadow asiondoke na sanduku lenye vimelea vya V-COBOS wakati huo huo ndani ya boti hiyo mapigano makali kati ya Bosco na Wazari wa afya Dokta Gondwe yalikuwa yakiendela
Upande wa pili Najma anaanza kufuatilia na kuuchimba ukweli kuhusu vimelea vya V-COBOS.

Jez nini kitafuata?

SASA ENDELEA....
Shadow alikimbia akapanda juu kabisa ya boti Tino naye akamfuata hakutaka kumpa upenyo wa kuondoka na lile sanduku. Sasa walikuwa juu kabisa ya boti hiyo iliyokua ikienda kwa kasi ikipasua mawimbi ya bahari ya hindi. Si Shadow wala si Tino wote walikuwa vizuri kwenye suala zima la mapambano ya bila kutumia siraha.
Mara punde purukushani kati ya Bosco na Waziri wa afya Dokta Gondwe ilihama kutokea ndani ya boti sasa wakahamia nje. Hapo Dokta Gondwe aliweza kumuona Tino akipigana na yule mtu aliyeondoka na sanduku lake lakini cha ajabu Dokta Gondwe hakutaka kushughulika naye yeye akaendelea kukomaa na Bosco.

"Huwezi kuondoka hapa mpaka uniambie ni wapi ilipo dawa ya virusi vya COBOS" Dokta Gondwe aliongea kwa nguvu huku akifuta damu iliyokuwa ikimtoka puani
"Unajisumbua bure Dokta hupati chochote kutoka kwangu, na nitahakikisha nasambaza picha zako chafu mtandaoni" Bosco alijibu huku akitema damu
"Siwezi kukupa hiyo nafasi kijana leo ni ama zako ama zangu" alisema Dokta Gondwe huku akikimbia na kwenda kumvaa Bosco kwa mara nyingine wakaanza tena kupigana. Wakati huo pia juu ya boti bado mpambano kati ya Tino na Jasusi Shadow ulizidi kupamba moto.

Boti iliyokuwa ikienda kwa kasi bila kuongozwa na mtu yeyote sasa ilikuwa ikielekea nchi kavu ikiwa ibakiza mita chache kugusa ardhi mara Jasusi Shadow alilishika lile sanduku kisha akalitupa ndani ya maji kitendo hicho kilimshangaza sana Tino na kwakuwa hakutaka kuvipoteza vimelea vya V-COBOS haraka alijitosa majini kulifuata sanduku lile, sekunde chache baadae Jasusi Shadow naye akajitosa majini kumfuata.

Boti ilienda kwa kasi ikatoka ndani ya maji nakupaa juu mita chache kisha ikatua nchi kavu na kupinduka upande mmoja. Dokta Gondwe na Bosco ambao walikuwa hawelewi hili wala lile wajikuta wakijipigiza vibaya kwenye kuta za boti hiyo

Dokta Gondwe aliumia vibaya mno, aliinuka kwa kujikongoja akatazama pande zote na hapo ndipo alipobaini kuwa boti ilikuwa nchi kavu kwa sasa, aliendelea kuangaza macho yake kila mahali hakumuona Bosco, hakumuona Tino wala Jasusi Shadow.

"Ameenda wapi huyu mpuuzi?" alisema Dokta Gondwe huku akishuka kutoka kwenye boti akazunguuka upande wa pili kuangalia, hakuona mtu lakini mara alisikia vishindo nyuma yake akageuka haraka kuangalia hapo ndipo alimuona Bosco kwa mbali akikimbia kuelekea msituni. Dokta Gondwe hakuwa na nguvu kabisa ya kuendelea kumfuatilia, tayari alikuwa amejeruhiwa na kuchoka karibu kile sehemu ya mwili wake, alikuwa hoi.

Dokta Gondwe aliutazama ule msitu mdogo alikokimbilia Bosco kisha akafungua simu yake akaangalia ramani ya eneo hilo, mara akatabasamu.
"Huwezi kwenda kokote kijana lazima nikupate" alisema Dokta Gondwe baada ya kubaini kuwa kule alikokwenda Bosco ilikuwa ni Rasi yaani sehemu ya ardhi iliyoingia majini, kwa maana hiyo ili Bosco atoke ilikuwa ni lazima arudi alikotoka kwani alikoenda ilikuwa ni sehemu iliyozunguukwa na maji pande zote tatu.

Dokta Gondwe alibinya simu yake akapiga namba fulani kisha akaweka simu sikioni.
"Hallo"
"Ndiyo bosi nakusikia" sauti nzito ilisikika upande wa pili
"Nahitaji msaada njoo na kikosi chote cha Kunguru weusi nakutumia ramani nilipo, nawahitaji sasa hivi"
"Sawa bosi, lakini Kamanda Tino hayupo aliondoka asubuhi sana aka...."
"Nyie njooni Tino mtamkuta huku"
Aliongea Dokta Gondwe akakata simu kisha akamtumia mtu huyo uelekeo wa mahali alipo. Baada ya hapo alituma ujumbe mfupi wa maandishi kwenda kwa Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa.

,,,,,,,,,,,,Profesa nimefanya kama ulivyonishauri lakini mambo ni mazito sana huku baharini, yaani huwezi kuamini Waziri mkubwa kama mimi nahangaika huku badala ya kukaa bungeni, hawa wamexico wananitesa sana najuta kuchua ofa yao kweli nitafika mbinguni nimechoka sana,,,,,,,,,,

Baada ya kutuma ujumbe huo Dokta Gondwe alipiga hatua akaenda kukaa pembeni ya ile boti kusubiri kikosi cha Kunguru weusi. Jambo la ajabu ni kwamba alikuwa hajali kabisa kuhusu Tino na yule mtu aliyechukua sanduku lake, akili yake yote iliielekeza kwa Bosco


Vita ya Tino na Jasusi Shadow haikuishia kwenye ile boti, bado iliendelea hata ndani ya maji. Wakati Tino akilifuata sanduku lililokuwa linazama kwenye kina kirefu cha bahari Jasusi Shadow naye alikuwa nyuma yake akiogerea kwa kasi kumfuata. Wote walionekana ni wazoefu wa kuogerea na jambo lingine muhimu kila mmoja alikuwa na mtungi wa gesi uliomsaidia kupumua akiwa ndani ya maji.
Waliendelea kuvutana na kugeuzana wakiwa ndani ya maji kila mmoja akitaka kuwa wa kwanza kulifikia sanduku lile. Mwisho walizama mpaka chini kabisa wakagusa ardhi chini ya bahari. Jasusi Shadow alipata mwanya akafanikiwa kumbana vizuri Tino kisha akamchomolea ule mpira unaopitisha gesi kutoka kwenye mtungi akaukata kabisa, hapo Tino alijikuta anaanza kutapatapa baada ya kukosa hewa, mbaya zaidi walikuwa wamezama kwenye kina kirefu cha maji haikuwa rahisi kupata pumzi ya kutosha itakayomuwezesha kufika juu.
Jasusi Shadow alisogea hadi lilipo sanduku akalichukua kisha akaanza kuogerea kupanda juu akimfuata Tino ambaye kwa sasa alikuwa anaelekea kupoteza fahamu baada ya kukosa hewa na kunywa maji mengi.
Shadow alimfikia Tino akamshika na kuogerea naye hadi alipotokeza juu ya maji wakati huo tayari Tino alikuwa amepoteza fahamu hajitambua. Shadow alimbeba na kutoka naye hadi nchi kavu, akamlaza chini kisha akaanza kumminya tumbo kwa nguvu, Tino akawa anayatapika maji mengi aliyokunywa bila kupenda yakatokea mdomoni na puani. Shadow hakutaka kumuacha Tino afe, hilo halikuwa agizo la Sultana bosi wake ambaye pia alikuwa ni mama mzazi wa Tino, licha ya wanafamilia hao wawili kuwa na vita kali wakipigania vimelea vya V-COBOS lakini hakuna siku Sultana alimuagiza Shadow amuue Tino.

Baada ya kutoa huduma hiyo ya kwanza Shadow alimbeba Tino akaingia naye msituni hatua kadhaa kutoka usawa wa bahari akachukua kamba na kumfunga chini ya mti mmoja mkubwa. Wakati huo wote Tino alikuwa hajitambua.
Shadow alichukua lile sanduku akamtazama Tino kwa sekunde kadhaa kisha akageuka na kuondoka zake, akatokomea msituni.


Upande wa pili ndani ya gereza la Kanondo, gereza ambalo wafungwa walikuwa wakiishi maisha malaini sana tofauti kabisa na magereza mengine. Hapo ndipo alipokuwa ameifadhiwa kijana Osward mtoto wa kigogo mmoja maarufu kama mzee Matula, alikuwa hapo kwa zaidi ya miezi mitatu akisubiri kesi yake ya mauaji iliyokuwa bado inaendelea kuunguruma mahakamani.
Najma alifika kwa ajili ya kufanya mazungumzo nyeti na Osward ambaye alifurahi sana baada ya kumuona kwa mara nyingine tangu alipomuona siku iliyopita.
"Siamini kama umekuja kuniona tena Najma, nilipoambiwa na askari kuwa kuna mwanamke amekuja kuniona nikawa najiuliza ni nani huyo kumbe ni wewe mpenzi" Alisema Osward huku furaha yake ikionekana wazi kwa nuru iliyokuwa inang'aa usoni kwake, hakika alikuwa akimpenda sana Najma.

"Hebu kaa nina mazungumzo muhimu na wewe" Alisema Najma huku akionekana kutofurahiswa hata kidogo na maneno ya Osward.
"Sawa nimekaa, nambie mguu wako unaendeleaje?"
"Salama nilishapona"
"Kwa nini jana ukakubali kuondoka na inspekta Aron hujui kama yule ni adui yetu mkubwa na ndio sababu ya mimi kuendelea kuwa humu hadi leo?"
"Anafanya kazi yake acha kumlaumu, kama hukuua basi ukweli utajulikana tu kuwa mpole"
"Mmh mbona leo wewe ni mkali hivyo, uko sawa kweli Najma wangu?"
"Ki ukweli siko sawa, nitakuwa sawa kama utanijibu kwa uaminifu maswali yote nitakayokuuliza Osward" alisema Najma huku akikaa vizuri kwenye kiti
"Swali gani? uliza tu"
"Nataka kujua zile Safari ambazo baba alikuwa akikuagiza kwenda Mexico ulikuwa unaenda kufanya nini?" Najma aliuliza swali lililomfanya Osward ashtuke lakini akajitahidi kuficha mshtuko wake
"Kwani kuna nini mbona ghafula?"
"Ghafula nini si unijibu tu"
"Aah! Ni..nimambo mambo fulani fulani tu ee...lakini sana nilikuwa naenda kusimamia biashara zake kule Mexico"
"Biashara gani? nazijua bishara zote anazofanya baba sijawahi sikia hata siku moja akasema anabiashara Mexico unanidanganya Osward"
"Ni kweli anabi..."
"Sikia acha nikurahisishie swali naona unataka kuzunguuka sana, ni hivi unaelewa nini kuhusu virusi vya COBOS?" Najma alibadilisha swali lililomfanya Osward ashtuke sana hakuweza kuficha mshtuko wake tena.
"Nambie unajua nini ku..."
"Shiii!! Shiii! Najma tulia hutakiwi kutaja hilo neno hapa" alisema Osward huku akimtaka Najma anyamaze
"Kwa nini?"
Osward aliangaza macho huku na huku kisha akamsogelea Najma na kuongea kwa sauti ya chini
"Kuwa makini na hilo neno, utajitafutia matatizo"
"Kwa nini?"
"Najma nakuomba nakuomba sana kama umeanza au unataka kufuatilia kuhusu virusi vya COBOS basi acha sasa hivi kabla hujafika mbali, hili ni suala nyeti sana, kuna watu wakubwa na wazito wako nyuma ya hii ishu Najma sitaki kupoteza mpenzi wangu naomba acha na hili suala mara moja" Osward aliongea kwa msisitizo tena kwa kumaanisha sana huku akiwa ameikukutanisha mikono yake kama mtu anayeomba toba.
Najma alibaki katika hali ya mshangao, hakuelewa ni kwa nini Osward aliongea kwa uzito kiasi kile hapo akili yake ikafunguka akaamini kuwa suala la virusi vya COBOS ni kweli lipo na nizito sana, baba yake Dokta Gondwe anahusika pia.

Je, nini kitafuata?
ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya.........23
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

23-(Najma- nautaka ukweli)

ILIPOISHIA....
Najma alibaki katika hali ya mshangao, hakuelewa ni kwa nini Osward aliongea kwa uzito kiasi kile hapo akili yake ikafunguka akaamini kuwa suala la virusi vya COBOS ni kweli lipo na nizito isivyo kawaida, baba yake Dokta Gondwe anahusika pia.

SASA ENDELEA...
"Niambie kila kitu Osward, ni nini kinaendelea? ni jambo gani ambalo baba yangu analifanya kwa siri?" aliuliza Najma
"Najma sitaki ujiingize kwenye hili tafadhali naomba nielewe"
"Nimeshajiingiza tayari na huwezi kunitoa mpaka nihakikishe naelewa kila kitu, nambie Osward ni kweli baba anavyo vimelea vya V-COBOS? anataka kuvitumia kuua watu?" Najma aliuliza maswali mfurulizo. Osward alitulia kwa muda asijue amwambie nini Najma ambaye alikuwa amemganda haswa.
"Sawa nitakwambia kitu ninachokijua lakini chonde chonde usije kufanya jambo lolote ukahatarisha maisha yako kumbuka nimekwambia huu ni mpango wa watu wakubwa sana Dunia hata baba yako hawezi kuwazuia"
"Nambie nakusikiliza"
"Sijui kiundani sana ila ninachofahamu ni kwamba virusi hivi viliingia nchini kipindi Profesa Cosmas Kulolwa akiwa madarakani kama Rais, wakati huo baba yako alikuwa Waziri wa afya kama alivyo sasa ni watu wachache sana wanaelewa uwepo wa hivi virusi nchini mpaka sasa. Mpango uliopo ni kwamba siku moja hivi virusi vitaachiwa na kuleta janga lingine Duniani kama ilivyotokea kwa huu ugonjwa wa korona" alieleza Osward

"Sasa kwa nini baba afanye hivyo? Kwa nini ahatarishe maisha yake na yetu pia?"
"Hapana sivyo kama unavyofikiria Najma, kuna tofauti kubwa kati ya hivi virusi vya COBOS na virusi vya korona. Iko hivi kirusi cha COVID-19 hatujui kama kilitengenezwa au laa lakini hiki kirusi cha COBOS kimetengenezwa na tayari kuna kinga na tiba yake hivyo kabla ya kusambaza wote ambao wako kwenye mpango huu watajikinga wao na wapendwa wao kisha ndipo mengine yafuate" Alieleza Osward

"Ooh! Mungu wangu, hii dunia ina viumbe wa aina gani jamini, hebu niambie ukweli Osward baba yangu kalazimishwa au kataka mwenyewe?"
"Sijui kwa kweli?"
"Hujui nini? Si wewe ndio huwa anakuagiza huko Mexico unashindwa vipi kujua au lenu moja ninyi ni washikirika wao si ndio? mnatakaa kuua watu kwa manufaa yenu yaani hata hamuwazi kwa nini wamevileta hivyo virusi huku badala ya kuanzia kuvisambaza huko kwao, mna uhakika hiyo dawa ni sahihi? inatibu?"
"Najma acha kuwa mfukunyuku utakufa bado mdogo nimekwambia huu ni mpango wa watu wakubwa Duniani achana nalo wewe ni nani hadi utake kuingilia?"
"Mimi ni Najma mtoto wa waziri wa afya Dokta Gondwe ambaye amezuia mpango wa wapumbavu wachache waliotaka kuleta maafa na kuua watu wasio na hatia, hivyo ndivyo historia itakavyo andikwa hata kama nitakufa sawa wewe, naondoka" Najma aliongea kwa kujiamini kisha akachukua mkoba wake na kuondoka zake.
Alitembea kinyonge kutoka nje ya gereza hilo akaingia ndani ya gari yake akajitupa kwenye kiti, kichwa kilikuwa kikimuuma sana alilibeba jambo ambalo liko nje ya uwezo wake, Najma alifunga mlango wa gari kisha akawa amejiinamia akijaribu kuyatafakari yale aliyoelezwa na Osward. Bado lilikuwa ni suala gumu lisiloingia akilini kirahisi, alimpenda na kumuamini sana baba yake Dokta Gondwe.

Sekunde chache baada ya Najma kutoka nje ya lile gereza, Osward alisimama huku akihema kwa nguvu ilikuwa ni kama amechanganyikiwa hivi. Najma alikuwa amekuja na ajenda nzito siku hiyo ajenda ambayo hakuwa ametegemea kuisikia kutoka kwake. Hofu yake kubwa ilikuwa si virusi vya COBOS bali ni usalama wa Najma. Alimpenda sana mwanamke huyo mrembo, Hulka yake ya kutaka kuingilia suala la virusi vya COBOS ilikuwa ni sawa na kujipalia makaa ya moto, ukweli alikuwa akihatarisha maisha yake.

"Hii imekaaje? Dokta Gondwe kafanya uzembe gani hadi Najma amejua kuhusu vimelea vya V-COBOS, hapana hii haiwezekani kabisa ni lazima nifanye kitu bila hivyo watamuua, watamuua Najma wangu" aliwaza Osward huku akiumiza akili yake kufikiri nini afanye
"Muda wako umeisha unatakiwa kurudi sero" alisema askari magereza mmoja aliyemsindikiza Osward wakati alipokuja kuonana na Najma
"Hapana subiri, Seleman, Seleman Selemaniiii....." Alisema Osward kisha akaanza kupiga hatua kuelekea ilipokuwa ofisi ya mkuu wa gereza, yule askari akasimama mbele yake kumzuia lakini Osward alimsukuma pembeni kisha akaendelea upiga hatua kusonga mbele hapo wakaongezeka askari wengine wawili
"Hivi wewe unamwitaje mkuu wa gereza kama bibi yako?" alihoji askari mmoja aliyeongezeka
"Nataka kuonana naye"
"Osward umeanza tena vurugu zako za kila siku, hivi unajikuta nani wewe?"
"Nina shida ya muhimu nataka kumuona Selemani" Osward liongea kwa ukali na mara hiyo mlango wa ofisi ya mkuu wa gereza ukafunguliwa, akatoka SP Seleman.
"Kuna nini mbona kelele nyingi?" SP Seleman aliuliza kwa ukali
"Ni Osward mkuu, anataka kuingia ofisini kwako kwa nguvu" alieleza askari mmoja.
SP Seleman alimtazama Osward kwa macho makali, kisha akawaonyesha ishara askari wake akarudi ofisini. Wale askari waliokuwa wakimzuia Osward walimuacha na kuondoka.
Osward aliweka sawa vifungo vya nguo yake kisha akapiga hatua kuingia ofisi ya mkuu wa gereza akafika na kukaa kwenye kiti.
"Nikimweleza baba yako mambo unayoyafanya huku unajua nini kitafuata?"
"Samahani"
"Samahani? leo unasema samahani? Haya nini shida, vurugu zote za nini?"
"Naomba simu yako nahitaji kuongea na mtu wangu" alisema Osward
"Sasa kwa nini usiwe mstaarabu ni lini umeomba simu nikakunyima, unataka kila mtu aelewe kuwa tumeshikwa masikio na baba yako" SP Selemani aliongea kwa ukali na kusimama akamtazama Osward kwa sekunde kadhaa kisha akachukua simu yake iliyokuwa mezani akampa. Haraka Osward aliingiza namba za Big' kisha akapiga, wakati huo SP Selemani alirudi kwenye kiti akakaa.

Simu ya Big' iliita upande wa pili ikiwa mikononi mwa Inspekta Aron ambaye kwa sasa alikuwa kule msituni kwenye nyumba ya siri ya marehemu baba yake.
Inspekta Aron alichukua simu ya Big' ambaye kwa sasa ni marehemu akatazama namba ya mpigaji, akachukua simu yake na kuiingiza ile namba haraka akijaribu kuzilinganisha
"Nilijua tu ni wewe SP selemani" Inspekta Aron alijisemea mwenyewe baada ya kuhakikisha namba inayopiga kuwa ni ya mkuu wa gereza la Kanondo SP Seleman alipo hifadhiwa muharifu wake Osward.

Simu iliita na mwisho ikakata, Osward akapiga tena mara ya pili ikaita kwa muda mwisho ikapokelewa. Kukawa kimya kila mtu akisubiri mwenzake azungumze kwanza
"Hallo Big'" mwisho Osward aliongea akiwa mwenye wasiwasi kidogo
"Hilo ndio jina la mtu uliyemtuma aje kuniua?" alisema Inspekta Aron, Osward alitoa macho kwa mshangao, sauti aliyoisikia ilikuwa ya mtu mwingine tofauti na aliyemtegemea
"Aron" Osward aliita
"Ndiyo ni mimi"
Alijibu Inspekta Aron na hapo Osward akanyanyua mkono wake wenye simu juu kisha akaushusha chini kwa nguvu akaibamiza simu sakafuni ikasambaratika vipande vipande.
"Nini wewe, kwa nini umevunja simu yangu?" SP Seleman aliuliza kwa mshangao huku akisimama tena kwenye kiti

"Inspekta Aron, nitakuua mwenyewe kwa mikono yangu nitakukatakata vipande vipande na kuwapa mbwa nyama yako" Osward aliongea akiwa amekunja ngumi na kuuma meno kwa hasira. Inspekta Aron alikuwa amembana kila kona, kuanzia kwenye kesi ya mauaji inayomkabili, kwa kipenzi chake Najma na sasa kwa mtu wake wa kazi Big', hali ilikuwa ni ngumu mno upande wa Osward, hata matumaini ya kushinda kesi yake yalififia ghafula.
Upande wa pili Inspekta Aron alikuwa akitabasamu baada ya kuona anazidi kumpiga bao mtuhumiwa wake
"Ukiwa na hasira utaendelea kufanya maamuzi yasiyo sahihi yatakayonifanya niendelee kukusanya ushahidi wa kutosha kukufunga Osward" Inspekta Aron aliwaza, akapiga hatua kurudi sebureni. Alipomtazama Annah aligundua kuwa amelala pale juu ya kochi. Inspekta Aron alimuinua taratibu na kumbeba akaanza kupandisha ngazi kuelekea vyumba vya juu vya nyumba hiyo iliyojengwa kwa mbao.
"Unaniepeleka wapi" Annah aliuliza kwa sauti ya kudeka akiwa bado na usingizi
"Twende ukalale chumbani"
"Mmh hii nyumba inachumbani kumbe"
"Unaichukulia poa eti?" Aliuliza Aron huku akifungua mlango wa chumba kimoja akaingia na kwenda kumlaza Annah kitandani
"Woow! Mzuri natamani hata niishi huku milele" Annah aliongea na kutabasamu, Inspekta Aron akawa kimya
"Mnh! unanisafisha kidonda saangapi?"
"Ooh! Nilisahau hata hivyo muda bado"


Upande wa pili Dokta Gondwe alionekana akiwa amekaa na kujiinamia pembeni ya ile boti iliyoruka kutoka bahari hadi nchi kavu, alishtushwa na breki kali ya gari aina ya Noah nyeusi ambayo ilifika na kufungua breki kali mbele yake. Punde wakashuka wanaume saba wote wakiwa wamevaa makoti meusi pia walivaa maski nyeusi usoni zilizozuia sura zao kuonekana, mikononi mwao walikuwa wameshikiria bunduki aina ya SAR 21 zinazotoa miale mikali yenye rangi nyenduku
Dokta Gondwe alipowaona alitabasamu kisha akapiga hatua kuwafuata, hiki kilikuwa ni kikosi chake maarufu kama Kunguru weusi.

Je, nini kitafuata?
Tino yuko wapi?
Bosco atatoka salama?
Najma atafanya nini?
Vipi kuhusu Osward?
Nani atabaki na vimelea vya V-COBOS?
ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kasasi)
Sehemu ya...........24
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

24- (Sura ya kujificha)
ILIPOISHIA....23
mikononi mwao walikuwa wameshikiria bunduki aina ya SAR 21 zinazotoa miale mikali yenye rangi nyenduku
Dokta Gondwe alipowaona alitabasamu kisha akapiga hatua kuwafuata, hiki kilikuwa ni kikosi chake maarufu kama Kunguru weusi.

ILIPOISHIA....
Dokta Gondwe ilipiga hatua akaenda kusimama mbele ya kikosi hicho hatari
"Nina kazi muhimu sana" Alisema Dokta Gondwe
"Tupo hapa bosi tunakusikiliza" alijibu mmoja wa watu hao
"Kuna kijana kaingia kwenye huu msitu hapa nataka mmlete kwangu akiwa hai, hana kwa kukimbilia msitu huu umezunguukwa na maji pande zote kasoro huku tulipo namtaka kabla jua halijazama

"Sawa bosi, lakini vipi kuhusu kamanda Tino!?"
"Ongoza wewe kikosi Tino anakazi nyingine muhimu, mmoja abaki hapa wengine wote ingieni msituni kagua kila mahali juu ya miti vichaka vyote fumueni msirudi hapa kama bado hamjampata" Dokta Gondwe aliongea kwa msisitizo, wanaume wakaingia kazini.

***********
{TANGAZO:- Epuka matapeli simulizi hii imetungwa na SAUL DAVID simu 0756862047, Tafadhali usinunue kwa mtu mwingine tofauti }
******-*-

Hali ya Bosco haikuwa nzuri hata kidogo, ukiachana na ngumi alizopigwa na Dokta Gondwe lakini pia aliumia vibaya sana wakati ule boti iliporuka kutoka baharini hadi nchi kavu na baadae ikapinduka. Alikuwa akitembea huku akipepesuka, kila alipokwenda mbele alikutana na kizuizi cha maji ya habari, alipoenda upande mwingine alikuta hali ni ileile mwisho akachoka. Hakuwa na wasiwasi sana kwani aliamini ameshamuacha mbali Dokta Gondwe hakujua huku nyuma mheshimiwa kaita kikosi cha Kunguru weusi kuja kumsaidia.

"Bosco, Bosco Bo.. Bosco...." Wakati Bosco akizidi kuzurula msituni mara alisikia sauti ya mtu ikimuita, aliishtukia sana na kugeuka.
Chini ya mti mmoja alimuona mtu akiwa amekaa amenyoosha miguu huku mikono yake ikiwa imezunguushwa nyuma ya mti kisha ikafungwa. Bosco alipomtazama vizuri alimfahamu alikuwa ni Tino bosi wake

"Mkuu!...mkuu! vipi?" Aliuliza Bosco huku akijikongoja kukimbia, akafika na kuanza kumfungua zile kamba

"Uko sawa bosi nini kimetokea?" aliuliza Bosco
"Dokta Gondwe yuko wapi?" Badala ya kujibu swali Tino akauliza swali
"Nimemuacha huko mbali ufukweni" alijibu Bosco, hapo Tino akavuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu

"Yule mpuuzi kaondoka na sanduku" Alisema Tino
"Nani?"
"Hukumuona yule jamaa nilikuwa napambana naye"
"Nilimuona kwa mbali ndio nauliza ni nani?"
"Simjui hata sura yake sikuiona lakini pia mambo yake yananichanganya"
"Kivipi bosi?"
"Alinizidi nguvu tukiwa ndani ya maji, nikakata tamaa nikaamini ataniua lakini cha ajabu kanisaidia nina hakika yeye ndiye aliyeniokoa kutoka kwenye maji na kunileta hapa"
"Mmh! lakini pengine bado anajambo wewe ndio maana kakufunga hapa huenda atarudi" alisema Bosco
"Hawezi kurudi angalia hapo" alisema Tino huku akimuonyesha Bosco pembeni ya mti, Bosco alipotazama akaona kisu kidogo
"Aliacha hicho kisu kidogo maana yake alitaka nijifungue mwenyewe kwa kukata hizi kamba" alisema Tino akijaribu kufikiri kwa kina kuelewa kitendo hiki kilichofanywa na jasusi Shadow.

"Sikia"Alisema Tino mara baada ya kusikia vishindo karibu kabisa na eneo hilo, Bosco naye alisikia pia. Wakatega sikio huku wakiangaza macho yao pande zote kuangalia na hapo ndipo walipowaona watu wawili wakiwa na bunduki mkononi.
"Shiiit! ni Kunguru weusi" alisema Tino huku akijaribu kufikiria afanye nini. Shida haikuwa kwake bali kwa kijana wake Bosco. Kunguru weusi lilikuwa ni moja kati ya vikosi anavyoviongoza Tino akiwa chini ya Dokta Gondwe.

"Unawajua"
"Ndiyo ni kikosi hatari cha Dokta Gondwe, itakuwa kaamua kuongeza nguvu apate sanduku lake akukamate na wewe pia" alieleza Tino
"Tunafanyaje sasa bosi?"
"Ondoka hapa kimbia hakikisha hawakukamati, jifiche kokote hata ikibidi jifukie chini ya ardhi Bosco nitakuwa karibu kukusaidia kuhakikisha hawakukamati sawa"
"Sawa mkuu"
"Haya nenda kuwa makini"
Bosco alinyata na baada ya kufika mbali akaanza kukimbia na kutokomea msituni, dakika chache baadae wale watu wawili walifika hadi pale alipo Tino, walishuka sana baada ya kumuona kiongozi wao akiwa kwenye hali mbaya.
"Kamanda Tino uko sawa? Nini kimetokea" aliuliza mtu mmoja huku mwingine akipiga mruzi uliotoa sauti kama mlio wa ndege. Dakika tatu baadae kikosi kizima cha Kunguru weusi walifika eneo hilo na kumzunguuka kamanda wao

"Niko sawa msijali, kuna mtu nlikuwa napambana naye kanizidi ujanja na kukimbia" alieleza Tino
"Kaelekea wapi tumfuatilie"
"Hapana ni kitambo sana"
"Unamaana gani kusema ni kitambo Dokta katuagiza tumsake kila kona na kasema amekimbilia ndani ya huu msitu mda si mrefu"
"Mtu gani? Mwenye sanduku?"
"Sanduku? Hajatuambia habari za sanduku, kasema tumfuatilie kijana amevaa suti ya ugoro"
"Hakuna mtu mwingine kawambia mnatakiwa kumfuatilia mwenye sanduku?"
"Hapana katuelekeza mmoja tu na kasema tumpeleke akiwa hai, kwani wako wangapi Kamanda Tino?"
"Subiri kwanza mpigie simu nionge naye" alisema Tino huku akijaribu kuwachelewesha makusudi ili Bosco akimbie na kufika mbali.
Simu ilipigwa kwa Dokta Gondwe ikaita kwa sekunde kadhaa kisha ikapokelewa.
"Mkuu tunaendelea na kazi lakini tumempata kamanda Tino yuko hapa hali yake sio nzuri sana nampa simu" alieleza yule mtu kutoka kikosi cha Kunguru weusi kisha akampatia Tino simu azungumze na Dokta Gondwe

"Hallo bosi"
"Ndiyo Tino pole"
"Asante bosi, samahani nimeshindwa kumthibiti yule jamaa aliyechukua sanduku kakimbia"
"Achana naye huyo wa sanduku namtaka huyu mwingine kijana mdogo mdogo ambaye nilikuwa napambana naye wakati ule" alieleza Dokta Gondwe
"Vipi kuhusu huyu wa sanduku?" Aliuliza Tino
"Achana naye nimesema, kwanza wewe rudi upumzike waache wenzio ndio waifanye hiyo kazi"
"Lakini bosi mimi ni....."
"Tino unachelewesha kazi, hebu rudi huku nimekwambia" Dokta Gondwe alifoka kisha akakata simu
Tino hakuwa na nguvu ya kuendelea kubishana na Dokta Gondwe lakini jambo lililomshangaza ni namna Dokta Gondwe alivyokuwa akimuhitaji sana Bosco kuliko sanduku lenye vimelea vya V-COBOS.

"Au lile sanduku ni tupu halina kitu? Au pengine amekata tamaa kuhusu vimelea vya V-COBOS kwa sasa anapambana kuhakikisha picha zake za ngono hazisambazwi mtandaoni?" Tino alikuwa akijiuliza maswali ambayo hakuwa na majibu yake.
Mwisho alijikongoja kurudi kama alivyoagizwa na bosi wake akawaacha Kunguru weusi wakiendelea na msoka mkali ndani ya msitu huo kuhakikisha wanampata Bosco


Najma alirudi nyumani, akaoga akavaa kijinguo chepesi cha kulalia kisha akajitupa kitandani akiwa amelala chali. Akawa anatazama juu huku akivuta kumbukumbu ya mambo yaliyotokea ndani ya hizi siku chache tangu arudi kutoka Nairobi-Kenya. Alimkumbuka Mzee Matula tajiri ambaye ni baba wa Osward, mzee anayemtaka kimapenzi baada ya kuona ameshindwa kumlaghai sasa ameamua kutumia nguvu ya ushawishi kulazimisha ndoa kati yake na Osward ambaye bado yupo gerezani. Kumbukumbu za Najma zikampeleka mbali na hapo akamkumbuka Inspekta Aron mwanaume ambaye awali alimchukulia kama adui lakini ghafula wanazoeana ndani ya mda mfupi na kuwa marafiki wakubwa. Alikumbuka namna alivyokuwa akimchua kwenye paja mahali alipoumia, Najma akatabasamu.
Ghafula tabasamu lake likapotea pale alipokumbuka kuhusu vimelea vya V-COBOS, taarifa alizopewa kuwa baba yake ni mmoja kati ya watu waliopo kwenye mpango huo hatari zilimkosesha raha kabisa.

,,,,,,,Kama ukijaribu kujiingiza kwenye hili utakufa Najma,,,,,
Maneno haya ya Osward yalijirudia rudia kwenye kichwa cha Najma na kuzidi kumpa wasiwasi. Akaona kabisa kuna kila sababu ya kumtafuta mtu ambaye atafanya kazi hii ya kuchimba kwa undani kuhusu vimelea vya V-COBOS wakiwa pamoja. Najma akamkumbuka tena Inspekta Aron akaamini huyu ndiye mtu pekee atakayemfaa kwenye kazi hii. Alichukua simu yake akapiga namba ya Inspekta Aron, simu iliita kwa sekunde kadhaa kisha ikapokelewa.

"Hallo mpenzi" Najma aliongea kwa sauti laini
"Nambie babygirl" Inspekta Aron akaitikia upande wa pili kisha wote wakacheka kwa pamoja
"Sasa mbona unanicheka?" Inspekta Aron akauliza huku akipandisha ngazi kwenda chumba cha juu alikolala Annah, mkononi alikuwa amebeba shuka akafika na kumfunika Annah kisha akatoka tena.
"Umenifurahisha tu" alijibu Najma akiendelea kucheka
"Nimekufurahisha kwa lipi sasa?"
"Niliambiwa mapolisi huwa hawako romantic kabisa sasa nashangaa wewe umejifunzia wapi"
"Hahaha! umenifundisha wewe"
"Mmh tangu lini jamani, sijui chochote mimi"
"Nitajuaje?"
"Utajua tu"
"Haya nambie Najma unaendeleaje"
"Niko poa, now naendelea vizuri"
"Kweli ee!"
"Kweli nashangaa hata daktari wangu haujaja kuniona au unamuogopa baba"
"Aah! wapi huwa siogopi mtu mimi"
"Mmh! Muongo mbona jana alipokuta umenibeba ulipomuona kidogo tu unitupe chini"
"Hahahah Najma acha uongo mungu anakuona"
"Hahaha! sasa Aron"
"Yes nambie"
"Kuna jambo nataka tuzungumze mimi na wewe, vipi tunaweza kuonana leo?"
"Saa ngapi"
"Muda wowote kwanzia sasa"
Inspekta Aron alitulia kwa muda kutafakari, ilikuwa ni ngumu kutoka na kumuacha Annah mazingira hayo ambayo tayari alikuwa na wasiwasi nayo
"Mbona kimya au huna nafasi?"
"Aa..! Hapana nafasi itapatikana sema tu niko mbali kidogo ila tutaonana usijali"
"Sawa utanishtua basi... Hallo... Hallo ... Aron" alisema Najma lakini akashangaa Inspekta Aron ameacha kusikika ghafula na mwisho simu ikakatwa
"Ana nini huyu, sipendagi wanaume wa hivi mimi" Najma alilalamika kisha akatupa simu yake pembeni akajifunika gubigubi.

Upande wa pili si kwamba Inspekta Aron aliacha kujibu kwa makusudi hapana, kunajambo aliliona.
Wakati anazungumza na Najma kupitia dirishani alimuona mtu anakuja kwenye nyumba hiyo. Mtu huyo likuwa amevaa nguo nyeusi kuanzia juu mpaka chini, usoni alifunika sura yake kwa kuvaa maski nyeusi na kofia nyeusi aina ya kapero. Mgongo alikuwa na begi kubwa na mkononi alishikilia sanduku dogo, huyu alikuwa ni Jasusi Shadow.

Inspekta Aron alisogea dirishani akawa anamfuatilia mtu huyo ambaye alitembea bila wasiwasi wote akasukuma mlango na kuingia ndani. Inspekta Aron alipandisha ngazi akasogea vyumba vya juu kule alikolala Annah kisha akatafuta nafasi ya kuchungulia chini akawa anafuatilia kila anachokifanya mtu huyo ambaye alionekana ni mwenyeji kabisa na nyumba hiyo.
Jasusi Shadow ambaye awali alifanya kazi na baba yake Aron yaani marehemu Jenerali Phillipo Kasebele sasa alikuwa ameweka makazi yake katika nyumba hiyo mara tu baada ya mzee huyo kufariki. Wakati Inspekta Aron akizidi kumtazama mtu huyo kwa namna alivyovaa aliweza kugundua kuwa huyu ndio yule mtu aliyekutana naye asubuhi ya siku hiyo ndani ya hospitali ya Mountenia, akakimbia baada ya kumchoma sindano iliyomkosesha pumzi. Inspekta Aron akawa makini zaidi huku akifuatilia kila hatua ya mtu huyo hatari.
Jasusi Shadow akiwa hajui kama mle ndani kuna watu, aliendelea kuwa bize na mambo yake. Alishusha begi lake chini, akaweka chini ya meza lile sanduku analoamini lina vimelea vya V-COBOS akafungua friji akachukua maji ya kunywa akaweka mezani, akavua koti lake kubwa akalining'iniza kwenye msumali uliopigiliwa kwenye ukuta wa mbao wa nyumba hiyo kisha na yeye akajitupa kwenye kiti.
Jasusi Shadow alivuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu alionekana amechoka sana baada ya purukushani nzito kule baharini. Akasogeza maji yake karibu. Taratibu akavua kofia yake na mwisho akavua ile maski, kwa mara ya kwanza Inspekta Aron akaiona sura ya Jasusi Shadow, sura ambayo hata marehemu baba yake hakuwahi kuiona lakini leo sura ya Jasusi Shadow inaonekana.

Je nini kitafuata?
Vipi pia kuhusu Bosco, Tino na Dokta Gondwe?
Najma atafanya nini?
ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..........25
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

25-(Bosco kwenye mikono ya Kunguru weusi)
ILIPOISHIA....
Jasusi Shadow alivuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu alionekana amechoka sana baada ya purukushani nzito kule baharini. Akasogeza maji yake karibu. Taratibu akavua kofia yake na mwisho akavua ile maski, kwa mara ya kwanza Inspekta Aron akaiona sura ya Jasusi Shadow, sura ambayo hata marehemu baba yake hakuwahi kuiona lakini leo sura ya Jasusi Shadow inaonekana.

SASA ENDELEA...
Jambo moja la msingi katika kipindi chote alichokuwa akifanya kazi na marehemu Jenerali Phillipo Kasebele ilikuwa ni kutoonyesha sura yake kwa mtu yeyote yule hata baada ya kuendelea kufanya kazi na Sultana mke wa Kasebele bado sheria yake ilibaki kuwa pale pale, hakuna mtu anayeweza kuiona sura yake. Lakini leo kwa bahati mbaya anaiweka wazi sura yake mbele ya Inspekta Aron pasipo kujua.

Shadow alikunywa maji haraka haraka kisha akafungua droo ya meza akatoa kompyuta yake ndogo na kuiweka mezani, akafungua droo nyingine ambayo ndani yake kulikuwa na simu ndogo nyingi kwa makadirio ya haraka zilifika 15, akachagua moja kisha akapiga namba fulani na kuiweka simu sikioni. Simu iliita kwa zaidi ya dakika moja baadae ikapokelewa

"Shadow" sauti ya Sultana akiwa hospitali ya Mountenia ilisikika kwenye simu
"Ndiyo ni mimi madam" Jasusi Shadow aliitikia
"Kazi imekwendaje kijana wangu?"
"Nimefanikiwa mama, nimechukua mzigo ninao hapa"
"Ooh! Hongera sana kijana wangu, hatuna muda wa kupoteza mpigie mwenako kisha tukutane Ambross"
"Sawa madam" shadow aliitikia kisha akakata simu.
Maongezi yote hayo Inspekta Aron alikuwa akiyasikia mubashara akiwa pale juu lakini kwa bahati mbaya hakuweza kuitambua sauti ya mama yake madam Sultana

Baada ya kukata simu Jasusi Shadow aliandika ujumbe kwenda namba aliyoihifadhi kwa jina la 'shem J'

,,,,,,,,,, Tayari nimefanikiwa kuchukua vimelea vya V-COBOS, madam kasema tukutane Ambross jioni hii,,,,,,,,

Baada ya kutuma ujumbe huo Shadow livaa koti lingine refu jekundu akachukua maski na kofia yake akavaa kama ilivyokuwa kawaida yake. Alichukua lile sanduku akasogea nalo hadi kwenye kabati moja kubwa akalifungua, ndani ya kabati hilo kulikuwa na picha kubwa ya marehemu Jenerali Phillipo Kasebele ambaye ni baba wa Tino na inspekta Aron.

Shadow alipiga sulute na kuonyesha heshima kubwa mbele ya picha hiyo kisha taratibu akatoka nje, akarudisha mlango wa nyumba hiyo akaondoka zake.
Inspekta Aron aliyashuhudia yote haya akiwa kwenye kona moja katika vyumba vya juu vya nyumba hiyo.
Alitamani kumfuatilia Jajusi Shadow lakini akasita, alikumbuka siraha kali anazotumia mtu huyo si wakumsogerea kizembezembe.
Baada ya kuhakikisha ameondoka Inspekta Aron alishuka ngazi hadi sakafu ya chini alipokuwa Jasusi Shadow, akaanza kuchunguza kwa makini kila alichokiona wakati ule, aliitazama ile kompyuta akajaribu kuiwasha lakini aligundua imewekwa nywira hivyo ni ngumu kufunguka, alifungua pia zile droo na kuanza kupekuwa kitabu kimoja baada ya kingine.
Maswali kadhaa yaliibuka kichwani kwa Inspekta Aron ilkiwa ni pamoja na kutaka kujua undani wa mtu huyo ni nani? Pale hospitali alifuata nini? Kwa nini apige saluti ya heshima mbele ya picha ya marehemu baba yake?. Haya ni maswli ambayo Inspekta Aron alitamani kupata majibu yake haraka iwezekanavyo.

Akiwa anaendelea na uchunguzi wake mara alisikia vishindo vya Annah akiteremka ngazi kuja alipo. Haraka Inspekta Aron aliacha kufanya kile alichokuwa akikifanya akajikausha kama vile hakuna jambo lililotokea. Hakutaka kumwambia Annah kinachoendelea ndani ya nyumba hiyo akiamini pengine angempa wasiwasi binti huyo yatima.

"Vipi?" Aliuliza Aron
"Poa mbona sasa umekaa peke yako"
"Hamna kuna mambo nayaandaa hapa si unajua weekend karibu inaisha kesho kutwa kazini"
"Okay! bila shaka muda wa kunisafisha kidonda umefika" Alisema ana huku akimuonyesha Aron lile begi la huduma ya kwanza alilokujanalo
"Yes! Njoo ukae hapa" alisema Aron, Annah alisogea na kukaa pembeni yake Inspekta Aron alisogeza lile begi la dawa akatoa vifaa muhimu kwa ajili ya kumsafisha Annah kidonda.
"Ulikuwa unalia tena ee!?" Aliuliza Aron baada ya kumtazama Annah usoni
"Hapana nilisha lia vya kutosha Aron, najua ipo siku mungu atanilipia kwa wale wote walioshiriki kuwaua kikatili mama na baba yangu, naamini siku hiyo ndio roho zao zitapumzika kwa amani" Annah aliongea kwa uchungu, ilibidi Aron abadilishe mada haraka ili kutoruhusu Annah atawaliwe na simanzi kwa mara nyingine.

"Toa nguo yako basi nikuhudumie" alisema Aron. Annah akavua kibode chake akabaki na sidiria pekee, awali alikuwa akiona aibu mwisho akazoea.
Taratibu Inspekta Aron alifungua kamba moja ya sidiria ya Annah huku akiwa makini asije kuyaacha wazi matiti ya binti huyo mrembo kisha akakifunga kidonda kilichokuwa pembeni kidogo ya ziwa la kulia la Annah akakisafisha akakifunga tena bandeji nyingine kwa umakini wa hali ya juu. Wakati wote huo Annah alikuwa akimchunguza Aron kwa macho yaliyojaa huba akajikuta anazidi kuvutiwa zaidi na mwanaume huyo ambaye alikuwa ameuteka moyo wake vilivyo.

"Aron" Annah aliita
"Naam"
"Nikuombe kitu"
"Yes kuwa huru Annah"
"Kesho kutwa ni siku ya kusikilizwa kesi ya Osward na kutoa hukumu, kama tukimaliza kila kitu kikaenda vizuri naomba uniruhusu nije kukaa huku" Alisema Annah
"Ukae huku kivipi?"
"Nikae huku na wewe Aron, sitaki kukaa mbali na wewe naogopa" alisema Annah, Inspekta Aron akatulia kwa muda akitafuta jibu sahihi la kumpa.


Upande wa pili Waziri wa afya Dokta Gondwe,Tino pamoja na mmoja wa watu kutoka kikosi cha Kunguru weusi walionekana wakiwa wamesimama pembezoni mwa bahari jirani na msitu mmoja ambao ndipo Bosco alikokimbilia na sasa alikuwa akisakwa kila kona na kikosi cha Kunguru weusi. Walikubaliana na Dokta Gondwe wasirudi hadi pale watakapo hakikisha wamempata Bosco.

Tino alikuwa akimtazama dokta Gondwe kwa macho ya kuibia ibia akaona namna mzee huyo alivyokuwa hana amani, aliamini kama atampoteza Bosco basi kuna uwezekano mkubwa akasambaza picha zake chafu kwani hakumpa vimelea alivyokuwa anavihitaji.
Tino naye alitulia akiwa anawaza nini atafanya kama Bosco atakamatwa kwani kulikuwa na kila dalili za kikosi cha Kunguru weusi kumkamata ukizingatia kwanza hali ya Bosco haikuwa nzuri ki afya

Ni kweli nusu saa baadae Kikosi cha Kunguru weusi walichomoza kutoka msituni huku wakimkokota Bosco aliyekuwa amelegea sana baada ya kupigwa vikali na watu hao. Tino alitoa macho kwa mshangao asiamini anachokiona lakini hali ilikuwa tofauti kwa Dokta Gondwe ambaye yeye alionyesha tabasamu pana mara tu baada ya kumuona.
Tino na Bosco walitazamana kisha Tino akampa ishara kuwa aendelee kubaki kwenye mpango wao bila kuharibu chochote, ingawa Bosco alikuwa kwenye hali mbaya lakini alimsikiliza na kumuamini sana bosi wake Tino. Bila kuchelewa waliingia kwenye gari safari kuelekea kambini ilianza. Katika kambi hiyo, huko ndiko mambo na mikakati yote ya kiovu ya mheshimiwa Dkt Gondwe ilikuwa ikipangwa.


Nusu saa baadae tayari Dokta Gondwe aliwasili kambini akiwa na kikosi chake, walimfungia Bosco ndani ya chumba kimoja chenye giza nene wakamuacha humo. Baada ya hapo Dokta Gondwe aliomba mazungumzo na kijana wake mwaminifu Tino, wakakaa kwenye viti chini ya mti mmoja mkubwa uliokuwa nje ya kambi hiyo.

"Pole kwa yote kijana wangu" Dokta Gondwe alianzisha mazungumzo
"Asante bosi nimeshapoa"
"Vizuri, sasa nataka nikuruhusu ukapumzike kwanza kutokana na kazi ngumu na haya yaliyotokea leo najua yule bwana amekuumiza sana" Alisema Dokta Gondwe
Akili ya Tino iliweza kufanya kazi vizuri akajua tu kwa vyovyote vile Dokta Gondwe anataka kumuweka mbali ili asijue lolote kuhusu uhasama wake na Bosco ambaye anazo video na picha za ngono alizolala na mke wake.
"Hataki nipate nafasi ya kujua kinachoendelea, anaogopa nitajua tukio la yeye kulala na mke wangu Jesca" aliwaza Tino kisha akainua uso wake na kumtazama Dokta Gondwe.
"Lakini bosi kwa mara ya kwanza nimefanya kazi na wewe pasipo kupata maelezo ya kina, sitaki kukuingilia sana lakini mambo yanaweza kubadilika huko mbele nikawa msaada kwako, samahani nataka kujua huyo dogo tuliyemkamata leo ni nani lakini pia kwa nini hujataka tushughulike sana na yule bwana aliyeondoka na sanduku lako?" Tino aliuliza maswali yenye mtego ndani yake. Dokta Gondwe alijikohoresha kidogo kisha akajibu.

"Ni kweli wewe ni kijana wangu wa pekee sana Tino, unastaihili kujua kila kitu kama ninavyofanya siku zote lakini leo umepatwa na jambo kubwa, umeumia na hauko sawa, nenda kapumzike kwanza ukirudi nitakuelewesha kila kitu" Aliahidi Dokta Gondwe ahadi ambayo anajua kabisa hawezi kuitumiza.
Ilikuwa hivyo na baadae Tino akaamua kukubaliana na matakwa ya bosi wake.

Lakini kabla hajatoka nje kabisa ya kambi hiyo Tino akiwa kama mkubwa wa kambi hiyo alikuwa ni mzoefu wa njia zote za siri, alijipenyeza na kuingia ndani ya kile chumba cha giza alichofungiwa kijana wake Bosco.

"Bosco! Bosco!" Tino aliita kwa sauti ya chini. Bosco aliyekuwa amefungwa mikono na miguu kwenye kiti alifumbua macho yake kutazama, licha ya kuwa na giza lakini aliweza kutambua uwepo wa bosi wake mle ndani. Sekunde chache baadae alimuona Tino mbele yake ambaye alikuwa na chupa ya maji mkononi akaifungua na kumnywesha.
Bosco aliyafakamia yale maji akayanywa upesi upesi akamaliza chupa yote ya lita moja na nusu.

"Pole Bosco sina mda mrefu hapa najua unapitia kipindi kigumu sana lakini usijali mimi nipo nitakulinda, kwa sasa naondoka nakwenda kufanya kitu ambacho kitamfanya Dokta Gondwe asikuguse hata unywele wako" alieza Tino kwa sauti ya kunong'ona
"Utafanyaje bosi?"
"Naenda kuachia picha moja kwenye mitandao ya kijamii, picha ya ngono ya Dokta Gondwe"
"Mmh! hapana bosi Usifanye hivyo kwa sasa huyu ni waziri mkubwa serikalini, utasababisha balaa jingine alafu vipi kuhusu mkeo?"
"Usijali Bosco najua kitu sahihi cha kufanya, akishaziona hizo picha wewe endelea kumtisha mwambie kama atakugusa basi utaachia video nzima mtandaoni, mwambie akueleze kwa kina kuhusu lile sanduku na ukweli wa vimelea vya V-COBOS hawezi kuendelea kubishana na wewe hatokuwa na hiyi nguvu tena" Alieleza Tino.
Je, nini kitafuata?
Ni kweli lile sanduku lina vimelea vya V-COBOS?
Sultana atafanya nini baada ya Jasusi Shadow kupeleka sanduku?
Vipi kuhusu Inspekta Aron,Annah na Najma?
ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..............26
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862847

26-(Skendo)

ILIPOISHIA.......25
"Usijali Bosco najua kitu sahihi cha kufanya, akishaziona hizo picha wewe endelea kumtisha mwambie kama atakugusa basi utaachia video nzima mtandao, mwambie akueleze kwa kina kuhusu lile sanduku na ukweli wa vimelea vya V-COBOS hawezi kuendelea kubishana na wewe hatokuwa na hiyi nguvu tena" Alieleza Tino

Je nini kitafuata?

SASA ENDELEA...

Tino alirejea nyumbani alipokuwa akiishi yeye mkewe Jesca pamoja na Inspekta Aron.
Alikumbuka mara ya mwisho alipokuwa hapo aligombana vikali na mkewe Jesca kwa kosa alilofanya kumuweka kifaa kilichokuwa kikimsaidia mdogo wake Aron kujua mahali alipo. Siku hiyo Tino alimpigia kibao kikali ambacho kilikuwa kimebeba hasira ya makosa mawili si lile la kumuwekea kifaa pekee bali na kosa kubwa ambalo lilikuwa ni ukweli mchungu kwa Tino baada ya kushuhudia video ya mkewe Jesca akimsaliti kwa kufanya mapenzi na Waziri wa afya Dokta Gondwe ambaye pia ni bosi wake.
Tino aliporejea nyumbani alikuta mkewe Jesca anajiandaa kutoka, alikuwa amevaa suruali nyeupe inayomwaga chini kitop miwani na kofia vyenye rangi nyeupe pia, alikuwa amependeza si kidogo.

"Unaenda wapi?" Tino alimuuliza mkewe mara baada ya salamu
"Hospitali" Jesca alijibu kwa kifupi huku akionekana hayupo kwenye mudi ya kuongea na mumewe
"Kufanyaje hospitali mda huu?"
"Naenda kumuona mama na kutibiwa pia hukumbuki uliniumiza.."alieleza Jesca huku akitazama pembeni. Ni kweli mara kwa mara Jesca alikuwa na utaratibu wa kwenda kumuona mama mkwe wake yaani Sultana kule hospitali ya Mountenia.
Kwa namna alivyokuwa amevaa moyo wa Tino uligoma kabisa kukubaliana na maelezo ya Jesca akahisi labda anakwenda kumsaliti tena na bosi wake Dokta Gondwe.
Baada ya kusema hivyo Jesca alitoka na kuondoka zake, aliujua udhaifu wa mumewe kuwa alikuwa akimpenda sana hivyo aliitumia hiyo kama fimbo ya kumchapia, akayatawala mahusiano yao kwa kiasi kikubwa. Baada ya Jesca kuondoka Tino naye hakukaa sana alifanya kile kilichomleta kisha akaondoka kuelekea ilipokuwa ofisi yake ya siri, ile ofisi ambayo anarekodi na kupiga picha watu mbalimbali wakiwa faragha na wapenzi wao kupitia kamera za siri alizotegesha kwenye nyumba mbalimbali za wageni.

***********
{TANGAZO:- Epuka matapeli simulizi hii imetungwa na SAUL DAVID simu 0756862047, Tafadhali usinunue kwa mtu mwingine tofauti }
******-*-

Upande wa pili katika hospitali ya kimataifa ya Mountenia, gari ya wagonjwa(ambulance) ilionekana inatoka kwa kasi huku ikipiga king'ora kwa sauti kubwa ikaingia mtaani. Gari hiyo ilienda kwa kasi sana na baada ya kwenda mwendo wa wastani wa dakika 10 baadae ikiwa katikati ya mji king'ora kilizima dereva akakata kona kulia akaiacha barabara kuu na kuingia mtaani. Baadae gari hilo liliingia kwenye kichochoro kimoja likasimama mbele ya kichochoro hicho kulikuwa na gari nyingine dogo aina ya Nissan imesimama pia.
Mara tu baada ya ile gari ya wagonjwa kusimama mlango ulifunguliwa akashuka mama mmoja mrefu mnene akiwa amevalia dera nzuri la batiki mtandio mweusi, hijabu na miwani yenye rangi nyeusi pia, sura yake ilikuwa imefunikwa na barakoa aliyoivaa. Mama huyo alishuka na kuhamia kwenye ile gari dogo Nissan na mara tu baada ya kuingia madereva wote waliwasha gari zikapishana moja ikatokea upande huu wa kichochoro na nyingine ikatokea upande wa pili.

Ile gari aliyopanda mama aliyekuja na gari ya wagonjwa Nissan iliingia katikati ya mji kwa mwendo wa kawaida sana.
Yule mama akavua ile barako taratibu, amini usiamini alikuwa ni Madam Sultana mama wa Tino na Aron yule anayeigiza kuwa ni mgonjwa akiwa amelazwa hospitali ya Mountenia kwa zaidi ya miezi sita mpaka sasa
Hivi ndivyo namna Madam Sultana livyokuwa akiingia na kutoka katika hospitali ya Mountenia kupitia gari la wagonjwa, akawa anaendelea na mipango yake ya siri huku watu karibu wote wakijua kuwa mama huyo ambaye ni mume wa marehemu Jenerali Phillipo Kasebele ni mgonjwa mahututi.
Wakati gari ikizidi kwenda Sultana alichukua simu yake akampigia kijana wake Jasusi Shadow.
Jasusi Shadow alionekana katikati ya mji akiendesha pikipiki akielekea Ambross kama alivyokubaliana na Sultana. Wakati simu yake inaita alisimama pembeni ya barabara akaichukua simu yake na kupokea
"Ndiyo Sultana"
"Uko wapi kwa sasa?"aliuliza Sultana
"Naelekea Ambross Sultana"
"Upo na vimelea?"
"Ndiyo"
"Ulimtaarifu mwenzako?"
"Ndiyo nilimtumia ujumbe wa maandishi"
"Kwa nini? Si ungempigia"
"Nlihofu pengine anaweza kuwa karibu na mumewe, huwa tunafanya hivyo siku zote"
"Sawa hebu jaribu kumpigia,mimi nimeshatoka hospitali inatakiwa tufike Ambross kwa wakati tayari tumeshapata vimelea hatuna mda wa kupoteza" Alisema Sultana kisha akakata simu
Dakika hiyo hiyo Jasusi Shadow alipiga namba nyingine aliyoihifadhi kwa jina la 'Shem J' akapiga
Simu iliita kwa dada mmoja aliyekuwa ndani ya taxi, amini usiamini alikuwa ni Jesca mke wa Tino. Jesca alitoa simu yake ndani ya mkoba wake akapokea.

"Nambie shadow" alisema Jesca mara tu baada ya kupokea simu
"Vipi umeshatoka"
"Kitambo sasa nakaribia Ambross"
"Sawa vizuri, mama alitaka kujua"
"Usijali"
"Poa kuwa makini"
"Poa poa"

Jesca akakata simu huku akitabasamu...
"Hatimaye lile suala ambalo tumelipigania kwa kipindi kirefu mimi na Sultana leo linakwenda kutimia, nimefanya mambo mengi sana kwa ajili ya kupambania virusi vya COBOS, nimekubali kuolewa na mwanaume nisiyempenda lakini pia nimelala na Waziri wa afya Dokta Gondwe yote katika harakati za kuhakikisha tunapata chupa zote mbili za vimelea vya V-COBOS" Aliwaza Jesca huku tabasamu mwanana likizidi kuchanua usoni pake.

Haraka za Sultana kuvitaka vimelea vya V-COBOS hazikuanza leo, ni tangu kipindi cha uhai wa mumewe Jenerali Phillipo Kasebele.
Mumewe alimuamini akamshirikisha siri hii nzito ya vimelea vilivyoletwa nchini vikitokea Mexico wakawa wanapanga mipango kwa pamoja namna watavyozuia janga hili, walipanga kuokoa maisha ya watu kwa kuvitafuta na kuviteketeza vimelea vya V-COBOS akiwa yeye mumewe na jasusi Shadow. Lakini Sultana aliingiwa na tamaa akaona hiyo ni fursa ya kuwa billionea akawa anamzunguuka mumewe kimya kimya. Kuna wakati aliwaza hata kumuua lakini akiwa katika harakati hizo mwisho mumewe akafariki kwa kuuwawa kikatili na mwanae Tino. Hii ilimrahisishia kazi Sultana sasa rasmi vita ikawa kati yake na mtoto wake Tino ambaye naye alikuwa akivitaka vimelea hivyo.
Alichokifanya Sultana ni kumtafuta mwanamke mrembo ambaye alimtumia kama chambo akajilengesha kwa Tino na mwisho Tino akampenda hadi kufikia hatua ya kumuoa. Jesca akawa mke halali wa Tino lakini kumbe alikuwa akifanya kazi na mama mkwe wake yaani madam Sultana. Jesca akawa akawa anafuatilia nyendo zote na Tino na kila alichokigundua alilipoti haraka kwa Sultana.
Wakati Tino anapanga kumbana mama yake ili amueleze ilipo chupa ile ya kijivu yenye dawa na kinga dhidi ya virusi vya V-COBOS ndipo hapo Sultana aliugua ghafula akijifanya mgonjwa akalazwa katikati hospitali ya Mountenia na huko ndiko akawa anaendesha mipango yake kwa siri. Tino akawa anasubiri siku ambayo mama yake ataamka wakati huo huo akawa anaendelea kufanya kazi na Dokta Gondwe ili kuvipata vimelea vya V-COBOS bila kujua kuwa mkewe Jesca alikuwa akimfuatilia kwa ukaribu.

Pamoja na hayo Jesca hakuishia hapo alijirengesha kwa makusudi na kujiweka karibu na Waziri wa afya Dokta Gondwe ambaye naye hakulaza damu akamtongoza na kulala naye, hii yote ikiwa ni harakati za kuvipata vimelea vya V-COBOS, hivyo ndivyo ilivyokuwa.


Nusu saa baadae Tino alifika kwenye ile ofisi yake ya siri ndani ya duka lake la nguo. Aliingia ndani akawakuta vijana wake wakiendelea kupiga kazi na kuingia pesa kama ilivyokuwa ada. Baada ya salamu Tino alienda kwenye meza yake, akawasha kompyuta pamoja na mitambo mingine muhimu.

Baada ya hapo Tino aliicheza ile video ya mke wake Jesca akiwa anafanya mapenzi na bosi wake Dokta Gondwe. Tino aliitazama video hiyo mpaka mwisho baada ya hapo alichukua picha moja kutoka kwenye video hiyo akakata na kuitoa sura ya mkewe Jesca.
Picha ilimuonyesha waziri Dokta Gondwe akiwa faragha na mwanamke ambaye sura yake haikuonekana.

"Sasa ni wakati wako wa kuonja joto la jiwe Dokta Gondwe" alisema Tino na hapo akabonyeza kitufe fulani kwenye kompyuta tayari ile picha ikaingia mtandaoni na kuanza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii WhatsApp, Instagram, Twitter pamoja na Facebook.
Ilikuwa ni habari kubwa iliyoteka macho na masikio ya watu wengi, picha ya utupu ya mheshimiwa Waziri wa afya Dokta Gondwe akiwa faragha na mwanamke asiyejulikana, vijana wa mjini wanaita 'connection'.

Upande wa pili timu ya watu watatu Madam Sultana, Jesca na jasusi Shadow walionekana wakiingia taratibu ndani ya jengo moja la siri lililokuwa na maandishi makubwa juu yaliyosomeka 'Ambross'.
Madam Sultana alikuwa katikati mkono wake wa kushoto alikuwepo mkwe wake Jesca na upande wake wa kuume alikuwepo Jasusi Shadow akiwa ameshika lile sanduku lenye vimelea vya V-COBOS. Walitembea kwa madaha wakiingia ndani ya jengo hilo la Ambross'.

ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya...........27
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

27-(Virusi feki)
ILIPOISHIA...26
Madam Sultana alikuwa katikati mkono wake wa kushoto alikuwepo mkwe wake Jesca na upande wake wa kuume alikuwepo Jasusi Shadow akiwa ameshika lile sanduku lenye vimelea vya V-COBOS. Walitembea kwa madaha wakiingia ndani ya jengo hilo la Ambross'.
Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA...
Ambross ilikuwa ni maabara kubwa ya mtu binafsi mwarabu kutoka Misri bwana Ajmal amir. Haikuwa maarufu sana ingawa ilikuwa ikifanya mambo makubwa na wakati mwingine kutoa msaada hata kwa maabara kuu ya serikali.
Ajmal Amir alikuwa ni mzee kiasi mwenye umri kama miaka 59 hivi. Alivalia koti jeupe, suruali nyeusi na miwani aliwapokea kwa uchangamfu mkubwa Sultana na timu yake, wakaongozana moja kwa moja na hadi ofisini kwake. Ofisi ya Amir ilikuwa imezuungukwa na ukuta wa kioo pande zote hata aliyekuwa nje aliweza kuwaona watu waliomo ndani ya ofisi hiyo. Wote walikaa kwenye viti wakiizunguuka meza moja ya duara.

"Karibu shana Madam Surutana" Amir aliongea kiswahili kibovu kuwakaribisha Sultana Jesca na jasusi Shadow
"Asante Ajmal Amir tumekaribia" aliitikia Sultana
"Bira shakhaa mumepatya virushii?"
"Ndio maana umetuona wote watatu tuko hapa, kijana wangu kafanikiwa kuvileta virus vya COBOS" alijibu Sultana huku kiachia tabasamu
"Okay Good, but kwanini hii mutu siku zyote iko inaficha su..syura yake?" Aliuliza Amir huku akimtazama Jasusi Shadow
"Aah! ni aina ya maisha anayoishi usijali" alijibu Sultana
"Okay, because you trust him, i have to do it so"(sawa, kwa sababu unamwamini natakiwa kufanya hivyo pia) alisema Amir huku safari hii alibadilishana lugha na kuongea kingereza, akanyoosha mkono kuliomba sanduku kutoka kwa Jasusi Shadow.
Jasusi Shadow aligeuka kumtazama Sultana, Sultana akatikisa kichwa ikiwa ni ishara kuwa ampe, shadow akafanya hivyo.
Amir aliliweka lile sanduku juu ya meza kisha kwa uangalifu mkubwa akalifungua.
Wote walitazama ndani kuangalia kilichomo. Naam kulikuwa na chupa ya kijana iliyohifadhiwa kwenye chemba moja maalum ndani ya sanduku hilo. Jesca na Sultana walitazamana kisha wakatabasamu.

"Good work" (kazi nzuri) alisema Amir huku akitabasamu pia
"ok I have to confirm first if it is really the V-COBOS parasite then we will plan how to start spreading this disease and everything"(Sawa natakiwa kuthibitisha kwanza kama kweli ni vimelea wa V-COBOS baada ya hapo ndio tatapanga namna ya kuanza kuusambaza huu ugonjwa na kila kitu) Alisema Amir kisha akasimama akachukua sanduku na kuondoka nalo. Kauli hii ilimfanya Jasusi Shadow ashtuke kiasi akageuka kumtazama Sultana.

Wakati huo Amir alionekana akiingia ndani ya chumba kingine ambacho kiliwa kimezunguushiwa vioo pia, hivyo walikuwa wakiona kila anachokifanya. Safari hii alibadilishana mavazi akavaa vazi lililomfunika kuanzia juu mpaka chini, akafanana na wale watu ambao hutoa huduma kwa watu walioathirika na magonjwa yanayosambaa kwa njia ya hewa.

"Sultana" Jasusi Shadow aliita
"Ongea shadow"
"Nimesikia vibaya au? Mbona Amir anazungumzia habari za kusambaza ugonjwa kwani huu ndio mpango wetu?" Aliuliza Shadow swali lililowafanya Jesca na Sultana watazamana.
Sultana alivuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu kisha akageuka kumtazama Shadow.
"Shadow" Sultana aliita
"Ndiyo mama"
"Kila kitu kilibadilika siku ambayo Jenerali Phillipo alikufa, kwa sasa mpango wetu ni kutumia hawa vimela kutengeneza pesa na sio kuwasambaratisha" alisema Sultana kauli iliyomfanya Shadow atoe macho kwa mshangao
"Madam" Shadow aliita kwa nguvu huku akisimama
"Mmm mmh! Hebu tulia kwanza Shadow" alisema Sultana
"Lakini huu haukuwa mpango wa bosi, lengo lake halikuwa hili, alipanga akipata hawa vimelea awaharibu kabisa wapotee kwenye uso wa dunia sasa inakuwaje wewe unakwenda kinyume mama?" Jasusi Shadow aliongea kwa ukali kidogo, hapo Sultana akasimama huku akiwa ameikunja sura yake.
"Nimekwambia ule mpango ulikufa siku alipokufa huyo bosi wako, kwa sasa utanisikiliza mimi na kunitii mimi kama ulivyokula kiapo mbele ya bosi wako wakati anakata roho" alifoka sultana akatulia kwa muda kisha akaendelea
"Unajua tumepitia mangapi hadi kufika hapa tulipo? Unajua Jesca kajitoa kiasi gani hadi kufanikisha hili, nimelala miezi sita hospitali kuhakikisha nafanikiwa kwenye hili Shadow, kaa kwa kutulia na ufuate maelekezo yangu sawa" Sultana alizidi kufoka, hapo ikambidi Jasusi Shadow awe mpole na kuanza kufikiri kitu sahihi cha kufanya, mambo yalikuwa yamebadilika ghafula sana, hakuwa akijua mpango huu wa Sultana.


Nchi ilikuwa imezizima kwa kashfa kubwa iliyokuwa ikitembea mtandaoni, picha ya Waziri wa afya Dokta Gondwe akiwa faragha na mwanamke ilikuwa ikisambaa kwa kasi na kuvuka mipaka hadi nchi za nje. Kila kona habari hiyo ilikuwa imeshika kasi, serikali nayo haikutaka kukaa kimya tayari sheria ilitakiwa kufuata mkondo wake ambapo Dokta Gondwe alitakiwa kukamatwa mara moja.

Yalikuwa ni majira ya saa mbili usiku Inspekta Aron alikuwa bado kule mstuni kwenye nyumba ya marehemu baba yake. Walikuwa wakipata chakula cha usiku akiwa pamoja na Annah hapo ndipo alipoziona taarifa hizo kupitia simu yake ya mkononi. Inspekta Aron alishtuka sana, ilikuwa ni kashfa na skendo nzito kwa mtu mkubwa serikali kama Dokta Gondwe.

"Najmaa..." Inspekta Aron aliita kwa sauti ya chini akiwaza Najma atakuwa kwenye hali gani baada ya kupata taarifa hizo zinazo muhusu baba yake. Inspekta Aron aliacha kula akashikilia simu kwa mikono miwili akampigia Najma. Simu iliita lakini haikupokelewa, akajaribu tena na tena lakini bado majibu yakawa ni yale yale. Akatuma meseji kadhaa akimtaka Najma apokee simu yake lakini bado jitihada zake hazikuzaa matunda.

Najma alionekana akiwa ndani ya baa moja yenye hadhi ya chini sana iliyopo pembeni ya mji akiwa amelewa chakali. Taarifa zile za baba yake ndio haswa zilimpelekea kufanya hivyo, wala hakuwa na muda na simu yake ambayo kila wakati ilikuwa ikiita ndugu jamaa na marafiki zake wakijaribu kumpigia.


Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa alizipokea taarifa hizi akiwa nyumbani kwake na familia yake wakipata chakula cha usiku. Taarifa hizo zilimfanya Profesa Cosmas Kulolwa alinuke taratibu na kutoka akawa anaelekea chumbani bila hata kuiaga familia yake.
"Baba unaenda wapii!?" Aliuliza mtoto wa mwisho wa Profesa Kulolwa, binti mdogo mwenye miaka minne aliitwa Doris.
Kulolwa hakujibu chochote aliingia chumbani akawasha Tv kutazama, habari kubwa ilikuwa ni hiyo.

"No way my friend" Hii ndio kauli pekee aliyoisema Profesa Kulolwa.

Siku hiyo Tino hakurudi nyumbani aliendelea kukaa ofisini huku akifuatilia namna taarifa za picha ya utupu ya mheshimiwa Dokta Gondwe ilivyotikisa nchi. Alijua wazi taarifa hizi zitamchanganya pia mkewe Jesca, licha ya kwamba sura yake haikuonekana lakini aliamini atakuwa na wasiwasi mwingi.


Bosca akiwa ndani ya kile chumba cha giza alichofungiwa alishtushwa na kelele za sauti ya Dokta Gondwe akiita huku akija kwa kasi, akakaa vizuri kwenye kile kiti walichomfunga.
"Ohoo kumekucha, bosi Tino ashafanya yake" Alisema Bosco akitabasamu. Punde mlango ulifunguliwa kwa nguvu na hapo Dokta Gondwe aliingia na kwenda kumvaa Bosco moja kwa moja, akamkaba shingoni kwa nguvu zote

"Umefanya nini wewe mwanaharamu, umefanya nini nakuuliza?" alisema Dokta Gondwe huku akiendelea kumkaba kwa nguvu Bosco kiasi cha kumfanya aanze kutapatapa baada ya kukosa hewa
Mwisho Dokta Gondwe alimuachia hukua kimsindikiza na kibao kizito usoni, Bosco akatema damu kisha akawa anacheka.
Kitendo hicho kilimkasirisha zaidi Dokta Gondwe akachomoa bastola kutoka kiunoni kwake akaikoki na kuiweka juu ya kichwa cha Bosco.

"Wewe ndio umesababisha tufike huku Dokta Gondwe unatakiwa kujilaumu mwenyewe kwanza kabla ya kuniadhibu mimi, na huo ni mwanzo tuu" alisema Bosco kisha akaendelea kucheka. Kauli hii ilimnyong'onyesha Dokta Gondwe maneno aliyoyasema Bosco yalikuwa na ukweli ndani yake. Baada ya kuliona hilo Bosco aliinua macho na kumtazama Dokta Gondwe usoni, akaongea
"Ile ni picha tu mheshimiwa acha kuchanganyikiwa sijatuma video yote, najua unaweza kujitetea na kufuta hiyo kashfa, uwezo huo unao ila kwanza fanya ninalotaka bila hivyo nitaachia video yote na utakuwa huna namna tena daktari" Bosco aliongea kwa kujiamini.

Hapo kidogo akili ya Dokta Gondwe aliyeonekana kuchanganyikiwa ilianza kufunguka, akawa anajirambaramba mdomo huku akiyatafakari maneno ya Bosco.

"Unataka nini sema?" Aliuliza Dokta Gondwe

Upande wa pili Sultana Jesca na Jasusi Shadow waliokuwa bado ndani ya lile jengo la Ambross waligeuka kumtazama bwana Ajmal Amir ambaye alikuwa anarejea akiwa na lile sanduku mara baada ya kumalizia kufanya vipimo vyake, sura yake ikionekana kuwa na huzuni kiasi.


"Unataka nini sema?" Dokta Gondwe alirudia swali lake
"Kwanza hutakiwi kunigusa hata kidogo nitoke hapa nikiwa salama, pili nataka vimelea vya V-COBOS. Ni hivyo tu kama utatimiza hayo basi ninao uwezo wa kukufutia kashfa hii" aliongea Bosco

"Nitafanya hivyo usijali, nitafanya niamini" Dokta Gondwe alijibu kwa upole
"Utawezaje wakati lile sanduku la vimelea kuna mtu aliondoka nalo kule baharini? au ni mtu wako?" aliuliza Bosco huku akimtazama dokta Gondwe usoni.

Ajmal Amir aliingia ofisini kisha akalitupa lile sanduku la vimelea mezani uso wake ukiwa bado umekunjamana. Sultana, Jesca na Jasusi Shadow walishangazwa na kitendo hicho, wote kwa pamoja wakamtazama Amir kwa macho ya kuuliza.


"Hapana sio mtu wangu" Dokta Gondwe alijibu swali la Bosco
"Sas ni nini?" Bosco aliuliza
"Lile sanduku ni fake halina vimelea vya V-COBOS" aliongea Dokta Gondwe kauli iliyomfanya Bosco atoe macho kwa mshangao, mwisho akatabasamu.


Sultana, Jesca na Jasusi Shadow walishangazwa na kitendo hicho, wote kwa pamoja wakamtazama Amir kwa macho ya kuuliza
"Hakuna vimelea humu, ni FEKI, it's real fake" alisema Ajmal Amir kauli iliyowafanya wote watoe macho kwa mashangao.

Je, nini kitafuata?
ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya.............28
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

28-(Kutekwa kwa binti wa Waziri)
ILIPOISHIA...
Sultana, Jesca na Jasusi Shadow walishtushwa na kitendo hicho, wote kwa pamoja wakamtazama Amir kwa macho ya kuuliza
"Hakuna vimelea humu, ni FEKI, it's real fake" alisema Ajmal Amir kauli iliyowafanya wote watoe macho kwa mashangao.
Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA...
"Unasema nini Amir?" Aliuliza Sultana akiwa haamini maneno aliyoyasikia
"Sultana! kwenye shanduku hakukuwa vimelea bali ni kemikali za kuua wadyudu" alieleza Amir kiswahili bado kikionekana kumpa shida. Kauli hii iliyozidi kumchanganya Sultana si yeye pekee hata Jesca na jasusi Shadow pia wakionekana kutoamini kinachoendelea wakati huo. Lakini huo ndio ulikuwa ukweli wenyewe sanduku halikuwa na vimela vya V-COBOS na ndio sababu wakati ule Dokta Gondwe mweyewe alikuwa akimfuatilia sana Bosco kuliko mtu aliyeondoka na sanduku.

"No! No! Nooo!" Sultana alilalamika na kupigiza mikono yake juu ya meza kwa nguvu, akageuka na kumtazama Jasusi Shadow.
"Shadow ni nini hiki umeleta ee!? kwa nini lakini? Unajua nikiasi gani nimekuwa nikiingoja hii siku? unajua ni kiasi gani nimejitoa kupata hivi vimelea? miezi sita niko hospitali shadow miezi sita, No siwezi kukubali, siweziii" Sultana aliongea kwa jazba sana kila mmoja akawa kimya akimsikia.

"Sina muda wa kuendelea kusubiri tena Shadow, ni lazima tufanye kitu. Tunatakiwa kuvamia maabara kuu ya serikali tuchukue vimelea vya V-COBOS sisi wenyewe" Sultana alikuja na wazo jipya
"Lakini Madam..." Shadow aliongea, sultana akadakia
"Hakuna cha lakini Shadow utaifanya hii kazi wewe mwenyewe, tukiendelea kusubiri mambo yanaweza kuharibika tukajikuta tunakosa kilakitu. Kama unahitaji msaada wa vijana wa kukusaidia niambie muhimu ndani ya siku tatu uwe umeleta vimelea hapa" aliongea Madam Sultana kwa sauti iliyojaa mamlaka.
Jasusi Shadow akatulia kwa muda mwisho akatikisa kichwa kukubaliana na maelezo ya Sultana.
Mwisho walimaliza mazungumzo na jukumu kubwa likabaki kwa Jasusi Shadow ahakikishe anaingia ndani ya Maabara kuu ya serikali kisha achukue vimelea vya V-COBOS. Kazi hii aliwahi kuifanya miaka mitatu iliyopita akiwa chini ya marehemu Jenerali Phillipo Kasebele lakini alifanikiwa kitoka na chupa ya kijivu yenye kinga na tiba dhidi ya vimelea hao. Ile chupa ya kijani ikiendelea kubaki chini ya uangalizi mkali wa Waziri wa afya na mkemia mkuu wa serikali.

Wakati Sultana na timu yake wanatoka nje ya jengo la Ambross, Jesca aliyekuwa akichezea chezea simu yake alipigwa na butwaa ghafula akasimama, Sultana alimuona.

"Nini kuna shida?" Aliuliza Sultana
"Mama ona"alisema Jesca kwa sauti ya chini iliyojaa kitete, akampatia simu Sultana ambaye aliipokea na kutazama picha iliyokuwa juu ya kioo cha simu hiyo. Naam ilikuwa ni ile picha ya waziri wa afya Dokta Gondwe akiwa faragha na mwanamke ambaye hakuonekana sura yake ila Jesca alijua ni yeye"
"Huyu mwanamke ni wewe, ndio ile siku?" Sultana aliuliza maswali mawili mfurulizo
"Ndiyo mama ni mimi, sijui hata imekuwaje" Jesca aliongea kwa woga
"Mmh! hebu subiri huna haja ya kupaniki mwanangu tulia" alisema Sultana, akamgeukia Shadow ambaye alikuwa haelewi mada inayoendelea wakati huo. Ni kama Jesca alijua nini anataka kufanya haraka akainyakua ile simu yake kutoka mikononi mwa Sultana
"Hapana mama usimuonyeshe" Alisema Jesca
"Unafanya nini wewe! Unafikiri kuna mwingine wa kukusaidia zaidi ya shadow?"
"Mama lakini...!"
"Lakini nini hakuna namna nyingine mwanangu hebu nipatie hiyo simu" sultana alifoka, taratibu Jesca aliirudisha ile simu kwa Sultana naye alimkabidhi Jasusi Shadow.
"Angalia hiyo ni siku ambayo mwenzako alitoa utu wake kwa ajili tu ya kupigania mpango wetu wa kuvipata vimelea, inaonekana hiyo siku alirekodiwa tafuta ujue ni nani yupo nyuma ya tukio hili kisha mzuie haraka" alisema Sultana
"Sawa haina shida Madam" Shadow alijibu kwa unyenyekevu mkubwa akairudisha simu mikoni kwa Sultana.


Upande wa pili Bosco na Dokta Gondwe walionekana wakiwa wamekaa ndani ya chumba kimoja kilichokuwa katika ile kambi ya Dokta Gondwe. Tayari Bosco alikuwa ametolewa nje ya kile chumba cha giza alichofungiwa awali na sasa walikuwa chumba kingine tofauti wanafanya mazungumzo ya mwisho na Dokta Gondwe.

"Nitakuacha uende, lakini nataka kujua ni vipi utaifuta hii skendo uliyonipa" alisema Dokta Gondwe huku akimtazama Bosco kwa macho yanayotia huruma.
"Usijali kila kitu kitakuwa sawa daktari muhimu utimize ahadi yako bila kusahau kunipa vimelea wa V-COBOS"
"Usijali mpaka sasa natafutwa na polisi nahitaji kuwa huru hivyo vyote unavyotaka nitafanya, wewe nihakikishie tu usalama wangu na hiyo picha mliyoweka mtandaoni"
"Naomba simu"
"Simu!! simu yangu?"
"Ndiyo"
Dokta Gondwe alisita lakini baadae akachukua simu yake na kuumpatia Bosco.
Simu ilikuwa imezimwa Bosco akaiwasha kisha akapiga namba fulani anazozifahamu . Sekunde chache baadae simu ilipokelewa upande wa pili kupitia kompyuta na aliyepokea alikuwa ni Tino.

"Mkuu naachiwa huru, nipe maelezo" Bosco aliongea moja kwa moja bila hata salamu, akawa anasikia maelezo anayopewa na Tino ambaye alitumia dakika karibu tano kisha akatoweka hewani. Bosco aliizima simu na kumrudishia Dokta Gondwe.
"Iko hivi daktari tunazo picha nyingi kama hizo, tutafanya editing na kutengeneza picha ya mtu mwingine kwenye mazingira hayo hayo na utaonekana sio wewe ile ya kwanza ni feki, hii itasaidia angalau kuzima skendo yako baada ya hapo utatumia uwezo wako kujieleza mbele ya vyombo vya habari kukanusha na kuwaaminisha watu kuwa yule sio wewe" alieleza Bosco.
Dokta Gondwe alitulia kwa muda akijaribu kuyatafakari maelezo hayo ambayo mwanzo hayakumuingia akilini lakini baadae akaona ni njia sahihi ya kupunguza makali ya skendo hiyo ambayo ilikuwa ni hatari pia kwa kibarua chake.

Baadae walikubaliana ikiwa ni saa nne usiku Bosco akatoka nje ya kambi hiyo yenye ulinzi mkali, nje alikuta kuna gari imeandaliwa na Dokta Gondwe inamsubiri. Kabla ya kuingia kwenye gari hiyo Bosco aligeuka na kumtazama Dokta Gondwe aliyekuwa nyuma yake amemsindikiza.

"Hutakiwi kufanya ujanja ujanja wa aina yoyote ile tena, kumbuka hii ni nafasi yako ya mwisho tunavitaka vimelea ndani ya siku tatu tu" alisema Bosco kisha akaingia kwenye gari. Dokta Gondwe aligeuka na kuwa mpole sana, ile jeuri yake yote ilipotea ghafula, alikuwa aneshikwa mahali pabaya mno.
Dereva aliendesha kwa kasi na baadae akamuacha Bosco katikati ya mji. Baada ya Bosco kuhakikisha hakuna anayemfuatilia alianza safari kuelekea ofisi ya siri ya bosi wake Tino.

Bosco alifika ofisini kwa bosi wake akiwa salama kabisa, alikuta tayari Tino amemuandalia chakula cha kutosha. Bosco alikifakamia na kuanza kula, alikuwa na njaa kali tangu ile asubuhi alipokuwa kwenye boti hakuwa amekula chochote hadi mda huu. Siku hii ilikuwa ngumu sana kwao lakini bado hawakuwa na sababu ya kukata tamaa kwani kulikuwa na kila dalili ya wao kushinda vita hii.

"Kwa hiyo Dokta Gondwe amesema yule mtu aliyeondoka na lile sanduku hakuwa mtu wake?"
Tino aliuliza mara tu baada ya Bosco kumaliza kula, walikaa na kuanza mazungumzo.
"Yes! anasema hata yeye hamfahamu" alijibu Bosco
Tino alitulia kimya akawa anakuna ndevu zake akijaribu kutafakari kwa kina yule mtu atakuwa ni nani hasa.
"Ukweli ni ngumu sana kuelewa Bosco, yule mtu angekuwa mbaya angeniacha nifie kwenye maji alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo lakini badala yake alinisaidia"
"Bosi ni wazi kuwa kwenye vita hii hatuko peke yetu, huenda kuna watu wengine wanavitaka hivi virusi vya V-COBOS kama sisi" alieleza Bosco kauli ambayo ilikuwa na ukweli ndani yake. Vita ya kuvitaka virusi vya V-COBOS kutoka Mexico ilikuwa ni kali sana na ndiyo kwanza ilikuwa inaanza.


Ukiwa ni usiku wa saa sita Inspekta Aron hakuwa amepata hata repe la usingizi, kuna mambo kadhaa yalikuwa yakimnyima usingizi kwanza ni Najma kutokupokea simu yake tangu usiku wa saa mbili na pili ilikuwa ni yule mtu hatari ambaye ameifanya nyumba hiyo makazi yake. Alihofu anaweza kurudi mda wowote akawakuta wamelala akawadhuru, licha ya moyo wake kumwambia kuwa mtu huyo sio mbaya lakini bado alihitaji kurithibitisha hilo.

"Kwa hiyo haulali leo Aron, nini shida" Annah aliuliza akionekana kukwera na inspekta Aron ambaye mda wote alikuwa amesimama wima akizunguuka zunguuka mle chumbani.
"Nitalala Annah usijali"
"Lakini hauko sawa Aron au kuna tatizo lingine tena limetokea?"
"Hakuna Annah mmm! We pumzika tu" alisema Inspekta Aron kwa sauti ya kubembeleza na safari hii alisogea akakaa pengine ya Annah pale kitandani, akawa anamshika shika nywele zake taratibu akimtaka alale. Aron hakutaka kumuweka wazi Annah mambo yaliyokuwa yakiendelea wakati huo, hakutaka kumpa wasiwasi zaidi.
Annah alihisi mwili unakufa gazi ghafula, wakati Aron akimshika shika kichwani alijikuta anapata msisimko wa ajabu ambao hakuwahi kuupata kabla na hapo mapigo yake ya moyo yakabadikika. Inspekta Aron aliliona hilo, haraka akaacha kufanya kile alichokuwa akikifanya.

"Uko sawa" Inspekta Aron aliuliza huku akimtazama Annah usoni
"Mmm! niko sawa"alijibu Annah akiwa na aibu kiasi, akageuka kumtazama Aron, sasa wakawa wanatazamana kwa macho yanayozungumza.
Walidumu katika hali hiyo kwa zaidi ya dakika moja, mtetemo wa simu ya Inspekta Aron ndio uliowashtua. Inspekta Aron alikurupuka na kusimama haraka mara tu baada ya kuona jina la mpigaji, alikuwa ni Najma mtoto wa Dokta Gondwe.

"Hallo! Najma uko wapi? uko salama,? kwa nini ulikuwa hupokei simu yangu?" Inspekta Aron aliuliza maswali matatu mfurulizo mara tu baada ya kupokea simu ile akionekana kuwa na shauku kubwa. Kukawa kimya Najma hakuongea kitu upande wa pili wa simu.

"Hallo..Najma!" Aron aliita kwa sauti ya chini, taratibu akaanza kuingiwa na wasiwasi. Mara sauti nzito ya kiume ikasikika upande wa pili
"Tumemteka huyu mwanamke, ili kumpata tunataka utuletee kiasi cha shilingi milioni kumi usiku huu kabla hakujapambazuka. Ukileta ujanja wowote au kutoa taarifa polisi basi atakufa kifo kibaya saana"

Je, nini kitafuata?
Najma yupo salama?
Vipi kuhusu skendo ya waziri Dokta Gondwe?
Nini matokeo ya hisia za Annah kwa Inspekta Aron?
Nini hatima ya vita hii dhidi ya vimelea vya V-COBOS?

ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(vita ya kisasa)
Sehemu ya.............29
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

29- (Usiku wa wokozi)
ILIPOISHIA...
"Tumemteka huyu mwanamke, ili kumpata tunataka utuletee kiasi cha shilingi milioni kumi usiku huu kabla hakujapambazuka. Ukileta ujanja wowote au kutoa taarifa polisi basi atakufa kifo kibaya saana"

SASA ENDELEA...

(DAKIKA 30 KABLA YA NAJMA KUTEKWA)...
Siku hiyo Najma alilewa sana, mara tu alipoiona ile picha chafu ya baba yake mtandaoni aliumia sana akashindwa kuvumilia. Alitafuta baa moja iliyokuwa pembeni kabisa ya mji, akiwa huku alikunywa na kulewa sana.
Saa sita kasoro muhudumu wa baa hiyo alimfuata na kumtaka Najma aondoke kwani ulikuwa ni wakati wa wao kufunga baa. Najma alilipa bili akainuka huku akipepesuka akawa anaelekea lilipo gari lake. Akiwa amebakiza hatua kadhaa kulifikia kumbe alikuwa akiviziwa na vijana wanne ambao ni vibaka maarufu wa mtaani huo. Tangu saa tatu Najma alipoingia baa vibaka hao walianza kumfuatilia wakiamini wasingekosa chochote kitu kutoka kwa mwanamke huyo wa kishua.
Wakati Najma anafungua mlango wa gari yake ndipo hapo walipojitokeza, wakamkaba na kumziba mdomo wakabeba juu juu na kutokomea naye vichohoroni. Ilikuwa ni usiku sana hakuna mtu aliyeshuhudia tukio hilo mbaya zaidi eneo hilo lilifanana na yale maeneo ya uswahilini hakukuwa na ulinzi wowote mida na nyakati kama hizo vibaka walikuwa kazini.

Waliingia na kumshuka Najma ndani ya pagara moja ambapo ndipo ilipokuwa maskani yao. Wakati huo pombe yote ilikata kichwani kwa Najma, akawa anapiga kelele kuomba masaada bila mafanikio yoyote.

"Hivi nyie mnanijua mimi ni nani eeh! mna......aaaah!" Najma aliongea kwa kufoka huku akisimama, lakini kabla hajamalizia sentensi yake kibao kikali kilitua kwenye paji la uso wake kikamrudisha tena chini. Najma alipata maumivu makali ambayo hakuwahi kuyapata kabla, ilikuwa ni nadra sana kwa mtoto wa kishua kama yeye kupigwa kwa kiwango kile.

"Kimyaa..!!" Alisema yule mwanaume mwenye mikono migumu aliyempiga Najma kibao. Wakati huo wale vibaka wengine waliendelea kupekua pekua mkoba na mifuko ya nguo alizovaa Najma.
Najma alipiga kelele tena kuomba msaada lakini hakuna aliyesikia wala kujali.
Ilifika mahali wale vibaka wakawa wanaingiza mikono hadi kwenye sidiria yake wakitafuta hela. Hali ikiuwa ni mbaya mno kwa Najma hakujua hatima yake itakuwa nini dhidi ya vibaka hao dakika mbili baadae nguo zake zilikuwa zimechanwa chanwa hovyo.
"Mmepata nini?" Kibaka mmoja aliwauliza wenzake ambao walianza kuleta vile vitu walivyopata kutoka kwa Najma. Kulikuwa na pesa kiasi cha shilingi laki tatu simu ya Najma aina ya iPhone 13 Pro Max pamoja na simu ndogo, Nokia. Walivikusanya na kumpa mwanaume huyo ambaye alionekana kuwa ni kiongozi wa wengine.

"Sasa mzee si tunamaliza kabisa then tusepe au" alisema mmoja wa wale vibaka huku akifungua mkanda na kuvua suruali yake akaanza kumfuata Najma pale chini, Najma akawa anarudi nyuma kwa woga, mara akatokea kibaka mwingine akamsukuma mwenzake pembeni kisha akawahi yeye na kumlalia Najma kwa juu huku akivua suruali yake haraka haraka, hapo ukaibuka ugomvi mkali kati ya vijana hao watatu kila mmoja akitaka kuwa wa kwanza kumuingilia Najma mwanamke aliyekuwa na kila sifa ya kuitwa pisi kali.
Najma alichoka kupiga kelele na sasa akawa anatetemeka kwa hofu. Alitegemea muujiza wa mungu pekee ndio utakaomuokoa kubakwa na wanaume hao walionyesha matamanio makubwa ya kufaidi penzi lake.

"Acheniii" Mara yule mwanaume kiongozi wao lipaza sauti kuwazuia. Wote waligeuka na kumtazama kwa mshangao, haikuwa kawaida yake kabisa.
"Mshikaji wetu vipi mbona unataka kuzingua tena, tunaachaje pisi kali kama hii au unataka kuanza wewe njoo basi mwanangu umalize sisi tuendelee" alilalamika mmoja wa wale vibaka
"Nimesema acheni hamuelewi"
"Kwa nini sasa jomba?"
"Tunaweza kupiga pesa ndefu hapa nyie hamuoni, huyu demu mpunga upo hebu subirini"
Alisema yule mwanaume kisha akachukua simu ya Najma akawa anaikagua. Kulikuwa na simu nyingine sana zilizopigwa bila kupokelewa, akatazama namba iliyopiga mara nyingine sana ilikuwa ni namba ya Inspekta Aron. Yule bwana akaona hiyo ndio namba sahihi ya kupiga na kumtisha ili aweze kuleta pesa. Jambo lingine lililomfanya ayaamini maamuzi yake ni kutoka na namna namba ya Inspekta Aron ilivyohifadhiwa kwenye simu ya Najma aliandikwa
'In. Aron '
arama hii ya kopa ndiyo hasa iliyomfanya achague kupiga namba hiyo.

Simu iliita upande wa pili kwa Inspekta Aron ambaye haraka aliipokea na kuanza kuuliza maswali na kulalamika kwa nini Najma hajapokea simu yake. Yule bwana alitulia kwa muda kisha akaongea.

"Tumemteka huyu mwanamke, ili kumpata tunataka utuletee kiasi cha shilingi milioni kumi usiku huu kabla hakujapambazuka. Ukileta ujanja wowote au kutoa taarifa polisi basi atakufa kifo kibaya saana"
Kauli hiyo ilimfanya Inspekta Aron akose nguvu ghafula almanusura aidondoshe simu yake lakini akajikaza.
"Tafadhali usimdhuru wala kumfanyia chochote millioni kumi sio tatizo kwangu nitazileta hapo haraka, niambie uko wapi"
"Unauhakika?"
"Niamini mimi braza tumalize hili tafadhali usimguse huyo mwanamke nakuja sasa hivi, nielekeze tu uko wapi"
"Sawa hiyo hela ipo?"
"Ipo nitakuja nayo usijali"
" Njoo Makutano mtaa wa karongo juu ukifika hapo piga simu"
"Sawa sawa, nakuja sasa hivi mkuu"
Inspekta Aron alikata simu, akageuka kumtazama Annah ambaye naye alikuwa ameinuka pale kitandani akifuatilia maongezi yake, alihisi kunatatizo.

"Ni nani katekwa Aron?" Aliuliza Annah
"Najma "
"Najma? Ndio nani?"
"Aah! ni mtoto wa...eeh ni rafiki yangu tu" alijibu Aron huku akisita kumueleza kuwa Najma ni mtoto wa Dokta Gondwe mtu aliyehusika kuwaua wazazi wa Annah siku chache zilizopita.
"Kwa hiyo ndio unaenda saa hizi Aron? si utoe kwanza taarifa polisi"
"Hapana usijali mimi mwenyewe ni polisi"
"Hapana Aron huwezi kwenda peke yako, vipi kama watukudhuru? Mimi nitabaki na nani Aron?" Aliuliza Annah huku akitoka pale kitandani akakimbia na kwenda kumkumbatia Aron kwa nguvu
"usiniache Aron" Annah alisisitiza huku akizidi kujishikilia kwenye mwili wa Aron
Aron alijikuta yupo njia panda asijue afanye nini, wanawake wawili yaani Najma na Annah wote walikuwa wakimuhitaji kwa wakati huo. Hapo ndipo alipomkumbuka yule bwana anaekuja kwenye nyumba hiyo na kutoka yaani Jasusi Shadow akaona kabisa sio salama kama ataamua kumuacha Annah peke yake ndani ya nyumba hiyo.

"Basi tunaenda wote, usijali nitakulinda sawa" alisema Aron akiwa amemshika Annah mabegani kwa mikono yote miwili
"Kweli?"
"Kweli, nilikuahidi nitakulinda nyakati zote siwezi kukuacha ukae mbali na mimi" Alisema Inspekta Aron maneno yaliyopenya moja kwa moja na kuusuza moyo wa Annah.
"Hiyo hela wanayoitaka unayo?"
"Hapana ila usijali ninao mpango, muhimu tuwahi kabla hawajamdhuru" alieleza Inspekta Aron.
Baadae walitoka ukiwa ni usiku wa kiza kinene wakatembea hadi pale Inspekta Aron alipolificha gari lake, wakaingia na safari ya kurudi mjini ikaanza.

Inspekta Aron aliendesha gari yake kwa kasi kubwa sana ndani ya nusu saa tu tayari walishaingia mjini, akafuata barabara inayoelekea Makutano mtaa wa karongo kama alivyo elekezwa.
Dakika 15 baadae walifika, Inspekta Aron akasimamisha gari pembeni ya barabara. Baada ya hapo akapiga simu kama alivyoelekezwa lakini kwa sasa simu ya Najma haikupatikana. Inspekta Aron akahisi kuchanganyikiwa akajaribu tena na tena lakini bado simu ilikuwa haipatikani.
"Nini hiki tena!!" Aliwaza Inspekta Aron. Sasa uvumilivu ulimshinda akashuka ndani ya gari na kufunga mlango
"Annah baki humu nakuja sawa" alisema Inspekta Aron huku akichomoa bastola yake na kuiweka sawa.
"Hapana siwezi kubaki mwenyewe Aron" Annah alibishika akafungua mlango na kushuka. Inspekta Aron hakutaka kuendelea kubishana naye hakuwa na muda huo kabisa.
Wakaingia vichohoroni huku Inspekta Aron akiita jina la Najma kila baada ya hatua kadhaa. Wakati huo mwanga wa mwezi ulianza kuonekana angalau wakawa waoana wanakoelekea.


Usiku huo ulikuwa ni mrefu pia kwa upande wa Tino na Bosco ambao bado walikuwa ofisini wakiangalia namna ya kukamilisha makubaliano waliyoyaweka na Waziri wa afya Dokta Gondwe. Kwanza ilikuwa ni kumsafishia jina na baada ya hapo kazi itabaki kwake kuwaletea virusi vya COBOS na kama asipofanya hivyo Bosco alimuhakikishia kuwa angeachia video yake chafu mtandaoni.

Kwa kuwa kile chumba ambacho Dokta Gondwe na Jesca mke wa Tino walikitumia kufanya uchafu wao bado kilikuwa na kamera siri, walitafuta picha za watu wengine waliowahi kufanya mapenzi ndani ya kile kile chumba wakafanya uhariri wa kitaalamu sana wakabadilisha picha ile ya Dokta Gondwe na kuweka sura ya mtu mwingine kisha wakaituma tena mtandaoni.

Kama ilivyokuwa mwanzo usiku huo huo picha hiyo ilianza kusambaa kwa kasi sana kwenye mitandao ya kijamii wengi wakiamini kuwa ile picha ya mwanzo ilikuwa si harisi yaani Dokta Gondwe alisingiziwa tu lakini wengine bado waliendelea kuamini kile walichokiamini mwanzo.
Mkanganyiko huo ulimpa nguvu mpya mheshimiwa Dokta Gondwe ambaye hakuwa amelala, akapata tumaini jipya na sasa akawa anajipanga ni namna gani atakwenda kukanusha kashfa hiyo ili kuleta utulivu nchini.
Jambo la kwanza alilolifanya Dokta Gondwe alipiga simu kwa viongozi wengine wakubwa akiwemo Rais aliyepo madarakani kwa sasa ambaye pia ni mwenyekiti wa chama chake, wakakubali kuwa naye bega kwa bega kuhakikisha wanaizima skendo hiyo ambayo ilikuwa ikichafua chama chao na serikali kwa ujumla.

***********
{TANGAZO:- Epuka matapeli simulizi hii imetungwa na SAUL DAVID simu 0756862047, Tafadhali usinunue kwa mtu mwingine tofauti }
******-*-

Wakati wale vibaka wakisubiri simu kutoka kwa Aron, kuna mmoja wao alikuwa akimtazama sana Najma usoni, alifanya hivyo kwa zaidi ya dakika kumi ni kama vile alikuwa anahakikisha jambo baadae akasogea hadi pale wenzake walipokuwepo. Wakati huo Najma alikuwa amekaa na kuegemea ukuta huku akiwa amenyoosha miguu yake. Hakuwa na ujanja wa kujiokoa wala kufanya chochote mbele ya vibaka hao.

"Oya mazee" alisema yule kijana, wenzake wakageuka kumsikiliza
"Hivi mnajua huyu demu ni nani?"
"Kivipi yani mbona unataka kuleta miyeyusho"
"Hapana mwana kuna kitu nimesanuka"
"Tusanue na sisi basi"
"Ni hivi, huyu demu ni mtoto wa Dokta Gondwe yule Waziri wa afya"alisema yule kijana kauli iliyowashtua sana wenzake, yule mkubwa wao akapiga hatua akasogea hadi alipo Najma akapiga magoti mbele yake kisha akawa akammulika na tochi usoni. Baada ya kufanya hivyo alirudi kwa wenzake

"Oya tusepe"
"Nini?" Wote wakauliza kwa pamoja
"Tusepe wana tusepe, huu msara"
"Ni kweli ama!?"
"Ndio hivyo wanangu kitanuka sasa hivi huyu mtoto wa mkubwa linaweza kuja jeshi zima la nchi hapa, tusepeee!!" alieleza yule bwana, hapo wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha wakatimua mbio kila mmoja akatawanyika kuelekea upande wake

Najma alibaki mwenyewe akiwa haelewi nini kinaendelea, alishangaa tu wale vibaka wamekimbia na kumuacha mwenyewe.
Hakutaka kupoteza muda naye aliinuka na kutimua mbio, akawa anaanguka na kusimama mara kadhaa, aliumia lakini hakuja.

Baada ya kukimbia kwa zaidi ya dakika mbili Najma alisikia kwa mbali sauti ya kiume ikimuita.
"Aron" Najma alijisemea mwenyewe baada ya kuibani sauti ya mwanaume huyu. Haraka alianza kukimbia akikatisha vichohoroni kufuata uelekeo wa sauti hiyo huku naye akiita jina la Aron kwa nguvu.

Aron na Annah wote waliisikia sauti ya Najma akiita, Aron akaongeza kasi kufuata uelekeo wa sauti ile. Haukupita muda kwa mbali alimuona Najma anakuja huku akikimbia,Najma naye akamuona Inspekta Aron.
Alikimbia na kwenda kumkumbatia kwa nguvu sana, Hapo machozi yakaanza kumtoka tena akawa analia huku kichwa chake akiwa amekilaza kwenye kifua cha Inspekta Aron aliyemkumbatia kwa nguvu sana.

"It's okay Najma usilie uko salama sasa" Alisema Aron huku akimpiga piga Najma mgongoni.
Wakati huo Annah alikuwa amesimama hatua kadhaa pembeni yao akawa anawatazama huku wivu ukianza kumshika taratibu hisia zake zikimwambia kuna uwezekano wawili hawa wakawa wanapenda.

Je nini kitafuata?
Picha hii ya pili itaweza kuzima skendo ya waziri wa afya?
Dokta Gondwe atatimiza ahadi yake kuleta virusi vya COBOS?
Vipi hukusu Jesca,sultana na jasusi Shadow?
Nini kitatokea Annah akigundua kuwa Najma ni mtoto wa Dokta Gondwe muuaji wa wazazi wake?

ITAENDELEA.....
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya................30
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
30- (Masaa 72 ya mwisho)
ILIPOISHIA.....
"It's okay Najma usilie uko salama sasa" Alisema Aron huku akimpiga piga Najma mgongoni.
Wakati huo Annah alikuwa amesimama hatua kadhaa pembeni yao akawa anawatazama huku wivu ukianza kumshika taratibu, hisia zake zikimwambia kuna uwezekano wawili hawa wakawa wanapendana.

SASA ENDELEA...

Nusu saa baadae Inspekta Aron, Najma na Annah walikuwa ndani ya gari wakiondoka eneo la Makutano. Aron akiwa ndio dereva alimuuliza Najma kama anaweza kumrudisha nyumbani kwao usiku huo lakini Najma alikataa. Hakuwa tayari kurudi nyumbani kuonana na baba yake ambaye alikuwa ametia aibu nzito mtandaoni.
Inspekta Aron akajikuta majukumu yake yanakuwa makubwa, mwanzo alikuwa na Annah lakini sasa Najma ameongezeka hakujua atawapeleka wapi usiku huo.
Alitamani kwenda nao hotelini lakini akahofia usalama wa Annah ambaye alikuwa akiwindwa na watu wa Dokta Gondwe. Aliwaza waende nyumbani lakini akakumbuka kuhusu kaka yake Tino kuwa ni mmoja kati ya wa watu wanaoamini Annah amekufa.
Kurudi kule msituni kwenye nyumba ya siri ya marehemu baba yake ilikuwa ni habari nyingine, hakujua yule bwana mficha sura atakuwa amerudi au laa!.

Mwisho Inspekta Aron alipata wazo la kwenda nyumbani kwa Inspekta Jada askari mwenzake ambaye walikuwa wakifanya kazi kwa ukaribu sana. Alimpigia simu akamuelekeza hali ilivyo na bila hiyana jada aliwakaribisha nyumbani kwake.


Dakika kumi baadae tayari walishafika nyumbani kwa Inspekta Jada wakaingia ndani. Kwa kuwa alishaelezwa kila kitu Jada alimuhudia Najma ipasavyo, akampa maji ya kuoga nguo za kubadilisha na kumpa huduma ya kwanza kwenye michubuko aliyopata wakati alipokuwa akikimbia. Baada ya kuhakikisha ametoa huduma zote muhimu Jada alimfuata Inspekta Aron aliyekuwa amesimama nje akipunga upepo.

"Pole Aron"alisema Jada huku akisogea na kusimama pembeni Aron
"Asante Jada mambo yamekuwa ni mengi sana hivi karibuni"
"Ni kweli ndio kazi zetu inabidi kuvumilia tu"
"Sawa, vipi Najma yuko salama hakuna kibaya walichomfanya"
"Hapana nimemuliza kasema walijaribu kutaka kumbaka lakini mungu mkubwa walimuacha"
"Afadhali"
"Lakini kwani alienda kule kufanya nini?"
"Sijui nahisi ni kwa sababu ya skendo ya baba yake ilimchanganya"
"Mmh! hii ambayo haieleweki, naona kunapicha nyingine tena kama ile inasambaa mtandao, itakuwa walimu-edit pengine"
"Kuna nyingine tena?"
"Ndiyo nimeingia mtandaoni wakati nawasubiri nikaiona"
"Afadhali hakikisha basi unamuonyesha Najma angalau itasaidia kumuweka sawa"
"Okay, vipi kuhusu Annah?"
"Kama nilivyokwambia mpaka sasa wanaamini Annah amekufa, kesi ya Osward inasikilizwa kesho tutawasapraizi tu ghafula mahakamani watamuona Annah yuko hai. Hata hivyo kwa sasa Dokta Gondwe yupo kwenye matatizo nguvu kubwa ataelekeza huko kwenye skendo yake"
"Basi ingia ndani uoge upumzike"
"Annah ameshaoga?"
"Niliacha anaingia bafuni, alafu vipi anaendelea na jeraha lake?"
"Ooh! My God nimesahau kubeba dawa na vifaa vyake" Alisema Inspekta Aron huku akijishika kichwani, ni kweli alikuwa ameviacha vifaa na dawa za Annah kule kwenye nyumba ya siri msituni.
Mwisho walikubaliana kuwa atavifuata asubuhi. Inspekta Jada aliaga kuwa anakwenda kupumzika.
Wote walilala chumba kimoja yaani Annah na Inspekta Jada wakalala kitanda kimoja na kitanda kingine pembeni yao alilala Najma. Inspekta Aron yeye hakutaka kuyafumba macho yake hata kidogo, ulikuwa ni usiku mrefu mno kwake aliingia kwenye chumba kimoja ndani ya nyumba hiyo ya Inspekta Jada, humo kulikuwa na ubao mkubwa ukutani, Inspekta Aron akaanza kuumiza kichwa chake akijaribu kuunganisha matukio huku akiandika majina ya wahusika kwenye ubao huo kama wafanyavyo polisi wapelelezi. Akawa anajaribu kuunganisha doti.
Aliwaza kuhusu kaka yake Tino,akawaza kuhusu mama yake Sultana anaeamini ni mgonjwa mahututi. Aron aliwaza pia kuhusu yule mtu aliyekutana naye hospitalini na kisha akamuona tena kule msituni ndani ya nyumba ya siri ya baba yake, aliwaza kuhusu Dokta Gondwe, Osward, Najma na Annah.
Mpaka inafika saa 12 asubuhi bado Inspekta Aron hakuwa amepata jibu kamili. Suala ambalo hadi dakika hiyo hakulijua ni kuhusu vita kali ya vimelea vya V-COBOS iliyokuwa ikiendelea chini chini. Asilimia kubwa ya watu waliokuwa wakimuumiza kichwa walikuwa ndani ya vita hiyo kali, Inspekta Aron bado alikuwa hajui chochote.
Mwisho alitoka kwa hasira akaingia kwenye gari yake safari ya kuelekea msituni kule kwenye nyumba ya siri ikaanza.


Ikiwa ni majira ya saa 1 asubuhi Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa aliamshwa na mlio wa simu yake iliyokuwa ikiita sana, alipoitazama ilikuweka ni simu kutoka Mexico.
Profesa Kulolwa aligeuka kumtazama mke wake bado alikuwa amelala akapokea simu ile.

"Yes Mr. director"(ndiyo mkurugenzi) alisema Profesa Kulolwa
"Please contact us online, right now"(tuwasiliane mtandaoni tafadhali, sasa hivi) sauti ilisikika upande wa pili wa simu
"Okay sir" (sawa mheshimiwa)
Profesa Kulolwa alijibu kwa unyenyekevu mkubwa. Alivaa koti haraka akatoka chumbani na kuingia ndani ya chumba kingine ambacho kilikuwa ni ofisi ndani ya nyumba yake.
Alikaa na kufungua kompyuta yake ndogo kisha moja kwa moja akaingia kwenye mtandao wa Skype.
Moyo wake ulifyatuka paa!! Mara baada ya kuona kilichokuwa kikiendelea mtandaoni wakati huo. Timu ya wazungu sita kutoka maabara ya ZMLST nchini Mexico ilikuwa imekaa ndani ya ofisi moja wakiwa online tayari kuanza kikao, Profesa Kulolwa akawa ni mmoja kati ya washiriki wa kikao hicho kinachofanyika kwa njia ya mtandao.
"Welcome Professor Kulolwa" (karibu Profesa Kulolwa) alisema Profesa Fernando mzungu mwenye asili ya kituruki ambaye ndiye mkurugenzi mtendaji wa maabara maarufu dunia kote ya ZMLST.
"Thank you for your welcome sir, I am glad to see you all once again I hope you are fine"(Nashukuru kwa ukaribisho wako mheshimiwa, nafurahi kuwaona nyote kwa mara nyingine tena natumaini hamjambo) Alisema profesa Kulolwa akionyesha unyenyekevu wa hali ya juu, kama ungemuona usinge amini kama huyu amewahi kuwa Rais wa nchi tena mwenye mamlaka makubwa kuliko mtu yeyote.

"without wasting time please let us go straight to the point. It has been a three years now since we lost the gray bottle with COBOS virus treatment and vaccine. you promised us you would track down and restore the bottle within a short time but so far you have been silent. yesterday we heard a great scandal about your colleague Dr. Gondwe, can you tell us what is real going on so far (bila kupoteza muda naomba twende moja kwa moja kwenye point. ni miaka mitatu sasa tangu tumepoteza chupa ya kijivu yenye tiba na kinga ya virusi vya COBOS, mlituahidi mtafuatilia na kuirejesha chupa hiyo ndani ya mda mfupi lakini mpaka sasa mpo kimya. Jana tumesikia skendo kubwa kumuhusu mwenzako Dokta Gondwe, unaweza kutuambia ni nini kinaendelea mpaka sasa)
Lilikuwa ni swali ambalo profesa Kulolwa alitegemea kuulizwa. Alichukua leso nakufuta kijasho chembamba kilichokuwa kimeanza kumtoka akakohoa kidogo na kuanza kueleza uhalisia wa mambo jinsi yalivyo.
Profesa Kulolwa hakuficha kitu, kwanza aliomba radhi wao kushindwa kuipata chupa ya kijivu iliyoibiwa tangu mda mrefu lakini pia akaeleza kwa kina chanzo cha skendo ya Dokta Gondwe. Alieleza kila kitu jinsi Dokta Gondwe alivyotembea na mke wa kijana wake wa kazi baadae akarekodiwa kwa siri kisha mtu aliyemrekodi akavitaka vimelea vya V-COBOS na asipofanya hivyo basi atazituma video na picha hizo chafu mtandaoni. Dokta Gondwe akapanga mpango wa kumkamata na kumdhibiti muhusika lakini mwisho akajikuta picha yake chafu ipo mtandaoni.
Watu hao kwenye kikao walimsikiliza profesa Kulolwa kwa makini na baada ya maelezo hayo wakamtaka atoke mtandaoni kwa muda ili wao wajadili nini cha kufanya.
Profesa Kulolwa alifanya kama alivyoagizwa akawa anasubiri kwa hamu kubwa kutaka kujua ni maamuzi gani ambayo ZMLST watayachukua. Aliwajua vizuri watu hao hawakuwa na masihara hata kidogo.
Wakati akisubiri punde barua pepe iliingia kwenye kompyuta yake alipoitazama akagundua imetoka mexico kwa Profesa Fernando mkurugenzi wa maabara ya ZMLST.
Hali akitetemeka mikono Profesa Kulolwa aliifungua na kuanza kuisoma, iliandikwa hivi...

,,,,,,,Tulikuwa kimya kwa sababu tulitaka upepe wa ugonjwa wa COVID-19 upotee na kuisha kabisa, sasa ni wakati wetu wa kuingia kazini, tunakuja rasmi nchini kwako kuendelea mpango wetu wa kusambaza ugonjwa wa kirusi cha COBOS. Tunajua kila kitu kinachoendelea, tunao wapelelezi wetu wa siri huko, tumesikia kuwa ile chupa ya kijivu iliibiwa na aliyekuwa mkuu wa majeshi marehemu Jenerali Phillipo Kasebele na sasa inaaminika chupa hiyo ipo mikononi mwa mkewe Sultana ambaye ni mgonjwa mahututi. Tunasikitika kuona habari kuhusu vimelea vya V-COBOS zimekuwa zikisambaa siku hadi siku jambo ambalo ni hatari sana katika mapango wetu na hii yote imetokana na uzembe wenu hasa huyo Dokta Isaack Gondwe. Hivyo basi makubaliano tuliyofikia ni kwamba kwanzia leo wewe ndio utakuwa kiongozi wa wenzio huko pia kwa usalama wa vimelea vya V-COBOS tunakuagiza UMUUE Dokta Gondwe ndani ya masaa 48 kuanzia sasa. Tutatuma watu waje wakusaidie kuirejesha chupa ya kijivu kabla sisi hatujaja rasmi kusambaza vimelea vya V-COBOS, jukumu la kumuua Dokta Gondwe tunaliacha kwako profesa.
Tunakutakia utekelezaji mwema.,,,,,,,,,,

Profesa Kulolwa Rais mstaafu alimaliza kuisoma barua pepe hiyo kisha akafuta tena jasho.
"Nilijua tu mwisho wako utakuwa kama hivi Dokta Gondwe" alisema Profesa Kulolwa huku akiifunga kompyuta yake


Dakika 45 baadae Inspekta Aron alifika kwenye nyumba ile ya siri msituni, akafungua mlango na kuingia ndani kwa tahadhali.
Macho yake yalitua sebureni ambapo alimuona mtu akiwa amempa mgongo huku akiwa amekaa kwenye kiti na kujiinamia.
Inspekta Aron alitoa bastola yake haraka na kumnyoshea, lakini cha ajabu mtu huyo hakuogopa wala kufanya chochote, aliendelea kubaki katikati hali ile ile, alikuwa ni jasusi Shadow wakati huo akionekana kuwa mwenye mawazo sana.

Hali akiwa hajavaa maski Jasusi Shadow alisimama na kugeuka taratibu. Sasa akawa anatazamana uso kwa uso na inspekta Aron ambaye aliishikilia bastola yake vizuri akawa makini zaidi akikumbuka kile kilichotokea hospitali ya Mountenia.

"Hata baba yako tu hakuwahi kuiona sura yangu lakini wewe jana umeiona" aliongea Jasusi Shadow huku akitabasamu kidogo
"Wewe ni nani?" Inspekta Aron aliuliza na kuongeza umakini, alimuelewa vizuri Jasusi Shadow kuwa ni hatari kuliko kawaida

"Nakuuliza wewe ni nani na kwa nini uko hapa?" Inspekta Aron aliuliza tena kwa msisitizo
"Mimi ni mtu ambaye kwa mara nyingine tena naelekea kushindwa kuitimiza ahadi niliyompa baba yako, nafikiri ni wakati sahihi sasa wa wewe kuvaa viatu vya baba yako na kuingia vitani uiokoe nchi yako na dunia yetu, Inspekta Aron Phillipo Kasebele" Jasusi Shadow aliongea maneno yenye utata yaliyoibua maswali rukuki kichwani kwa Inspekta Aron.

Je, nini kitafuata?
ZMLST nao wamesimama tena na kulivalia njuga suala la virusi vya COBOS, je ninani ataibuka mshindi Sultana? ZMLST? Tino? au Dokta Gondwe?
Vipi kuhusu Aron na Jasusi Shadow?
Ni nini hatima ya wanawake hawa wawili yaani Najma na Annah!!
ITAENDELEA...

TUKUTANE TENA SEASON 3 AMBAYO ITAKUWA HEWANI HIVI PUNDE


Weka COMMENT YAKO SUBSCRIBE MKEKA HUU KUPATA UPDATE ZA MUENDELEZO

Name: Saul David Mwanawima
Email: saulstewarty@gmail.com
Phone: 0756862047
2022
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya...........31
Mtunzi: Saul David
Email: saulstewarty@gmail.com
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...MSIMU ULIOPITA
Maabara ya ZMLST kutoka nchini Mexico wanaamua kulivalia njuga suala la usambazaji wa virusi vipya vya COBOS mara tu baada ya maambukizi ya virusi vya COVID-19 kupungua. Wanamuagiza Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa kumuua waziri wa afya Dokta Isaack Gondwe ambaye wanaamini ndiye chanzo cha uzembe uliojitokeza hadi kupoteza kinga na tiba dhidi ya vimelea hao hatari.
Wakati huo huo Dokta Gondwe bado anahangaika kusafisha jina lake mara tu baada ya picha zake chafu za utupu kusambaa mtandaoni.
Upande wa pili Sultana anamuagiza Jasusi Shadow kuvamia maabara kuu ya serikali na kuviiba vimelea vya V-COBOS wakati huo huo Jasusi Shadow anakutana uso kwa uso na inspekta Aron ndani ya nyumba ya siri msituni.
Ni nini hatima ya vita hii?
Nani ataibuka mshindi na kuvipata virusi vya COBOS?
Vipi kuhusu duara la hisia za kimapenzi kati ya Osward, Annah, Najma na Inspekta Aron?

SASA ENDELEA...
"Hatuyumbishwi na maneno ya watu, hatuyumbishwi na mipango miovu ya watu wenye lengo la kuchafua chama changu na serikali yangu, mimi kama Waziri wa afya nitaendelea kusimama kidete na kuitumikia serikali yangu kwa moyo mmoja, ndugu zangu waandishi wa habari pamoja wa wanachi wote mnaonitazama wakati huu narudia tena kusisitiza kuwa zile picha chafu mlizoziona mtandaoni sio zangu, zimetengenezwa kwa lengo la kunichafua mimi na serikali yangu. Nawaahidi kuwa hatuto kaa kimya kuruhusu mambo kama haya yaendelee, nawahakikishia aliyefanya hivi atakamatwa na kuwajibishwa mara moja, hatuwezi kuendelea kuvumilia na kuyafumbia macho mambo ya hovyo kama haya kwenye nchi yetu, hili suala limeitia aibu nchi yetu, majirani zetu wanatucheka nasisi hatuwezi kuikubali aibu hii, aliyefanya hivi atakamatwa na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ili iwe funzo kwa watu wengi wenye nia ovu kama yake. Namshukuru mheshimiwa Rais kwa kusimama upande wangu na tayari tumeshaunda tume ya wataalamu ambayo itafuatilia kwa kina suala hili ili kumbaini mhusika. Nitaendelea kuongea na ninyi tena na tena hadi pale tutakapofika tamati, niwaombe wananchi wenzangu, ndugu zangu, wapiga kula wetu muendelee kuwa katika hali ya utulivu, tutakuja na majibu yote ya maswali yenu ndani ya muda mfupi kuanzia hivi sasa...."
Hii ilikuwa ni asubuhi ya siku iliyofuata na haya yalikuwa ni maneno ya Waziri wa afya Mheshimiwa dokta Gondwe ambaye mara tu baada ya Tino na Bosco kusambaza picha nyingine mtandaoni zenye maadhari kama yale lakini zikiwa na sura ya mtu tofauti na yeye hapo alipata nguvu mpya akaitisha mkutano wa waandishi wa habari haraka na kuanza kutema cheche kusafisha jina lake.
Haikuwa kazi nyepesi hata kidogo kuzibadili akili za watu lakini kwa kuwa alikuwa ni mwanasiasa mbobevu taratibu alianza kuaminika na maelfu ya watu huku wengine wakilaani vikali kwa mtu aliyehusika kumtengenezea Waziri skendo hiyo chafu.


"Mwanasiasa ni mwanasiasa tu hebu muangalie anavyoongea kwa hisia utadhani sio yeye ni kweli kasingiziwa" Alisema Tino akiwa na Bosco ndani ya ile ofisi yao ya siri wakifuatilia ule mkutano wa waandishi wa habari na Dokta Gondwe kupitia televisheni. Wakati huo Tino na Bosco walikuwa wakipata kifungua kinywa, walikesha na kulala ofisini humo kwa lengo la kuhakikisha wanafuatilia kwa kila hatua mpaka pale zitakapotimia siku tatu ambazo walikubaliana na Dokta Gondwe kuwa ataleta vimelea vya V-COBOS kwao.

"Wanasiasa wote ni matapeli" Alisema Bosco
"Hayo matusi sasa"
"Mimi nakwambia mkuu, hivi ni nani atashindwa kumuone huruma Dokta Gondwe kwa namna anavyozungumza bado kidogo atatoa machozi wewe subiri"
"Atajua yeye, muhimu atimize ahadi yake bila hivyo basi tutarusha video nzima mtandaoni sijui ataongea nini tena"
"Ahahaha! Bosi safari hii hachomoki lazima tu atatuletea vimelea"
"Vipi kama akija na mpango mpya, tusijiamini sana mdogo wangu" Tino aliongea kwa kumaanisha huku akibadirisha chaneli lakini chaneli zote habari ilikuwa ni ile ile mkutano wa Waziri wa afya na waandishi wa habari

Upande wa pili nyumbani kwa Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa naye alikuwa ametulia sebureni akifuatilia kwa ukaribu mkubwa mazungumzo ya waziri wa afya Dokta Gondwe. Miguuni kwa Kulolwa alikuwa amempakata binti yake mdogo Doris mtoto wake wa mwisho.

"Umechelewa sana rafiki yangu Dokta Gondwe, natakiwa kukuua mapema sana kabla haujaharibu mambo zaidi, pole sana" Alisema Profesa Kulolwa huku akizima Tv akapokea simu yskey iliyokuwa ikiita.
"Baba mbona umezimaa" Doris alilalamika
"Hebu subiri, nenda chumbani kwa mama mwambie akuvalishe sweta" Alisema Profesa Kulolwa huku akimshusha chini Doris na kumuacha aende.

"Eeh! Nambie" Profesa Kulolwa alianzisha mazungumzo kwenye simu ile
"Utaratibu wote umekamilika tunakubiri wewe mheshimiwa" sauti ilisikika kutoka upande wa pili wa simu ile
"Sawa nisubiri hapo nakuja" Profesa Kulolwa alijibu kifupi kisha akakata simu, hizi zote zilikuwa ni harakati za kuandaa mazingira kuhakikisha anatekeleza agizo alilopewa na maabara ya ZMLST kumuua waziri wa afya Dokta Gondwe.
Baada ya kukata simu Profesa Kulolwa aliandika ujumbe huu wa maandishi kwenda namba isiyojulikana kisha akautuma.
,,,,,,,,,,Peleka mbele siku ya kusikilizwa kesi ya Osward mahakamani, iwe kesho sio leo,,,,,,,,,,,


****
TANGAZO
Simulizi hii imetungwa na SAUL DAVID 075686204, epuka tapeli usikubali kununua kutoka kwa mtu mwingine tofuauti. Haki zote zimehifadhiwa
*****""
Nyumbani kwa Inspekta Jada siku hiyo aliamka asubuhi na mapema kuwaandalia kifungua kinywa wageni wake yaani Annah pamoja na Najma. Alifanya hivyo kabla ya muda wa kwenda kazini haujafika lakini pia leo ilikuwa ni ile siku waliyoisubiri kwa hamu siku ambayo kesi ya Osward itasikilizwa kwa mara ya mwisho na kutolewa hukumu mahakamani. Tayari walikuwa na shahidi wa pekee na tegemezi kwao, Annah. Hakuna aliyejua kuhusu mipango mingine ya kusogezwa mbele siku ya kusikilizwa kesi hiyo.
Najma alikuwa wa kwanza kuamka kabla ya Annah, akiwa bado kitandani aligeuka na kumtazama Annah ambaye bado alikuwa amelala. Najma bado hakuwa akimtambua mwanamke huyu na wala hakujua ni kwa nini yupo karibu sana na inspekta Aron. Hata usiku wa jana pindi Inspekta Aron alipokuja kumsaidia alipotekwa na vibaka alikuwa pamoja na mwanamke huyo.

Wakati akizidi kumtazama ghafula Annah akafumbua macho, wakatazamana. Najma alikurupuka na kujaribu kuzuga kama vile alikuwa hamuangalii mwenzake.
"Za asubuhi" Annah alisalimia kwa sauti ya upole
"Nzuri umeamkaje" Najma aliitikia salamu
"Safi tu, unaendeleaje?"
"Niko poa, shukrani jana sikupata nafasi ya kukushukuru wewe na Aron"
"Hamna usijali mi si chochote mshukuru sana Aron" alijibu Annah kisha wakatazamana tena kila mtu akimuangalia mwenzake kwa jicho la udadisi.

Maongezi yao yalikoma mara baada ya kusikia sauti ya kile kilichokuwa kikiongelewa kutoka kwenye Tv aliyoiwasha Jada sebureni. Wote walitulia tuli baada ya kusikia jina la Dokta Gondwe likitajwa.
Najma alikuwa kwanza kutoka hadi sebureni akifuatiwa na Annah.
Najma, Annah na Jada wote walikodolea macho kwenye Tv ndipo hapo waliposhuhudia yale maongezi ya waziri wa afya Dokta Gondwe akiongea na waandishi wa habari kuhusu skendo yake ya picha za utupu zilizosambaa mtandaoni.

"Nilijua baba yangu hawezi kufanya hivi" Najma aliongea huku machozi ya furaha yakimlenga lenga.
"Umesema, Baba?" Annah aliuliza huku akigeuka kumtazama Najma ambaye hakuwa amemsikia, macho na akili yake alikuwa ameelekeza kwenye Tv. Baadae alihisi ni kama Annah anamuangalia sana akageuka na kumtazama.

"Nini?" Najma aliuliza huku akimtazama Annah kwa macho ya kuuliza
"Umesema Dokta Gondwe ni baba yako?" Aliuliza Annah akitaka kujihakikishia kile alichosikia mwanzo. Najma alitikisa kichwa kukubali akiwa bado anamtazama Annah kwa macho ya kuuliza.

"Wauajii! Wauajii! Wauajiiiiiii"Annah aliongea taratibu na mwisho akapaza sauti huku kifua chake kikiaanza kujaa hasira. Hakuwa akijua kumbe Najma ni mtoto wa Dokta Gondwe mtu aliyehusika na mauaji ya wazazi wake wote wawili.
Taratibu Annah akaanza kupiga hatua kumsogelea Najma ambaye alibaki amesimama wima akimtazama asielewe kinachoendelea.

"Annah please acha" Jada aliongea akijaribu kumzuia Annah, lakini haikusaidia.
"Anaongea nini huyu mwanamke? Nani muuaji?"
"Ninyi ninyi ndio wauajiiii!! Mmewaua wazazi wangu unauliza hujui wewe hujui kama baba yako ni muuaji?" Annah alifoka huku akitaka kumrukia Najma lakini kwa bahati nzuri Inspekta Jada akawahi kumzuia.

"Niache, niache nimesema"
"Muache aje, muache aje nimuonyeshe, anawezaje kumzungumzia baba yangu vibaya kiasi hiki" Najma naye alicharuka na kuanza kufoka kwa hasira
Vurugu ya aina yake ikaibuka nyumbani kwa Inspekta Jada


Upande wa pili kule msituni bado hali ilikuwa ni tete kati ya Inspekta Aron na Jasusi Shadow
"Nakuuliza wewe ni nani na kwa nini uko hapa?" Inspekta Aron aliuliza tena kwa msisitizo
"Mimi ni mtu ambaye kwa mara nyingine tena naelekea kushindwa kuitimiza ahadi niliyompa baba yako, nafikiri ni wakati sahihi sasa wa wewe kuvaa viatu vya baba yako na kuingia vitani uiokoe nchi yako na dunia yetu, Inspekta Aron Phillipo Kasebele" Jasusi Shadow aliongea maneno yenye utata yaliyoibua maswali rukuki kichwani kwa Inspekta Aron.
"Unajaribu kucheza na akili yangu si ndio? Wewe baba yangu unamjuaje?"
"Mbona ni rahisi tu Aron, umeuliza kwanini niko hapa, jibu ni dogo niko hapa kwa sababu ni sehemu ambayo nilikuwepo siku zote enzi za uhai wa baba yako na hata sasa. Shusha siraha yako chini tuzungumze Aron"

"Hebu tulia kwanza, huwezi kunilaghai kirahisi kwa maneno yako. Unafikiri sikukumbuki? Sikia wewe ndio yule tulikutana hospitali ya Mountenia ukanikimbia, leo tena nimekukuta hapa, unaweza kuniambia pale hospitali ulifuata nini? Na huku nako umefuata nini?" Inspekta Aron alizidi kuuliza maswali mfurulizo huku safari hii akiwa makini sana kwani anakumbuka mara ya kwanza mtu huyo alimzidi nguvu kwa kutumia siraha ya ajabu kutoka mdomoni mwake.
"Tunamengi sana ya kuongea Inspekta Aron, nipo kwenye misheni kubwa niliyoachiwa na baba yako. Nataka tuunganishe nguvu mimi na wewe ili tuiokoe Dunia jaribu kunielewa basi shusha siraha yako chini tuzungumze" Jasusi Shadow alijieleza. Wakati huo simu ya Inspekta Aron ilikuwa ikiita mfurulizo kwa mara ya tatu sasa.
Hali akiwa makini kupita kiasi aliingiza mkono wake wa kushoto mfukoni huku ule wa kulia akiwa bado amemnyoshea Jasusi Shadow bastola.
Akachukua simu yake akapiga jicho pembeni kutazama jina la mpigaji, alikuwa ni Inspekta Jada, Aron akapokea.

"Aron" sauti ya Jada ilisikika upande wa pili
"Vipi Jada unaweza kusubiri kidogo"
"Hapana Aron uko wapi rudi nyumbani haraka hawa mabinti wanapigana"
"Nini? Kwa nini yani?"
"Annah kajua kuwa dokta Gondwe ni baba yake Najma, tafadhali hebu rudi haraka Aron wataumizana nashindwa kuwazuia" Jada aliongea kwa msisitizo kisha akakata simu.
Inspekta Aron alibaki ameduwaa huku maswali yasiyo na majibu yakipita kwa kasi kichwani kwake. Aliinua macho yake akamtazama tena Jasusi Shadow usoni, alikuwa ametulia vile vile kama awali shadow alikuwa anania ya dhati kuunganisha nguvu na inspekta Aron lakini ilikuwa ni ngumu kwa Inspekta Aron kumuamini. Akawa bado yuko njia panda, atafanya nini mbele yake kuna Jasusi Shadow na nyumbani kwa Inspekta Jada hali si shwari, Aron hakuwa na jibu.
ITAENDELEA....
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya............32
Mtunzi: Saul David
Email: saulstewarty@gmail.com
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Aliinua macho yake akamtazama tena Jasusi Shadow usoni, alikuwa ametulia vile vile kama awali shadow alikuwa anania ya dhati kuunganisha nguvu na inspekta Aron lakini ilikuwa ni ngumu kwa Inspekta Aron kumuamini. Akawa bado yuko njia panda atafanya nini mbele yake kuna Jasusi Shadow na nyumbani kwa Inspekta Jada hali si shwari, Aron hakuwa na jibu.
Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA...
"Geuka nyuma" Aron alimuamriasha jasusi Shadow
"Lakini Aron...."
"Nimesema geuka nyuma" Alisisitiza tena kwa mara ya pili, pasipo ubishi wowote Jasusi Shadow akafanya kama alivyoagizwa, akageuka nyuma. Haraka Inspekta Aron alimfuata huku akichomoa pingu yake akaishika mikono ya Jasusi Shadow akaizunguusha nyuma kisha akaiunganisha na kumfunga pingu. Shadow aliendelea kubaki katikati hali ya utulivu akitazama tu mambo anayoyafanya Inspekta Aron, alijua ni vigumu sana yeye kuaminika lakini alijipa moyo akijua utafika wakati yeye na Aron wataungana na kuwa kitu kimoja.
Inspekta Aron alimkalisha shadow juu ya kiti kimoja cha chuma, akachukua kamba zilizokuwa kabatini akamfunga, baada ya hapo akatoka na kuondoka zake.
Alitembea kwa haraka hadi pale katikati ya kichaka kikubwa ambapo huwa analiacha gari lake, akafungua mlango akaingia na kuondoka kwa kasi akiwa na lengo la kuwahi nyumbani kwa Jada. Taarifa ya ugomvi kati ya Annah na Najma ilimshtua sana ndio sababu akaamua kuachana na Shadow kwanza.


Jasusi Shadow akiwa amefungwa pingu kisha kufungwa kwenye kiti, alibaki ametulia huku macho yake yakiitazama picha kubwa ya marehemu Jenerali Phillipo Kasebele ambaye ni baba wa Inspekta Aron lakini pia ni bosi wake ambaye walifanya kazi kwa kipindi kirefu sana enzi sa uhai wake.
Jasusi Shadow alivuta kumbukumbu ya miaka kadhaa nyuma iliyopita.....
ilikuwa ni siku moja akiwa ndani ya nyumba hiyo ya siri pamoja na Jenerali Phillipo Kasebele siku hiyo Aron alifika hapo ghafula bila kutoa taarifa ilibidi Jasusi Shadow ajifiche kwani Aron hakutakiwa kumuona akawacha baba na mtoto wakizungumza mambo fulani fulani aliyoyasikia akiwa kwa mbali.

"Umekuwaje umekuja bila taarifa Aron?"aliuliza Jenerali Phillipo
"Aah! Baba ulishasema hapa ni nyumbani kwani lazima nitoe taarifa au ndio kama kawaida yako hutaki nijue kila kitu kuhusu wewe" alisema Aron.
"Hahaha kijana wangu unamaneno mengi sana huenda ulitakiwa kuwa mwanasiasa nimekulazimisha tu uwe askari, haya nambie najua haujaja bure, sema kitu kidume wangu"
"Yeah! ni kweli baba, hujarudi nyumbani tangu juzi nimeona nikufuate nije kukuaga likizo imekishwa natakiwa kurudi jeshini kesho"

"Nina mambo mengi mwanangu nikisema nirudi nyumbani basi vitu vingi vitaenda hovyo kwenye hii nchi yetu, huu ndio mwaka wako wa mwisho ukimaliza utaingia darasani miezi sita kisha rasmi utaitwa Inspekta Aron hapo utaanza kunisaidia baadhi ya majukumu muhimu" alisema Jenerali Phillipo huku akiweka mkono wake kwenye mabega ya mwanae kisha wakawa wanatembea na kuingia ndani ya chumba kimoja kidogo kilichokuwa kimejitenga pembeni. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na viti vingi vya mbao vilivyopangwa vizuri na mbele kabisa kulikuwa na ubao mkubwa mweusi. Chumba hicho kilikuwa ni kama darasa hivi.
Aron alitupa macho kutazama ubaoni aliona maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa chaki, yalisomeka
,,,,,,V-COBOS,,,,,,,
Aron aliyasoma na kuyatamka
"V-COBOS ina maana gani baba?"
"Sio muhimu kwa sasa" alisema Jenerali Phillipo huku akichukua ufuto akayafuta yale maneno.

"Tatizo lako baba ni msiri sana, hivi kwa nini unakuwa hivyo lakini au huniamini?" Aron alilalamika na kuuliza swali
"Mwanangu kila jambo litakiwa kufanyika kwa wakati wake sahihi, siwezi kukupa mfupa utafune angali najua hauna meno"
Aron alimtazama baba yake kwa macho yanayoonyesha kwamba ameelewa msamiati aliyouzungumza.
"Mwanangu Aron siku nyingine utakapoyaona haya maneno V-COBOS au kuyasikia mahali popote basi hakika hiyo ndiyo siku maisha yako yatabadilika na rasmi utaanza kufanya kazi kama ninazozifanya mimi wakati huu" Alisema Jenerali Phillipo huku akiachia tabasamu ambalo Aron alizoea kuliona usoni kwa baba yake kila anapozungumza naye.
Baada ya mazungumzo hayo baadae baba na mwana waliagana Aron akaondoka na hii ndiyo ilikuwa siku ya mwisho Inspekta Aron kuzungumza uso kwa uso na baba yake ambaye kwa sasa ni marehemu.

Mara baada ya Aron kuondoka, Jasusi Shadow alijitokeza kutoka kule alipokuwa amejificha.

"Mkuu ni kwa nini hutaki Aron ajue chochote kuhusu vimelea vya V-COBOS, kwani haumwamini?" aliuliza Jasusi Shadow

"Kila kitu na wakati wake Shadow, nikiwa hai sitoruhusu kimuingiza mwanangu kwenye kazi hii hatari kumbuka tunapambana na maadui wengi na wakubwa kutoka ndani na nje ya nchi yetu, tukisema wote tuelekeze nguvu zetu huku vipi kama adui akitushambulia na kutudhibiti wote kwa pamoja? Nani tabaki kuokoa jahazi linalozama. Aron ni kijana mzuri sawa lakini ataanzia pale nitakapoishia mimi, hata ikitokea mimi nikafa leo basi usithubutu kumuingiza Aron kwenye hili subiri mpaka mda sahihi utakapofika wewe endelea tu kufanya kazi na mke wangu madam Sultana" alieleza Jenerali Phillipo.

"Sasa mkuu mda sahihi wa Inspekta Aron kuingia kwenye hii kazi ni upi?"
"Mpaka pale atakapokuwa na ulinzi wa kutosha"
"Una maana gani?"
"Namaanisha mpaka pale Aron atakaposhika nafasi au cheo kikubwa ambacho hawezi kuyumbishwa na viongozi wala rushwa"
"Mmh! Itamchukua mda"
" Hapana, Aron atakapoanza kazi najua atawavutia watu wengi na haitachukua mda kupewa nafasi za juu, kuna watu wangu wapo serikali watakuwa wanamuangalia hata usijali" Alisema Jenerali Phillipo Kasebele.
Ni kama alijua siku moja atakufa, haya ndiyo maagizo muhimu aliyoyaacha kwa kijana wake mwaminifu Shadow jasusi kutoka kenya ambaye aliendelea kufanya kazi na Sultana huku akiamini mambo yapo kama yalivyokuwa awali lakini anashangaa kuona lengo la Sultana linakuwa tofauti kabisa na matakwa ya marehemu mumewake na hii ndiyo sababu Shadow akawaza kuunganisha nguvu na Inspekta Aron ili kuona ni namna gani wanaweza kulizuia suala hili hatari la usambazaji wa virusi vya V-COBOS kwa pamoja.

Akiwa pale kwenye kiti alichofungwa Jasusi Shadow aliendelea kuwaza ni namna gani ataweza kumshawishi Inspekta Aron ili akubali kuungana naye, japo alijua ni mapema tofauti na matakwa ya baba mzazi.
Ni Madam Sultana pekee ndiye aliyekuwa kijua ni wapi ilipo chupa ya kijani yenye kinga na tiba dhidi ya vimelea vya V-COBOS hii ndiyo sababu Jasusi Shadow aliendelea kuwa mtiifu kwa Madam Sultana.

"Kila siku maadui wanazidi kuongezeka, alikuwepo Dokta Gondwe akaja Tino na sasa madam Sultana" aliwaza Jasusi Shadow.


Nusu saa baadae Inspekta Aron alionekana akipaki gari yake nje ya nyumba ya Inspekta Jada, akapiga hatua ndefu ndefu kuingia ndani wakati huo simu yake ilikuwa inaita akachukua na kuipokea.

"Hallo"
"Hallo Inspekta Aron" sauti ya kiume kutoka upande wa pili wa simu ile ilisikika, huyu alikuwa ni mwanasheria aliyekuwa anasimamia kesi ya Osward upande wa mashtaka
"Nambie Andrea"
"Nimepokea simu sasa hivi naambiwa siku ya kusikilizwa kesi ya Osward imebadilishwa sio leo tena ni kesho" alisema mwanasheria kauli iliyomfanya Inspekta Aron asimame ghafula

"Kwa nini yani? Mboba imekuwa ghafula sababu ni nini?"
"Sijaambiwa sababu Inspekta"
"Sasa kwa nini usiulize, sheria ipi imetumika kuhairisha siku ya kusikiliza kesi mbona mnanichanganya, na wewe unajua kabisa kuwa maisha ya shahidi wetu Annah yapo hatarini kwa nini unaendelea kuwapa muda " Aron alifoka
"Jaribu kuwa mtulivu Inspekta Aron hili ni agizo ambalo naona limetoka ngazi za juu kabisa, unaelewa Osward ni mtoto wa nani hapa nchini naona wanajaribu kufanya kila linalowezekana kuhakikisha hafungwi"
"Kwa hiyo tunafanyaje sasa"
"Naomba nifuatilie kwanza ni sababu zipi zilizowafanya wahairishe kusikiliza kesi leo, endelea kuwa makini, mlinde sana Annah" Mwanasheria aliongea kwa msisitizo kisha akakata simu.
Inspekta Aron alitulia kwa sekunde kadhaa akijaribu kuitafakari taarifa hiyo mpya aliyopewa
"Wanajaribu kufanya nini hawa? au wameshagundua kuwa Annah yupo hai?hapana sio rahisi, sasa ni nini kinaendelea?" Inspekta Aron alikuwa akijiuliza maswali yasiyo na majibu. Hakuelewa kuwa tayari Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa alikuwa ameingilia mchezo na sababu za kuifanya kesi hiyo ipelekwe mbele bado zilikuwa hazijajulikana.

"Umekuja badala ya kuingia umeganda hapo mlangoni Aron, nini shida?" Inspekta Jada aliuliza mara baada ya kumuona Inspekta Aron amesimama mlangoni
"Wako wapi hao? bado wanapigana?" Badala ya kujibu swali Inspekta Aron aliuliza swali
"Hapana wameacha ila bado hali si shwari Inspekta kwa nini hukuwatambulisha hawa mabinti yaani wamelala pamoja na hawajuani"
"Inspekta Jada unawaza nini wewe, yaani kirahisi tu ningeanza kumwambia Jada huyu ni Annah shahidi wa kesi ya mchumba wako Osward. Alafu nimwambie Annah huyu ni Najma mtoto wa Dokta Gondwe ambaye ndiye aliyehusika na mauaji ya wazazi wake"

"Hapana sina maana hiyo lakini angalau ungewapa hata mwanga si...."
Alisema Jada lakini kabla hajamalizia sentensi yake alitulia ghafula mara baada ya kumuona Najma anakuja.

"Asante kwa msaada wako Aron nataka kwenda nyumbani sasa" alisema Najma kauli iliyowafanya Jada na Aron watazamane
Kimya kilitawala kwa muda wa sekunde kadhaa.

"Okay, twende nikupeleke"alisema Aron
"Inspekta ni muda wa mahakamani huu" alisema Jada
"It's okay nitaenda mwenyewe hata usijali Aron"
"Noo, nitakupeleka. Jada.." Inspekta Aron aliita kisha akasogea karibu na Jada akamuelekeza hali halisi kuhusu kuhairishwa kwa kesi ya Osward siku hiyo. Jada alitaka kuuliza maswali lakini Aron akamzuia

"Kaa na Annah kwanza nakuja sio mda" alinong'ona Inspekta Aron kisha akaondoka kumuwahi Najma ambaye tayari alikuwa ameshatoka nje, wakaingia kwenye gari.

"Samahani kwa kila kilichotokea Najma" alisema Inspekta Aron
"Ni nani yule mwanamke?" Najma aliuliza swali lililojaa wivu ndani yake
"Anaitwa Annah" Inspekta Aron alijibu kifupi huku akiwasha gari safari ya kumpeleka Najma nyumbani kwao ikaanza
"Kwa nini anasema baba yangu ni muuaji, Aron usinambie anachokisema yule mwanamke ni kweli"
Najma aliongea huku akimtazama Inspekta Aron usoni.
"Sina uhakika Najma, lakini kuna asilimia kubwa ikawa ni kweli samahani kama nitakuwa nakuudhi tena ila uliniomba niwe naongea ukweli kwako" alisema Aron

Najma alitulia kwa muda huku akijaribu kuzitafakari tuhuma hizo mpya zinazomuandama baba yake mzazi, alijaribu pia kuunganisha na matukio mengine kama zile taarifa kuhusu vimelea vya V-COBOS alizopewa na Osward na hii skendo mpya ya picha za utupu za baba yake ambazo zilisambaa mtandao siku ya jana, akawa njia panda kuna wakati moyo wake ulisema ni kweli baba yake si mtu mzuri lakini kuna wakati moyo huo huo ulikataa.


Dakika 15 baadae tayari gari Inspekta Aron alikuwa nje ya jumba la kifahari la mheshimiwa Waziri wa afya Dokta Gondwe.

"Vipi leo huingii ndani?" Aliuliza Najma baada ya kuona Inspekta Aron kasimamisha gari nje kabisa ya geti

"Hapana siingii, shuka tu nitakusindikiza mpaka ndani usijali"
"Mmh nikajua unamuogopa baba"
"Hahaha hapana siwezi"
Kimya kilitawala Najma akawa anamtazama Inspekta Aron usoni kisha bila kusita Najma alisogea na kumbusu kwenye shavu la kushoto.

Aron alibaki ameduwaa akiwa ametazama mbele, ni kama vile mwili wake ulikuwa umeshika ganzi ghafula, hali hiyo ilimshangaza pia Najma akatazama mbele kule alikokuwa anatazamana Inspekta Aron, laa! haula alimuona baba yake Dokta Gondwe akiwa amesimama mbele ya mlango mdogo wa geti la nyumba yako.

Najma alishtuka sana na kuogopa, aliamini kwa vyovyote vile baba yake atakuwa ameona kitendo alichokifanya kwa Inspekta Aron na mbaya zaidi Dokta Gondwe alikuwa na uadui mkubwa dhidi inspekta Aron istoshe Najma alikuwa ni mke mtarajiwa wa Osward.

Je, nini kitafuata?
Vipi kuhusu Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa atafanikiwa kutekeleza jukumu alilopewa na maabara ya ZMLST kumuua Dokta Gondwe?
Kwa nini ametaka kesi ya Osward isogezwe mbele?
Vipi kuhusu wale wazungu wanaokuja kutoka Mexico kwa lengo la kusambaza vimelea vya V-COBOS?
Na je, Jasusi Shadow ataweza kumshawishi Inspekta Aron waungane?
Vipi kuhusu Tino na Bosco?
Vipi kuhusu Sultana na Jesca?

SASA TUNAENDA KUUWASHA MOTO NDANI YA SEASON 3... KARIBU
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya.............33
Mtunzi: Saul David
Email: saulstewarty@gmail.com
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...

Najma alishtuka sana na kuogopa, aliamini kwa vyovyote vile baba yake atakuwa ameona kitendo alichokifanya kumbusu Inspekta Aron na mbaya zaidi Dokta Gondwe alikuwa na uadui mkubwa dhidi inspekta Aron istoshe Najma alikuwa ni mke mtarajiwa wa Osward.

SASA ENDELEA...
Walibaki katika hali ya kuduwaa kwa zaidi ya sekunde 30, Dokta Gondwe naye aliendelea kusimama wima pale getini huku akiwatazama, ni kweli alishuhudia wakati ule binti yake Najma anambusu Inspekta Aron.

"Mimi naenda Aron" alisema Najma huku akitazama chini kwa aibu, ilikuwa ni kama amefanya vile kwa bahati mbaya, akafungua mlango wa gari na kushuka, Inspekta Aron naye akafanya hivyo
"Vipi bado unataka kunisindikiza?" Najma aliuliza huku akimtazama Aron usoni
"kwani kuna ubaya? usijali nataka kumsalimia baba yako"
"Mmh!!"
"Kweli"
"Haya twende"
Inspekta Aron na Najma waliongozana hadi pale alipokuwa Dokta Gondwe, Najma alikimbia na kwenda kumkumbatia baba yake kwa furaha iliyoambatana na huzuni kwa wakati mmoja. Alitambua wakati anaopitia baba yake hasa baada ya zili picha zake za utupu kusambaa mtandaoni.

"Ulienda wapi mwanangu, unataka kuniua baba yako kwa presha?" Dokta Gondwe aliuliza huku akizidi kumkumbatia binti yake kwa nguvu.
"Am sorry daddy"
"Haya tangulia ndani basi nakuja" Alisema Dokta Gondwe kisha akamuachia binti yake ambaye aligeuka nyuma na kumtazama Inspekta Aron. Najma akatikisa kichwa ikiwa ni ishara ya kutoa asante nyingine kwa mwanaume huyo ambaye alijitoa kwa ajili yake usiku wa jana, Inspekta Aron naye akatikisa kichwa kuipokea shukrani hiyo kisha Najma akaingia ndani.

Sasa wakabaki Inspekta Aron Dokta Gondwe wanatazamana uso kwa uso hali iliyodumu kwa sekunde kadhaa.

"Najua kilichotokea kwa binti yangu usiku wa jana, nashukuru ulienda kumsaidia" Alisema Dokta Gondwe kauli iliyomfanya Inspekta Aron ashtuke kiasi, hakujua ni vipi Dokta Gondwe amezipata zile taarifa alihofu pengine anaweza kuwa ametambua pia kuwa Annah yupo hai kwa sababu alikuwanaye katika tukio la jana usiku kumuokoa Najma kutoka kwenye mikono ya vibaka.

"Nilikuwa na hofu baada ya kuambiwa asubuhi hii kuwa binti yangu hakulala hapa nyumbani, nilituma vijana wangu wafuatilie nikapata habari kuwa alitekwa na ulienda kumsaidia asante sana kijana" Alisema Dokta Gondwe.
Inspekta Aron alitikisa kichwa kupokea asante hiyo huku akiwa makini kusikia kama Dokta Gondwe atasema kitu kuhusu Annah, lakini haikuwa hivyo.

"Lakini usijisahau bwana mdogo, Najma ni binti yangu mimi na tayari ni mchumba wa Osward nafikiri unalijua hilo vizuri kabisa"
"Naelewa, niambie ni wewe uliyepeleke mbele siku ya kusikilizwa kwa kesi ya Osward?" Aliuliza Inspekta Aron huku akimtazama Gondwe kwa macho ya adadisi, taarifa hii ilionekana kuwa ngeni kabisa kwa Dokta Gondwe.
Kabla hajajibu swali hilo mara kuna sauti nzito ya kiume ilisikika kutokea nyuma ya Inspekta Aron ikijibu.

"Sio yeye ni mimi"
Inspekta Aron aligeuka nyuma haraka kuangalia ni nani aliyeongea, hakuwa mwingine bali kaka yake Tino ambaye ndio alikuwa anafika nyumbani kwa dokta Gondwe.

Inspekta Aron aliduwaa kidogo kwani hakuwa ametegemea ujio wa kaka yake mahali hapo, hali ilikuwa hivyo hata kwa Dokta Gondwe pia hakuwa ametegemea kabisa kukutana na kijana wake Tino asubuhi hiyo wala hakujua amefuata nini.
Tino alikuja mwenyewe kwa matakwa yake na lengo lake ilikuwa ni kuja kumsabahi bosi wake wakati akisubiri mpango wake wa kumfanya Dokta Gondwe alimletee vimelea vya V-COBOS kwa tishio la zile picha za utupu, huu ndio ulikuwa mpango uliomleta.
Tino alipiga hatua akaenda na kusimama pembeni ya Dokta Gondwe bosi wake kisha akageuka.
Sasa wote wakawa wanatazamana Inspekta Aron ambaye naye aliwatazama kwa zamu, mmoja baada ya mwingine.

"Mliwauwa wazazi wa annah mkaona haitoshi mmetafuta kila namna mmemuua binti asiye na hatia ambaye ni shahidi wa mwisho na wa pekee ambaye alibaki kwenye kesi ya Osward. Sasa ni nini kingine mnaogopa hadi mpeleke kesi mbele?" Aliuliza Inspekta Aron.

"Siku zote umekuwa mtu wa maneno mengi yasiyo na ushahidi wowote mdogo wangu, naona kabisa kazi yako inakushinda. Hivyo ndivyo ulivyofundishwa? Sasa nikuonye kwa mara ya mwisho dogo, siku moja uvumilivu utatushinda tutakugeuzia kibao na kukushtaki kwa hizi tuhuma zote za uongo unazotupa kila siku, alafu jaribu kuwa na heshima hata kidogo Aron huyu ni kiongozi wako Waziri mkubwa sana serikali unapata wapi huo ujasiri" Tino aliongea kwa kujiamini sana.
Aron alika kimya kwa muda kisha akapiga hauta na kusogea karibu kabisa na kaka yake, wakawa wanatazamana uso kwa uso

"Sijawahi kuanzisha jambo nikalishindwa kaka, wewe na huyu bosi wako siku si nyingi mtalipa kwa maovu yenu. Usije kuyasahau haya maneno hata siku moja brother" Aron aliongea kwa kujiamini kisha akageuka na kuondoka akiwaacha Dokta Gondwe na Tino wanamsindikiza kwa macho.

Wakati haya yakiendelea Najma binti wa Dokta Gondwe alikuwa ghorofani chumba cha juu kabisa akiangalia yale yaliyokuwa yakiendelea kati ya baba yake, Tino na Inspekta Aron. Hakuwa akiyasikia mazungumzo yao lakini aliamini lazima kuna mabishano yalikuwa yakiendela kati yao.
Najma alijikuta akiwaza mambo mengi sana, akakumbuka yale maelezo aliyopewa na Osward kuhusu baba yake kuwa mmoja kati wa watu wanaoshiriki katika mpango hatari wa kusambaza ugonjwa utakaosababishwa na virusi vya V-COBOS. Alijua pia namna Inspekta Aron anavyohangaika kupambana na baba yake licha ya kwamba hakujua chochote kuhusu virusi vya COBOS, Najma akaona hana sababu ya kuendelea kukaa kimya. Ukimya wake ulikuwa ni sawa na kuruhusu vifo vya mamilioni ya watu kutoka ulimwenguni kote kama mpango wa kiovu ambao baba yake ni mshirika ukifanikiwa. Haraka alichukua simu yake ndogo akaingiza namba ya Inspekta Aron akapiga.

"Hallo...Aron ni mimi Najma hii ni namba yangu pia, naomba usiondoke nisubiri hapo kwenye gari" Najma alitoa maelezo upesi akakata simu na kuanza kushuka chini.
Sekunde chache baada tayari alikuwa sakafu ya chini ya nyumba yao akatoka nje akakutana na baba yake akiwa pamoja na Tino wakiwa ndio wanaingia.

"Vipi wapi tena!?" Dokta Gondwe aliuliza huku akimtazama binti yake aliyeonekana mwenye haraka.
"Nakuja niko hapa nje naongea na Aron mara moja" alisema Najma huku tayari akiwa amefungua geti akatoka nje.

"Hawa wameanza mazoea lini?" Aliuliza Tino
"Hata sielewi kwa kweli" alijibu Dokta Gondwe
"Wazuie hili linaweza kuwa tatizo jingine baadae, kwani huoni kama kuna kitu kati yao bosi"
"Naona lakini kumzuia Najma kwa vitu anavyovipenda huwa ni ngumu sana, sitaki kugombana naye"
"Hapana mzee tafuta njia uwatenganishe kabla hili suala halijawa kubwa, kumbuka Osward ataachiwa huru sio mda vipi kama akikuta hali imebadilika"
"Yah! ni kweli alafu umenikumbusha, imekuwaje yani kesi ya Osward isogezwe mbele kwa nini?" Aliuliza Dokta Gondwe
"Mmh! Mimi najua labda wewe ndio umefanya hivi pengine kusubiri haya yanayoendelea mtandaoni yaishe?"
"Hapana sio mimi Tino, atakuwa ni nani sasa?"
"Sijui kwa kweli, mawazo yangu yote nilijua ni wewe, siku hizi umekuwa msiri sana bosi kwa nini hata hujataka kunishikirikisha kwa kina kuhusu hii kashfa inayoendelea mtandaoni, kwa nini usiniruhusi nimtafute mtu aliyekuchafua" Tino alitoa kauli iliyojaa unafiki mkubwa ndani yake, alikuwa akielewa kila kitu kinachoendelea na yeye ndiye haswa aliyemchafua Dokta Gondwe mtandaoni.

"Nitakwambia kila kitu usijali hili ni jambo la kisiasa zaidi halihitaji nguvu kubwa kushinda" Dokta Gondwe alidanganya lakini ukweli ulibaki kuwa ule ule hakutaka Tino apate nafasi ya kujua tukio la yeye kumsaliti kwa kulala na mke wake Jesca.


"Nambie Najma kuna nini tena?" Ilikuwa ni sauti ya Inspekta Aron akiuliza mara tu baada ya Najma kuingia ndani ya gari yake.

"Aron" Najma aliita
"Niambie"
Najma alitulia akavuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu kisha akaongea...
"Unajua au ulishawahi kusikia kuhusu hili neno V-COBOS" hii ilikuwa ni kauli iliyopenya kwenye masikio yote mawili ya Inspekta Aron kisha ikaivuruga akili yake. Inspekta Aron aligeuka kwa kasi na kumtazama Najma usonu huku akiwa ametoa macho, hali hiyo ilimtisha sana Najma.

Inspekta Aron aliikumbuka kauli aliyowahi kuambiwa na marehemu baba yake miaka kadhaa iliyopita, alisema
"Mwanangu Aron siku nyingine utakapoyaona haya maneno V-COBOS au kuyasikia mahali popote basi hakika hiyo ndiyo siku maisha yako yatabadilika na rasmi utaanza kufanya kazi kama ninazozifanya mimi wakati huu kwa ajili ya nchi yangu" Alisema Jenerali Phillipo.

Maneno hayo yalijirudia rudia kwenye kichwa cha Inspekta Aron wakati huo akiwa anamtazama Najma usoni.

[Ni sh elf 1 tu kupata simulizi hii softcopy (PDF)
LIPIA KWA MPESA NAMBA 0756862047 jna SAUL Kisha njoo WhatsApp inbox namba hiyo hiyo]
Je, nini kitafuata?
Najma atamueleza Inspekta Aron siri hii?
Inspekta Aron atafanya nini?
Ni nini mpango wa Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa?

,

ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya................34
Mtunzi: Saul David
Email: saulstewarty@gmail.com
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Mwanangu Aron siku nyingine utakapoyaona haya maneno V-COBOS au kuyasikia mahali popote basi hakika hiyo ndiyo siku maisha yako yatabadilika na rasmi utaanza kufanya kazi kama ninazozifanya mimi wakati huu kwa ajili ya nchi yangu" Alisema Jenerali Phillipo.
Maneno hayo yalijirudia rudia kwenye kichwa cha Inspekta Aron wakati huo akiwa anamtazama Najma usoni.

SASA ENDELEA...
"Aron kwani vipi mbona hivyo?" Aliuliza Najma
"Unaweza kuniambia hiyo V-COBOS ni kitu gani?"
"Kwa nini? mimi nimekuliza wewe kama unafahamu"
"Hapana Najma sijui chochote ila niliwahi kusikia mahali tafadhali unaweza kuniambia kwa kina nini maana yake?" Inspekta Aron aliuliza kwa bashasha huku akijivuta kusogea karibu zaidi na Najma.
Najma alitulia akijaribu kuwaza amjibu nini Inspekta Aron ambae ama kwa hakika alionyesha ni kweli kabisa hajui kitu kuhusu V-COBOS.
Najma alijikuta anapata kigugumizi cha ghafula akashindwa ajibu nini kwani alijua ni lazima Aron atakuwa na maswali mengine mengi ambayo hana majibu yake. Aliogopa pia kama atamueleza ukweli wote aliopewa na Osward kule gerezani basi angekuwa anamuweka kwenye wakati mgumu baba yake kiasi cha kumfanya Inspekta Aron azidi kumfuatilia. Najma alijikuta yupo njia panda hakujua afanye nini na nini asifanye.

"Najma"
"Abeeh"
"Mbona unakaa kimya tena?"
"Aron mimi pia sijui chochote lakini..."
"Hujui? ulilisikia wapi hilo neno Najma? Tafadhali nakuomba usinifiche chochote niambie kitu unachokijua"
"Aron ni kweli sijui chochote, jana nilisika wakizungumza kwenye redio so nimetaka tu kujua"
"Redio? Redio gani saa ngapi? Kipindi gani?"
"Aa.. Aron nime..."
"Najma nambie vizuri basi mmh"
"Ni redio ya Wasafi Fm kipindi cha.. cha.. afya"
"Afya?"
"Ndi..ndiyo afya"
"Wasafi Fm? Afya?" Inspekta Aron aliuliza huku akimtazama Najma usoni ambae alipepesa macho yake Inspekta Aron akajua kabisa anadanganywa.
Kwa kumbukumbu zake hakuwahi kusikia Wasafi Fm wakawa na kipindi cha afya, ilikuwa ni redio iliyoanzishwa hivi karibuni, hawakuwa na vipindi vingi tofauti na kupiga miziki kwa muda mrefu.

"Sawa basi nitafuatilia nikijua ni kitu gani nitakuambia" Alisema Inspekta Aron baada ya kubaini kuwa Najma hayuko tayari kumuambia ukweli anaoujua

"Sawa baadae basi" Alisema Najma akashuka kwenye gari akawa anaondoka huku nafsi yake ikimsuta. Kumwambia Inspekta Aron ukweli anaoujua ilikuwa ni jambo sahihi zaidi kuliko kuficha ili tu kumlinda baba yake. Inspekta Aron akawa anamsindikiza Najma kwa macho hadi alipoingia ndani.

"Ni wazi kuwa Najma kunakitu anakifahamu lakini anasita kusema kwanini? hii COBOS maana yake ni nini? Kwa nini baba alisema siku nikisikia tena hili neno maisha yangu yatabadilika?" Inspekta Aron alijiuliza maswali ambayo hakuwa na majibu yake, hapo akajikuta anamkumbuka yule mtu aliyedai kuwa aliwahi kufanya kazi na baba yake yaani Jasusi Shadow. Kwa kuwa alikuwa kwenye mikono yake Inspekta Aron aliona huo ndio wakati sahihi wa kwenda kumuuliza Shadow maswali kadhaa aliyokuwa nayo kichwani pengine angepata mwanga wapi pa kuanzia. Inspekta Aron aliwasha gari yake na kuondoka kwa kasi kubwa safari ya kuelekea kule msituni kwenye nyumba ya siri mahali alipomfungia Jasusi Shadow ilianza.


Nusu saa baadae tayari Inspekta Aron alikuwa amekwishafika kule msituni, alipaki gari yake kama ilivyokuwa kawaida yake kisha akatembea haraka haraka kuelekea kwenye ile nyumba ya baba yake. Alifika na kuingia ndani moja kwa moja akiwa na shauku kubwa ya kufanya kazungumzo na Jasusi Shadow.

Inspekta Aron alipoingia ndani na kutupa macho mbele hakuamini alichokiona, kiti kilikuwa kitupu Jasusi Shadow hakuwepo pale alipomuacha.
Haraka Inspekta Aron alichomoa bastola yake hali akichukua tahadhali zote muhimu, alimjua vizuri Jasusi Shadow kuwa sio mtu wa kubeza hata kidogo.
Aliangaza macho huku na huku ndipo alipoiona pingu aliyomfunga Jasusi Shadow ikiwa imefunguliwa na kutupwa sakafuni. Kwa namna alivyokuwa amemfunga haikuwa rahisi kuamini kuwa Jasusi Shadow alijichomoa kwenye zile kamba na kisha kifungua pingu akiwa mwenyewe bila msaada wowote, naam huyo ndio Jasusi Shadow.

Inspekta Aron aliona kipande cha karatasi kikiwa kimewekwa juu ya kile kiti alichomfunga shadow, taratibu akasogea na kulichukua lile karatasi lililokuwa na maandishi yaliyoandikwa na kalamu ya wino mweusi, akayasoma.

,,,,,,,,,,,,Tuna kazi kubwa ya kufanya mimi na wewe, Tumebeba jukumu kubwa la kuyaokoa maisha ya mamilioni ya watu wasio na hatia ambao kama tusipojitoa kwa ajili yao watakufa wote, nitarudi tena kwa ajili yako Inspekta Aron siku ukiona au kisikia maneno haya V-COBOS utakuwa ni wakati wako sahihi wa kuianza kazi aliyoiacha baba yako, kuwa makini tayari unamaadui kila kona,,,,,,,,,,,,,,,,

Inspekta Aron aliyasoma maelezo hayo akayarudia tena na tena kisha akalikunja lile karatasi huku akifunga ngumi na kukunja sura kwa hasira.
***
TANGAZO
Simulizi hii imetungwa na SAUL DAVID 075686204, epuka tapeli usikubali kununua kutoka kwa mtu mwingine tofuauti. Haki zote zimehifadhiwa
*****""

"Hamna tofauti na baba yangu, kila mtu anaona sio wakati sahihi wa mimi kujua ukweli, nini kinaendelea kwaniiiiii!!!?" Inspekta Aron aliongea kwa sauti na makelele yaliyopasua anga, akapiga magoti sakafuni akionekana mtu aliyejaa simanzi kubwa.

"Sio baba, sio Najma wala sio wewe wote mnaendelea kuniweka gizani, huo wakati sahihi ni upi, eti baba? Ona sasa tayari nimeshalisikia hilo neno ulilosema V-COBOS lakini hakuna kitu kilichobadilika hakunaaa!" Aliongea Inspekta Aron wakati huo kwa mbali alionekana Jasusi Shadow akiwa anamtazama kupitia dirisha lililokuwa wazi.
Shadow alikuwa amesimama nyuma ya miti mingi iliyokuwa jirani kabisa na nyumba hiyo, alimtazama Inspekta Aron kwa sekunde kadhaa kisha akatabasamu kidogo.

"Like father like son" (kama baba kama mtoto) Alisema Jasusi Shadow kisha akavaa maski yake akabeba begi lake na kuanza kutembea akielekea katikati ya msitu mnene.

"Wewe ni mtu sahihi sana Aron, Kwanza ngoja nikapambane na mama yako Sultana nijue ni wapi ilipo kinga na tiba dhidi ya vimelea vya V-COBOS baada ya hapo nitarudi tena kwako kwa pamoja tutazuia huu mpango hatari" Aliwaza Jasusi Shadow wakati akitokomea msituni.


Yalikuwa ni majira ya saa 6 usiku, ndani ya gereza la Kanondo Osward alishitushwa na sauti ya kufuri la mlango wa chumba chake ukifunguliwa. Wakati huo umeme ulikuwa umekata gerezani hapo jambo ambalo halikuwa kawaida kabisa. Osward Aliamka na kukaa kitandani, sekunde chache baadae mlango ukafunguliwa akaingia askari magereza mmoja.

"Inuka haraka nifuate" alisema yule askari kwa sauti ya chini.
"Wewe ni nani?"
"Utajua mbele wewe nifuate, kuna mtu muhimu anataka kukuona" alieleza yule askari kisha akageuka na kuanza kuondoka. Osward alijiuliza mara mbili mbili akitamani kujua kinachoendelea, haraka alishuka kitandani akaanza kumfuata yule askari nyuma nyuma huku akiwa na tahadhali sana.
Yule askari alionekana nimzoefu wa njia za siri za gereza hilo baada ya mwendo kama wa dakika tatu hivi tayari umeme ulirudi lakini Osward na askari magereza walikuwa wamefika mbali wakiwa wanafuata njia za siri zilziopita chini ya ardhi ya gereza hilo.
Dakika tano baadae walipanda ngazi kuelekea juu na baadae wakijuta wako nje kabisa umbali kama wa hatua mia mbili kutoa ulipokuwa uzio wa gereza la Kanondo.

Osward aliendelea kumfuata nyuma yule askari ambae alikatisha katikati ya msitu mdogo na Baada wakakuta barabara moja ya vumbi na mbele ya barabara hiyo kulikuwa na gari moja aina ya Jeep ikiwa imesimama katikati ya barabara.

"Ingia kwenye hilo gari" Alisema yule askari
Osward akamtazama usoni, yule askari akamuonyesha ishara kuwa asiwe na wasiwasi wowote.
Osward akapiga hatua taratibu akafungua mlango wa nyuma wa lile gari akaingia. Kulikuwa na dereva peke yake ambaye mara tu baada ya Osward kuingia aliwasha gari na kuondoka kwa mwendo wa wastani.
Kimya kilitawala kwa muda. Osward akawa anawaza akitamani kujua ni nini hasa kilikuwa kinaendelea, awali liwaza huenda ikawa ni mipango ya Dokta Gondwe anataka kumtorosha lakini bado alihitaji maelezo zaidi.
"Tunaelekea wapi?" Osward aliuliza baada ya mwendo kama wa dakika saba hivi.
"Tayari tumefika" alisema yule dereva huku akifunga breki ya gari.
Osward alipotazama mbele kwa msaada wa mwangaza wa mbalamwezi aliona kuna uwazi mkubwa ambao mwisho kabisa wa uwazi huo kulikuwa na korongo kubwa sana. Pembeni ya korongo hilo kulikuwa na gari nyingine tatu nyeusi za kifahari zikiwa zimesimama huku watu kama 8 hivi waliovalia suti nadhifu nyeusi wakipiga hatua huku na huku. Lakini kulikuwa na mtu mwingine mmoja ambaye yeye alikuwa amejitenga mbeni kabisa na wenzake, alikuwa amegeuka upande wa pili akitazama upande ule wenye korongo kubwa.

"Shuka, mfuate yule mtu kule pembeni" Alisema yule dereva

Osward alifungua mlango na kukanyaga ardhi taratibu alianza kutembea kuelekea kwa yule mtu aliyekuwa amesimama pembeni kwa kujitenga peke yake. Osward alitembea kwa tahadhali huku akiwatazama wale watu wenyewe suti nyeusi ambao hawakuonyesha kumjali wao waliendelea kupiga hatua kuhu na huku wakilinda usalama wa eneo hilo.
Hatimaye Osward alifika na kusimama hatua kadhaa nyuma ya yule mtu. Akawa anasubiri kwa hamu ageuke ili aweze kumtambua, awali aliwaza kuwa anaweza kuwa ni Dokta Gondwe lakini baada ya kumkaribia alibaini kuwa hakuwa yeye.

Taratibu yule mtu aligeuka, akavua kofia na miwani yake. Osward alitoa macho kwa mshangao baada ya kuiona sura ya mtu huyo, alimfahamu vizuri sana.
Hakuwa mwingine bali Mheshimiwa Profesa Cosmas Kulolwa, Rais mstaafu wa awamu iliyopita.
"Mheshimiwa...!!" Osward aliita kwa sauti ndogo iliyoambatana na mshangao
"Karibu Osward, kijana wangu mtiifu" Alisema Profesa Cosmas Kulolwa huku akiachia tabasamu
Je, ninj kitafuata?

ITAENDELEA...
WhatsApp: ,0756862047
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom