THE MODERN WAR: Simulizi ya kijasusi mapenzi na upelelezi

Aisee wahalifu Mara zote huwa hawana maisha ya amani na katika ulimwengu wao kutenda kosa kubwa kwa ajili ya kurekebisha kosa dogo sio tatizo.
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..........59
Mtunzi: Saul David

ILIPOISHIA....
"Ni wakati wa kuchukua maamuzi magumu Osward, huyu kiumbe ni bomu hatakiwi kabisa kuishi, najua unajua nini cha kufanya kumziba mdomo mchumba wako, ama umuue wewe au umuache tukusaidie" Alisema Tino kwa sauti ya kunong'ona kisha akachukufua funguo ya gari mezani akaweka koti lake sawa na kuondoka akimuacha Osward ameduwaa.

SASA ENDELEA....
Mwisho Osward naye alitoka nje ya ile nyumba akapiga hatua kuingia ndani ya gari waliyokuja nayo, akamkuta tayari Najma alishaingia na kukaa siti ya mbele pembeni ya dereva huku sura yake ikiwa imekunjamana kwa hasira. Osward alimtazama Najma kwa sekunde kadhaa bila kuzungumza chochote akawasha gari tayari kuondoka.

"Nipeleke kituo cha polisi" Alisema Najma kabla Osward hajaliondoa gari.
"Najma can you stop this please!!(Najma unaweza kuacha hili tafadhali) Alisema Osward huku akipigapiga usukani kwa mikono yote miwili, maneno na msimamo aliokuwa nao Najma vilifanya kuwa na hasira pia.
"No" (hapana)
"Hivi ni mara ngapi nakueleza kuhusu uhatari wa hili jambo na hutaki kunielewa"
"Nakuelewa sana Osward, lakini naomba na wewe pia unielewe. Nipeleke kituo cha polisi"
"Am sorry Najma siwezi" Alisema Osward kisha akaanza kuendesha gari akakunja kona kulia na kufuata uelekeo tofauti na barabara ya kwenda kituo cha polisi
"Osward stop! Nimesema simamaaaaa...." Najma aliongea kwa sauti kubwa huku akiishika mikono ya Osward iliyoshikilia usukani. Gari iliyumba mara kadhaa almanusura wapate ajali lakini kwa bahati nzuri Osward akawahi kukanyaga breki gari ikasimama.

"Hivi unajua unachokifanya Najma?" Osward alifoka
"Najua, najua kila kitu... Sikiliza Osward, kamwe sitoacha kifo cha baba yangu kipite bure na wala sitoacha wafanikishe huu mpango wa kusambaza vimelea vya V-COBOS hapa nchini kwetu unanielewa? nitahakikisha napambana kwa nguvu zangu zote"
"Hizo nguvu ndio huna Najma huna hizo nguvu elewa, wewe ni kama sisimizi tu kwao watakukanyaga kisha wao watasonga mbele"
"So wewe unatakaje? Nikae kimya? Ee nikae kimya baba yangu kauliwa kikatili vile? Nikae kimya nishuhudie nchi ikiingia kwenye janga lingine kama ilivyokuwa Korona. Mimi sio kama wewe Osward hatufanani hata kidogo"
"Kukaa kimya ni kheri zaidi kwa sababu ukijaribu kupiga hatua moja wao watapiga hatua kumi mbele yako, hilo ndilo jambo lililomuua baba yako" Aliongea Osward kauli iliyomfanya Najma apoe ghafula na kumtazama. Ilikuwa ni kauli iliyomponyoka Osward kwa bahati mbaya hata yeye hakuwa ametegemea kuzungumza vile.
"So do you know exactly what killed my Dad, right?" (Kwa hiyo kumbe unajua vizuri kabisa nini kilimuua baba yangu si ndio?) Najma aliuliza hali akiwa amemkodolea macho Osward ambaye alitulia kimya.
"Naongea na wewe Osward"
"Kabla sijakujibu kuna kitu nataka nikuonyeshe"
"Kitu gani?"
"Twende nyumbani"
Alisema Osward kisha akawasha gari kwa mara nyingine wakaendelea na safari huku mara hii Najma akiwa mpole sana. Yale maneno aliyoyasema Osward yalijirudia rudia kichwani kwake, bado alitamani kumuelewa.

Nyuma ya gari alilopanda Osward na Najma lilionekana gari lingine likiwafuatilia, alikuwa ni Tino ndani ya gari hiyo wakati huo alikuwa akiongea na Bosco kijana wake wa karibu kwenye simu.

"Aisee mambo yamebadilika dogo, huwezi kuamini Osward tuliyekuwa tunajadili kumteka kaja nyumbani" alieleza Tino.
"Eti nini, kaja kufanyaje!?"
"Kaja na yule mtoto wa Waziri Dokta Gondwe eti anapeleleza kifo cha baba yake. Kwa bahati mbaya anaonekana anajua kuhusu vimelea vya V-COBOS katutisha kuwa anataka kwenda kutoa ripoti polisi"
"Mmh! Mbona hatari hiyo, atavuruga kila kitu huyo mwanamke"
"Nimemwambia Osward ashughulike naye mapema kabla hajaharibu mambo hivi nipo nawafuatilia nione mwisho wao, siwezi kuruhusu akutane na polisi kama Osward akishindwa nitamchapa risasi mwenyewe"
"Duh sawa bosi basi nipe location ulipo sasa hivi nije na vijana" alisema Bosco kisha simu ikakatwa.
Wakati huo Tino alikuwa makini kulifuatilia gari waliyopanda Osward na Najma kila kona inakopita lakini jambo la kushangaza nyuma ya gari la Tino kulikuwa na mtu kwenye pikipiki ambaye naye ilikuwa akifuata nyuma kila kona anayopita Tino.


Upande wa pili msafara wa gari tatu nyeusi aina ya Noah ulizidi kushika kasi huku Jesca mke wa Tino akiwa gari ya mbele kama kiongozi wa msafara huo. Yalikuwa yamepita masaa kadhaa tangu waianze safari hiyo, sasa waliacha barabara kuu na kuhamia barabara ya vumbi iliyokuwa inakatisha katikati ya msitu mnene. Njiani alikuwa akiendelea kupanga mipango na watu wake kuhakikisha huko wanakokwenda wanarudi na chupa ya kijivu ambayo inakinga na tiba dhidi ya vimelea vya V-COBOS chupa hiyo inasemekana ipo kwenye mikono ya chifu wa kabila mahali wanapoelekea.


IKULU...
Sandra, Jajusi Shadow, Fungo, Inspekta Aron pamoja na Mheshimiwa Rais Dkt Alfredo Zumo walikuwa ndani ya kile chumba cha siri ndani ya Ikulu. Tayari walifanikiwa kumuokoa Jajusi Shadow kutoka Ngome ya Ambross na sasa hata hali yake ya kiafya ilikuwa imeimalika kiasi.
Kwa sasa Jajusi Shadow alikuwa akiwasimulia yale yaliyompata.

"Kama nilivyoeleza kuwa Sultana alipata mashaka na mimi akahisi namzunguuka hivyo aliniweka chini ya ulinzi akajaribu kunihoji. Niliweza kumshawishi kwa namna tofuauti lakini bado haikuwa kazi nyepesi mwisho aliamru nikafungiwe kule kwenye ngome yake ya Ambross" Alieleza Jasusi Shadow.
"Kwa hiyo unataka kusema mahusiano yako na Sultana tayari yameharibika hivyo hatuwezi tena kupata ile chupa ya kijivu kupitia yeye?" Aliuliza Mheshimiwa Rais.
"Hapana, ni kweli mahusiano yameharibika lakini kuna taarifa ninazo ambazo zinaweza kutufanya tukatambua ni wapi ilipo chupa ya kijivu"
"Zipi?"
"Nilimtisha Sultana nikamwambia kuwa wazungu kutoka Mexico wamekuja na tayari wameshajua ni wapi chupa ya kijivu ilipo wanakwenda kuichukua, aliogopa na mara moja akawatuma watu wake kuifuata.."
"Yes! Bila shaka ndio ule msafara tuliona unatoka ngome ya Ambross kabla ya sisi kuingia" alidakia Sandra.
"Sahihi walikuwa ni wao, hatujui wanakoelekea ila kwa mujibu wa maelezo yao niliwasikia wakisema ni kwenye kabila lenye ulinzi mkali alafu pia chupa ipo mikononi mwa chifu wa kabila hilo, huko ndiko Sultana na marehemu mumewe Jenerali Phillipo Kasebele walikwenda kuiifadhi chupa ya kijivu"
Alieleza jasusi Shadow. Kimya kikatawala kwa sekunde kadhaa.

"Jambo la muhimu hapo ni kufuatilia msafara wa hao watu wa Sultana, Mheshimiwa Rais unaweza kutusaidia tukawanasa kupitia satellite!?" Fungo alitioa wazo likiambatana na swali kwa Mheshimiwa Rais
"Hapana nafikiri naweza kujua ni wapi wanaelekea bila hizo satellite"
"Kivipi Mheshimiwa?"
"Wakati nafanya kazi na marehemu jenerali Phillipo Kasebele nakumbuka aliwahi kunieleza kuwa anamahusiano ya karibu na chifu wa kabila moja hivi sikumbuki vizuri jina la hilo kabila, hebu nisubirini nakuja mara moja ngoja nikaangalie kwenye mafaili yangu" Alisema Rais kisha akawa anapiga hatua kuelekea mlangoni.
"Mheshimiwa suburi kwanza" Mara Inspekta Aron aliongea wakati Rais akiwa mlangoni tayari kutoka, wote wanne wakageuka na kumtazama Aron.

"Nafikiri hilo kabila nalijua pia, baba aliwahi kunieleza" Alisema Aron kauli ikiyomfanya Rais asogee karibu yake kumsikiliza.
"Aliwahi kunipeleka huko nikiwa mdogo, nina hii alama mkononi alisema ni kama nembo ya hilo kabila walinichora wakati nikiwa huko na wazazi wangu nilikuwa mdogo sana sikumbuki kitu, baba amekuwa na mahusiano mazuri na hili kabila kwa muda mrefu" alieleza Inspekta Aron huku akiwaonyesha alama fulani ambayo ipo mkono wake wa kushoto chini kidogo ya kiwiko. maelezo ya Aron bado yaliibua maswali mengi vichwani kwa wanaomsikiliza.

"Kwa hiyo unajua jina la hilo kabila, ni kabila gani? liko wapi?" Aliuliza Jasusi Shadow
"Hapana sijui jina, ninachokumbuka baba alisema hilo kabila lipo ndani ya kisiwa" alieleza Inspekta Aron
"Yes nimekumbuka ni kisiwa, kisiwa cha BOBNIA" alidakia Mheshimiwa Rais
"Bobnia!?" Shadow, Fungo na Sandra waliuliza kwa pamoja halikuwa jina geni kwenye masikio yao
"Ndio kisiwa cha Bobnia marehemu aliwahi kunieleza kuhusu hilo nimekumbuka vizuri sasa" Rais alilisitiza. Wakati huo Fungo alifungua kompyuta yake na kuanza kuibonyeza kwa kasi sana, vidole vyote kumi vya mikono yake vilifanya kazi.

"Hebu oneni" alisema Fungo huku akigeuza uso wa kompyuta yake kuwaonyesha wenzake. Kilichoonekana ilikuwa ni ile alama ambayo pia ipo kwenye mkono wa kushoto wa Aron.

"Hii ni alama ya kabila la WATSAVO wanapatika kisiwa hicho cha BOBNIA"
Alieleza Fungo.
"Angalia taarifa zake tueleze vizuri kuhusu hicho kisiwa na hilo kabila"

"Wanasema Bobnia ni kisiwa kinachopatikana bahari ya hindi kilometa hamsini na nne kutokea ufukwe wa bahari kijiji cha Namtumbi upande wa kaskazini mashariki. Kabila la WATSAVO ni kabila maarufu linalopatikana katika kisiwa hicho. Ni kabila lenye tamaduni za ajabu sana na inaaminika kuwa kuna watu maalum ambao wanavyovibali vya kuingia na kutoka ndani ya kisiwa hicho , huwezi kwenda kienyeji . Watu waliolazimisha kuingia wamekuwa wakipotelea huko na hawakuwahi kuonekana. Ki ufupi ni kisiwa chenye maajabu, hata watafiti mbalimbali wamekuwa wakiogopa kwenda"
Alieleza Fungo.
"Hii ina maana gani, kwa nini marehemu alichagua kuipeleka chupa ya kijivu huko!?" Aliuliza Rais
"Nadhani ni kwa sababu ya usalama kama ulivyosikia sifa la hilo kabila pengine aliamini ikiwa huko haitofikiwa kwa urahisi"
"Tunafanyaje?" Aliuliza Jajusi Shadow
"Inabidi twende, Kikosi cha Sultana wameondoka leo hii na gari zao itawachukua siku mbiki kufika katika kijijini cha Namtumbi ndipo wapande boti kuelekea kisiwani" Alieleza Fungo
"Sawa ninyi mtaenda kwa helkopta mtafika hicho kijiji cha ufukweni kabla yao" Alieleza Rais
"Lakini sifa za hilo kabila mimi zinanitisha jamani"
"Sandra acha kuamini mambo ya kufikirika pengine ni hisia potofu za watu kuhusu hicho kisiwa"
"Unafikiri itakuwa rahaisi kuingia kisiwani na kisha tukaipata hiyo chupa?" Sandra aliuliza swali lingine
"Inabidi tupambane kwa kila hali, kumbuka tunafanya hivi kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wetu na Dunia yote kwa ujumla. Kwa maelezo niliyoyasikia hiyo chupa ipo kwa chifu wa kabila hilo. Tutatumia njia ya diplomasia kuzungumza naye isipofanya kazi tutatumia nguvu. Ndio maana mmeona hata watu wa Sultana wameondoka na siraha kama wanaenda vitani" Alieleza jasusi Shadow.
Kimya kilitawala huku kila mmoja akiwa anawaza kuhusu jukumu hilo jipya la kuifuata chupa ya kijivu ndani ya kisiwa cha Bobnia.

Je, nini kitafuata?
Osward anataka kumuonyesha nini Najma?
Ni nani anayemfuatilia Tino?
Vipi kuhusu Sharma Khumar na Annah?
Chupa ya kijivu ya ANTIDOTE ipo ndani ya kisiwa cha ajabu, hii ni kweli au ni imani kama Rais alivyosema.

TWENDE PAMOJA
ITAENDELEA...

Simulizi hii ni Tsh 1000 tu lipia kwa mpesa namba 0756862047 jina Saul au Airtel money namba 0788967317 jina Saul
Kisha njoo WhatsApp namba hzo hzo
 
Mimi nasoma riwaya ambazo naona zina page angalao 1000 na kuendelea .

Nawasubiria mpigwe alosto halafu mm naja natiririka tu.

Sitaki ujinga kbisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom