THE MODERN WAR: Simulizi ya kijasusi mapenzi na upelelezi

SIMULIZI RIWAYA

JF-Expert Member
Feb 19, 2022
415
1,274
THE MODERN WAR

(Vita ya kisasa)
Sehemu ya.........01
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

UTANGULIZI
Mwanzo ilikuwa ni vita rahisi sana, vita dhidi ya ndugu yangu wa damu aliyeenda kinyume na kanuni za maisha ya utu. Sikujua kwa kufanya hivi ningeamsha vita nyingine kubwa ambayo ipo juu kabisa ya uwezo wangu na uwezo wa nchi yangu. Vita na ndugu yangu imegeuka na kuwa vita ya ulimwengu mzima.

Cha ajabu ni kwamba ili kushinda vita hii haihitaji mtutu wa bunduki wala siraha yoyote. Natamani kuacha kupambana lakini siwezi kwa sababu tayari nimeshaanza. Kuendelea maana yake nimekubali kuwakabili maadui wenye rangi nyeupe ambao wamejipanga kwa zaidi ya miaka 10 kuhakikisha wanashinda.

Hatima ya Dunia yangu, Nchi yangu, Rais wangu, ndugu na familia yangu ipo mikononi mwangu. Kwa bahati mbaya ni kwamba licha ya nchi yangu kuwa na uwezo mdogo wa kupambana lakini imejikuta inatumika kama chungu cha kuandalia vita hii kali bila kujua, isitoshe tunapigana na kitu tusichokiona.

Naweza kusema sasa ni wakati wa mapenzi, sayansi na teknolojia kuipeleka Dunia vile inavyotaka.
Naam kwa mara ya kwanza historia inakwenda kuandikwa, historia ya vita ambayo haijawahi kutokea popote duniani, ndio sababu nasema hii ni VITA YA KISASA (THE MODERN WAR) niite Inspekta Aron"

SEHEMU YA KWANZA- (KIFO CHA SHAHIDI WA MWISHO)

SASA TUANZE SIMULIZI YETU....

"Mume wangu niue mimi, muache mwanangu aishi tafadhali bado ni binti mdogo naomba usimuue"
"Mama naogopa...!"

"Usiogope mwanangu kila kitu kitakuwa sawa, usijali sawa Annah"
"Mheshimiwa, mtihani ulionipa ni mgumu sana hivi nawezaje kumuua mwanangu au mke wangu, naanzaje kumwaga damu zao"

"Kama huwezi basi acha nitakusaidia mimi mwenyewe, nimekwambia chagua moja umuue mtoto wako au mke wako"

"Mheshimiwa siwezi tafadhali nipe adhabu nyingine, waache mke wangu na mwanangu waondoke nitafanya chochote unachotaka, niko chini ya miguu yako mkuu"

Haya yalikuwa ni mazungumzo ya watu zaidi ya watano waliokuwa ndani ya jengo moja chakavu lililokuwa limetelekezwa kabla ya ujenzi kukamilika, jengo hilo lilikuwa limejitenga pembeni kidogo ya mji.

Alikuwepo Dokta Isaack Gondwe ambaye ni waziri wa afya akiwa na vijana watatu nyuma yake ambao wote walikuwa wameziba nyuso zao kwa vitambaa vyeusi. Walikuwa wamesimama mbele ya familia moja ya watu watatu yaani baba mama na binti yao mdogo mwenye umri wa miaka 22 aliitwa Annah.

"Baba Annah nimekukabidhi bastola umuue mmoja kati ya mke au mtoto wako kisha nikuache uende lakini umeshindwa, basi acha vijana wangu wafanye kazi yao" alisisitiza Dokta Gondwe huku akibinua mabega yake kwa kejeri

Kwa mara nyingi tena Baba Annah aliinua juu mkono wake wa kulia ulioshikilia bastola akaielekeza walipokuwa wamesimama mke na binti yake Annah, hali akitetemeka alivuta pumzi ndevu na kuishusha taratibu, kijasho chembamba kikawa kinamtoka mzee huyo.

Mama Annah alimkumbatia binti yake akamziba usoni na kiganja cha mkono wake hakutaka mwanae aone kinachoendelea, naye akafumba macho kwa uchungu akiwa tayari kwa lolote litakalotokea.

Mara ghafula Baba Annah aligeuka kwa kasi akabadilisha uelekeo na kuilekeza bastola yake walipokuwa wamesimama Mheshimiwa dokta Isaack Gondwe na vijana wake, bila kusita akabinya kitufe cha kufyatua risasi huku akiwa amemlenga Dokta Isaack Gondwe kichwani lakini risasi haikutoka ,akajaribu tena mara ya pili na ya tatu lakini hali ikawa ni ile ile, baba Annah akahisi kuchanganyikiwa.

"Hahahah, ha ha ha, ha ha ha haaa" Dokta Gondwe alicheka tena kwa sauti kubwa sana, kisha akaongea
"Nilijuaa...! nilijua tu wewe ni msaliti, unajifanya mjanja sio? ona sasa umeumbuka mbele ya familia yako mzee hii ni mara ya pili unanisaliti, niliwaomba msitoe ushahidi wowote mahakamani lakini mkapanga kunigeuka wewe na familia yako pamoja na kukuhonga pesa nyingi bado ukapanga kunigeuka. Sasa unanisaliti tena kwa mara ya pili unataka kuniua, bahati mbaya bastola niliyokupa haina risasi hahahaha"

"Ulaaniwe Dokta Gondwe, mungu akulaani, utakufa kifo kibaya, wewe na watu wako wote mtakufaa, hata hicho cheo ulichonacho najua ni cha dhuruma, nakwambia utakufa" Baba Annah aliishia kutoa laana kwa mheshimiwa Dokta Isaack Gondwe mara baada ya kubaini kuwa hana ujanja tena.

"Acha makelele yako, laana kama hizo zilishakuja nyingi sana, hata marehemu mama yangu alinilaani tangu nikiwa tumboni lakini hadi leo hakuna laana iliyofanya kazi" alisema Dkt Gondwe huku akiinamisha kichwa chake chini kutega sikio kumsikiliza kijana wake mwingine ambaye aliingia ndani ya jengo hilo wakati anazungumza.

Kijana huyo hakuwa amefunika sura yake kama wengine, alimnong'oneza maneno kadhaa kwa takribani sekunde 30 hivi, Dokta Gondwe akaonekana kushtuka kiasi kisha akapaza sauti akifoka.

"Kwa nini, kwa nini kila siku yeye tu? hii inawezekanaje? kajuaje tuko hapa? huyu mdogo wako anataka nini? kwa nini unashindwa kumdhibiti? hivi askari ni yeye tu hakuna wengine aah!" Dkt Gondwe alifoka huku akiondoka, akapiga hatua kadhaa kisha akageuka tena.

"Unajua cha kufanya Tino, natangulia kwenye gari" alisema Dkt Gondwe kisha akatoka nje ya lile jengo.
Tino ambaye ndiye aliyeonekana kuwa na mamlaka kuliko vijana wengine wa Dkt Gondwe, alichomoa bastola iliyokuwa kiunoni kwake. Bila kuuliza alimfyatulia risasi Baba Annah, risasi iliyopenya sikio la kushoto ikatokea sikio la kulia, alifanya hivyo pia kwa Mama Annah, kisha akamalizia kumpiga risasi ya kifua Annah. wote wakaanguka chini na kupoteza maisha.

Lilikuwa ni tukio kubwa na zito, kuua watu watatu kwa wakati mmoja. Lakini kwa Tino ilikuwa ni tofauti kabisa, alifanya kwa urahisi sana kama anakunywa maji vile, ilionyesha wazi hii ilikuwa ni kazi aliyoizoea.
Baada ya kufanya hivyo Tino na wale vijana wengine waliandaa mazingira kuonyesha kuwa Baba Annah alimuua mke na mtoto wake kwa kuwapiga risasi kisha na yeye akamalizia kwa kujipiga risasi mwenyewe.

Baadae walitoka na kuingia ndani ya gari mbili zilizoegeshwa nje ya jengo hilo, wakaondoka kwa kasi kuwakimbia polisi ambao kwa mujibu wa maelezo ya Dokta Gondwe alimaanisha wapo njiani wanakuja na mmoja kati ya polisi hao ni mdogo wake na kijana wake wa kazi yaani Tino.
⭐⭐⭐

Ni kweli, dakika chache tu baada ya Dokta Gondwe na vijana wake kuondoka, gari za polisi zisizopungua sita zilifika na kufunga breki kali nje ya jengo hilo na punde polisi walishuka na kuanza kumiminika kwa kasi kuingia ndani ya jengo hilo huku siraha zao zikiwa mbele Ilikuwa ni ishara tosha kuwa polisi hawa walikuwa na taarifa kamili ya kile kilichokuwa kinaendelea ndani ya jengo hilo.

Walikagua vyumba vyote vya jengo hilo, hawakupata mtu yeyote zaidi ya miili ya Baba Annah mama Annah na Annah mwenyewe, kwa haraka haraka ilionyesha wazi kuwa Baba Annah ndiye aliyetekeleza mauwaji hayo kwani mkono wake wa kulia alishika bastola iliyotumika.

Lakini hicho sicho alichokuwa akikiona na kukiwaza Inspekta Aron, kijana ambaye ni polisi mpelelezi kutoka kituo cha kati Handeni. Yeye aliyatazama mazingira ya mle ndani kwa utulivu wa hali ya juu, akaitazama ile miili mmoja baada ya mwingine huku akichukua baadhi ya vielelezo muhimu kama ilivyokuwa ada kwa polisi wengine.

"Tumempoteza shahidi mwingine" Alisema Inspekta Jada, polisi ambaye alikuwa akifanya kazi kwa ukaribu sana na Aron. "Yah! tumechelewa kidogo sana, tungewahi tungeweza kuwaokoa pengine" alisema Aron huku akisogea pembeni pamoja na Jada wakiwaacha polisi wengine wakiendelea na kazi.

"Huenda walipata tena taarifa kama tunakuja" Alisema Jada
"Usiseme huenda, huo ndio ukweli wenyewe Inspekta Jada hii serikali ina watu wa hovyo sana" Aron alilalamika "Usijali Aron jitihada zako zitazaa matunda siku moja, ki ufupi unajituma sana, uwe na subra siku moja tutawakamata wote"

"Inshallah iwe hivyo, lazima nitamkamata Tino"
"Mmh! unahisi kaka yako Tino kahusika kwenye hili tukio pia"
" Ndiyo lazima alikuwepo hapa, subiri uone" Alisema Inspekta Aron akachukua simu yake akaitafuta namba aliyoihifadhi kwa jina la 'Bro Tino' akapiga. Simu iliita kwa dakika kadhaa bila kupokelewa mwisho ikakata, akapiga tena.
⭐⭐⭐

Upande wa pili Tino na bosi wake ambaye ni Waziri wa afya Mheshimiwa Dokta Isaack Gondwe tayari walishafika mjini. Tino akiwa ndiye dereva alikuwa ameegesha gari pembeni ya barabara na pembeni ya gari hiyo kulikuwa na gari nyingine ya serikali V8 ilikuwa imepaki ikimsubiri Dokta Gondwe ambaye bado alikuwa na mazungumzo na kijana wake tegemezi Tino.

"Tino, kama sikosei hii ni mara ya nne kama sio ya tano nakwambia kuhusu huyu mdogo wako Inspekta Aron unaemlealea sana, hili ni bomu ambalo litakuja kutulipukia baadae" Dkt Gondwe aliongea kwa msisitizo

"Usijali bosi, huyu ni mdogo wangu najua namna ya kumdhibiti niachie mimi, kuwa na amani bosi" Tino aliongea kwa kujiamini huku akipiga jicho pembeni kuitazama simu yake iliyokuwa ikiita mpigaji akiwa ni Aron mdogo wake.

"Haya mimi nakwenda, tayari tumeshaua mashahidi wote nina hakika tutashinda kesi mahakamani na mkwe wangu Osward atakuwa huru, lakini jua vita yetu bado ni kali sana na ndio kwanza tunaanza"
"Sawa mkuu"

Dkt Isaack Gondwe alishuka kwenye gari akapiga hatua na kuingia kwenye gari nyingine ile V8 dereva akawasha gari wakaondoka. Tino aligeuka na kuitazama simu ambayo ilikuwa ikiita kwa mara ya pili sasa, akapokea.

"Nambie dogo"
"Ulikuwa hapa Tino, ni wewe tena si ndiyo?" Inspekta Aron alisikika upande wa pili akiuliza
"Wapi mbona sikuelewi unazungumzia nini?"

"Najua unanielewa vizuri bro, sasa sikia nakuhakikisha kwamba lazima nitakukamata, nitathibitisha uchafu wako wote, mtafungwa wewe pamoja na mtandao wako mzima"

"Come down mdogo wangu, punguza vitisho huna ushahidi wowote wa kunifunga na hautokuja kufanikiwa kamwe, sahau" "Nisikilize kwa makini kaka labda nisiwe hai, yaani kwa mikono yangu nitakupeleke je..."
"Kaa kimya Aron huna faida yoyote wewe, nahangaika usiku na mchana kutafuta mamilioni ya pesa kwa ajili ya matibabu ya mama yetu, lakini wewe unafanya nini? unahangaika kutaka kunizuia, unaakili kweli wewe?"

"Mama yangu hawezi kuendelea kutibiwa kwa pesa zako chafu kaka, hata angekuwa anajitambua ninauhakika asingekubali hili"

"Kwa hiyo unatakaje, nimuache afe?"
"Kufa au kupona kwa mama yangu ni mpango wa Mungu sio wako Tino"
"Ni mama yetu sio mama yako, kumbuka hilo" alisema tino kisha akakata simu kwa hasira

"Vipi amesemaje?" Aliuliza Inspekta Jada mara tu baada ya kukata simu. "Kauli zake ni zile zile za kila siku, anadai anatafuta hela kwa ajili ya mama kule hospitali" Aron alijibu kinyonge.

"Pole Aron, nakuonea huruama sana, mungu akufanyie wepesi ni miezi sita mpaka sasa unapambana kwa ajili ya matibabu ya mama yako gharama ni kubwa lakini bado kaka yako naye anazidi kukuchanganya" alisema Inspekta Jada akionekana kuguswa na hali aliyokuwa akiipitia Inspekta Aron. Kabla Aron hajazunguza chochote mara kuna askari alionekana akikimbia kuwafuata, akafika na kusimama mbele yao huku akihema kwa nguvu.

"Vipi kwema?" aliuliza Aron akionekana mwenye shauku ya kujua kilichomleta, vivyo hivyo kwa Jada.
"Yu..yule binti kule nda..ndani ha..hajafa ni mzima" alisema yule askari kauli iliyowafanya Aron na Jada watazamane.

Je, nini kitafuata?
Nini hatima ya Vita kati ya ndugu hawa wawili yaani Aron na Tino?
Kwa nini Tino yupo karibu na Waziri wa afya?
Annah hajafa ni mzima huu unaweza kuwa ushahidi wa mwisho wa Inspekta Aron?
Kwa nini VITA YA KISASA?

Hii ni sehemu ya kwanza, majibu ya maswali haya utayapata ndani ya simulizi hii maridhawa iliyojaa visa vingi vya kusisimua. Mauaji, tamaa, mapenzi, urafiki, hila,chuki, drama, vita, usaliti, siasa, visasi, mahaba, kushinda na kushindwa pamoja na mambo mengine yasiyotazamiwa bila kusahau LOVE STORY kali ndani yake.

Naam hii ndio MODERN WAR(vita ya kisasa)
 
THE MODERN WAR
(vita ya kisasa)
Sehemu ya..........02
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047.

02-( KIKAO CHA SIRI)
ILIPOISHIA 01...
"Vipi kwema" aliuliza Aron akionekana mwenye shauku ya kujua kilichomleta, vivyo hivyo kwa Jada.
"Yu..yule binti kule nda..ndani , ha..hajafa ni mzima" alisema yule askari kauli iliyowafanya Aron na Jada watazamane

SASA ENDELEA....
"Nini? Unauhakika?" Aliuliza Aron
"Ndiyo afande, yule binti ni mzima hajafa"
Haraka Jada na Aron walikimbia kuelekea ndani ya lile jengo kwenda kuhakikisha ukweli wa taarifa hiyo
"Jada ita gari ya wagonjwa upesi" Alisema Aron huku akiendelea kukimbia lakini mara akasimama na kumtazama Jada ambaye tayari alishatoa simu mfukoni.

"Hapana usipige, mwite Dokta Zyunga afike hapa haraka na vifaa vyote muhimu tutampeleka hospitali kwa siri hatakiwi kujua mtu mwingine zaidi yetu" alisema Inspekta Aron, Jada akafanya kama alivyoagizwa.


Nusu saa baadae Inspekta Aron mdogo wake Tino alikuwa ndani ya hospitali kubwa ya kimataifa maarufu kama MOUNTENIA HOSPITAL, Aron alikuwa amesimama nyuma ya mlango mkubwa wa kioo uliokuwa na maandishi makubwa juu yake yaliyosomeka 'MAJOR THEATER'(Chumba cha upasuaji mkubwa). Aliwatazama madaktari waliokuwa wakiendelea kupambana kuyaokowa maisha ya Annah ambaye alifikishwa hospitalini hapo kwa siri kubwa. Tayari Annah alikuwa ameshawapoteza wazazi wake wote wawili waliouwawa kikatili masaa machache yaliyopita ikiwa ni agizo la Waziri wa afya Dokta Gondwe.
Madaktari walifanikiwa kuitoa risasi iliyokuwa imezama upande wa kulia wa kifua cha Annah. Kwa bahati nzuri risasi haikuwa imeleta madhara wala kugusa viungo muhimu kama mapafu na ini, kwa sasa jitihada nyingine za kibingwa zilikuwa zikiendelea kuyanusuru maisha ya binti huyo yatima.
Inspekta Aron aliendelea kusimama pale nje huku akimuomba mungu wake ayaokoe maisha ya binti huyu muhimu sana kwake.
"You're my last hope Annah, please don't die"(wewe ndio tumaini langu la mwisho Annah tafadhali usife) Alisema Inspekta Aron huku akiwa amekutanisha mikono yake kumuomba mungu
Annah alikuwa ndiye shahidi pekee aliyehai dhidi ya kesi ngumu ya mauaji aliyofanya kijana Osward ambaye ni mkwe wa Dokta Gondwe. Kesi hiyo ilikuwa ni daraja pia la kuwatia hatiani kaka yake Tino pamoja na Waziri wa afya Dokta Gondwe ambao wamekuwa wakifanya matukio mengi ya kiharifu lakini anashindwa kuwatia nguvuni kwa sababu ya kukosa ushahidi.


Upande wa pili ndani ya hoteli moja kubwa ya kifahari Waziri wa afya Mheshimiwa dkt Isaack Gondwe alionekana akiwa katika kikao cha siri yeye pamoja wa wazungu watatu, alikuwepo pia Rais mstaafu wa awamu ya nne mheshimiwa Profesa Cosmas Kulolwa pamoja na mkemia mkuu wa serikali bwana Andiwelo Katabi. Kilikuwa ni kikao cha siri kilichobeba ajenda nzito mno.
Wakati wakiendelea na mazungumzo mara kuna ujumbe mfupi wa maandishi uliingia kwenye simu ya Dkt Isaack Gondwe, akaufungua haraka na kuusoma.

,,,,,Yule binti Annah hajafa bado yuko hai, Inspekta Aron kamchukua kaondoka naye kwa siri hatujui alikompeleka, nitakupa taarifa zaidi naendelea kufuatilia,,,,,,,

Dkt Isaack Gondwe alikurupuka kutoka kwenye kiti akasimama ghafula kiasi cha kuwafanya watu waliokuwepo ndani ya chumba hicho wamtazame kwa pamoja.
"Aah! excuse me" (kumradhi) alisema Dkt Gondwe, akapiga hatua na kutoka nje ya kile chumba haraka.
Dokta Gondwe aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali akatoa simu yake ndogo Samsung, akaibonyeza haraka haraka akapiga namba aliyokuwa ameihifadhi kwa jina la 'SELE GEREZA' simu iliita kwa sekunde kadhaa mwisho ikapokelewa upande wa pili.

"Naam Mheshimiwa Waziri" Mkuu wa gereza la Kanondo SP Seleman alizungumza upande wa pili wa simu
"Tafadhali naomba kuongea na Osward sasa hivi kuna dharula"
"Mheshimiwa kwa sasa wafungwa wapo kantini wanakula, subiri kama dakika 15 hivi"
"Afande Sele hivi unaelewa mtu akisema ni dharula, kwanza Osward sio mfungwa yupo hapo kusubiri tarehe ya kesi yake kusikilizwa"
"Anatuhuma za mauaji ndio sababu yuko hapa, najua unaelewa taratibu zetu Mheshimiwa Waziri sipendi tubishane subiri kidogo nijaribu kukusaidia"
"Sawa nasubiri"
Simu ikakatwa, Dokta Gondwe akabaki amesimama nje ya kile chumba ambacho ndani yake kulikuwa na kikao cha siri kikiendelea. Habari za Annah kuwa hai zilimchanganya sana mbaya zaidi wakati wanafanya mauaji yeye na Tino hawakuwa wamefunika sura zao hivyo ilikuwa ni hatari kubwa kama Annah atanusurika kifo.
"Doctor, there's something wrong?"(Daktari kunakitu hakipo sawa) Dokta Gondwe alishtushwa na sauti ya mzungu mmoja aliyetoka nje kumtazama.
"Nothing wrong Mr Codrado, two minutes please am coming"(Hakuna shida bwana Codrado, dakika mbili tafadhali nakuja)
"It's you're time to talk Doctor Gondwe, let's go inside please we don't have time"(ni zamu yako kuongea Dokta Gondwe, tuingie ndani tafadhali hatuna muda) alisisitiza yule mzungu na mara hiyo simu ya Dokta Gondwe ikaita.
"Dakika moja nakuja"
"What?"(nini?)
"Moja tu moja bwana Codrado"
"What do you mean!?"(unamaanisha nini!?) aliuliza Codrado akiwa hajaelewa kiswahili
"One minute"(dakika moja) Alisema Dkt Gondwe, Codrado akarudi ndani akionekana kutofurahishwa na alichokifanya Waziri wa afya. Punde tu baada ya Codrado kuondoka dkt Gondwe akapokea simu haraka
"Baba mkwee" sauti nzito ya kiume ilisikika upande wa pili wa simu ile
"Ndiyo Osward ni mimi, tafadhali sogea sehemu salama tuzungumze jambo"
"Nimeshasogea baba hivi ni kweli mmeshindwa kufanya chochote hadi sasa nakalibia kumaliza miezi miwili huku gerezani" Osward alilalamika
"Usijali mwanangu tupo kwenye hatua za mwisho mashahidi wote tumesha wamaliza nakuhakikishia safari hii tukirudi tena mahakamani unaachiwa huru"
"Asante mkwe nikitoka tu cha kwanza nafunga ndoa na binti yako Najma"
"Sawa lakini hilo tutaongea ukitoka, kuna kitu nataka kukuliza"
"Uliza tu baba mkwe"
"Hivi wakati unafanya mauaji yule binti wa yule mzee naye alikuona?" Aliuliza dkt Gondwe akiwa na shauku ya kusikia jibu kutoka kwa Osward.
"Kale kabinti wanakaita mmm! Annah si ndiyo?"
"Ndiyo Annah huyo huyo"
Osward alibaki kimya kwa muda akijalibu kuvuta kumbukumbu siku aliyofanya mauaji.
"Kwa kweli kumbukumbu zangu hazipo sawa baba mkwe, sikumbuki kitu kuhusu Annah"
"Dah! hii ni kazi nyingine sasa"
"Kivipi mzee?"
"Tulifanikiwa kuwakamata familia nzima tukawapiga risasi wote lakini kwa bahati mbaya Annah hajafa yupo kwenye mikono ya Inspekta Aron sasa hivi"
"Aron yule mdogo wake na Tino"
"Ndiyo, jamaa anatusumbua sana yule"
"Sasa sikia baba mkwe, uweni wote, muueni huyo binti haijarishi aliniona au hakuniona muueni na huyo Inspekta Aron hapo mtakuwa mmemaliza kila kitu" Osward aliongea kwa msisitizo.

"Sawa tutafanya hivyo lakini kuhusu kumuua Inspekta Aron hilo tusubiri kwanza, baadae Osward nipo kwenye kikao muhimu nitakupigia tena" Alisema Dkt Gondwe kisha akakata simu.

Osward alibaki amesimama wima akionekana kutofurahishwa na kauli ya mwisho kutoka kwa mheshimiwa Waziri wa afya. Osward alimchukia sana Inspekta Aron huyu ndiye alikuwa chanzo cha yeye kufunguliwa tuhuma za mauaji na alikuwa akipambana kwa nguvu zote kukusanya ushahidi kuhakikisha Osward anafungwa. Osward aliamini kama Inspekta Aron atakufa basi kila kitu kitakuwa rahisi kwake.

"Wanamlealea kwa sababu ni mdogo wake na Tino si ndiyo, basi mimi siwezi kuendelea kuvumilia" Osward aliongea kwa jazba huku akibinyabinya simu ya mkuu wa gereza, akapiga namba fulani na kuweka simu sikuoni, iliita kwa muda mwisho ikapokelewa.

"Oya big! Osward hapa naongea, nakuhitaji hapa magereza chapu kwa haraka" Osward aliongea kwa kifupi kisha akakata simu, alitembea taratibu hadi pale alipomuacha mkuu wa gereza SP Seleman akamrudishia simu yake.

"Vipi rudi sasa kwa wenzako mbona umekaa tena, mfuata askari yule pale anakusubiri akusindikize" alisema SP Seleman baada ya kuona Osward anakaa badala ya kurudi kwa wafungwa wenzake.
"Kun mtu nimemwita nina mazungumzo naye muhimu"
"Sikiliza Osward, najua wewe ni mtu mkubwa unawatu huko nje baba yako mzee Matula ni tajiri mkubwa pia Waziri wa afya anakukingia kifua lakini nataka kukwambia ukiwa hapa jaribu kuwa na nidhamu, wewe hauna tofauti yoyote na wenzako waliopo humu ni lazima ufuate kanuni na taratibu zetu, kukupa simu yangu ni heshima tu kwa mheshimiwa Waziri na si vinginevyo, tabia zako tangu umeingia hapa zimekuwa ni mbovu na hazivumiliki tena naongea kama mkuu wa gereza" SP Seleman alifoka akimtazama Osward kwa macho makali. Osward hakujibu chochote, alimtazama tu SP Seleman namna alivyokuwa akifoka, akatabasamu.
"Wapi nitakutana na mgeni wangu?" Osward aliuliza akionyesha wazi kuwa maneno ya Seleman hayajamuingia hata kidogo.
SP Seleman alitoa ishara fulani kwa askari aliyekuwa karibu, askari akasogea na kumtaka Osward amfuate. Wakaongozana hadi eneo maalumu ambalo wafungwa hukutana na watu wengine kutoka nje ya gereza kama vile ndugu na jamaa zao wanaokuja kuwatembelea.
Osward alimkuta mtu aliyewasiliana naye kwenye simu dakika chache zilizopita tayari ameshafika amekaa anamsubiri. Alikuwa ni mwanume mnene, mrefu mweusi karibu kila mahali isipokuwa viganja vya mikono yake pekee. Mwili wake ulikuwa umejazia na endapo ukimuona hauna sababu ya kujiuliza mara mbili mbili kuwa huyu ni mtu wa mazoezi tena sio mazoezi tu bali mazoezi makali.

"Ooh Big' umeshafika tayari"
"Yeah, unanijua mimi mambo yangu nayaendesha kizungu"
"Hahahah kama kawaida yako"
"Vipi unatoka lini humu? kambini mambo hayaendi bila wewe mkuu" aliuliza yule bwana wa miraba minne
"Soon nitaungana na ninyi, sasa sikia kuna kazi ndogo hapa nataka nikupe"
"Ipi hiyo nambie"
"Unamjua yule askari jau ambaye ni chanzo cha mimi kuwa huku"
"Ee si yule mdogo wake Tino, anaitwa Aron"
"Yes! huyo huyo"
"Vipi tumuondoe?"
"Hayo ndio majibu, bila hivyo nitaozea humu ndani, yule jamaa jau sana wanamlealea kwa sababu ni mdogo wake Tino"
"Haina noma Osward ni hilo tu au kunalingine?"
"Ni hilo tu ila hakikisha kifo chake kisilete utata si unamjua kaka yake naye ni balaa jingine sitaki mambo mengi mimi" Osward alisisitiza

Je nini kitafuata?
Aron atakuwa salama?
Na je atafanikiwa kumlinda Annah?
Vipi kuhusu kile kikao cha Waziri wa afya na wazungu kutoka Mexico?

ITAENDELEA...
 
MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..........03
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

03- (PICHA YA NGONO)
ILIPOISHIA...02
"Hayo ndio majibu, bila hivyo nitaozea humu ndani, yule jamaa jau sana wanamlealea kwa sababu ni mdogo wake Tino"
"Haina noma Osward ni hilo tu au kunalingine?"
"Ni hilo tu ila hakikisha kifo chake kisilete utata si unamjua kaka yake Tino naye ni balaa jingine sitaki mambo mengi mimi" Osward alisisitiza

SASA ENDELEA...

"Usijali shughuli yangu unaijua huna haja ya kunieleza sana ila nina zawadi yako hapa" Alisema Big
"Ipi tena?" Osward aliuliza na mara hiyo Big alitoa picha ndogo mfukoni kisha akamkabidhi.
Osward aliitazama ile picha huku akitabasamu. Ilikuwa ni picha ya mwanamke mmoja mrembo sana.

"Najma! Najma! malkia wangu, hahaha nitaua mtu tena kwa ajili yako, vipi anaendeleaje huko mtaani?"
"Yupo tu kama kawaida kwao geti kali, tangu arudi kutoka Nairobi baba yake Dokta Gondwe anamfungia ndani hamruhusu kudhurula hovyo"

"Hahaha! Najma kama Najma, Basi poa poa Big' asante nenda kafanya kazi tutaonana tena" alisema Osward na mwisho wakaagana na Big mwanaume wa miraba mnne aliyepewa jukumu la kumuua Inspekta Aron


Upande wa pili Tino alionekana akiingia ndani ya duka moja kubwa la nguo, lilikuwa ni duka lake binafsi lililoko katikati ya mji. Alimsalimia mfanyakazi wake ambaye aliitikia salamu ile kisha wakapeana ishara fulani ambayo ni wao tu ndio walikuwa wakielewa.

Tino akapiga hatua hadi kwenye kona moja ya duka hilo, akaangaza macho huku na huku, hakuna aliyekuwa akimuona, akabinya kitufe fulani kilichokuwa kimejificha nyuma ya nguo, mara ukaonekana mlango uliokuwa ukifanana na ukuta wa chumba hicho ukifunguka kuelekea ndani, Tino akaingia haraka na kuufunga.

Sasa alikuwa ndani ya chumba kingine ambacho kilikuwa ni chumba chake cha siri, kilikuwa ni chumba kikubwa sana mfano wa ofisi, huko kulikuwa na watu wengine saba wa kike na wa kiume, wote walikuwa bize na kompyuta, hakuna aliyekuwa amekaa bure kila mmoja alikuwa makini na anachokifanya.

"Karibu bosi" mmoja wa wale vijana alimkaribisha Tino.
"Asante, vipi kuna mteja?"
"Ndiyo wapo wawili, lakini wa tatu Bosco kasema umuangalie mwenyewe kwanza"
"Mmh kwa nini?"
"Sijajua lakini nahisi anasababu za muhimu" alijibu yule kijana ambaye ndiye aliyeonekana kiongozi wa wenzie katika ofisi hiyo ya siri ya Tino.

Hii ilikuwa ni ofisi ambayo ilikuwa ikimuingizia Tino kiasi kikubwa cha pesa ingawa kazi aliyokuwa akiifanya katika ofisi hii haikuwa harali.
Kabla ya kufungua ofisi hiyo Tino alizunguuka katika nyumba za wageni 'guest' mbalimbali katika mikoa tofauti tofauti, kila chumba alichoingia Tino alitegesha kamera za siri ambazo ilikuwa ni ngumu sana kuziona. Alifanya hivyo katika maeneo na nyumba za wageni tofauti tofauti na baada ya hapo akawa na mitambo maalumu ambayo kupitia kamera zile aliweza kuona kila kinachoendea ndani chumba husika.

Tino alikuwa akikusanya video za watu wengi tofauti tofauti waliokuwa wakiingia na kutoka kwenye vyumba alivyotega kamera zake. Tino aliwataka hasa wale wanaoingia na kufanya mapenzi ndani ya vile vyumba, hivyo akawa na picha/video nyingi za ngono, akishazikusanya anaanza kumfuatilia mtu mmoja baada ya mwingine mpaka anahakikisha anapata mawasiliano yake. Baada ya hapo Tino hutoa vitisho kwa muhusika akimtaka alete kiasi cha pesa atakachompangia na kama asipofanya hivyo basi atazisambaza video zake chafu mitandao.

Hivi ndivyo namna ofisi ya Tino ilivyokuwa ikifanya kazi, alijipatia pesa nyingi sana ndani ya muda mfupi. Haikuwa rahisi mtu kukubali picha au video zake za ngono zisambazwe mtandaoni, walifanya kila namna na kulipa pesa anayoihitaji Tino.

"Ukitoa taarifa polisi, au kwenda kulalamika kokote, basi utakuwa umevunja makubaliano yetu kinachofuata picha na video zako zitakuwa mtandaoni" hii ndio kauli aliyozoea kuitoa mara kwa mara kuwaziba mdomo wahusika.

Licha ya kwamba Tino alikuwa akifanya kazi chini ya Waziri wa afya Mheshimiwa dkt Isaack Gondwe lakini kazi hii ndio iliyokuwa ikimuingizia pesa kwa kiasi kikubwa. Kuwa karibu na Waziri wa afya alikuwa na sababu zake nyingine tofauti.

"Umesema kuna video ngapi leo" Tino aliuliza swali lake kwa mara nyingine.
"Ziko video za wateja wawili, lakini moja Bosco kasema uitazame kwanza"
"Sawa mmeshapata mawasiliano ya wahusika?"
"Tumepata ya mmoja, huyu wa pili bado tunaendelea kumsaka"
"Siku hizi mmepunguza kasi sijui kwa nini, kuna video ya X ipo hapa kwa zaidi ya siku tatu ila mapaka leo hamjampata muhusika na jamaa anaonekana anapesa ndefu sana"
"Ni kweli bosi ule mfumo wa serikali tulioudukua ukawa unatusaidia kupata namba za hawa watu siku hizi hatuutumii tena walibadilisha namba ya siri"
"Sawa basi tuanze na huyo mtu mliepata namba zake"

Tino na vijana wake walisogea hadi kwenye meza ya kompyuta ambayo ilionekana kuwa kubwa zaidi ya zingine wakakaa kwa kuizunguuka. Bila kuchelewa wakachukua namba za yule mtu ambae video yake ya ngono ilikuwa mikononi mwao, wakapiga simu.

Simu iliita kwa muda lakini haikupokelewa, walijaribu mara kadhaa lakini hali ikawa ni ile ile.

"Basi achana naye, mtumie baadhi ya picha WhatsApp kisha mpe vitisho akifungua atatutafuta mwenyewe" Alisema Tino na kusimama

"Bosco nimeambiwa kuna video unataka niitazama kwanza si ndiyo, ina nini kwani?"
"Aah ee..ni..ni vema ukaitazama kwanza" alijibu Bosco kijana wa Tino akionyesha kutojiamini kabisa, hali hii ilimfanya Tino kuingiwa na wàsiwasi, haikuwa kawaida ya Bosco kuwa katika hali ile, alikuwa ni kijana jasiri na mzoefu wa kucheza na kompyuta, alimtegemea.

"Hebu twende tukaone" alisema Tino, wakaongozana hadi ilipo kompyuta aliyokuwa anaitumia kijana Bosco, akaifungua na kuitafuta ile video.

"Kaa utazame bosi" alisema Bosco huku akimpisha Tino akakaa kwenye kiti kisha akaicheza ile video.

Kadri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo hali ya Tino ilizidi kubadilika, hakuamini kile anachokiona. Ilikuwa ni video ikimuonyesha mke wake wa ndoa Jesca akiwa anafanya mapenzi na mwanaume mwingine na baada ya kumuangalia mwanaume yule kwa makini alikuwa si mwingine bali bosi wake yaani mheshimiwa Dkt Isaack Gondwe Waziri wa afya.

Tino alisimama akionekana kuchanganyikiwa akaikatisha ile video, hakuweza kustahimili kuendelea kuitazama, jasho lilianza kumtoka huku mikono yake ikitetemeka. Akaicheza tena ile video kuhakikisha alichokiona, hali ilikuwa ni ile ile alichokiona mwanzo kilikuwa ni kile kile hata sasa mkewe na bosi wake Dkt Gondwe walikuwa ndani ya huba zito. Maumivu aliyoyapata moyoni hayakuwa na mfano, alimpenda mno mke wake Jesca. Wakati huo simu yake ilikuwa ikiita, alipotazama mpigaji alikuwa ni bosi wake Dkt Isaack Gondwe. Bosco alitamani kumshika bosi wake amfariji lakini aliogopa, Tino alikuwa kwenye hali mbaya sana.
Aliuma meno kwa hasira huku mikono yake ikitetemeka akajikaza na kuipokea simu ile.

"Tino kijana wangu ni nini unafanya? mbona umekuwa mzembe sana siku hizi" Dkt Gondwe alisikika upande wa pili wa simu.

Tino ambae safari hii macho yake yalikuwa yamebadilika na kuwa mekundu alipata kigugumuzi cha mdomo, akashindwa ajibu nini, picha ya mkewe akiwa amelala na mtu anaeongea naye kwenye simu wakati huu bado haikufutika kichwani kwake.

"Unanisikia lakini, mbona uko kimya kuna dharula Tino tena dharula kubwa sana naomba tukutane nyumbani kwangu baada ya nusu saa namalizia kikao hapa" alisema Dkt Gondwe.
"Sawa bosi" alijibu Tino kisha simu ikakatwa.
***********
{TANGAZO:- Epuka matapeli simulizi hii imetungwa na SAUL DAVID simu 0756862047, Tafadhali usinunue kwa mtu mwingine tofauti }
******-*-
"Iweke hii video kwenye simu yangu kisha uifute, mimi na wewe ndio tunajua kuhusu hili wengine wasijue chochote" Tino alitoa maagizo kwa kijana wake Bosco kisha akatembea haraka kuelekea ilipokuwepo bafu na choo ya ofisi hiyo ya siri.

Akiwa huko Tino alisimama mbele ya kioo kimoja kikubwa akawa anajitazama hali akiwa amekunja ngumi na kuuma meno yake kwa hasira, alionekana kuchanganyikiwa kupita kiasi.
Alifungua droo ya kabati moja iliyokuwa pembeni ya kile kioo akatoa bomba la sindano na kijichupa kidogo cha dawa, akajifunga mkono wake kisha akavuta kiasi fulani cha ile dawa na kujidunga kwenye mshipa.
Baada ya hapo Tino akavuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu kisha akaendelea kujitazama kwenye kioo huku akizungumza.

"Usijali Tino hili nalo litapita, jambo unalopigania ni kubwa mno, hauwezi kufanikiwa kirahisi, lazima upitie changamoto kama hizi" Tino alikuwa akijisemea mwenyewe huku akijitazama kwenye kioo, aliongea kwa uchungu sana kiasi cha kuifanya midomo yake itetemeke na macho kuzidi kuwa mekundu.

"Usifanye lolote Tino utapoteza muelekeo tulia kama hakujatokea chochote, najua mke anauma lakini vumilia, muda utafika utalipa kisasi, umevumilia mangapi mpaka sasa, usife moyo Tino, usijaribu kumuondoa dkt Gondwe huyo ndio njia yako kuelekea mafanikio, kama mipango yako ikikamilika nakuhakikishia utaitikisa Dunia nzima, mataifa yote kutoka pande zote za Dunia wataliita jina lako Tino Phillipo Kasebele. Pambana Tino pambana bila kurudi nyuma siku ukiupata ufalme wako hakuna atakaeweza kukuzuia, sio mmarekani wala sio mchina wote watasafiri na kuja kukupigia magoti, pambanaa..." baada ya kusema hivyo Tino alicheka kwa sauti kubwa sana, hii ilionyesha wazi kuna jambo lingine kubwa na la siri alikuwa akilifanya kijana huyu ukiacha ile kazi anayoifanya chini ya Waziri wa afya dkt Gondwe, ukiacha pia kazi anayoifanya ya kurekodi picha za ngono kwa wateja wanaoingia vyumba vya wageni alivyotegesha kamera, bado ilionyesha kuna kitu kingine kikubwa anakifanya.

Ni kitu gani hicho?
Hili ni balaa jingine ndani ya MODERN WAR...
Ukiacha ule mpango wa Osward kutaka kumuua Inspekta Aron, vipi kuhusu Tino na Waziri wa afya?
Tino atafanya nini?
Bosi katembea na mkewe...
Ni mpango gani alionao kiasi cha kuamini ataitikisa Dunia nzima?

ITAENDELEA...THE MODERN WAR
(vita ya Kisasa)
Sehemu ya...............04
Mtunzi: saul david
Email: saulstewarty@gmail.com

04-(PICHA TATU ZA X)
ILIPOISHIA...03
baada ya kusema hivyo Tino alicheka kwa sauti kubwa sana, hii ilionyesha wazi kuna jambo lingine kubwa na la siri alikuwa akilifanya kijana huyu ukiacha ile kazi anayoifanya chini ya Waziri wa afya dkt Gondwe, ukiacha pia kazi anayoifanya ya kurekodi picha za ngono kwa wateja wanaoingia vyumba vya wageni alivyotegesha kamera, bado ilionyesha kuna kitu kingine kikubwa anakifanya.

SASA ENDELEA...
Kicheko cha Tino kiliwafanya wale vijana ndani ya ofisi yake watazamane kwa macho ya kuulizana, hawakujua bosi wao kapatwa na nini isipokuwa Bosco peke yake, sekunde chache baadae Tino alitoka.
"Vipi umeshaifuta hiyo video kwenye kompyuta yako?" Tino alimuuliza kijana wake Bosco
"Ndiyo bosi nimeifuta na kuiweka kwenye simu yako kama ulivyosema" alijibu Bosco
Tino alitulia kwa muda ni kama alikuwa akitafakari jambo fulani muhimu, baada ya sekunde kadhaa akasogea na kukaa pembeni ya Bosco.

"Nisikilize Bosco, irudishe tena hiyo video kwenye kompyuta yako, mimi na wewe tunakwenda kucheza mchezo hatari hakikisha hakuna mwingine anajua, nitakuwa nakupa maelekezo nini cha kufanya sawa" alisema Tino akionekana bado ni mtu mwenye maumivu makali licha ya kujaribu kujisahaurisha lakini taswira ya mkewe akifanya mapenzi na bosi wake mheshimiwa Dkt Isaack Gondwe haikufutika kichwani kwake.

"Nimekuelewa bosi" alijibu Bosco, Tino akasimama na kumpiga piga mgongoni huku akitabasamu.
"Sasa ni wakati wako wa kucheza mziki wangu mheshimiwa Dokta Gondwe" Tino aliwaza huku akiwa bado ameachia tabasamu lenye maumivu ndani yake.


Upande wa pili katika hospitali ya Mountenia bado madaktari walikuwa wakiendelea kupambana kuyaokowa maisha ya binti Annah. Yalikuwa yamepita masaa manne mpaka sasa Inspekta Aron ambaye ni mdogo wake Tino bado hakubanduka pale mlangoni hata kidogo, alitamani kushuhudia kwa ukaribu kila kilichokuwa kinaendelea kwa binti huyo muhimu sana kwake. Mwisho oparesheni ilimalizika, mlango wa chumba cha upasuaji ukafunguliwa.

"Dokta Zyunga niambie, kazi imekwendaje? huyu mwanamke atapona?" Inspekta Aron aliuliza maswali mfurulizo mara tu baada ya daktari kutoka.

"Usijali Aron sisi tumefanya kwa upande wetu, mungu ndio ataamua hatima ya Annah, siwezi kukuahidi chochote kwa sasa tusubiri" alieleza Dokta Zyunga
"Asante daktari naamini atapona"
"Endelea kumuombea Mungu atamsaidia, Enhe! sasa taratibu za ulinzi zipoje nakumbuka umeniambia huyu mgonjwa ni wa siri anatakiwa kulindwa pia si ndiyo?"
"Ndiyo, askari wangu wako hapa, tuelekeze tu chumba atakacholazwa Annah sisi tutaweka utaratibu mzuri wa kumlinda"
"Sawa Inspekta, nifuate"

Dokta Zyunga na inspekta Aron waliongozana hadi kwenye chumba ambacho kilikuwa tayari kimeandaliwa kwa ajili ya Annah kupumzishwa mara tu atakapotolewa kwenye chumba cha upasuaji.

Licha ya kwamba inspekta Aron alimleta Annah hospitalini hapo kwa siri kubwa lakini hakutaka kujiaminisha moja kwa moja kuwa yupo salama bado aliona kuna umuhimu wa kuweka ulinzi ili kuongeza usalama. Aliwaelewa vizuri watu anaopambana nao alijua wazi kuwa mtandao unaoshirikiana na kaka yake Tino ni mkubwa tena wenye nguvu sana.
Hisia za Aron zilikuwa ni sahihi kabisa kwani mpaka sasa tayari Dokta Isaack Gondwe alikuwa ameshapata taarifa kuwa Annah yuko hai hajafa na tayari alishamwita kijana wake Tino kumkabidhi jukumu la kuhakikisha Annah anakufa.
Baada ya taratibu zote za ulinzi kukamilika Aron alitoka nje ya hospitali ya Mountenia, akaingia kwenye gari yake na kuondoka akiwaahidi askari wake watatu aliowaacha kuwa angerudi baada ya muda mfupi.


Zilikuwa zimepita dakika kadhaa baada ya Dokta Gondwe na wale wazungu kutoka Mexico kumaliza kikao chao cha siri. Sasa alikuwa ameketi nje ya nyumba yake kwenye bustani nzuri ya maua akifanya mazungumzo na mmoja wa watu wake wa karibu maarufu kama Mzee Matula, tajiri mkubwa aliyekuwa amewashika masikio viongozi wakubwa serikalini Dokta Gondwe akiwa mmoja wao.

"Enh! nambie dkt Gondwe, uhakika wa kushinda kesi upo, mwanangu Osward amekaa sana mahabusu ni wakati wake wa kurudi uraiani sasa" alisema Mzee Matula
"Usijali kila kitu kipo kwenye uangalizi wangu kama nilivyokwambia awali, tayari nimesha wasambalatisha mashahidi wote, hakuna kesi tena mwanao Osward ataachiwa huru" alijibu dkt Gondwe.
"Hahaha hapo ndio huwa unanifurahisha dkt Gondwe, kwa hiyo mashahidi wote kwisha habari yao"
"Yaani wote, kasoro katoto kamoja tu ndio kamenusurika kufa, hivi nimemwita Tino yupo njiani nafikiri kufikia kesho jioni kila kitu kitakuwa sawa"
"Mmh jitahidi bwana kesi itasikilizwa baada ya siku nne tu kwanzia leo, nataka Osward abaki huru ana kazi ya kufanya"
"Usijali Matula kila kitu kipo kwenye mpango, tukikaua haka kabinti hakuna ushahidi utakaobaki kuthibitisha Osward alifanya yale mauaji, hakuna"
"Sawa nimekuelewa dkt Gondwe, enhe vipi pia kuhusu lile suala letu"
"Lipi?"
" Kuhusu ndoa ya kijana wangu Osward na binti yako Najma?"
"Aaa!! tusubiri kwanza bado hata hawajazoeana si unajua Najma tumemlazimisha tu kuolewa na Osward alikuwa hataki, tuwaache kwanza wazoeane ndio haya mengine yafuate"
"Hahahah wazoeane kitu gani dkt Gondwe sisi wazazi ndio tunajua kilichochema kwa wenetu, any way basi tusubiri hii kesi iishe kwanza kisha...ooh naona kijana wako kafika" aliongea Mzee Matula lakini akasita kuendelea mara tu baada ya kumuona Tino anakuja.
"Ni mbabe kweli kweli cheki anavyotembea" alisema Mzee Matula
"Sanaa, hanaga Mchezo na kazi, nikimwambia ua anaua chinja ana chinja kanisaidia vitu vingi mno ni mwaminifu sana" alieleza dkt Gondwe wakati huo Tino alikuwa jirani kuwafikia, macho yake alikuwa ameyakaza kumtazama mheshimiwa Dkt Isaack Gondwe bosi wake aliyemzunguuka na kulala na mke wake.
Moyo ulizidi kumuuma lakini alijikaza kisabuni akajitahidi kutoonyesha tofauti yoyote ile. Alifika na kukaa pembeni yao, baada ya salamu Mzee Matula aliaga na kuondoka akawaacha Tino na bosi wake Dkt Gondwe wazungumze

"Annah hajafa" hii ndio iliyokuwa kauli ya kwanza kutoka kwa dkt Gondwe, Tino alionyesha mshtuko kiasi.
"Nimeambiwa hali yake sio nzuri amepelekwa hospitali kwa siri, yupo kwenye mikono ya mdogo wako Inspekta Aron" dkt Gondwe alitoa maelezo huku akimtazama Tino usoni.
"Unanielewa lakini mbona uko kimya?"
"Nakuelewa bosi"
"Eee ndio hivyo, sitaki kukulaumu sana kwa sababu najua ni kazi kidogo tu, kumuua huyu binti, tafuta ni wapi mdogo wako Aron kamficha, hakikisha unammaliza kabla hajafungua kinywa chake kuzungumza"
"Sawa bosi haina shida" Alijibu Tino na mara hiyo kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya dkt Gondwe akachukua simu yake na kuutazama, ulikuwa ni ujumbe katika mtandao wa WhatsApp, ujumbe ulioambatana na picha tatu.

Dkt Gondwe alionyesha mshtuko mkubwa mara tu baada ya kuziona zile picha. Zilikuwa ni picha zikimuonyesha akiwa mtupu yeye pamoja na mwanamke ambaye ni mke wa kijana wake aliyenaye mezani wakati huu yaani Tino.
Mapigo ya moyo ya dkt Gondwe yalibadilika yakawa yanaenda kasi huku mikono yake ikitetemeka.

"Vipi bosi uko sawa" Tino aliuliza kama vile hajui chochote lakini ukweli ni kwamba alielewa kila kitu kinachoendelea kwenye simu ya bosi wake, mipango yote hii alifanya na kijana wake Bosco.

"Aah ..ee..ni..niko sawa usijali" dkt Gondwe alijibu kwa kubabaika akilazimisha tabasamu, macho yake yakahamia kwenye ule ujumbe ulioambatana na picha zile, akausoma.

,,,, Hizo ni picha tu, nina video ya dakika 55 tangu mlipoingia hadi mlipotoka, ukifuata maelekezo yangu hakuna kitakacho haribika, ukileta ukaidi basi nitaanika huu uchafu wako mtandaoni, utakuwa gumzo Duniani kote mheshimiwa Waziri afya,,,,

Dkt Gondwe alimaliza kuusoma ujumbe huo, safari hii jasho lilikuwa likimtiririka kama maji.

"Bosi mbona kama hauko sawa nini shida" Tino aliuliza tena kwa mara nyingine, akijifanya kushangazwa na hali aliyonayo bosi wake.

Je, nini kitafuata?
Tino anataka kumfanya nini bosi wake?
Vipi kuhusu Aron atafanikiwa kumlinda Annah angali na yeye yupo hatarini kuuwawa na watu wa Osward?
BADO TUNATENGENEZA MIZIZI YA SIMULIZI HII, HAKIKISHA UNASOMA SEHEMU INAYOFUA
 
THE MODERN WAR
(Vita Ya Kisasa)
Sehemu ya.............05
Mtunzi: Saul David
Email saulstewarty@gmail.com
WhatsApp: 0756862047

05-(KIGOGO BABA WA OSWARD)
ILIPOISHIA...04
,,,, Hizo ni picha tu, nina video ya dakika 55 tangu mlipoingia hadi mlipotoka, ukifuata maelekezo yangu hakuna kitakacho haribika, ukileta ukaidi basi nitaanika huu uchafu wako mtandaoni, utakuwa gumzo Duniani kote mheshimiwa Waziri afya,,,,
Dkt Gondwe alimaliza kuusoma ujumbe huo, safari hii jasho lilikuwa likimtiririka kama maji.
"Bosi mbona kama hauko sawa nini shida" Tino aliuliza tena kwa mara nyingine, akijifanya kushangazwa na hali aliyonayo bosi wake.

SASA ENDELEA...

Dokta Gondwe aliduwaa ghafula mwili wake wote ukiwa umekufa ganzi, hakuwa na uwezo wa kuongea, kusimama wala kufanya chochote kile.
Baada ya kuona Dokta Gondwe yupo kwenye hali hiyo Tino wala hakujali alisogeza kikombe cha kahawa aliyokuwa anakunywa Dokta Gondwe akaanza kunywa yeye taratibu huku akimtazama mzee huyo akiteseka na dalili zilizoonyesha wazi kuwa ni presha imepanda.
"Huu ni mwanzo tu Dokta Gondwe" aliwaza Tino huku akiendelea kunywa kawaha taratibu, wakati huo hali Dokta Gondwe ilizidi kuwa mbaya.


Wakati hayo yakiendela Mzee Matula baba yake Osward hakuwa amefika mbali, ndio kwanza alikuwa akielekea lilipokuwa gari lake la kifahari aina ya HUMMER H3, huku nyuma hakujua timbwili aliloliacha kati ya mheshimiwa Waziri wa afya Dokta Gondwe na kijana wake Tino.
Mzee Matula alifunguliwa mlango wa gari na moja kati ya walinzi wake watatu aliozoea kuongozana nao kila anapokwenda. Kabla hajaingia ndani ya gari mara alisikia sauti nzuri ya kike ikimwita.

"Najma..." Mzee Matula alisema kwa sauti ya chini huku akitabasamu taratibu akageuka, aliijua sauti hiyo ni ya nani.
Mwanamke mmoja mrembo kupindukia alionekana anakuja kuelekea pale alipo Mzee Matula, aliitwa Najma mtoto wa tatu wa mheshimiwa Waziri wa afya dkt Isaack Gondwe.

Najma alikuwa na kila sifa ya kuitwa mwanamke mrembo, alikuwa ni mrefu, umbo la wastani lililojengeka kwa kujikata vizuri kiuno kiasi cha kuzifanya hips zake nzuri kuonekana, alikuwa mzuri wa sura, macho yaliyolegea mashavu yenye vishimo yaliyofanya uzuri wake kuongezeka mara dufu, nywele zake ndevu zinazofika mgongoni. Hakika alikuwa ni mwanamke ambaye anaweza kumfanya kila mwanaume aliyekamilika kumtazama mara mbili.
Najma alikuwa amevaa suruali ya jeans, kijinguo chepesi kwa juu kilichoacha kitofu chake nje, alitembea kwa madaha kiasi cha kumfanya Mzee matula amtazame kwa macho yaliyojaa matamanio, hakumtazama kama binti anayetarajiwa kuolewa na mwanae.
Akiwa karibu kumfikia Mzee Matula mlinzi wake mmoja alisogea mbele na kunyoosha mkono wake kumzua Najma asisogee zaidi. Najma alimtazama yule mlinzi kwa macho makali na mara hiyo ikasikika sauti kutoka kwa mzee Matula.
"Muache aje"
Mlinzi akatoa mkono wake, Najma akapiga hatua kadhaa kisha akasimama mbele ya Mzee Matula huku akiwa ameweka mikono katika kiuno chake laini.
"Umependaza sana leo" alisema Mzee Matula akizidi kumtazama Najma kwa macho ya matamanio.
"Sijaja hapa kupongezwa na kizee kama wewe, nataka kujua lengo lako ni nini hasa?" Najma aliongea kwa ukali
"Kivipi Najma?"
"Hujui? Kwa hiyo baada ya wewe kunishindwa umeamua umtumie mtoto wako, yaani unamshawishi baba yangu akubali niolewe na mwanao Osward kwa faida yako wewe si ndio?" Najma alifoka

"Sikiliza Najma, pengine unaweza ukawa sahihi kama nilivyokuahidi awali nitatumia kila njia kuhakikisha nakupata" Alisema mzee Matula akionekana kujiamini.

"Ohoo! Kumbe, basi hongera zako ila kwa taarifa yako mimi kama Najma msimamo wangu uko pale pale hata kama baba yangu anakusikiliza kiasi gani lakini nakuhakikishia hakuna utakachofanikiwa"

"Hahahah, Najma unanifurahisha sana ujue, mbona tayari wewe na Osward ni wapenzi bado kidogo tu na mimi nianze kufanya yangu, nasubiri mfunge ndoa kwanza"
"Una uhakika mimi na huyu mwanao ni wapenzi? alafu nikuulize kwani Osward akinioa ndio mtakuwa mmenioa wote au?"
"Olewa kwanza atanielewa baadae" mzee Matula aliongea kwa jeuri akawa anaingia kwenye gari yake lakini mara akasita akageuka tena na kumtazama Najma kisha akaongea.

"Nashukuru pia kwa sababu haujataka kuwa shahidi mahakamani, najua ulikuwepo wakati Osward anafanya yale mauaji lakini haujasema chochote asante sana hayo ndio mapenzi, hahahah mkweee" Mzee Matula aliongea akionyesha kejeri za wazi wazi kisha akaingia kwenye gari walinzi wake wakafuata na mwisho wakaondoka.
Najma alibaki amesimama tabasamu lake likiwa limefifia usoni. Suala la Mzee Matula na mwanae Osward lilimnyima furaha kabisa, lakini angefanya nini wakati baba yake Dokta Gondwe anamshinikiza akubali kuolewa na Osward bila kujua mipango mingine aliyokuwa nayo Mzee Matula ambaye naye pia anamtaka Najma kimapenzi. Mbaya zaidi mzee huyo tajiri alikuwa akiheshimiwa sana na baba yake, kila alichokisema ilikuwa ni sheria kwa Dokta Gondwe.


Najma akiwa anarudi ndani kwa mbali alimuona Tino na baba yake wakiwa wamekaa nje katika eneo la bustani. Hakutaka kupita karibu yao kwa sababu alikuwa akimchukia Tino bila sababu, yaani ungeweza kusema hawajaendana damu. Najma akachagua kuingia ndani kupitia mlango wa nyuma. Wakati akipiga hatua aliinua macho yake akamuangalia baba yake Dokta Gondwe.
Pozi alilokuwa amekaa Dokta Gondwe kidogo lilimshangaza ni kama alikuwa ameinua mkono wake wa kulia na kuuweka shingoni kwa muda mrefu. Hakujua kuwa wakati huo baba yake alikuwa akihangaika angalau kuregeza tai ili apate hewa. Ikabidi Najma aanza kusogea taratibu, alimjua baba yake anamatatizo ya moyo, kuna wakati huwa anakauka ghafula na kupoteza fahamu.

Tino ambaye alikuwa bado anakunywa kahawa alikuwa na hisia za mbali kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, aliweza kubaini kuwa kuna mtu anakuja kutokea nyuma yake.

"Mzee, mzee Gondwe, mheshimiwa nini shida" Tino alikurupuka ghafula akasogea karibu na Dokta Gondwe akijifanya kama vile alikuwa hajamuona mwanzo. Kitendo hicho kilimfanya Najma aliyekuwa bado hajafika kuamini hisia zake zilikuwa sahihi haraka akaanza kukimbia kuwafuata Tino na baba yake pale walipo.

"Daddy! shida nini, eti Tino baba kapatwa na nini?" aliuliza Najma akiwa amebakiza hatua chache kuwafikia, Najma aliogopa sana.
"Sijajua nashangaa amebadilika ghafula tu" Tino alidanganya
"Hii ni presha itakuwa imepanda tena, lakini huwa haipandi bila sababu, au kuna taarifa mbaya umempa?" Najma alimtupia swali lingine Tino wakati huo akihangaika kuregeza tai na kufungua vishikizo vya shati la baba yake.

"Hapana sijampa taarifa yoyote mbaya" Tino alijitetea.
Haraka Najma aliitazama simu ya baba yake pale mezani lakini ghafula katika hali asiyotegemea baba yake Dokta Gondwe aliikwapua ile simu kwa kasi na kuiweka kwenye mfuko wa koti lake.
Hali hii ilimshangaza Najma akahisi moja kwa moja kuwa kuna kitu baba yake alikuwa anaficha na huo ndio ulikuwa ukweli wenyewe licha ya dokta Gondwe kuwa katika hali mbaya lakini hakutaka kuruhusu mwanae au Tino aipekue simu yake. Ilikuwa ni hatari kubwa kwake kwani wangeweza kuziona zile picha zake chafu za ngono alizotumiwa.

"Baba nini shida, unajisikiaje?" Najma aliuliza swali.
"Ni..nipelekeni chumbani, alafu Najma nita..tafutie zile dawa zangu za presha za kuweka chi..chi..chini ya ulimi" Dokta Gondwe aliongea kwa taabu kidogo.
Haraka Najma aliwaita walinzi waliokuwa wanazunguuka zunguuka nyumbani hapo, wakasaidiana kumnyanyua dokta Gondwe wakawa wanampeleka ndani.
Wakiwa wamemfikisha mlangoni mara dokta Gondwe aliwapa ishara kuwa wasimame kwanza.

"Tino hebu sogea karibu" alisema Dokta Gondwe, Tino akosogea karibu akainama na kutega sikio karibu na mdomo wa bosi wake.

"Usijali kuhusu mimi nitakuwa sawa, nenda kafanye kazi hakikisha yule mtoto Annah anakufa leo hii, anza kumfuatilia mdogo wako Inspekta Aron kwa ukaribu yeye ndiye amemficha yule binti" dokta Gondwe alinong'ona.
"Sawa bosi" alijibu Tino kisha akawa anamsindikiza kwa macho bosi wake akiwa amebebwa juu juu na walinzi wake wakaingia naye ndani ya nyumba.

"Na bado huu ni mwanzo tu mheshimiwa Waziri, nitahakikisha unavuta pumzi ya moto ukiwa hai, huwezi kulala na mke wangu alafu ukaishi kwa amani" alisema Tino huku akitabasamu.

"Umesemaje wewe?" Tino alishitushwa na sauti ya Najma aliyekuwa amesimama nyuma yake, hakuwa amemuona.

"Aah! kwani umesikia nini?" Tino alijibu swali kwa swali akiwa hana uhakika kama Najma ameyasikia maneno yake au laa kwani aliongea kwa sauti ya chini sana.

"Nani atavuta pumzi ya moto au nimesikia vibaya?" aliuliza Najma akitaka kuhakikisha alichokisikia.

"Hapana sijasema hivyo mimi, kwa heri naondoka, muangalie mzee tafadhali" alisema Tino kisha akaondoka zake akimuacha Najma anamsindikiza kwa macho.
"Tino" Najma aliita
Tino aliyekuwa amefika umbali wa kama hatua ishirini hivi alisimama kisha akageuka.
Akawa anamtazama Najma ambaye naye alibaki anamtazama huku sura yake ikionyesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.
Tino alinyanyua mabega yake juu ikiwa ni ishara ya kutaka kujua kwa nini amemuita. Licha ya kufanya hivyo lakini bado Najma aliendea kuwa kimya, mwisho akaongea.

"I'll be watching you from today"( nitakuwa nakuangalia kwanzia leo) Najma aliongea kauli yenye utata kisha akaondoka na kuingia ndani.
Tino alibaki amesimama wima, alijaribu kuitafakari kauli hiyo ya Najma yenye ujumbe mzito ndani yake, tayari ilionyesha wazi kuwa Najma ameshaanza kumuhisi vibaya Tino.

"Bado tuna safari ndefu sana mimi na baba yako, bado hata sijapata nachokitaka kwake, Najma ni mapema mno kuingilia utakufa bado mbichi" Tino alijiongeresha mwenyewe kisha akatabasamu na kuondoka zake.

Je nini kitafuata?
Ni kipi hasa Tino anakitafuta hadi kujiweka karibu na Waziri wa afya?
Bado anamsikiliza na kutii amri zake licha ya dkt Gondwe kulala na mke wake...
Vipi kuhusu sakata la Najma na mzee Matula?
Vipi kuhusu Aron, Annah na Big'?
. ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..............06
Mtunzi: Saul David
Email: saulstewarty@gmail.com
WhatsApp: 0756862047

06-(JESCA MALKIA WA NGONO)
ILIPOISHIA...05
"Bado tuna safari ndefu sana ya kwenda mimi na baba yako, bado hata sijapata nachokitaka kwake, Najma ni mapema mno kuingilia utakufa bado mbichi" Tino alijisemea mwenyewe kisha akatabasamu na kuondoka zake.
SASA ENDELEA...

Dokta Gondwe alikuwa amekaa juu ya kitanda chumbani kwake akawa anajaribu kupiga ile namba iliyomtumia picha zake chafu bila mafanikio.

"Huyu mtu kanitumia hizi picha sasa hivi inakuwaje mnasema namba haipooo...!!" Alisema Dokta Gondwe huku akiipigiza simu yake kitandani kwa nguvu.

"Baba, nini shida?" Najma aliuliza akiwa ameingia chumbani kwa baba yake bila taarifa, mkononi akiwa na kopo la dawa.
Dokta Gondwe alibaki anamtazama mwanae asijue ajibu nini, jambo lililokuwa mbele yake lilikuwa ni zito mno. Kwanza kabisa endapo akiruhusu zile picha au video zisambae mitandaoni ilikuwa ni kashfa na skendo kubwa sana ukizingatia yeye ni mtu mkubwa serikalini, Waziri wa afya. Pili mwanamke alielala naye siku hiyo alikuwa ni mke wa mtu tena mke wa kijana wake mwaminifu wa kazi zake haramu yaani Tino hii ilikuwa ni hatari kubwa, alihofu atampoteza Tino lakini pia atampoteza mke wake ambaye kwa sasa alikuwa katika mizunguuko yake nje ya nchi.
"Aibu gani hii" Dokta Gondwe aliwaza

"Haya chukua dawa zako umeze naona hata hutaki kuniambia shida ni nini umekaa kimya tu hata sikuelewi" alisema Najma akionekana kukasirika kiasi
"Sio hivyo mwanangu, hebu kaa hapa nikwambie kitu" Dokta Gondwe aliongea kwa upole akimtaka binti yake akae pembeni yake, Najma akafanya hivyo.

"Unajua nini mwanangu hebu nisikilize baba yako, ukitaka niwe salama matatizo kama haya yasinipate basi kubali kuolewa na Osward mtoto wa Mzee Matula" Dokta Gondwe aliongea kauli iliyomnyong'onyesha Najma.
"Baba una hakika hilo ndilo tatizo linalokusumbua? hakuna kitu kingine? inamaana mzee Matula anakutisha au?"
"Hilo ndio tatizo pekee mwanangu, unajua kabisa ni kiasi gani ile familia ya Mzee Matula ni muhimu kwetu, wao ndio wamenishika mkono tangu nikiwa mkuu wa mkoa mpaka sasa ni Waziri wa afya, nisipofanya kama anavyotaka nitapoteza kila kitu mwanangu, hebu fikiria uchaguzi ni mwakani tu hapa" alieleza dokta Gondwe

"Basi baba sawa nimekuelewa hata usijali, mbona nilisha kubali tangu kitambo hata leo tu naenda kumtembelea Osward kule gerezani, usiwaze baba presha yako itakutesa kama ukiwa hivyo" Najma aliongea akijaribu kumfariji baba yake akaamini suala hilo ndilo lilipelekea presha ya dokta Gondwe kupanda lakini haikuwa hivyo.
Mwisho Najma alitoka nje ya chumba cha baba yake akamuacha dokta Gondwe akihangaika tena kupiga ile namba bila mafanikio.

"Ona natuma meseji hata hazitoki, ni nani huyu unataka kucheza na akili yangu" Dokta Gondwe aliendelea kulalamika


Ndani nyumba moja kubwa iliyojengwa kisasa, nyumba ambayo awali alikuwa akiishi mwanajeshi mstaafu Jenerali Phillipo Kasebele ambaye kwa sasa marehemu.
Katika nyumba hiyo walibaki wakiishi vijana wawili watoto wa marehemu Philipo, wote walikuwa ni wa kiume. Wa kwanza aliitwa Tino na wa pili alikuwa ni Aron.
Tino na Aron waliishi kwa pamoja kama ndugu licha ya kutofautiana sana katika shughuli wanazozifanya. Tino alikuwa ni jambazi anayefanya kazi chini ya Waziri wa afya Dokta Gondwe wakati huo Aron akiwa ni polisi kitengo cha upelelezi ambaye kwa sasa anapambana kwa udi na uvumba kuhakikisha anauangusha mtandao mzima unaofanya kazi na kaka yake Tino.
Baada ya baba yao kufariki siku chache baadae mama yao maarufu kama Madam Sultana aliugua ugonjwa wa ajabu uliomlazimu kulazwa hospitali kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita akiwa hajitambua hata kupumua kwake ilikuwa ni kwa msaada wa mashine.
Gharama za matibabu ya Madam Sultana zilikuwa ni kubwa sana, walilipa si chini ya laki sita kila iitwapo leo. Licha ya serikali kutoa mamilioni ya mchango wa matibabu kwa mama huyo kama heshima ya marehemu mumewe aliyekuwa mwanajeshi lakini bado hali ilikuwa ni tete. Tino na Aron walijikuta wakitoa pesa nyingi sana kuendesha huduma za matibabu ya mama yao pale hospitali ya Mountenia.
Tino akawa anaitumia hii kama sababu ya kuharalisha uharifu wake akidai anafanya hivyo kutafuta pesa kwa ajili ya mama yake. Licha ya Inspekta Aron kumshauri kaka yake mara kadhaa kuachana na shughuli za ujambazi lakini Tino hakuacha, akazidi kufanya mauaji na matukio mengine ya kikatili.
Mwisho uvumilivu ukamshinda Inspekta Aron aliyekula kiapo kulitumikia jeshi la polisi ipasavyo akaamua kulivalia njuga suala hili. Akaweka undugu pembeni na kuanza kutafuta namna ya kumtia hatiani kaka yake Tino. Uadui kati yao ukaongezeka licha ya kuishi ndani ya nyumba moja lakini kila mmoja akawa ni adui mkubwa wa mwenzake.


Mchana majira ya saa nane Inspekta Aron alisimamisha gari yake nje ya nyumba yao, alikuwa ametoka Hospitali ya Mountenia kule alikolazwa mama yake lakini pia binti mdogo Annah ambaye alikuwa akitibiwa kwa siri.
Alishuka na kuingia ndani. Ile anakanyaga tu sebureni mara ghafula alikumbatiwa kwa nguvu na mwanamke aliyekuwa anamnyatia kwa siri kutokea nyuma yake.

"Aah shem hebu acha bwana nimeshakukataza hii michezo" Aron alilalamika akionekana kutofurahishwa na kitendo alichokifanya mwanamke huyo ambaye ni mke wa kaka yake Tino aliitwa Jesca. Ndiyo ni Jesca yule yule ambaye amemsaliti mumewe kwa kulala na mheshimiwa Waziri wa afya Dokta Gondwe.

"Aah! shem nae kama nimekumis siruhusiwi kukukumbatia jamani" alisema Jesca huku akilegeza sauti na kurembua macho yake.

"Sawa lakini mazoea kama haya sio mazuri, hata kaka Tino akijua hawezi kufurahia"
"Achana na kaka yako, hapa tupo mimi na wewe"
"Vipi kuna chakula nina njaa sana" Inspekta Aron akabadilisha mada makusudi. Alishamzoea shemeji yake huyo ambaye siku zote alikuwa na vijitabia vya ajabu ajabu isingekuwa msimamo wa Aron basi angelikuwa ashapitanaye.
"Yap! nishapika muda lakini mbona huniambii kama umemkamata huyo kibaka?"
"Usimwite hivyo ni mume wako kumbuka"
"Mume gani wa mchongo, nataka tu akamatwe atuachie uhuru"
"Hapana sijamkamata, ni kweli kile kifaa ulichoweka kwenye koti lake kilitusaidia kujua hadi mahali alipo, niliomba askari wa kunisindikiza kwenda kule ila wakanichelewesha makusudi pale kituoni kuna mtu anatuzunguuka, tulifika kwa kuchelewa"

"Duh! shem jamani kwa hiyo ikawaje"
"Ndio hivyo tulikuta tayari wameshafanya mauaji yaani wamemuua baba mama na mtoto wote kwa pamoja" Aron alidanganya hakutaka kuweka wazi kuwa binti Annah yupo hai.

"Huyu mwanaume laana tupu, usijali shem nipe kifaa kingine nitamuweka tena kwenye nguo yake hadi nihakikishe unamkamata"
"Kwa sasa subiri kwanza shem" alisema Aron huku akitazama simu yake iliyoingia ujumbe mfupi wa maandishi.

"Naondoka baadae"
"Mbona ghafula, alafu vipi kuhusu kula si umesema unanjaa?"
"Baadae, kuna jambo muhimu naenda kufuatilia kule gerezani alipo yule jamaa Osward" alisema Aron, akatoka nje akaingia kwenye gari yake haraka na kuondoka kwa kasi.
Wakati Inspekta Aron anatoka, getini akakutana na gari ya kaka yake akiingia ndani. Wakati magari yao yanapishana pale getini Ndugu hawa wawili walitazamana kwa macho makali kila mmoja akionyesha chuki ya wazi wazi dhidi ya mwenzake. Mwisho wakapishana kila mtu akaenda zake.

Mara tu baada ya Inspekta Aron kutoka nje na gari yake, bwana mmoja aliyekuwa amesimamisha pikipiki yake umbali wa hatua kadhaa kutoka kwenye nyumba yao alianza kumfuatilia Inspekta Aron nyuma taratibu. Mtu huyu alikuwa amevalia mavazi meusi kila sehemu kuanzia viatu,suruali,gloves,koti na mzula hata rangi ya ngozi yake pia ilikuwa ni nyeusi tii. Huyu hakuwa mwingine bali BIG' yule bwana wa miraba minne aliyetumwa na Osward wakati ule gerezani kuhakikisha anamuua Inspekta Aron. Sasa alikuwa ameianza kazi yake rasmi. Mgongoni alikuwa amebeba begi kubwa lenye rangi nyeusi pia.


Tino alishuka kwenye gari na kukanyaga ardhi nje ya nyumba yao. Akawa anatembea haraka haraka kuelekea ndani huku sura yake ikiwa imekunjamana kwa hasira.
Moyo wa mwanaume huyo ulikuwa umebaba hasira nzito dhidi ya mke wake baada tu ya kuishuhudia ile video ambayo mkewe alikuwa akimsaliti na bosi wake wa kazi mheshimiwa Dokta Gondwe.
Hakuwa amekutana wala kuwasiliana na Jesca mkewe, hii ndio ilikuwa mara yake ya kwanza tangu alipoitazama video ile chafu.

"Mumewangu kipenzi umeru...mamaaaaa!" Alisema Jesca lakini kabla hajamalizia sentensi yake kibao kizito kutoka kwa Tino kilitua kwenye paji lake la uso, kilikuwa ni kibao kizito mno kilichompeleka moja kwa moja sakafuni, damu zikawa zinamtoka puani.

"Una nini wewe mwanamke ni nini unakosa kwangu, kwa nini hata huwazi ikitokea mimi sipo nini kitakupata?" alisema Tino kisha akaingiza mkono kwenye mfuko wa koti lake akatoa kifaa fulani kidogo cheusi akakitupa sakafuni mbele ya mkewe Jesca.

"Umeniwekea hiki kifaa kwenye koti ili kumsaidia shemeji yako Aron ajue nilipo si ndio? ili iweje? nikifungwa mimi wewe utaishije hapa nyumbani? mama kule hospitali nani atamlipia gharama? Jesca hivi hua hauwazi haya yote kabla ya kufanya upumbafu wako?" Tino aliongea kwa ukali, akaingia chumbani akabalisha koti kisha akatoka tena na kuondoka zake.

Wala hakugusia habari za ile video aliyoiona lakini kwa uzito wa lile kofi alilompiga mkewe ni kofi lililokuwa limebeba hasira zote zikiwa ni pamoja na zile za mke wake kumsaliti.

Akiwa ndani ya gari iliyokuwa ikienda kwa kasi kubwa, Tino alikunja kona na kufunga breki kali pembeni ya barabara. Alitulia kimya akihema kwa nguvu mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio.
"Kwa nini? kwa nini umenifanyia hivi Jesca? kwa nini umenisaliti wewe mwanamke?" Tino aliongea kwa jazba akiugulia maumivu makali ya moyo huku akipiga piga usukani kwa mikono yote miwili, alionekana mwenye hasira isiyo na kipimo.

"Tulia Tino tulia, umebakiza hatua chache tu kuiweka Dunia nzima kwenye kiganja cha mkono wako" aliongea Tino akijaribu kujituliza mwenyewe.
Mwisho alituliza akili yake, akachukua simu akapiga namba aliyoihifadhi kwa jina la 'sniper K'

"Vipo mpo tayari....sawa jipangeni tukutane nje ya Hospitali ya Mountenia...leo tunamaliza kila kitu....ndiyo yule binti lazima afe leo...sawa njooni na vifaa vyote muhimu" Tino alimaliza mawasiliano kisha akakata simu, akapiga tena namba nyingine.

"Ee dogo Bosco, mtumie tena Dokta Gondwe kipande cha video yake ya X kama cha dakika moja hivi, mpe vitisho tena kisha upotee hewani kama kawaida..poa...poa" Baada ya mazungumzo hayo Tino akakata simu.
Je nini kitafuata?
Tino anataka kumuua Anna...
Tino anataka kuiweka Dunia kiganjani kwake...
Big anataka kumuua Inspekta Aron...
Inspekta Aron anataka kumlinda Annah...

Hali bado ni tete ndani ya MODERN WAR tukutane sehemu ya 7.
 
THE MODERN WAR
(vita ya kisasa)
Sehemu ya............07
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
07-(V-COBOS)
ILIPOISHIA....06
"Ee dogo Bosco, mtumie tena Dokta Gondwe kipande cha video yake ya X kama cha dakika moja hivi, mpe vitisho tena kisha upotee hewani kama kawaida..poa...poa" Baada ya mazungumzo hayo Tino akakata simu.

SASA ENDELEA....

Aron aliendesha gari kwa mwendo wa kasi sana, dakika kumi na moja pekee zilimtosha kufika lilipo gereza la Kanondo. Hakujua kuwa tangu alipotoka nyumbani nyuma yake kuna mtu alikuwa akimfuatilia kwa lengo la kuyaondoa maisha yake.
Kanondo lilikuwa ni gereza la kawaida lenye wafungwa wachache mno, hata ulinzi wake haukuwa wa kutisha sana. Hii ni kutoka na aina ya wafungwa walikuwa wakiletwa hapo, walikuwa ni wale wenye kesi nyepesi nyepesi. Hapa ndipo walipochagua kumleta Osward mtoto wa tajiri mkubwa na maarufu nchini mzee Matula. Osward alihifadhiwa katika gereza hilo pindi anaposubiria mwenendo wa kesi yake ya mauaji iliyokuwa bado ikiunguruma mahakamani.
Inspekta Aron alipaki gari yake hatua kadhaa kutoka lilipokuwa geti kuu la kuingia ndani ya gereza hilo. Akiwa anajiandaa kushuka mara kwa mbali alimuona mwanamke mmoja mrembo sana anashuka kwenye taxi, akaanza kutembea taratibu naye akielekea kwenye geti kuu la kuingia gerezani.

Aron alimkodorea macho mwanamke huyo ambaye alikuwa na kila sifa ya kuitwa mrembo. Haikuwa mara yake ya kwanza kumuona alishakutana naye si chini ya mara tatu, alimjua vizuri ni Najma mtoto wa Waziri wa afya Mheshimiwa dokta Gondwe.

Akiwa karibu kufika lilipo gari lake, Aron alifungua mlango wa gari na kushuka taratibu, uso kwa uso akawa anatazamana na Najma.

"Ni wewe tena? sitaki maswali yako tafadhali niko bize" Najma aliwahi kuzungumza huku akijifanya mwenye haraka, tayari alishaijua nia ya Inspekta Aron kusimama mbele yake.
"Uko hapa kumtembelea Osward?"
"Yes"
"Najma hebu subiri kidogo basi tuongea"
"Inspekta Aron mbo..."
"Najma watu wanakufa, unajua leo wamekufa wangapi kwa sababu ya kitu unachokificha" Aron aliongea kwa ukali
"Nini? Mimi naficha nini Inspekta? Nilishakwambia sikuwepo wakati yale mauaji yanafanyika, sijui kama Osward aliua au laa! sijui chochote sikuona kwa nini unanilazimisha nikatoe ushahidi ambao sina uhakika nao" Najma naye alifoka.

"Lakini ulifika mapema pale Osward alipofanyia mauaji, nataka kujua angalau nini uliona Najma"
"Una uhakika gani kama nilifika? nikamate na mimi basi ukanihoji"
"Najma usipaniki tafadhali, pengine unaweza kuwa sahihi au umeamua tu kumlinda mpenzi wako Osward lakini kumbuka watu wanakufa, mashahidi wote niliowategemea kwenye kesi hii wanauwawa kikatili, wewe huwazi ni kwa nini? Najma najua unahuruma na utu pia tafadhali naomba fanya kitu ili haki itendeke" Inspekta Aron aliongea kwa hisia sana, maneno hayo kidogo yalionekana kumuingia Najma akawa kimya kwa sekunde kadhaa.

Wakati huo wote Big aliyetumwa kumuua Inspekta Aron alikuwa kwa mbali akisikiliza mazungumzo kati ya Najma na inspekta Aron.
"Huyu Inspekta kweli ni jau! Anakiherehere utadhani ameahidiwa kombe, kifo ndio adhabu pekee anayostahili huyu mbwa" Big alijisemea mwenyewe huku akivua begi lake kubwa na kuliweka juu ya tenki la mafuta la pikipiki.

Baada ya Najma kukaa kimya kwa sekunde kadhaa mwisho aliinua uso wake akamtazama tena Aron usoni.

"Ungekuwa wewe ungefanyaje? Ungekubali kushirikiana na mtu ambaye anataka kuwafunga gerezani baba na mpenzi wako? Hapana siwezi niuwie radhi Inspekta, siwezi" Najma aliongea kisha akaanza kuondoka kulielekea geti la kuingia gerezani.

"Najma.. Najma.. Najma...Na.." Inspekta Aron aliita lakini Najma aliendea kutembea kama vile hamsikii.

Inspekta Aron alibaki amesimama akijikuna kichwani, alishajaribu mara kadhaa kumshawishi Najma akubali kutoa ushahidi lakini jitihada zake siku zote ziligonga mwamba.
Aliwaza ni namna gani atafanikisha kung'oa mizizi ya mtandao wa kiharifu wa Dkt Gondwe ambao ndiyo chanzo cha kaka yake Tino kuharibikiwa.

Aron akiwa bado kwenye dwimbi la mawazo mara kuna askari magereza mmoja alifika na kuingia kwenye gari yake akakaa siti ya nyuma. Aron alishtushwa na mlio wa mlango wa gari ukifungwa ndipo akagutuka na kumchungulia mtu aliyeingia kwenye gari yake. Alimfahamu haraka naye akaingia kwenye gari.

"Enhe! nambie afande ni nini umepata? nimekuja haraka sana mara baada ya kupata ujumbe wako" Aron alianzisha mazungumzo mara tu baada ya kuingia ndani ya gari.
"Umefika tangu mda nimekuona nikashindwa kuja kwa sababu ulikuwa bize na mtoto wa Waziri, vipi umempenda au" alisema yule askari magereza
"Achana na hizo habari ndugu yangu mambo hayako kama unavyodhani nambie nimeitikia wito wako"
"Okay ni hivi, kama ulivyonambia kuwa nikusaidie kufuatilia nyendo za Osward akiwa humu gerezani"
"Mnh"
"Sasa leo tena kunakitu kimetokea, Osward aliitwa na mkuu wa gereza akapewa simu akawa anazungumza na mtu kutoka nje sikujua ni nani ila baadae kama dakika 7 hivi Osward alipata mgeni jamaa fulani hivi jeusi limejazia sana, niliwapiga picha nitakuonyesha" yule afande alianza kutoa maelezo

Wakati wakiendelea na mazungumzo hayo mara ghafula walisikia kishindo kikubwa kutoka ndani gerezani ikifuatiwa na kelele nyingi za watu.
Inspekta Aron na yule afande walitazamana kila mmoja asijue nini kimetokea, kadri muda ulivyokwenda ndivyo makelele yale yalizidi kuongezeka.

"Najma!" Inspekta Aron aliongea kwa sauti ya chini huku akishuka haraka kwenye gari akaanza kukimbia kuelekea ndani ya gereza, akili yake ilihisi moja kwa moja kuwa Najma atakuwa amepeta shida, hakujua hisia hizi zimetoka wapi ghafula, askari magereza naye akawa anamfuata nyuma.
Wote kwa pamoja walikimbia hadi lilipokuwa eneo maalum la watu kuonana na wafungwa pindi wanapowatembelea hapo ndipo kelele zilipotokea

Punde tu baada ya Inspekta Aron kuondoka na yule askari magereza, Big alishuka kwenye pikipiki yake taratibu akanyata hadi lilipokuwa gari la Aron.
Alikuwa na kifaa furani mkononi kilichofungwa nyaya kitaalamu sana. akaangaza macho huku na huku hakuna aliyekuwa akimuona.
Taratibu aliinama chini ya uvungu wa gari la Aron akakibandika kile kifaa kisha akabonyeza vitufe fulani kwenye rimoti iliyokuwa mkononi mwake, kile kifaa kikatoa mwanga mwekundu ulioanza kuwaka na kuzima. Hili lilikuwa ni bomu la kutengenezwa kwa mkono, Big alionekana ni mbobezi wa kutengeneza aina hii ya mabomu.

"Kwisha habari yako Aron, ukiingia tu kwenye gari nakugeuza majivu" Alisema Big na hapo akaondoka kurudi ilipokuwa pikipiki yake akiwa na ile rimoti mkononi akawa anamsubiri ndege wake arudi kwenye kiota.


Kama alivyohisi Inspekta Aron ndivyo ilivyokuwa, kulikuwa na ugomvi mkubwa uliotokea kati ya Osward na wafungwa wenzie wawili waliokuja na kumvamia wakati akifanya mazungumzo na Najma.
Osward na wale wafungwa wawili walikuwa wakipigana na kurushiana viti na meza, ugomvi ulikuwa ni mkubwa mno hali iliyowafanya wafungwa waliokuwa upande wa pili kuanza kupiga yowe wakishangilia na hizi ndizo kelele alizozisikia Aron.
Askari walifika na kuzuia ugomvi huo licha ya kwamba kwa kiasi walikuwa wamechelewa lakini angalau waliweza kuwadhibiti.
Punde Inspekta Aron akaingia kwa kasi, aliangaza macho huku na huku ndani ya sekunde kumi tayari aliweza kubaini kilichokuwa kikiendelea.

"Najma" Aron aliita mara baada ya kumuona Najma akiwa amejikunyata kwenye kona moja ya ukuta huku akilia kwa maumivu, alikuwa amejeruhiwa kwenye mguu wake wa kushoto.

Inspekta Aron alikimbia kumfuata pale alipo, akafika na kuchuchumaa mbele yake.
"Vipi uko sawa Najma?"
"Mguu wangu, nimeumia mguu" Najma alilalamika, wakati huo askari wengine walifika kumtazama akiwemo mkuu wa gereza SP Seleman.
Aron alijaribu kuushika mguu wa kushoto wa Najma uliojeruhiwa. Najma akapiga kelele kutokana na maumivu makali aliyoyapata, alikuwa ameumizwa sana

"Hebu mwiteni daktari upesi" alisema SP Seleman
"Haina haja Afande acha nitamchukulia umakini usijali, unamjua huyu ni binti wa Waziri wa afya Dokta Gondwe" Aron alitoa maelekezo akiwa amegeuka kuwatazama askari magereza waliokuwa wamesimama nyuma yake.

"Aaa! Inspekta Aron uko hapa? Umefika saa ngapi mbona hujaja ofisini kwangu?" SP Seleman aliuliza kwa mshangao, alikuwa akifahamiana vizuri na inspekta Aron.
"Ndio naingia mkuu, hebu sogeeni kidogo nipite"alisema Aron huku akimnyanyua Najma akaanza kuondoka naye.

"Nitarudi mkuu ngoja nimuwahishe mtoto wa mheshimiwa hospitali"
"Umekuja na gari yako?"
"Ndiyo ipo nje kule" alijibu Aron Najma akiwa mikononi mwake.
Osward aliyekuwa ameshikiliwa na askari wawili alimtazama Aron kwa macho makali huku akilaumu ni kwa nini Big hajafanya kazi yake mpaka sasa. Hakupendezwa kabisa na kitendo cha Inspekta Aron kumbeba Najma.

Inspekta Aron alitembea taratibu akiwa makini kutoutikisa mguu wa kushoto wa Najma uliojeruhiwa. Baada ya hatua kadhaa aliinama akamtazama Najma usoni, Najma akakwepesha macho yake aliyokuwa ameyagandisha kwa muda mrefu akimtazama mwanaume huyo. Ni dakika chache tu zilikuwa zimepita walitoka kukwaruzana vikali lakini sasa anamtendea ukarimu wa hali ya juu.
Inspekta Aron aliendelea kutembea kuelekea lilipo gari lake bila kujua hatari iliyokuwa mbele yake kwani kulikuwa na bomu limetegeshwa chini ya gari hilo. Yeye aliwaza kumuwahisha Najma hospitali ya Mountenia alikomuacha Annah pia.


Waziri wa afya Mheshimiwa dokta Gondwe alikuwa bado chumbani kwake aliendelea kuhangaika na ile namba iliyotumika kumtumia picha zake akiwa faragha na Jesca mke wa Tino.
Mpaka sasa tayari alikuwa ameshatumiwa picha na video nyingine fupi ikimuonyesha alivyokuwa akifurahia penzi na mke wa mtu, mheshimiwa akazidi kuchanganyikiwa.
Kitanda kilikuwa hakilaliki wala kukalika mda wote alikuwa wima anapiga hatua tano mbele tano nyuma. Aliwaza ampigie Waziri mwenzake kitengo cha mawasiliano amsaidie kufanya udukuzi lakini roho ikasita, aliogopa uchafu wake kuonekana.

Mara simu yake ikaita, haraka Dkt Gondwe akaitazama ile namba inayompigia akabaini ilikuwa ni ile ile iliyotumika kutuma zile picha zake chafu WhatsApp, haraka akapokea.

"Ndugu sema kiasi chochote unachotaka mimi nitakupatia sema chochote nitakupa tafadhali usiziweke hizo video mtandaoni nakuomba" dkt Gondwe alianza kujieleza hata kabla ya salamu.
Sauti nzito yenye mwangwi iliyojaa kitetemeshi ilisikika upande wa pili ikimjibu
"Mheshimiwa Waziri hatuhitaji pesa zako, kunakitu kingine tofauti tunakitaka kutoka kwako"
"Nini? ni nini mnataka nitafanya chochote mtakachosema"
"Vizuri sana Dokta, tunachohitaji kutoka kwako ni vimelea vya V-COBOS"
"Nini?" Dkt Gondwe aliuliza kama vile hajasikia alichoambiwa, hakuwa ametegemea kabisa kama angelisikia neno hili kutoka kwa mtu huyo mwenye sauti ya ajabu. Dkt Gondwe alibaki ameduwaa asijue ajibu nini.
Mambo yote haya alikuwa akiyaendesha kijana wake Tino ambaye kwa sasa alikuwa nje ya hospitali ya Mountenia tayari kwa kazi ya kumuua binti Annah kama alivyoagizwa lakini alikuwa anajua kila linaloendelea kwa bosi wake Dkt Gondwe, naam ni Tino mwenyewe ndiye aliyekuwa akitaka vimela vya V-COBOS

***********
{TANGAZO:- Epuka matapeli simulizi hii imetungwa na SAUL DAVID simu 0756862047, Tafadhali usinunue kwa mtu mwingine tofauti }
******-*-

Upande wa pili tayari Tino na kikosi cha watu watano walikuwa wamefika nje ya hospitali ya kimataifa ya Mountenia tayari kwa zoezi zima la kuhakikisha wanamuua Annah binti wanayeamini ni shahidi pekee aliyesalia katika kesi ya mauaji inayomkabili Osward mkwe wa bosi wao Dokta Gondwe.
"Tino unauhakika Aron alimleta huyo binti kwenye hii hospitali?" Mmoja kati ya vijana wa Tino aliuliza swali kabla hawajashuka kwenye gari.
"Ndiyo ninao uhakika"
"Lakini mkuu hii hospitali ni kubwa sana ghorofa nne tena inavyumba kibao tutajua vipi mahali wamemficha?"
"Tutajua tu usijali"
"Kivipi Tino tuko wachache tutakagua hospitali nzima? au tuwateke wafanyakazi?"
"Acha maswali mengi, ninao mpango wa kujua ni wapi alipo Annah, wewe fuata maelekezo yangu" Tino aliongea kwa kujiamini.

Je, nini kitafuata?
Tino atafanikiwa kumuua Annah?
Vipi kuhusu Aron na Najma wanaokuja hospitalini hapo lakini gari walilopanda lina bomu chini yake?
Vimelea vya V-COBOS ni kitu gani?
Tino anajua nini kuhusu V-COBOS?
SASA TUNAENDA KUINGIA KWENYE KIINI CHA SIMULIZI YETU, USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA.
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..........08
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

08-(HOSPITALI YA MOUNTENIA)
ILIPOISHIA....07
Gari waliyopanda Inspekta Aron na Najma mtoto wa Waziri wa afya inabomu chini yake. Wakati huo pia Waziri wa afya anaambiwa alete vimelea vya V-COBOS ili video zake chafu zisisambazwe mtandaoni. Upande wa pili Tino akiwa na kikosi cha watu watano wanajiandaa kuingia hospitali ya kimataifa ya Mountenia kwa ajili ya kumuua Annah ili kufuta ushahidi
Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA....

"Inspekta Aron, Inspekta Aron" Yule askari magereza alikuwa akiita wakati Aron analikaribia gari lake akiwa amembeba Najma.
Inspekta Aron alisimama na punde yule askari alifika karibu yake akasimama na kumnong'oneza kwa sauti ya chini ambayo Najma hakuweza kusikia chochote.

"Hatukumalizana, yule bwana aliyekuja hapa kuongea na Osward nilifanikiwa kumpiga picha nataka nikuonyeshe pengine zinaweza kuwa msaada"
"Ooh sawa lakini mazingira sio rafiki, hebu nitumie hizo picha WhatsApp nitaziangalia baadae" Aron alijibu kwa sauti ya chini pia. Mwisho walikubaliana, Inspekta Aron akaendelea kutembea kwa kasi kuelekea kwenye gari yake

"Usijali Najma utakuwa sawa" alisema Aron wakati akifungua mlango wa nyuma wa gari, akamsaidia Najma kuingia taratibu kisha akafungua mlango.
Wakati huo Big' alikuwa amesimama kwa mbali akiwatazama huku ile rimoti ya bomu alilolitega chini ya gari ya Inspekta Aron ikiwa mikononi mwake.

"Ooh! shit nini tena hiki, yule si Najma?" Big alijiuliza mara baada ya kumuona yule mwanamke aliyebebwa na inspekta Aron
"Yes ni Najma mwenyewe mambo gani tena haya" Big' alijijibu mwenyewe baada ya kuhakikisha yule mwanamke aliyebebwa na Inspekta Aron ni Najma.
Haikuwa rahisi tena kulilipua gari la Inspekta Aron wakati Najma akiwa ndani yake. Lengo ilikuwa ni kumuua Inspekta Aron pekee na sio Najma ambaye ni mpenzi wa aliyemuagiza kazi hiyo yaani Osward.
Wakati Inspekta Aron anaingia kwenye gari tayari kuondoka aligonganisha macho na Big' aliyekuwa amesimama kwa mbali akiwatazama, laiti kama Inspekta Aron angekubali kutazama zile picha kutoka kwa yule askari magereza wakati ule basi zingemsaidia kubaini chochote lakini kwa sasa hakumtilia maanani kabisa bwana Big' mtu hatari anayetaka kuyaondoa maisha yake. Inspekta Aron akaingia kwenye gari akaliwasha na kuanza kuondoka kwa mwendo wa taratibu sana.

"Kwanza Najma kapatwa na nini, kwanini abebwe vile na yule bwege? Nitafanyaje sasa kumuua Aron? Hapa sina jinsi itabidi nitafute nafasi nyingine, nitasubiri mpaka Najma atakaposhuka" Big aliwaza mwisho akawasha pikipiki yake na kuanza kuifuatilia gari ya Inspekta Aron kwa nyuma kama ilivyokuwa mwanzo.


Safari iliendelea kwa mwendo wa wastani kuelekea hospitali ya Mountenia huku ndiko Inspekta Aron alichagua kumpeleka Najma akafanyiwe matibabu kwani alijua atakuwa karibu pia na Annah msichana aliyetakiwa kumlinda kwa udi na uvumba, hakujua tayari Tino na kikosi chake wameshafika eneo la hospitali kwa ajili ya kumuua Annah.
Inspekta Aron na Najma waligeuka mabubu kwa muda wote waliokuwa ndani ya gari kila mtu alikuwa akimuangalia mwenzake kwa macho ya kuibia ibia.


Nje ya hospitali ya kimataifa ya Mountenia majadiliano kati ya Tino na kikosi chake yalikuwa yakiendela wakiulizana ni vipi wataweza kukitambua chumba alicholazwa Annah.
"Kivipi Tino tuko wachache tutakagua hospitali nzima? au tuwateke wafanya kazi kisha tuwaulize?"
"Acha maswali mengi, ninao mpango wa kujua ni wapi alipo Annah, wewe fuata maelekezo yangu" Tino aliongea kwa kujiamini.

"Sawa basi tunakusikiliza mkuu"
"Ni kweli hatujui ni wapi Aron kamficha Annah lakini nina uhakika yupo ndani ya hii hospitali, sasa Aron mwenyewe ndiye atakayetupeleka hadi kwenye chumba alichopo Annah"
"Kivipi? tutamteka Inspekta Aron au?"
"Hapana sio hivyo nimewambia ninao mpango ninyi subirini mtaona"
Kikosi kizima kikawa kimya kusikiliza mpango ulivyo, walimuelewa sana Tino alikuwa akifanya mambo yake kwa akili sana na hii ndio sababu aliaminiwa sana na Waziri wa afya Dokta Gondwe.


Upande wa pili kwa mheshimiwa Waziri wa afya Dokta Gondwe mambo yalikuwa mazito mno, bado mpaka sasa alikuwa hajazunguza chochote mara tu baada ya ile sauti kutoka kwa mtu aliyekuwa anazungumza naye kumwambia wanahitaji vimelea vya V-COBOS. Dokta Gondwe alichoka mwili na akili.

"Najua hukutegemea kusikia kitu kama hiki Dkt Gondwe kwa sababu ni moja kati ya vitu unavyoamini ni siri kubwa lakini kwa sasa huna chaguo lingine, sisi tunahitaji hivyo vimelea vya V-COBOS tunajua unaouwezo wa kutupatia kutoka maabala kuu ya serikali, kama ukishindwa basi kubali kuaibika, tutaziachia hizi video zako za ngono mtandaoni. Tunakupa muda wa kufikiria tutakutafuta tena baadae mheshimiwa" Baada ya maelezo hayo simu ikakatwa
Dokta Gondwe aliitupia simu yake kitandani, macho yake akawa ameyakaza kutazama kabati kubwa la nguo lilikuwa mbele yake, wala presha yake haikupanda kama ilivyokuwa awali.
Dokta Gondwe alijua sasa ni wakati wa mapambano tena makali sana, suala la vimelea vya V-COBOS lilikuwa ni nyeti mno tena lililo chini ya mamlaka ya watu wakubwa kutoka nchini Mexico hawa ndio walioviingiza vimelea hivi kwa siri. Uwepo wa vimelea vya V-COBOS nchini ilikuwa ni siri ya watu wachache sana, hata serikali ilikuwa hailewi chochote.
Alishindwa kuelewa mtu huyu ni nani na kajuaje kuhusu vimelea hivi. Hakujua kama kijana wake Tino ndiye aliyekuwa akichezesha mchezo wote huu, licha ya kwamba alikuwa hospitali ya Mountenia kwa sasa lakini alielewa kila kitu kinachoendelea kwa bosi wake. Tino ndiye haswa aliyekuwa akivitaka vimelea hivyo vya V-COBOS, haikujulikana kaijuaje siri hii licha ya kwamba yupo karibu na mheshimiwa Dkt Gondwe lakini bado haikuwa rahisi kwake kujua.

Dokta Gondwe alisogea hadi lilipo lile kabati akachuchumaa na kufungua droo ya chini kabisa, akapekuwa vitabu vilivyokuwa ndani ya droo hiyo, akatoa kitabu kimoja kikubwa kisha akakifunua. Katika ya kitabu hicho kulikuwa na simu ndogo aina ya Huawei. Dkt Gondwe akaichukua na kubonyeza vitufe kadhaa kisha akaiweka sikioni.

Simu iliita upande wa pili kwa mheshimiwa Profesa Cosmas Kulolwa Rais mstaafu wa awamu iliyopita

Akiwa ndio anaingia chumba cha mazoezi Profesa Kulolwa alishituka baada ya simu yake kuita. Kilichomshtua si simu kuita hapana bali aina ya namba iliyompigia alitambua moja kwa moja kuna tatizo, Profesa Kulolwa akapokea simu.

"Nini shida?" Profesa Kulolwa aliuliza kwa sauti ya chini sana huku akiwa ametega sikio lake kwa makini
"Tuko kwenye hatari mkuu" dokta Gondwe alisikika upande wa pili akiongea kwa sauti ya chini vilevile
"Hatari ipi"
"Ni kuhusu vimelea vya V-COBOS"
"Imekuwaje tena? situlikubaliana kikao kinachofuata tukutane nao Ufaransa?"
"Hapana wala tatizo halipo kwao, tatizo tunalo sisi hapa nchini kwetu mkuu, kuna mtu kaingilia mchezo"
"Ooh! Mungu wangu, yanataka kutokea kama yale ya mwaka juzi, hebu naomba tukutane sasa hivi uko nyumbani nikufuate?"
"Hapana nyumbani si salama sana binti yangu Najma alisharudi kutoka Nairobi, tukutane ubarozini"
"Sawa"
"Sawa"
Simu zikakatwa.


Dakika kumi na sita zilitosha kabisa kumfikisha Inspekta Aron na Najma katika hospitali ya Mountenia. Tangu walipotoka kule Gerezani hakuna aliyekuwa amezungumza na mwenzake zaidi ya kutazamana kwa kuibiana. Hali hii pia ilimshangaza Najma mtoto wa kishua wa mheshimiwa Waziri wa afya ambaye yupo kwenye mtihani mzito wakati huu.
Najma alitamani kuwasiliana na baba yake amtaarifu kuhusu tatizo alilolipata kule gerezani wakati ameenda kumuangalia Osward lakini alisita kutokana na hali aliyonayo baba yake Dokta Gondwe, aliogopa kuifanya presha yake ipande tena.

Wakati Inspekta Aron akielekea sehemu maalum ya kuegesha magari nje ya hospitali ya Mountenia, ghafula roho yake ikafyatuka paa! kuna kitu aliona.
Ndiyo kilikuwa sio kitu cha kawaida, Inspekta Aron aliliona gari la kaka yake Tino likiwa ni moja ya magari yaliyosimama pale nje akajua moja kwa moja kaka yake Tino yupo hapo hospitali ya Mountenia.

"Mungu wangu, Annah! amekuja kumuua Annah" Inspekta Aron alisema kwa sauti ya chini lakini iliyoweza kupenya vizuri kwenye masikio ya Najma
"Vipi kuna nini? mbona hivyo? nani amekuja kuua?" Najma aliuliza maswali mfurulizo lakini Aron hakuwa na mda wa kueleza, alichomoa bastola yake kutoka kiunoni akaikoki kisha akairudisha tena ilipokuwa.

"Nakuja" alisema Aron, akafungua mlango na kutoka nje ya gari kwa kasi akaanza kuelekea lilipokuwa gari la kaka yake Tino. Alipofika akachungulia ndani ya gari akagundua hakuna mtu.

"Yupo ndani" Aron alijisemea mwenyewe na haraka akaanza kukimbia kuelekea mlango mkuu wa kuingia ndani ya hospitali hiyo kubwa ya kimataifa.
Najma aliyashuhudia yote haya akiwa ameachwa mwenyewe ndani ya gari, alishindwa kuelewa ni nini kinaendelea lakini tayari alishajua kuna kitu hakiko sawa. Alitamani kushuka ili aendelee kumfuatilia Inspekta Aron lakini hakuweza bado mguu wake ulikuwa unamuuma sana.

Inspekta Aron alikuwa akikimbia kwa kasi sana, akawa anapishana na wagonjwa pamoja na wahudumu wengine wa hospitali hiyo ambao waligeuka na kumtazama kwa mara ya pili wasijue mwanaume alikuwa kazini. Kwa kasi ile ile Aron alimaliza kupandisha ngazi za ghorofa ya kwanza sasa alikuwa anaelekea ghorofa ya pili.
Dakika nne pekee zikimtosha kufika hadi kilipo chumba cha siri alicholazwa Annah. Alifika na kuwakuta askari wake aliowaacha wakiwa wamesimama imara nje ya kile chumba.

"Anna yuko wapi?" Inspekta Aron aliuliza bila hata kusalimia, askari wake wakatazamana
"Yuko ndani mkuu" alijibu mmoja wa askari wale
Inspekta Aron alisukuma mlango na kuingia ndani kwa kasi macho yake akayatupa kitandani moja kwa moja.

JE, NINI KITAFUATA?
ANNAH YUKO SALAMA?
HIVI VIMELEA VYA V-COBOS NI KITU GANI HASA?
ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..........09
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

09-(TINO vs ARON)
ILIPOISHIA...
"Anna yuko wapi" Inspekta Aron aliuliza bila hata kusalimia, askari wake wakatazamana
"Yuko ndani mkuu" mmoja akajibu
Inspekta Aron alisukuma mlango na kuingia ndani kwa kasi macho yake akayatupa kitandani moja kwa moja.

SASA ENDELEA...
Annah alikuwepo kitandani tena alikuwa tayari amerejesha fahamu zake
"Annah upo sawa" Inspekta Aron aliuliza huku akisogea taratibu pale kitandani
"Mkuu daktari alituambia tusiruhusu mtu kuingia bila kuvaa PPE ni hatari kwa mgonjwa" mmoja wa askari aliongea akiwa amesimama mlangoni

"Najua usijali" Alisema Inspekta Aron huku akiinama na kushikiria magoti akaanza kuvuta na kutoa pumzi kwa nguvu, hakika alikuwa amechoka sana baada ya kukimbia kwa muda mrefu. Wakati ameinama akili yake ilikuwa ikifanya kazi, aliwaza kuhusu kaka yake Tino ambaye anao uhakika yupo ndani ya hospitali hiyo.

"Yuko wapi huyu? au amekuja kumuona mama, mbona sio kawaida yake" aliwaza Inspekta Aron akihisi labda Tino amekuja kumuona mama yao ambaye amelazwa hospitalini hapo tangu mda mrefu.

"Naitwa Aron mimi ni polisi mpelelezi, nipo hapa kwa ajili yako Annah pole kwa yaliyokukuta lakini usijali uko salama nikirudi tutaongea vizuri kwa sasa pumzika kwanza" Inspekta Aron alijieza kwa kifupi kisha akaanza kutoka

"Po..polisi" Annah aliita kwa taabu kidogo huku akiinuka na kukaa pale kitandani, Inspekta Aron aliyekuwa amefika mlangoni alisimama na kugeuka.
"Nakuomba mara moja" alisema Annah kwa sauti ya chini akimtaka Inspekta Aron asogee, akafanya hivyo.

Inspekta Aron akasogea na kukaa kitandani pembeni ya Annah na hapo ndipo alipopata wasaa wa kumtazama binti huyo kwa ukaribu zaidi, alikuwa ni mzuri sana licha ya uso wake kuonekana wenye majonzi baada ya kulia kwa muda mrefu lakini haikuwa sababu ya kuuficha uzuri wake, Annah alijaliwa mashallah.
"Eti ni kweli baba na mama yangu wamekufa yaani hawapo tena Duniani?" Annah aliuliza swali huku akishindwa kuyazuia machozi yaliyoanza kumtiririka kama maji kwa mara nyingine.
Inspekta Aron alijikuta anaingia kwenye jukumu lingine la kumbembeleza anyamaze, ni kweli Annah alikuwa katika simanzi nzito sana. Kumbukumbu ya wazazi wake wakiuwawa kikatili mbele ya macho yake ilimganda kichwani, kila alipofumba na kufumbua macho yake taswira ile ilimrudia. Annah alilia, alilia sana akiwalilia wazazi wake wakati huo akiwa amejilaza kwenye kifua cha Inspekta Aron aliyekuwa akimpiga piga mgongoni kumfariji.

"Annah ilikuwa na wewe ufe, walidhamiria kukua pia lakini mungu amekunusuru kwa makusudi kabisa ili tu uwawajibishe wote waliohusika kufanya unyama huu. Annah usiogope, upo na mimi nitakulinda hadi siku utakapopata haki yako" Inspekta Aron alijaribu kutoa maneno ya faraja kwa Anna.

"Lakini kwa nini, kwa nini yule Waziri wa afya ni katili kiasi hiki sisi tulimkosea nini, ee Mungu wangu kwa nini umenipa adhabu hii baba nitawezaje kuishi yatima mimi aaa.." Annah alilia
"Okay kwa hiyo unataka kusema miongoni mwa watu waliotekeleza mauji haya waziri wa afya alikuwepo?" Aliuliza Inspekta Aron
Annah akatikisa kichwa kukubali.
"Unahakika, ulimuona?"
Annah akatikisa kichwa chake tena kukubali.
Hizi zilikuwa ni habari njema sana kwa Inspekta Aron, sasa alianza kujiona shujaa ambaye atakwenda kuuangamiza mtandao mzima wa Dokta Gondwe.
Mwanzo alitegemea Annah na familia yake watasimama kama mashahidi kwenye kesi ya mauaji aliyofanya Osward ambaye ni miongoni pia mwa watu waliopo kwenye mtandao wa Dokta Gondwe. Lakini sasa Annah amekuwa pia shahidi atakayethibitisha kuwa dokta Gondwe anahusika na mauaji ya wazazi wake.
Kabla ya yote ilikuwa ni lazima Inspekta Aron ahakikisha anamlinda Annah kwa gharama yoyote ile. Alimjua mbaya wake wa kumdhibiti mapema ni kaka yake Tino, huyu ndiye aliyekuwa kibaraka mkubwa wa Dokta Gondwe.
Baadae Annah alitulia, Aron akaona hiyo ndio nafasi ya kutoka
"Pumzika kwanza Annah, natoka mara moja nitarudi baada ya muda mfupi" alisema Aron huku akimlaza Annah taratibu kisha akatoka, nje akawakuta askari wake watatu ambao tayari walionyesha kuanza kuchoka baada ya kukaa hapo kwa muda mrefu. Aron akawasogelea na kuwatazama mmoja baada ya mwingine
"Sikilizeni, mda wote mnatakiwa muwe makini kunamazingira ambayo si salama sana hapa hospitali narudia tena ongezeni umakini sawa"
"Sawa mkuu"
"Enh! Inspekta Jada bado hajarudi?"
"Hajarudi ali..aah huyo hapo kafika mkuu"
Inspekta Aron alipiga hatua kumfuata Inspekta Jada mwanamke aliyefanya kazi kwa ukaribu sana na yeye, ndiyo kwanza alikuwa anaingia. Wote wawili wakasogoea pembeni na kuanza kuteta jambo

"Enhe! Mambo yamekwendaje Jada"
"Nimefanikiwa kuongea na ndugu wa Annah watafanya mazishi ya baba na mama Annah kesho"
"Sawa kuhusu Annah umewambiaje?"
"Nimewambia yupo hospitalini mahututi, kwa sababu za kiusalama sijawambia ni wapi"
"Safi"
"Vipi hapa kwema?"
"Si kwema sana, Tino yuko hapa hospitali nadhani wameshajua Annah yupo hai wanamtafuta"
"Mmh! sasa tunafanyaje? Na vipi hali ya Annah?"
"Kaamka"
"Wow! vipi kaongea"
"Ndiyo, kasema dokta Gondwe alikuwepo miongoni mwa wale watu waliowaua wazazi wake"
"Nini? Inspekta Aron tunasubiri nini, tukachue arrest warrant tukamkamate"
"Hapana, yule ni Waziri wa afya mtu mkubwa huwezi kumkamata kizembe hivi...."
"Inspekta Aron lakini ni...."
"Sikiliza Jada, lengo letu si dokta Gondwe pekee ila mtandao wake mzima akiwemo kaka yangu Tino"
"Mmh! sawa nimekuelewa"
"Sawa nenda kakae na Annah jaribu kumuweka sawa kisaikolojia mimi nakwenda kumuangalia Tino kule chini alipolazwa mama"
"Sawa" alijibu Jada kisha kila mmoja akaelekea upande wake


Ghorofa ya kwanza upande wa kushoto mwishoni ndani ya hospitali ya Mountenia ndipo vilipokuwepo vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU).
Katika eneo hilo Tino kaka yake Aron alionekana amesimama nje ya chumba kimoja chenye mlango wa kioo. Ndani ya chumba hicho mama mmoja alikuwa amelala juu kitandani, pua na mdomo wake vilifunikwa na maski iliyounganishwa moja kwa moja na mtungi wa hewa ya oksijeni. Huyu hakuwa mwingine bali mama yake Tino na Aron mke wa mwanajeshi mstaafu ambaye kwa sasa ni marehemu Jenerali Phillipo Kasebele. Mama huyu maarufu kama madam Sultana kwa sasa alikuwa amemaliza miezi sita tangu alale kitandani hapo akiwa hajitambui, alikuwa akiumwa ugonjwa ambao hata madaktari wenyewe walishindwa kuutolea maelezo ya kueleweka.
Tino alikuwa amesimama wima mlangoni nje ya chumba hicho huku macho yake akiwa ameyakaza kumtazama mama yake pale kitandani. Mara simu yake ikatoa mlio ukiashiria kuna ujumbe wa maandishi, Tino akaufungua haraka na kuusoma.

,,,,,Mpango wako umefanya kazi mkuu, tayari tumeshajua ni wapi walipomficha Annah,,,,,

Tino alimaliza kuusoma ujumbe huo kisha akatabasamu, ni kweli walikuwa wamemchezea Inspekta Aron mchezo wa akili kiasi cha kumfanya yeye mwenyewe awapeleke hadi chumba alicholazwa Annah, kivipi? Ilikuwa hivi...
Tino alipaki gari lake katika eneo la wazi kwa makusudi kabisa aliamini kama mdogo wake Aron angefika na kuliona basi lazima angehisi moja kwa moja kuwa amekuja kumuua Annah hivyo angewahi kwenda kwenye chumba cha Annah kumuangalia na hivi ndivyo ilivyokuwa.
Mara tu baada ya Inspekta Aron kuanza kukimbia kuelekea ndani ya hospitali ya Mountenia tayari Tino alishawapanga vijana wake wawili ambao walianza kumfuatilia kwa nyuma hadi pale Aron alipofika na kuingia chumba alicholazwa Annah bila kujua anafuatiliwa.
Tino alijua pia kama Aron hata muona basi atakuja moja kwa moja ICU kuhakikisha kama kweli Tino yupo hospitali hapo kwa ajili ya kumuona mama yao madam Sultana.
Ni kama vile Tino alikuwa kwenye akili ya Inspekta Aron, kila alichokiwaza ndicho kilichotokea. Mara tu baada ya kimaliza kuusoma ule ujumbe alisikia mlango wa lifti ukifunguka na kufungua kisha vishindo vya mtu anaekuja nyuma yake taratibu vikasikika
Huyu hakuwa mwingine bali Inspekta Aron ambaye alitembea taratibu na kwenda kusimama pembeni ya kaka yake Tino. Wote wakawa wameelekeza macho yao mbele kumtazama mama yao hakuna aliyegeuka kumtazama mwenzake usoni. Walidumu katika hali hiyo kwa zaidi ya dakika tatu mfurulizo, hakuna aliyefungua kinywa kuongea na mwenzake kila mmoja alionekana akiwaza lake.
Tino aliwaza kumuua Annah lakini pia aliwaza kuhusu vimelea vya V-COBOS ambavyo ndiyo ilikuwa lengo lake kubwa na hii ndiyo sababu ya yeye kujiweka karibu na Waziri wa afya Dokta Gondwe. Tino hakuwa mtu wa kawaida kama alivyoonekana, alikuwa ni mtu mwenye siri na mipango mikubwa sana aliyofanya kimya kimya tena kwa akili sana, haijulikani ni wapi au ni vipi aliijua siri hii ya vimelea vya V-COBOS.
Inspekta Aron pembeni yake yeye aliwaza tu namna atakavyoendeleza jukumu lake la kuhakikisha anauangusha mtandao mzima wa Tino na Dkt Gondwe. Tayari anashahidi anaemtegemea na kumilinda kwa nguvu zote, Annah.

"Usijali mama atapona" hatimae aron alifungua kinywa kuzungumza. Tino alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha nae akajibu
"Ndiyo lazima apone, mama yetu hawezi kufa"
"Ni kweli hawezi kufa, baba alitukabidhi kwake"
"Atapona"
"Atapona"
Inspekta Aron na Tino waliongea kwa namna ya kufarijiana lakini kila mmoja akili yake ilikuwa mbali, wala haikuwa hapo.
ITAENDELEA....
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya...........10
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

10-(GODWIN MDUNGUAJI)
ILIPOISHIA...09
"Usijali mama atapona" hatimae aron alifungua kinywa kuzungumza. Tino alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha nae akajibu
"Ndiyo lazima apone, mama yetu hawezi kufa"
"Ni kweli hawezi kufa, baba alitukabidhi kwake"
"Atapona"
"Atapona"
Inspekta Aron na Tino waliongea kwa kufarijiana lakini kila mmoja akili yake ilikuwa mbali, wala haikuwa hapo....

SASA ENDELEA...
"Lakini sio kawaida yako kuja kumuona mama, leo nini kimekupata kaka" Aron alijaribu kumchimba kaka yake
"Sio kawaida yangu ndiyo, lakini huwa nakuja kwa hiyo hakuna cha ajabu hapo" Tino alijibu huku akitabasamu kiasi
"Nakumbuka mlikuwa mnagombana sana na mama, mara nyingi alikuwa anachukizwa sana na mienendo yako ukawa unakwepa hata kuonana naye, siku akiamka akasikia kama ulikuwa unakuja kumtembelea kama hivi atafurahi sana"
"Ni mama yangu, hata kama sikuwa naelewana naye lakini bado atabaki kuwa mama na ndio sababu nafanya juu chini kulipia matibabu yake kuhakikisha anapona"
"Kuua watu ndio kufanya juu chini" Inspekta Aron aliendelea kumuuliza kaka yake maswali ya kichokozi. Kabla Tino hajajibu chochote simu ya Aron iliita akaichukua kutoka mfukoni na kutazama mpigaji, ilikuwa ni namba ngeni, akapokea .

"Ndiyo, Inspekta Aron naongea...." Alisema Aron baada ya kupokea.
Mara Inspekta Aron akageuka taratibu na kumtazama Tino usoni, ilikuwa ni ishara tosha kuwa jambo alilolisikia upande wa pili wa simu ile halikuwa la kheri na lilihusiana moja kwa moja na kaka yake Tino.


Wakati ule Inspekta Aron ametoka ndani ya gari kwa kasi, alimuacha Najma ambaye hakuweza kufanya chochote kutokana na maumivu makali ya mguu aliyokuwanayo baada ya kuumia kule gerezani. Najma alishindwa kuelewa ni kipi kimemfanya Inspekta Aron atoke kwa kasi vile, akawaza pengine yupo kwenye majukumu ya kikazi. Na ndivyo ilivyokuwa, Inspekta Aron alikuwa akiwahi kwenda kumuangalia Annah akiamini kaka yake Tino ameingia hospitali ya Mountenia kumuua.

Wakati Inspekta Aron akiingia hospitali humo huku Najma aliwaona wale vijana wa Tino ambao walijitokeza nyuma ya gari walilokuwa wamejificha wakaanza kumfuatilia Inspekta Aron nyuma yake kwa siri.

Akili ya Najma iliweza kung'amua kuwa kuna jambo ambalo si la kawaida lilikuwa likiendelea katika hospitali hiyo. Alitamani kumjulisha Inspekta Aron kuwa nyuma yake kuna watu wanamfuatilia lakini angewezaje, hakuwa na mazoea na kaka huyo hata namba yake yasimu hakuwa nayo.

"Mungu wangu nitafanyaje" Najma aliwaza huku nafsi yake ikitamani sana kumsaidia Inspekta Aron kama yeye alivyomsaidia kule gerezani na kumleta hospitali licha ya kwamba hakuwa amehudumiwa hadi dakika hii.
Mara ghafula kuna wazo likamjia, haraka akachukua simu yake na kumpigia baba yake Dokta Gondwe. Simu iliita kwa muda mwisho ikapokelewa.

"Hallo baba"
"Ndiyo Najma mwanangu" Dkt Gondwe aliitikia upande wa pili akiwa katika jengo la ubarozi ndani ya chumba kimoja ambacho alikutana na Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa kwa ajili ya mazungumzo.

"Baba nina shida"
"Shida gani mwanangu"
"Noamba namba ya yule kaka askari aliyemfungulia Osward mashataka"
"Nani, Inspekta Aron?"
"Yes! huyo huyo"
"Za nini wewe?"
"Baba ninashida naye naziomba sasa hivi"
"Sawa, nakuliza unashida gani na inspekta Aron?"
"Hivi utaendelea kuniuliza maswali yako au unanipa hizo namba?" Najma aliuliza swali huku akijua fika udhaifu wa baba yake, asingeweza kuendelea kumbishia

"Sawa nakutumia sasa hivi" alijibu Dkt Gondwe kisha akakata simu. Badala ya kutuma namba Dokta Gondwe aliendeleza mazungumzo na Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa. walikuwa wakijadili suala nyeti kuhusu usalama wa vimelea vya V-COBOS. Hadi dakika hiyo walikuwa hawajui ni nani haswa anahitaji vimelea hivyo akimtisha Dokta Gondwe kwamba endapo atashindwa kumpatia vimelea vya V-COBOS basi atazisambaza video zake chafu mtandaoni.

Dokta Gondwe na profesa Kulolwa walijikuta kwenye mtihani mzito wakihohofia pia usalama wa maisha yao kwani watu waliokuwa nyuma ya mpango huo madhubuti wa vimelea vya V-COBOS hawakuwa na mchezo hata kidogo, hili lilikuwa ni suala nyeti sana. Waliogopa kufanya makosa ambayo yanaweza hata kuwaghalimu maisha yao.

Najma akiwa ndani ya gari la Inspekta Aron aliendelea kusubiri atumiwe zile namba na baba yake.
Kwa mbali Big' alionekana akiwa upande wa pili wa barabara usawa wa geti kubwa la kuingilia hospitali ya Mountenia. Alikuwa akichukungulia na kufuatilia kwa ukaribu gari la Inspekta Aron ambalo alikuwa ametega bomu chini yake. Uwepo wa Najma ndani ya gari hiyo ndio uliomzuia Big asifanye kazi yake. Aliendelea kusubiri akiamini utafika muda Aron atabaki mwenyewe ndani ya gari na hapo ndipo atamsambaratisha kwa kuruhusu bomu lile lilipuke, jambo jema kwake ni kwamba rimoti yake ilikuwa na uwezo wa kufanya kazi hata kama bomu likiwa umbali wa kimomita moja kutoka alipo.
Zilikuwa zimepita dakika tano mpaka sasa bado mheshimiwa Dkt Gondwe alikuwa hajamtumia binti yake namba ya Inspekta Aron.

Najma akiwa amekasirika aliwaza ampigie tena baba yake lakini mara kuna ujumbe ukaingia kwenye simu yake, tayari Dkt Gondwe alikuwa umemtumia namba.
Bila kuchelewa Najma alipiga ile namba, ikaita sekunde chache na kupokelewa.
"Aron" Najma aliita
"Ndiyo, Inspekta Aron naongea" sauti ya kiume iliyojaa kitetemeshi ilisikika upande wa pili, alikuwa ni Inspekta Aron mwenyewe wakati huo alikuwa amesimama na kaka yake Tino nje ya chumba alicholazwa mama yao.

"Aron, mimi ni Najma uko wapi? Uko salama? Wakati unaingia hospitali kuna watu wawili niliwaona wanakufuata nyuma, vipi kuna tatizo hawajakudhuru?" Najma aliuliza maswali mfurulizo akitamani kujua kama Inspekta Aron yupo salama, ulijikuta anajali sana usalama wa mwanaume huyo kiasi cha kufanya hadi yeye mwenyewe ajishangae na kujishtukia, haikuwa kawaida yake kabisa.
Maelezo ya Najma yaliifanya akili ya Inspekta Aron kuunganisha matukio kwa kasi akajua moja kwa moja ule ulikuwa ni mtego, kama alikuwa akifuatiliwa basi ilikuwa ni njama ya kutaka kujua ni wapi alipo Annah. Inspekta Aron alijikuta anajilaumu kwa nini hakushtuka mapema.
Hakuwa na sababu ya kujiuliza mara mbili mbili akajua moja kwa moja huo ulikuwa ni mpango wa mtu ambaye yuko pembeni yake wakati huu yaani Tino kaka yake.

Inspekta Aron ageuka taratibu na kumtazama Tino usoni huku simu ikiwa bado sikioni mwake.
"Hallo...hallo... Aron unanisikia" Najma alikuwa akiongea upande wa pili baada ya kuona Inspekta Aron yupo kimya hasemi chochote.

"Okay okay nimekupata" Inspekta Aron alijibu kwa kifupi sana kisha akakata simu hakutaka kumfanya kaka yake ajue kama ameshamshtukia mchezo alioufanya.

"Naondoka, tutaonana baadae" Aron aliaga na kuondoka, akaingia kwenye lifti kisha akapanda juu kuangalia usalama wa Annah kwa mara nyingine, tayari alishajua yupo hatarini.
Mara tu baada ya Inspekta Aron kuondoka, Tino naye hakutaka kupoteza muda aliteremka kwenye ngazi upesi akapiga hatua ndefu ndefu na mwisho alifika chini kabisa ya hospitali hiyo akatoka nje.
Akiwa mlangoni Tino alikutana na wale vijana wawili.

"Mpango umekwenda vizuri"alisema Tino huku wakiongoza kurudi kwenye gari lake
"Ndiyo tumeshajua chumba cha Annah"
"Sawa, sasa sniper G' najua unaelewa nini cha kufanya tafuta usawa mzuri kwenye ghorofa ya upande wa pili kule hakikisha unamchapa risasi ya kichwa huyu binti, nakupa masaa sita tu uwe umemaliza kazi" Tino alitoa maelezo kwa kijana wake ambaye alikuwa ni mtaalamu wa kutumia bunduki zile za masafa marefu yaani mdunguaji (Sniper)
Sniper G' kama jina maarufu lakini aliitwa Godwin alifungua buti la gari akatoa begi moja kubwa na refu akalivaa mgongoni kisha akaanza kuondoka kuelekea ghorofa iliyokuwa jirani na hospitali ya Mountenia, huku ndiko aliamini atapata usawa mzuri wa kumlenga Annah shabaha ya kichwa, akawaacha Tino na wenzake ambao waliingia kwenye gari na kuondoka.

Wakati heka heka hizi zikiendelea Najma alikuwa akishuhudia yote akiwa ndani ya gari ya Inspekta Aron, si yeye peke yake hata Big' naye akiwa nje ya hospitali upande wa pili wa barabara alikuwa akishuhudia pia



Je, nini kitafuata?
VIMELEA VYA V-COBOS NI KITU GANI?
ARON ATAWEZA KUMLINDA ANNAH DHIDI YA MDUNGUAJI(SNIPER G')?
VIPI KUHUSU BOMU CHINI YA GARI LAKE?
ITAENDELEA.....
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya.........11
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

11-(AISHIIIII-NAUMIA)
ILIPOISHIA..10
Mpango aliousuka Tino unaleta mafanikio chanya na hatimae anafanikiwa kukitambua chumba alicholazwa Annah, haraka anamtuma mdunguaji wake mashuhuri sniper G' kuhakikisha anamuua Annah. Wakati huo huo Inspekta Aron anashtukia mchezo alioufanya kaka yake Tino.
Upande wa pili majadiliano kati ya Waziri wa afya Dokta Gondwe na Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa yalikuwa yakiendela wakijadili kuhusu vimelea vya V-COBOS.

JE, NINI KITAFUATA?

SASA ENDELEA...
Ndani ya jengo la ubarozi mazungumzo nyeti kati ya Rais mstaafu mheshimiwa Profesa Cosmas Kulolwa na Waziri wa afya Dokta Isaack Gondwe yalikuwa yakiendela.

"Kwa hiyo unasema mtu aliyekutumia hizo picha zako za X ndiyo huyo anahitaji vimelea vya V-COBOS?" profesa Kulolwa aliuliza
"Ndiyo profesa yaani hapa nimechanganyikiwa sielewi nifanye nini, nimejaribu kumbembelaza akubali kuchukua pesa yoyote atakayo lakini wapi kakataa katakata, alafu kinachonishangaza huyu mtu kajuaje kuhusu vimelea vya V-COBOS"
"Dkt Gondwe sikiliza, aliyefanya hivi lazima awe ni miongoni mwa watu wanaoujua huu mpango wa vimelea vya V-COBOS anataka kutuzunguuka tu, anaweza akawa ni wa hapa hapa nchini kwetu au ni hawa wakubwa zetu kutoka Mexico wanageukana wenyewe kwa wenyewe"
"Ni kweli hilo hata mimi niliwaza, lakini kama ni wao mbona wanajua kabisa vimelea vipo ndani ya Maabala kuu ya serikali kwa nini asimtumie mkemia mkuu ambaye naye ni mmoja wetu anajua siri hii ya uwepo wa vimelea vya V-COBOS hapa nchini, kwa nini waje kunishambulia mimi"

"Acha kujiuliza kwa nini mimi, tufikiri tunafanyaje"
"Labda tuwape taarifa wakubwa kuwa kuna mtu anavitaka vimelea" Dkt Gondwe alitoa wazo
"Hapana hapo tutawasha moto mwingine kama ule wa mwaka juzi, kumbuka hili ni suala ambalo hawa ndugu zetu wazungu wamelipanga kwa zaidi ya miaka 10, siku wakivisambaza hivi vimela vya V-COBOS wanategemea kuvuna mabilioni ya pesa kutoka nchi zote Dunia, kumbuka walitaka kuviachia mwaka juzi lakini vikaibuka virusi vya korona wakasema tusubiri. Sisi tumeaminiwa Dkt Gondwe hatutakiwi kuwaangusha hata kidogo wakisikia kuna mtu anaviwinda vimelea kutoka kwetu nakuhakikishia watatuua" profesa Kulolwa alitoa maelezo ya kina.

"Sasa nitafanya profesa, huyu mtu ana video zangu za utupu, na mbaya zaidi siku hiyo nilikuwa na mke wa mtu tena mke wa kijana wangu ambaye namwamini sana"
"Sikiliza Dokta Gondwe, tumia akili fanya hivi mhakikishie kuwa utampa hivyo vimelea anavyovitaka kisha wewe muwekee mtego alafu mdhibiti. Mbona unavijana wazuri tu wa kazi wanaweza kufanya bila shida yoyote, kama huyu unamwita Tino yule jamaa ni professional sana mtumie"
"Mmh! Tino siwezi kumtumia kwa sababu yeye ndio haswa nilitembea na mke wake siku hiyo, yaani hizo picha na video nipo na mke wake vipi kama akitaka kujua undani wa hiyo kazi"
"Wewe mpe kazi usimwambie kwa nini anafanya"

Dokta Gondwe alitulia kwa muda akijaribu kuutafakari ushauri aliopewa na na Profesa Kulolwa, akaona kwa kiasi furani unafaa.

***********
{TANGAZO:- Epuka matapeli simulizi hii imetungwa na SAUL DAVID simu 0756862047, Tafadhali usinunue kwa mtu mwingine tofauti }
******-*-

Zilikuwa zimepita dakika 20 mpaka sasa tangu Aron alipokata simu ya Najma. Bado alikuwa ndani ya gari ya Inspekta Aron pale nje ya hospitali ya Mountenia, wasiwasi ulimjaa binti huyu wa kishua mtoto wa Waziri, ilifika mahali yeye mwenyewe akaanza kujishangaa imekuwaje anamjali sana Aron.
Akiwa katika hali hiyo mara kwa mbali alimuona Inspekta Aron anakuja akitokea ndani ya hospitali ya Mountenia. Mkono wa kulia alikuwa ameshikilia begi dogo jekundu lenye msalaba mweupe, lililokuwa ni begi la huduma ya kwanza 'first aid'.
Najma alijikuta akiingiwa na kaubaridi ka furaha akawa anamtazama Aron tangu alipokuwa mlango wa hospitali hadi alipofika kwenye gari.
Aron alifungua mlango wa kulia wa siti za nyuma alipokuwa Najma akaingia na kukaa pembeni yake.

"Uhuuu!" Aron alivuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu kisha akageuka kumtazama Najma usoni, wakatazamana.

"Vipi?" Aliuliza Aron
"Poa" Najma alijibu kwa sauti iliyotokea puani
"Sorry nilikuacha mwenyewe ghafula"
"Kulikuwa na nini mbona mikiki mikiki ilikuwa mingi hapa"
"Aah! ni mambo ya kawaida tu ndio maisha yetu sisi tushazoea"
"Ooh! kutumia bastola kila wakati, yaani sekunde yoyote unaweza kufa mmh! mnatabu sio siri"
"Kawaida, hata ungekuwa wewe ungeweza tu"
"Ahahaha wallah siwezi kabisaa" Najma aliongea na kucheka hali iliyofanya Aron auone mwanya wa binti huyo mrembo ambao ulizidisha uzuri wake maradufu, Inspekta Aron akajikuta ameduwaa akimtazama.
"Nini?" Aliuliza Najma
"Nini nini?" Aron akauliza pia
"Mbona unaniangalia hivyo?"
"Aah! kwani ajabu, mbona hata wewe hapo unaniangalia" alijibu Aron na wote wakacheka kwa pamoja, taratibu wawili hawa wakajikuta wamezoeana kwa muda mfupi sana. Wakati huo wakiwa kwenye kilele cha furaha hakuna aliyejua kuwa chini ya gari waliyopanda kuna bomu limetegeshwa.

"Alafu unajua nini Najma" alisema Aron
"Ee nambie mkaka, alaa! samahani nambie afande"
"Mmh! muone niite Aron hivyo hivyo, afande ni yule anashinda na magwanda kila siku"
"Sasa kwa nini wewe huvaagi hayo magwanda"
"Mimi ni afisa mpelelezi alafu acha kwanza niongee nilichotaka kusema usiniingilie"
"Hahahah! haya sema afande..ooh sema Aron"
"Muone, nataka nikushukuru ile simu yako ilikuwa ya muhimu sana kwangu"
"Simu gani?"
"Kwani sio wewe umenipigia simu ukasema kuna watu wananifuatilia"
"Ooh! sawa ni mimi enh kwani kuliwa nini"
"Ah! Mambo ni mengi Najma ila asante, lakini kwani namba yangu ulitoa wapi? " Aliuliza Aron wakati akifungua kile kijibegi cha huduma ya kwanza
"Kwa baba"
"Baba? Baba gani?"
"Baba yangu"
"Unamaanisha dokta Gondwe"
"Yeah"
Aron alitulia kidogo akitafakari jambo, jina la dokta Gondwe lilibadilisha kabisa hali ya hewa mle ndani, huyu ndiye alikuwa mbaya wake, mtu anaeamini kamshika masikio kaka yake Tino, na ndio huyu huyu aliyewaua wazizi wa Annah.
Ni kama Najma alielewa ni kiasi gani habari za baba yake zimemtoa Aron kwenye mudi, naye akabaki kimya.
"Haya sogeza mguu wako nikutibu ulipoumia" alisema Aron
"Mmh!" Najma aliguna huku akitoa macho kumtazama Aron, wakatazamana tena.
"Nini?"
"Kwani unajua ni wapi nimeumia?"
"Ee si mguuni"
"Sawa mguuni lakini sehemu gani"
"Aah sijui" alijibu Aron huku akimtazama Najma usoni. Najma akaelekeza kidole chake mahali alipoumia, ilikuwa ni kwenye paja lake la kushoto.
Inspekta Aron akajikuta anamtazama pembeni kwa aibu, Najma akatabasamu.

"Basi twende ndani hospitali, sikujua mimi" alisema Aron
"Sawa twende lakini..."
"Lakini nini"
"Au basi, twende"
"Kutembea vipi, huwezi kujitahidi hata kidogo" aliuliza Aron huku akifungua mlango wa gari tayari kutoka
"Hapana siwezi inabidi unibebe tena.... lakini Aron"
"Ee nambie"
"Hebu funga kwanza huo mlango"
Inspekta Aron akafungua, akageuka na kumtazama Najma kwa macho ya kuuliza.
"Ulishawahi kwenda beach?" Aliuliza Najma
"Eeh niliwahi mara nyingi tu, wauzaji wa madawa ya kulevya mara nyingi huwa nawakamata maeneo kama hayo"
"Ooh! Basi nitibu tu mwenyewe sio lazima tuingie hospitali"
"Una maana gani?"
"Kwani unashindwa nini na beach huwa unaenda uliyoyaona beach ndio utayaona hapa wewe nitibu tu usijali dakika 0" alisema najima kisha akasimama na kufungua kifungo cha suruali yake ya jeans kisha akaanza kuivua taratibu

Inspekta Aron aliduwaa akataka kusema jambo lakini tayari alishachelewa Najma alikuwa ameshavua suruali yake akaishusha hadi usawa wa chini ya magoti, akabaki na nguo ya ndani pekee
"Mungu wangu, nini hiki" Inspekta Aron aliwaza huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio akapoteza kabisa kujiamini.

Wakati haya yote yakiendela yule jamaa aliyetegesha bomu chini ya gari la Inspekta Aron (Big') alikuwa kwa mbali akishuhudia, kwa kuwa vioo vya gari hilo vilikuwa vikionyesha kwa mbali Big' aliweza kumuona Najma amesimama na kuvua suruali yake.

"Alaah! Haka ka afande kumbe sio poa, kwa hiyo anataka kupiga vyombo kwenye gari, hahaha haki ya mungu Najma ni demu wa hovyo mbona namuona kama yuko serious sana mambo gani ya aibu anafanya sasa huyu mtoto wa waziri, haya sasa hizi habari nikimwambia Osward si atapagawa. Lakini sio mbaya sio mda afande anakwenda kufa, burudika kwa mara ya mwisho" alisema Big' huku akila ndizi alizonunua kwa wapita njia muda mfupi uliopita.

"Endelea na kazi Aron miguu yangu inahisi baridi" alisema Najma kwa sauti laini iliyozidi kumuweka Aron kwenye wakati mgumu. Halikuwa jambo jepesi kustahimili kuyaangalia mapaja laini ya mwanamke mrembo kama Najma.

"Acha ujinga Aron " hii ilikuwa ni sauti iliyopita kwenye mawazo ya Aron na hapo akagutuka na kujikuta anavaa ujasiri kama mwanaume.
Alichukua vifaa muhimu kwenye lile begi, kisha akaiinua miguu yote miwili ya Najma na kuinyoosha juu ya siti za nyuma, akavaa mipira mkononi kisha akachukua dawa na kuinyunyiza juu ya paja la kushoto la Najma kisha akaanza kuisugua taratibu kumchua.

"Aaaa...oooooh...mamaa
.. ishiiiiiii...naumia Aron taratibu" Najma alilalamika
"Vumilia kidogo namalizia" alisema Aron huku akipunguza kasi ya kumsugua
Angalau maumivu yalipungua Najma akajikuta anaanza kumkagua Aron kwa ukaribu wakati akiendelea kumtibu. Alimkagua kwanzia juu mpaka chini mwisho akatabasamu mwenyewe.

"Aron" Najma aliita

ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya.............12
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

12-(INSPEKTA ARON NYUMBANI KWA WAZIRI)
ILIPOISHIA...
"Vumilia kidogo namalizia" alisema Aron huku akipunguza kasi ya kumsugua.
Angalau maumivu yalipungua Najma akajikuta anaanza kumkagua Aron kwa ukaribu wakati akiendelea kumtibu. Alimkagua kuanzia juu mpaka chini mwisho akatabasamu mwenyewe.

"Aron" Najma aliita

SASA ENDELEA....
"Yes nambie Najma" Aron aliitika huku akiendelea kumchua Najma taratibu
"Hivi kwa nini unamchukia sana baba yangu?" Aliuliza Najma, Aron akasita kuendelea kumchua akatulia kwa muda kisha akaendelea tena.
"Kwa nini umeuliza?"
"Nataka tu kujua"
"Hapana simchukii baba yako ila nachukizwa na matendo yake"
"Matendo yapi hayo Aron?"
"Unajua mimi ni askari najua ninachokifanya siwezi kukurupuka tu na kuanza kumshutumu baba yako kwa vitu vya uongo, nimefanya utafiti wa kutosha kilichobaki ni kupata tu ushahidi wa kuthibitisha matendo yake maovu"
"Sawa lakini ni mda mrefu sana umeanza kumuandama baba yangu mpaka leo hakuna chochote umethibitisha huoni kama shutuma zako ni za uongo"
"Sijashindwa Najma, sitakiwi kuongea sana juu ya hili ila kwa kuwa nakuamini basi nitakwambia kitu, Baba yako dokta Gondwe ni mtu mkubwa ukiacha yeye kuwa Waziri wa afya lakini amekuwa akifanya kazi na vigogo wakubwa wakubwa hapa nchini, ndio maana hata kesi ya Osward mtoto wa yule tajiri Mzee Matula kamkabidhi baba yako ndio asimamie kuhakikisha Osward hafungwi, baba yako anamtandao mpana wa uharifu amewaua mashahidi wote ili Osward ashinde kesi mahakamani, moja kati ya vijana anaowatumia baba yako kufanya uharifu ni kaka yangu anaitwa Tino" Aron alitoa maelekezo ya kina, wakati huo tayari alikuwa amemaliza huduma kwa Najma.
Najma alitulia huku akiivaa suruali yake taratibu akawa anayatafakari maelezo ya Inspekta Aron
"Kwa hiyo ndio maana ukawa unaniomba mimi nikatoe ushahidi kwa kesi ya Osward, mbona mimi sikuwa naye wakati wa tukio nilikutana naye wakati tayari mauaji yameshafanyika kwa hiyo sijui chochote Aron" alieleza Najma huku akipokea kopo la vidonge kutoka kwa Aron

"Sawa Usijali, hivi ni vidonge vya maumivu unameza viwili kutwa mara mbili vitakusaidia"
"Asante Aron kwa msaada wako Mungu akubariki sana"
"Asante pia, kaa vizuri basi nikupeleke nyumbani"
"Aah! Nitapanda taxi Aron hata usijali"
"Hapana huwezi kupanda taxi na mimi nipo, kuwa huru tu ngoja nikupeleke chapu" Alisema Inspekta Aron akafungua mlango akashuka na kuhamia upande wa dereva.
Kabla hajawasha gari Aron aliandika ujumbe wa maandishi kwa Inspekta Jada

,,, Natoka tena mara moja, usimuache Annah hata sekunde moja, nitarudi baada ya dakika kumi hivi,,,,

Baada ya kutuma ujumbe huo Inspekta Aron akawasha gari nakuanza safari kumpeleka Najma nyumbani kwa dokta Gondwe.
Big' naye alikuwa hachezi mbali mara tu baada ya kuliona gari la Inspekta Aron linatoka naye alianza kulifuata nyuma taratibu, lengo lake likiwa ni kuruhusu bomu lilipuke kwa kubinya rimoti yake mara tu Aron atakapo baki mwenyewe ndani ya gari.


Godwin maarufu kama Sniper G mdunguajia mashuhuri kutoka katika kikosi cha Tino tayari alikuwa ndani ya ghorofa moja refu sana lililokuwa jirani kabisa na hospitali ya kimataifa ya Mountenia. Ghorofa hilo lilikuwa ni hoteli ya kimataifa yenye nyota tano. Godwin alikodi chumba kilichokuwa usawa na kile chumba alicholazwa Annah upande wa pili.
Alisogeza meza na kiti karibu na dirisha, akafungua lile begi lake refu ambalo ndani yake kulikuwa na vifaa mbalimbali vilivyopangwa kwa ustadi mkubwa. Godwin alianza kiviunganisha vifaa vile kwa haraka kimoja baada ya kingine na baadae akafanikiwa kuiunda bunduki ya masafa marefu, sniper'
Aliiweka mezani bunduki ile yenye stendi, akafungua madirisha mawili ya vioo kisha akarudi na kukaa kwenye kiti nyuma ya bunduki ile.
Godwin alimalizia kwa kufunga lenzi maalum juu ya ile bunduki kisha akaishikilia saawia na kupima shabaha upande wa pili ilipo hospitali ya Mountenia katika chumba alicholazwa Annah.

Kupitia ile lenzi Godwin aliweza kuona kwa ukaribu kabisa kila kilichokuwa kikiendelea kwenye chumba cha Annah, habati nzuri kwake na mbaya kwao hawakuwa wamefunga mapazia ya chumba kile.
Alimuona Inspekta Jada akiwa amekaa kitandani pembeni ya Annah aliyekuwa amepumzika tena baada ya kulia sana mara tu alipopewa taarifa za mazishi ya wazazi wake.
Kwa sababu Annah alikuwa amelala hali hii ilimfanya Godwin kushindwa kuipata shabaha ya uhakika. Hakutaka kufanya makosa Godwin aliamua kusubiri mpaka pale Annah atakapo amka na kuinua kichwa chake angalau akae kama alivyokaa Inspekta Jada hivi sasa, hapo itakuwa rahisi kumtwanga risasi.

Upande wa pili Tino alionekana akiwa ndani ya ile ofisi yake ya siri ambayo inamuingizia pesa nyingi kwa njia ya kurekodi video za ngono kutoka vyumba mbalimbali vya wageni alivyotegesha kamera zake za siri.
Vijana wafanyakazi wa Tino walikuwa bize wakati huo kila mmoja na kompyuta yake. Meza aliyokuwepo Tino ilikuwa imejitenga pembeni kidogo kutoka walipokuwa vijana hao. Kupitia kompyuta iliyokuwa juu ya meza Tino alikuwa akiitazama ile video ya ngono ya mkewe akiwa na bosi wake dokta Gondwe. Video hii iligeuka na kuwa kama madawa ya kulevya kwake, kila wakati alikuwa akiiangalia na kupandisha morali ya kufanya kile alichokusudia kufanya.

"Umefanya makosa makubwa sana Dokta Gondwe, kutembea na mke wangu ni kosa kubwa ambalo litakughalimu katika kipindi chote cha maisha yako" Tino alijisemea mwenyewe kwa sauti ya chini huku akiicheza tena video ile ambayo ilikuwa imefika mwisho, ikaanza upya.
"Kupitia video hii nitahakikisha napata vimelea vya V-COBOS wala hutojua kama ni mimi. Mimi ndio nitakae kuwa muhusika wa kusambaa kwa ugonjwa huu wa Virus vya COBOS, Ulimwengu mzima utasimama kulitaja jina langu, V-COBOS itaitetemesha Dunia yote kuliko hata COVID19" Tino alizidi kujisemea mwenyewe.

Wakati akisema hayo simu yake ilikuwa mezani akisubiri taarifa mbili muhimu kwanza alikuwa akisubiri matokeo ya kijana wake mdunguaji mashuhuri sniper G' kama amefanikiwa kumuua Annah na pili alikuwa akisubiri wakati ufike awasiliane na Dokta Gondwe kujua kama atakubali kumpa vimelea vya V-COBOS au laa!


Safari ya Inspekta Aron akiwa na Najma ndani ya gari yake ilikuwa ikiendelea. Wawili hawa ambao walikuwa wamezoeana kwa muda mfupi kila mmoja alijikuta akifurahia uwepo wa mwenzake. Najma alijikuta anatamani kuendelea kuwa karibu na Aron hivyo hivyo kwa Aron, hakutaka wafike nyumbani mapema. Najma hakuwaza tena kuhusu Osward mtoto wa mzee matula mume wake mtarajiwa ambaye yuko gerezani akisubiri hukumu yake kusomwa.

Akiwa siti ya nyuma Najma alikuwa akimuangalia sana Inspekta Aron aliyekuwa ameshikilia usukani. Taratibu alijikuta anaanza kumpenda kaka huyo mwenye chembechembe za ucheshi, anaejielewa na kujiamini sana.
Najma alizidi kumtazama huku aking'ata lips za chini za mdomo wake.
Inspekta Aron aliacha barabara kuu na kuingia kwenye barabara za mtaa akielekea ilipokuwa nyumba ya Waziri wa afya Dokta Gondwe. Alimtazama Najma kupitia kioo cha mbele cha gari yake hapo ndipo alipogundua kuwa Najma alikuwa anamuangalia sana. Aron akageuka na kumtazama akatamani kusema jambo lakini kabla hajafanya hivyo mara ghafula kukatokea mtikisiko mkubwa baada ya gari kuingia kwenye dibwi dogo la maji, Aron hakuwa ameliona wakati amegeuka kumtazama Najma.

"Mamaa! Aron vipi unataka kuleta ajali" Najma aliongea kwa hofu
"Hii njia yenu inamabonde sana alafu inaelekea kwa Waziri wa afya si aibu hii" alisema Aron huku akihangaika kuichomoa gari yake kwenye lile dimbwi la maji mwisho akafanikiwa

"Kwani hukuona maji hapo mbele wenzio huwa wanapita pembeni mbona njia iko wazi" alisema Najma
"Sikuyaona nilikuwa nakuangalia wewe"
"Unaniangalia Mimi nimefanyaje?"
"Kwa sababu unaniangalia"
"Akuu! Wala hata"
"Kweli eeh!"
"Kabisa mimi niko bize na simu yangu"
"Unachat na mumeo Osward si ndio?" Aron aliuliza swali la mtego
"Mume gani? Alafu yupo gerezani nachat nae vipi"
"Aah! kwani kuna kitu mzee Matula anashindwa kufanya kwa mwanae, anaweza hata kumpelekea swimming pool kule gerezani" alisema Aron huku akisimamisha gari yake, tayari alikuwa amefika nje ya jengo kubwa lililojengwa kisasa, hio ndio ilikuwa nyumba ya Dokta Gondwe.

Aron alipiga honi mara kadhaa mlinzi akafungua mlango mdogo akachungulia, Najma alitoa kichwa chake nje akampungia mkono na hapo bila kusita Mlinzi akafungua geti, Aron akaingiza gari taratibu.
Wakati huo Big' na pikipiki yake alibaki amesimama umbali wa mita kadhaa kutoka ilipokuwa nyumba ya Dokta Gondwe akawa anamsubiri Inspekta Aron atoke mwenyewe ndipo atekeleze azma yake ya kumsambaratisha akiwa ndani ya gari lake kwa kulilipua lile bomu.

Akiwa hapo mara aliiona gari ya mheshimiwa Dkt Gondwe naye akiingia nyumbani kwake. Alikuwa ametoka ubarozini mahali walipofanya mazungumzo nyeti pamoja na Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa.

Inspekta Aron alishuka, akazunguuka nyuma ya gari na kufungua mlango, Najma akasogea akitaka kushuka

"Ee taratibu mama, usijali nitakubeba" alisema Aron baada ya kuona Najma anahangaika
"Mmmh"Najma aliguna huku akimtazama Aron kwa macho malegevu
"Mmh nini haya sogea" Najma alisogea na kupitisha mkono wake nyuma ya shingo ya Aron ambaye alimnyenyua taratibu kumtoa nje ya gari.
Najma akiwa mikononi mwa Inspekta Aron ile wanageuka tu uso kwa uso wakagonganisha macho na mheshimiwa Dkt Gondwe ambaye ndio kwanza alikuwa ameshuka kutoka kwenye gari yake.
Si Najma si Aron wote walishtuka kwani hawakuwa wametegemea kukutana na Mzee huyo katika mazingira hayo, wakabaki wanatazamana kwa zaidi ya sekunde 30 wasijue la kufanya, Najma akiwa mikononi mwa Inspekta Aron.

JE, NINI KITAFUATA?
VIPI KUHUSU BOMU?
VIPI KUHUSU TINO NA VIMELEA VYA V-COBOS?
DOKTA GONDWE ATAFANYA NINI?
VIPI KUHUSU PENZI AMBALO LINAWEZA KUCHIPUA KATI YA ARON NA NAJMA MTOTO WA ADUI YAKE?
ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya...........13
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

13-(SHARTI LA MTEGO)
ILIPOISHIA....
Si Najma si Aron wote walishtuka kwani hawakuwa wametegemea kukutana na Mzee huyo katika mazingira hayo, wakabaki wanatazamana kwa zaidi ya sekunde 30 wasijue la kufanya, Najma akiwa mikononi mwa Inspekta Aron.

SASA ENDELEA....
"We nishushe" Najma alinong'ona akimtaka Inspekta Aron amshushe chini
"Kuna nini? Najma nini shida?" Dokta Gondwe aliuliza huku akisogea taratibu kuwafuata pale walipo
"Aa.ni...niliumia kidogo wakati nikiwa kwa Osward kule gerezani baba" Najma alijieleza haraka haraka wakati huo Inspekta Aron alimshusha na kumuacha asimame mwenyewe, lakini Najma bado alionekana kuwa na maumivu Kiasi cha kujilazimisha kusimama kwa mguu mmoja, hakuwa na uwezo hata wa kusogea hatua moja.

"Mnashangaa nini mbebeni mpelekeni ndani" Dokta Gondwe alifoka, haraka walinzi aliokuwa wameambatana naye kutoka ubarozini walimfuata Najma wakamsaidia kumkokota na kuingia ndani.
"Asante Aron" Najma alitoa shukrani akiwa mlangoni, Inspekta Aron akatikisa kichwa kuipokea shukrani hiyo kisha akageuka kumtazama Dokta Gondwe ambaye alikuwa akipiga hatua kumsogelea.

"Inspekta Aron umepata wapi ujasiri wa kuingia nyumbani kwangu?" Aliuliza dokta Gondwe huku akisimama mbele ya Inspekta Aron, wakawa wanatazamana uso kwa uso.
"Kwani kuna ubaya gani Dokta, nimefanya msaada tu kwa binti yako, hata hivyo mimi na wewe sio maadui"
"Acha unafiki Aron, umekuwa ukiniandama zaidi ya miaka miwili mpaka sasa sijui unataka nini kwangu, hata hujui una deal na mtu wa aina gani"
"Samahani sidhani kama maneno yako ni sahihi sana kwa wakati kama huu, nenda kamuangalie binti yako kwanza. Dokta mimi na wewe wote tunawatumikia wananchi wetu wewe ni Waziri wa afya na mimi ni afisa mpelelezi hivyo yote ninayoyafanya natimiza wajibu wangu tu"
"Sasa katika kutimiza huo wajibu jaribu kuwa na mipaka, kuna sehemu sio za kugusa Aron, haya ondoka nyumbani kwangu" Dokta Gondwe aliongea kwa ukali
"Mimi sijavuka mipaka daktari ila napambana na waharifu wote kuhakikisha wanapata wanachostahili bila kujali cheo wala ukubwa wa mtu, ni hivyo tu mzee wangu" Inspekta Aron aliongea kwa kujiamini sana, wakati huo Dokta Gondwe alimkata jicho kali.
Inspekta Aron hakutaka kubishana zaidi, aliingia kwenye gari yake na taratibu akatoka nje ya jumba la dokta Gondwe, safari ya kurudi hospitali ya Mountenia ikaanza. Yalikuwa ni majira ya saa moja na nusu jioni, jua lilikuwa limezama na giza lilianza kuchukua nafasi yake.

"Dokta Gondwe anajiona nani kwani, sijawahi ona Waziri wa ajabu kama huyu, sijui hata serikali yangu iliwaza nini kumpa cheo kama hiki. Ona nyumba yake ina walinzi chungu nzima utadhani ni kasri la waturuki. Anafanya maovu mengi ndio sababu hata hajiamini" Inspekta Aron alikuwa akiwaza wakati huo anaendesha gari yake kwa mwendo wa wastani.

Big' alikuwa nyuma ya gari ya Inspekta Aron umbali kama hatua arobaini hivi akawa anamfuata taratibu na pikipiki yake, tayari alishajihakikisha kuwa Aron yuko peke yake ndani ya gari, sasa ulikuwa ni muda muafaka wa yeye kubonyeza kitufe cha remoti iliyokuwa mkononi mwake kuruhusu bomu alilolitega chini ya gari la Inspekta Aron lilipuke.

Alikuwa akisubiri sehemu nzuri ambayo atailipua gari ya Aron pasipo kuleta maafa kwa watu au nyumba jirani. Mwisho gari ya Inspekta Aron ilifika usawa ambao Big' aliona unafaa, akaishika rimoti yake vizuri.

"Hii itakuwa mfano kwa askari wote vimberembere kama wewe Inspekta Aron, ulazwe mahali pema" Alisema Big' kisha akabonyeza kitufe cha kuruhusu bomu kulipuka.


"Bosi..bosi! umelala" sauti ya Bosco ilimkurupua Tino aliyekuwa amejiinamia mezani akiwa kwenye dimbwi la mawazo

"Nambie vipi, sijalala?" Alijibu Tino
"Saa mbili imefika ni mda wa kumpigia Dokta Gondwe sasa"
"Aah sawa twende"
Tino na kijana wake Bosco waliongozana hadi kwenye meza nyingine iliyokuwa na mitambo ya pekee tofauti na meza nyingine katika ofisi hiyo. Hilo lilikuwa ni eneo maalum la kuwasiliana na watu ambao wao waliwaita wateja yaani wale waliowarekodi video za faragha. Mitambo hiyo ilitengenezwa maalum kwa ajili ya mawasiliano kwanza ilikuwa na uwezo wa kubadili sauti kwa mtu anayezungumza na mteja sauti ambayo hubadilika na kuwa sauti nzito yenye muungurumo mkali lakini pili mitambo hiyo pia iliifanya namba wanayotumia kutoka hewani na kuwa namba ambayo haipo kabisa hadi pale watakapo iruhusu wenyewe.

"Piga, nipe mimi hiyo maiki niongee naye" Alisema Tino akikaa kwenye kiti, Bosco akamsogezea kinasa sauti.
Simu iliita upande wa pili, Dokta Gondwe na Najma binti yake walikuwa sebureni wakipata chakula cha usiku. Wakati huo Dokta Gondwe alikuwa akimuhoji maswali binti yake ni vipi aliweza kukutana na inspekta Aron wakasindikizana hadi nyumbani kwake.
Maongezi haya yalisitishwa na mlio wa simu ya Dokta Gondwe iliyokuwa juu ya meza ikiita.
Almanusura Dokta Gondwe apaliwe mara tu ya kupiga jicho na kuiona namba ya mpigaji, ilikuwa ni simu aliyokuwa akiisubiri kwa hamu.
Haraka alichukua simu akainuka na kupiga hatua ndefu ndefu kuelekea chumbani kwake. Najma alibaki na maswali mengi kichwani yasiyo na majibu, hivi karibuni ameona mabadiliko makubwa sana kwa baba yake amekuwa na tabia ambazo hajazoea kuziona. Najma hakutaka kulaza damu, hali akichechemea alijisogeza hadi kwenye mlango wa chumba cha baba yake akatega sikio kusikiliza mazungumzo ya simu yaliyokuwa yakiendela kati ya baba yake na mtu ambaye hakumtambua.

"Ndio Dokta nilikupa muda ujifikirie nataka kusikia maamuzi yako je, unanipa vimelea au niziachie hizi picha mtandaoni" sauti nzito kutoka upande wa pili wa simu ya dkt Gondwe ilisikika, haikuwa rahisi hata kidogo kibaini kuwa ile ilikuwa ni sauti ya kijana wake Tino.
"Ndiyo nimeshafikiri vya kutosha nilikuwa nasubiri simu yako tu" alijibu Dokta Gondwe
"Sawa, nakusikiliza"
"Nitakupatia vimelea vya V-COBOS, lakini kwa masharti"
"Masharti? Masharti yapi?"aliuliza Tino
"Kwanza nataka unihakikishie unafuta picha na video zote ulizonirekodi siku hiyo, pili kabla sijakupa hivi vimelea vya V-COBOS nahitaji mazungumzo ya ana kwa ana na wewe, unajua hawa vimelea ni suala la Dunia nzima siwezi kutoa kirahisi pasipo kufanya mazungumzo, nina hakika hata wewe unaelewa umuhimu wake"
Upande wa pili Tino alitulia kwa muda akijaribu kumuelewa Dokta Gondwe
"Okay subiri nakupigia simu baada ya dakika tano" alisema Tino kisha akakata simu

"Anajaribu kutaka kufanya nini huyu mzee?" Tino alijiuliza huku akifikiri kwa kina kuhusu masharti haya ya Dokta Gondwe
"Bosi tunafanyaje?" Aliuliza Bosco
"Sijui! nahitaji kufikiri kwanza, kuna kitu anakitaka huyu mzee sitakiwi kufanya makosa la sivyo nitawakosa hawa vimelea" alisema Tino huku akijaribu kuituliza akili yake.
Dokta Gondwe naye alitulia kusubiri dakika tano ziishe kuona kama ndege atanasa kwenye mtego wake. Hivi ndivyo walivyokuwa wameshauriana kufanya na Profesa Cosmas Kulolwa Rais mstaafu


Upande wa pili - barabarani
"Hii itakuwa mfano kwa askari wote vimberembere kama wewe Inspekta Aron, ulazwe mahali pema" Alisema Big' kisha akabonyeza kitufe cha kuruhusu bomu kuripuka.
Tofauti na alivyotegemea gari ya Inspekta Aron haikuripuka, akabinya tena mara ya pili hali ikawa ni ile ile, akabinya mara ya tatu ya nne ya tano bado bomu halikuripuka

"Upuuzi gani huu" alisema Big' kisha akaongeza kasi ya pikipiki yake akasogea karibu kabisa na gari ya Inspekta Aron akiamini labda umbali ndio ulikuwa sababu ya bomu kutokuripuka, akabinya tena lakini bado hali ikawa ni ile ile.
Big' alijikuta anajawa na hasira, hakuelewa nini hasa sababu inayopelekea bomu lile lisiripuke. Kwa uzoefu wake hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kitu kama kile kutokea. Alijiamini katika kazi yake hata siku moja hakuwahi kufanya makosa.
Baada ya kuona hali imekuwa ngumu aliendelea kumfuata Inspekta Aron nyuma taratibu huku bado akiendelea kujaribu bahati yake kwa kubinya rimoti kila baada ya sekunde kadhaa, hakujali tena kuhusu mazingira.
Mwisho Inspekta Aron alifika hadi hospitali ya kimataifa ya Mountenia akiwa salama salmini, akapaki gari yake akashuka na kuingia ndani ya hospitali hiyo akiwahi kwenda kumuangalia Annah.

Muda mfupi baada ya Inspekta Aron kuingia ndani ya hospitali, Big' alionekana akizuga zuga kuizunguuka gari ya Inspekta Aron. Alipoona usalama upo hakuna mlinzi wala mtu yeyote anaemuangalia, kwa kasi aliinama chini ya gari ya Inspekta Aron akalichomoa lile bomu alilokuwa amelitega awali kisha akasogea nalo pembeni.

"Fu***ck" Big' alijikuta anatukana kizungu baada ya kubaini kitu kilichosababisha bomu lisiripuke. Bomu la Big' lilikuwa limeloa na kunywa maji ya kutosha.
Kama utakumbuka wakati ule Aron akiwa na Najma ndani ya gari walinusurika kupata ajali huku gari ikizama kwenye dimbwi la maji. Hapo ndipo bomu la bwana Big' lilipoingia maji likapoteza uwezo wake wa kufanya kazi ipasavyo

"Bado hujashinda Inspekta Aron, hauwezi kutoboa hadi asubuhi" alisema Big' huku akichomoa bastola yake kutoka kiunoni, akafungua magazini na kubaini ilikuwa na risasi za kutosha, akatabasamu.

Upande wa pili katika Hotel iliyokuwa jirani na hospitali ya Mountenia, Mdunguaji Godwin maarufu kama Sniper G bado alikuwa makini akisubiri Annah akae usawa mzuri aweze kumtwanga risasi ya kichwa, kwa maelezo aliyopewa na kiongozi wake Tino alimpa masaa sita tu ahakikishe anamuua Annah.

Upande mwingine tayari Tino alikuwa ametuliza akili yake na alijua nini cha kumjibu Dokta Gondwe juu ya yale masharti aliyompa ili ampatie vimelea vya V-COBOS, akapiga simu kwa mara nyingine haraka Dokta Gondwe akapokea.

JE, NINI KITAFUATA?
SAKATA LA TINO NA BOSI WAKE DOKTA GONDWE LITAFIKIA WAPI?
NI NINI KIINI CHA VIMELEA HAWA HATARI?
VIPI KUHUSU ANNAH,NAJMA, OSWARD NA ARON?

ITAENDELEA....
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu.............14
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

14-(MAWINDO NDANI YA HOSPTALI YA MOUNTENIA)
ILIPOISHIA...13
Tino alikuwa ametuliza akili yake na alijua nini cha kumjibu Dokta Gondwe juu ya yale masharti aliyompa ili ampatie vimelea vya V-COBOS, akapiga simu kwa mara nyingine haraka Dokta Gondwe akapokea.

SASA ENDELEA...
"Nimekubaliana na masharti yako" alisema Tino, Dokta Gondwe akatabasamu akiamini ushauri aliopewa na Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa unakwenda kufanya kazi.
"Sawa naomba tukutane....." Alisema Dkt Gondwe lakini Tino akamkatisha
"Hapana hutakiwi kupanga sehemu ya kukutana, mimi ndio nitakaepanga" alisema Tino
"Kivipi tena?"
"Mheshimiwa Waziri kama ulivyoomba kukutana na mimi nikakubali basi na wewe kubaliana na matakwa yangu kubali nipange sehemu ya kukutana na wewe"
Kimya kilitawala kwa sekunde kadhaa kisha Dokta Gondwe akaongea

"Sawa nakusikiliza"
"Tutakutana baharini"
"Baharini?"
"Ndiyo habari ya hindi kesho saa tano kamili asubuhi"
"Kivipi?"
"Utakuja na boti yako na mimi nitakuwa na boti yangu, njoo usawa wa Kilagosi ukiwa hapo nitakutumia location nilipo utanifuata na boti yako, unatakiwa kuja wewe peke yako ukiwa na vimelea vya V-COBOS, mazungumzo na mambo yote tutamaliza ndani ya hiyo boti kila mtu atapata anachokitaka" Tino alitoa maelezo
Dokta Gondwe alitulia tena kwa muda kisha akakubaliana na matakwa ya Tino baada ya hapo akakata simu.
Baada ya kukata simu Najma ambaye alisikia karibu asilimia 90 ya mazungumzo yale alijivuta tena na kurudi mezani akaendelea kula chakula huku akiyatafakari mambo muhimu mawili ambayo aliyasikia kwenye mazungumzo yale, la kwanza ni vimelea vya V-COBOS na jambo la pili lilikuwa ni picha chafu, Najma akatamani kuelewa zaidi.


"Boss inamaana utaenda kuonana na Waziri kivipi sasa?" Aliuliza Bosco
"Utaenda wewe badala yangu Bosco" alijibu Tino
"Mimi? Kivipi? anaweza hata kuniua"
"Sikiliza Bosco mimi nitakuwepo kukulinda, Dokta Gondwe akitaka kukuaa basi lazima atanitumia mimi na sio mtu mwingine, hata isipokuwa hivyo naweza kukulinda pia" alieleza Tino na mara dakika hiyo simu yake ikaita mpigaji alikuwa ni Dokta Gondwe

"Ona si nimekwambia bila shaka anataka kuzungumza juu ya hili hili jambo" alisema Tino kisha akapokea simu ya bosi wake
"Hallo bosi" Tino aliongea kwa unyenyekevu mkubwa, akawa Tino tofauti kabisa na yule aliyekuwa akimpa vitisho Dokta Gondwe dakika chache zilizopita

"Vipi umeshammaliza huyo Annah"
"Hapana bosi bado lakini..."
"Lakini nini Tino nimeshakueleza kuwa kipindi hiki unatakiwa uwe ngangali nikikuagiza kazi unafanya chapu tunaendelea na mambo mengine, vita ni kubwa kijana wangu"
"Bosi lakini nilikuahidi Annah hatoliona jua la asubuhi, leo lazima tumalize kazi niamini mimi"
"Sawa malizeni hiyo kazi haraka kesho kuna kazi nyingine muhimu nataka tufanye"
"Sawa bosi haina shida"
"Sawa, asubuhi na mapema nitafutie boti nzuri ambayo inaweza kubeba watu watatu kwa siri kamilisha hili kabla ya saa tatu asubuhi kisha tuonane"
"Nitafanya hivyo bosi"
Simu ikakatwa.

"Umeona sasa Bosco" alisema Tino baada ya kuhakikisha simu imekatwa
"Ndiyo bosi"
"Ndio maana nikakwambia wewe uende badala yangu, kwa tafsiri fupi kuna ujanja Dokta Gondwe anataka kuufanya ndio sababu anataka boti itakayobeba watu wake kwa siri"
"Hata mimi nimewaza hivyo bosi"
"Hapa kuna mawili huenda akaja na hao vimelea au asije nao, huenda akapanga kukuua au kukuteka sasa itabidi tucheze na akili yake"
Alisema Tino huku akionekana kuitafakari siku ya kesho kwa kina. Kama kawaida yake Tino alikuwa ni mtu anaetumia akili zaidi kuliko nguvu, hii ndio iliyokuwa siri kubwa ya mafanikio yake.

"Bosco" Tino aliita
"Naam bosi"
"Nataka ujue kuwa kuanzia leo wewe ndio mtu wangu wa karibu ninae kuamini sana, tayari umeshajua siri zangu nyingi sana, kama ulivyonilindia heshima kwa kutowaonyesha wenzako video ya ngono ya mke wangu naamini utafanya hivyo hata kwa mambo mengine. Utakuwa mkono wangu wa kuume kwa kila hatua nitakayopiga, tayari nimeshakueleza kwa kifupi kuhusu hivi vimelea vya V-COBOS ninavyovipigania kwa nguvu zote. Ni mimi na wewe ndio tutakwenda kuigeuza hii Dunia juu chini chini juu" Tino aliongea kwa hisia kali akiwa amemshika bega kijana wake Bosco


Godwin maarufu kama Sniper G bado aliendelea kusubiri, hakuwa amepata usawa mzuri wa kumlenga Annah shabaha. Tangu alipolala hakuwa ameinuka hata mara moja ilifika wakati Godwin akachoka kufumba jicho moja na kufumbua jingine akiwa ameishika ile bunduki ya masafa marefu, lakini ilimlazimu kuendelea kwani kwa kufanya hivyo ilimfanya aweze kuona kila kilichokuwa kikiendelea ndani ya chumba alicholazwa Annah.

Akiwa bado anakitazama chumba kile mara aliona mlango ukifunguliwa, kunamtu aliingia ndani. Godwin alichungulia vizuri akamtambua mtu huyo alikuwa ni Inspekta Aron.

"Yaani sikapendi haka ka jamaa, Tino asingekuwa kaka yako ningekaua mwenyewe bila kuagizwa na mtu yeyote" alisema Godwin huku akiiachia bunduki yake akasogea mbele akafunga yale madirisha ya chumba chake. Alimjua vizuri Inspekta Aron kuwa ni mtu makini sana kama angeendelea kukaa na bunduki yake pale dirishani pengine angemshtukia licha ya kwamba kulikuwa na umbali mrefu kutoka hospitali ya Mountenia hadi ilipo Hoteli hiyo.

Ni kweli mara tu baada ya Inspekta Aron kusalimiana na inspekta Jada alienda moja kwa moja hadi kwenye dirisha la chumba hicho alicholazwa Annah.
Inspekta Aron alikagua mazingira juu ya ghorofani chini pembeni kushoto kulia na mwisho mbele yake kulipokuwa na ile Hotel kubwa ya kifahari.

"Hukutakiwa kuacha pazia wazi" alisema Aron huku akirudisha mapazia na kufunga madirisha vizuri
"Ee jamani Aron unawasiwasi hadi sio poa"
"Alaah! ni kwa sababu tu hujawahi kukabiliana na watu wa Dokta Gondwe, hawa jamaa ni professional killer wana kila aina ya siraha ni watu waliojipanga sio kidogo"
"Haya sawa kwa hiyo inakuwaje ishu ya kumuamisha Annah chumba tofauti na hiki nakumbuka ulisema tayari Tino ameshajua"
"Shiiiii! mbona unaongea kwa sauti Annah hatakiwi kusikia utampa wasiwasi"
"Usijali hasikii chochote kalala tangu ulipoondoka"
"Kweli?"
"Yap wee humuoni" Alisema Jada na wote kwa pamoja wakageuka na kumtazama Annah aliyekua amelala pale kitandani

"Mmh maskini alafu haka kabinti ni kazuri, Inspekta Aron unafeli wapi owa basi mtoto mbichi kabisa huyu atakufaa" alisema Jada huku akitabasamu
"Hebu acha utani wako basi, aliyekwambia nahitaji mke ni nani"
"Kwa hiyo utaoa lini sasa?"
"Nikistaafu"
"Khee! Msikie huyu"
"Kweli, kwa kazi ninayoifanya sitakiwi kupenda kabisa"
"Kwa nini?"
"Maadui zangu watautumia kama udhaifu wangu, mwanamke wangu anaweza kujikuta anateseka bila hatia sitaki kumuweka hatarini mtoto wa mtu" alieleza Aron huku akipiga simu na kuiweka sikioni ikawa inaita
"Hahahah hayo ndo madhara ya kuangalia muvi za wazungu"
"Wala sio muvi Jada huu ni ukweli nakwambia"
"Kwa hiyo utakaa hivyo hadi lini, hivi hujawahi kutana na mwanamke alafu roho yako ikashtuka ukajikuta unaanza kumpenda penda hivi maana wewe ni mgumu sijawahi ona" aliuliza Jada swali ambalo liliugusa moyo wa Inspekta Aron kwa kiasi fulani akajikuta anakumbuka hali hiyo ilimtokea leo akiwa na mtoto wa Waziri wa afya yaani Najma

"Hapana sijawahi" Aron alidanganya
"Eeh basi ukapime"
"Subiri niongee na Dokta Zyunga... Hallo Dokta wapi.....ndio tupo kwa Annah humu tunakusubiri... yeah kuhusu kumuhamisha chumba....sawa...sawa Dokta" Aron alimaliza mawasiliano kisha akakata simu

"Kasemaje"
"Yupo ghorofa ya chini anakuja"


Big' alikuwa amekaa kwenye viti vilivyokuwa eneo la mapokezi sakafu ya chini kabisa ya hospitali ya Mountenia, ndio kwanza alikuwa anaingia akawa anajaribu kusoma mazingira ajue ataanzia wapi kumsaka Inspekta Aron.
Baada ya kujiridhisha na uchunguzi wake Big' alipiga hatua akasogea hadi eneo la mapokezi alipokuwepo dada mmoja aliyemkaribisha kwa sura ya upendo.
"Karibu kaka"
"Asante, namuulizia Dokta Zyunga"
"mmm una-appointment naye?"
"ndiyo"
"Sawa basi kaa pale msubiri kidogo alitoka mara moja"

Big' alifuata maelezo yale akarudi na kukaa kwenye vile viti alivyokuwa awali. Alichokifanya Big' ilikuwa ni kumtafuta Dokta Zyunga ambaye anajua huwa yupo karibu sana na inspekta Aron. Dokta Zyunga ndiye aliyeufanyia vipimo mwili wa mtu aliyeuwawa na Osward. Hivyo Big' aliamini kupitia Dokta Zyunga angeweza kumpata kirahisi Inspekta Aron ndani ya hospitali hiyo.

Dakika chache baadae Big' alimuona Dokta Zyunga anaingia haraka akasimama alipopita naye akaanza kumfuata nyuma huku akimpungia mkono yule dada wa mapokezi ikiwa ni ishara kuwa amempata mtu wake.
Dokta Zyunga alipoingia kwenye lifti Big' naye akaingia, ni wakati huo ambao Inspekta Aron alipiga simu wakawa wanazungumza kuhusu kumuhamisha Annah.
Lifti ilisimama Dokta Zyunga akashuka Big' naye akashuka, hapo Dokta Zyunga akageuka na kumtazama.
"Habari ndugu unaelekea wapi?"
"Nani mimi?"
"Ndiyo"
"Aah! Ee.. naelekea idara ya magonjwa ya wanawake"
"Mmh! sasa wewe na hayo magonjwa wapi na wapi"
"Aah.. ni mke wangu yupo kule ametangulia"
"Sawa panda ghorofa inayofuata mkono wako wa kushoto utaona korido moja ina mshare wa manjano fuata huo uelekeo utaona chumba kilichoandikwa 'Obstetric' ingia humo"
"Sawa nashukuru Dokta" Big alijibu kisha akaanza kupandisha ngazi akifuta maelezo ya Dokta Zyunga.
Baada ya kuona Dokta Zyunga hamzingatii tena Big' aliendelea kumfuatilia nyuma nyuma kwa siri huku safari hii akiwa makini zaidi asionekane


Dokta Zyunga alifika hadi kilipo chumba alicholazwa Annah bila kujua nyuma yake alikuwa akifuatiliwa kwa siri na Big'. Aliwakuta Inspekta Aron na Inspekta Jada wamesimama mlangoni

"Vipi nimechelewa?"
"Hapana umefika wakati muafaka" alijibu Jada
"Anaendeleaje mgonjwa wetu"
"Anaahueni kwa sasa amepumzika"
Dokta Zyunga aliingia moja kwa moja kumuangalia Annah, kisha akawa anamchukua vipimo muhimu kufuatilia maendeleo yake

"Haya Jada kapumzike mimi nitakaa na Annah hadi asubuhi utakuja kunipokea" alisema Aron
"sawa lakini Aron kama Annah ameshathibitisha kuwa mheshimiwa Waziri wa afya Dokta Gondwe alikuwepo wakati wa tukio kwa nini tusimkamate moja kwa moja"
"Jada sio kwamba sikuelewi, nakuelewa sana lakini hujui Dokta Gondwe ni kiumbe wa aina gani, maneno ya Annah pekee hayatotosha kumuweka hatiani"
"Mmh! sawa ngoja basi tumuhamishe alafu nitaondoka" alijibu Jada wakati huo Inspekta Aron alionekana kukaza macho yake kwenye kona moja ya ukuta hatua kadhaa mbele yao

"Vipi kuna nini"aliuliza Jada akimtazama Aron usoni
Badala ya kujibu Inspekta Aron alianza kupiga hatua taratibu akinyata kuelekea kwenye ile kona, wakati huo mkono wake aliuzunguusha taratibu nyuma ya kiuno chake akachomoa bastola. Inspekta Jada alibaki amesimama pale pale lakini naye akachomea bastola yake kwa tahadhari.

Akiwa amefika usawa wa ile kona Inspekta Aron aligeuka upande pili kwa kasi huku siraha yake ikiwa mbele, cha ajabu hakuona chochote akaangalia juu chini kushoto kulia hakuna kitu. Baada ya kuhakikisha kuna usalama alirudisha siraha yake mahali pake kisha akarudi alipotoka

"Kwani vipi Aron?" Aliuliza
"Ni kama nilimuona mtu anachungulia"
"Mmh! kweli?"
"Yeah lakini kupo shwari itakuwa niliona vibaya" alisema Aron, wakati huo Dokta Zyunga alitoka. Bila kupoteza muda wakaanza kufanya taratibu wa kumuhamisha Annah

Macho ya inspekta Aron yaliona kitu sahihi kabisa kwenye ile kona alikuwepo Big' akiwachungulia, mara baada ya kuona Inspekta Aron ameshtukia uwepo wake Big' aliondoka kwa kasi akashuka ghorofa ya chini kwa bahati nzuri Aron hakuweza kumuona.

"Nitarudi kwa ajili yako Aron muhimu nimejua ni wapi ulipo" alisema Big' wakati akiondoka.

USIKU...
Ilikuwa ni majira ya saa sita na nusu usiku, Godwin maarufu kama Sniper G alionekana akitoka kwa kasi nje ya Hoteli aliyokuwepo. Alikuwa kitembea na kugeuka nyuma mara kadhaa mkononi akiwa na lile begi lake kubwa ambalo ndani yake kulikuwa na bunduki yake ya masafa marefu.
Alitembea haraka haraka mwisho alitoka nje kabisa ya Hoteli hiyo. Mbele yake pembeni ya barabara kulikuwa na gari inamsubiri, alifika na kufungua mlango akaingia.

"Vipi?" Aliuliza mtu aliyekuwa amekaa kiti cha dereva mara tu baada ya Godwin kuingia, mtu huyu hakuwa mwingine bali Tino.
"Kila kitu kimekamilika mkuu" alijibu sniper G'
"Umemuua Annah si ndio"
"Ndiyo, risasi ya kichwa hawezi kupona" sniper G' aliongea kwa kujiamini
Tino aliwasha gari na kuondoka kwa kasi wakati huo simu yake ilikuwa ikiita, mmoja wa vijana wake alikuwa akimpigia, akapokea.
"Ee nambie dogo umeshapata aina ya boti ninayoihitaji?....sawa..kazi nzuri...haya mkapumzike sasa tuonane asubuhi kambini...ndiyo Godwin naye ameshakamilisha kazi yake hivi ndio nimetoka kumchukua....sawa" Tino alimaliza maongezi kisha akakata simu na kuongeza mwendo wa gari yake.
Upande wa pili ndani ya chumba alichokuwa Annah, damu ilionekana ikiwa imetapakaa kila kona.

JE, NINI KITAFUATA?
NI KWELI SNIPER G' KAMUUA ANNAH?
VIPI KUHUSU INSPEKTA ARON NA BIG'?
JE, SAKATA LA VIMELEA VYA V-COBOS LITAISHIA WAPI?

ITAENDELEA....
 
THE MODERN WAR
(vita ya kisasa)
Sehemu ya................15
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Ee nambie dogo umeshapata aina ya boti ninayoihitaji?....sawa..kazi nzuri...haya mkapumzike sasa tuonane asubuhi kambini...ndiyo Godwin naye ameshakamilisha kazi yake hivi ndio nimetoka kumchukua....sawa" Tino alimaliza maongezi kisha akakata simu na kuongeza mwendo wa gari yake. Upande wa pili ndani ya chumba alichokuwa Annah, damu ilionekana ikiwa imetapakaa kila kona.

SASA ENDELEA...
Usiku ule Tino na kikosi chake kinachofanya kazi chini ya Dokta Gondwe walirudi kambini kwao wakiamini mambo yote yamekwenda shwari, tayari Godwin aliwahakikishia kuwa amemtwanga Annah risasi ya kichwa kwa sasa ni marehemu, wote wakaamini hivyo.
Lakini upande wa pili ndani ya hospitali ya kimataifa ya Mountenia mambo yalikuwa ni tofauti kabisa na maelezo ya Godwin, ni kweli ndani ya chumba alichokuwa amelazwa Annah kwa mara ya kwanza kabla ya kuhamishwa kuna mwili wa mtu ulionekana ukiwa umelala sakafuni huku damu nyingi ikiwa imetepakaa kuuzunguuka mwili huo lakini haukuwa mwili wa Annah, je ni nini kilitokea?... Ilikuwa hivi.

MASAA MATATU (3) KABLA....
Wakati ule Inspekta Aron amefunika pazia la madirisha katikati chumba alicholazwa Annah hii ilimfanya Godwin(sniper G') kushindwa kuifanyia kazi yake maana hakuweza tena kuona kinachoendelea ndani ya kile chumba. Hata hivyo bunduki ile ya masafa marefu aliyoitumia Godwin ilikuwa ni bora sana kwani baada ya Inspekta Aron kufunika pazia Godwin alibadilisha lenzi ya bunduki yake akaweka lenzi nyingine ambayo ilikuwa na uwezo wa kupenya hadi ndani licha ya kwamba kulikuwa na kizuizi cha mapazia. Tofauti na lenzi nyingine lenzi hiyo haikuwa na uwezo wa kuonyesha sura ya mtu au kitu kwa uharisia wake, kila kitu/mtu kilionekana cha kijani.
Godwin aliweza kutofautisha huyu ni mtu na hiki ni kitu kutokana na umbo pamoja na mijongeo ya hapa na pale.
Kwa maana hiyo Godwin alikuwa na uwezo wa kuona kila kilichoendelea mle ndani lakini hakuweza kutofautisha kuwa huyu ni Annah huyu ni Inspekta Aron huyu ni Jada au huyu ni Dokta Zyunga hali hii ikafanya kazi yake kuwa ngumu kwani wakati huo watu walikuwa wakiingia na kutoka ndani ya chumba kile.

Kuliko kufanya kazi kwa kubahatisha Godwin aliona ni vema atulie hadi pale Annah atakapobaki peke yake mle ndani. Hakujua kuwa ile mitembeo ya hapa na pale ndani ya chumba cha Annah ilikuwa ni katika harakati za kumuhamisha, Godwin hakujua hilo badala yake akapumzika kitandani kusubiri wakati mwingine

Ikiwa ni majira ya saa tano usiku Big' alionekana akinyata kuelekea chumba alichokuwa amelazwa Annah awali. Kwa kuwa alisikia mazungumzo ya Inspekta Aron na Inspekta Jada ambao walikubaliana kuwa Aron ndiye atakayebaki usiku huo kumilinda Annah aliamini hiyo ndio itakayokuwa nafasi ya kumuua Inspekta Aron baada ya kunusurika kwenye lile bomu. Kwa bahati mbaya Big' hakuzisikia habari za Annah kuhamishwa chumba hivyo akaamini kabisa lazima Inspekta Aron atakuwa maeneo hayo kama sio nje basi ndani ya chumba cha Annah.

Baada ya kuhakikisha nje hakuna mtu, taratibu Big' alinyata hadi mlangoni, akanyonga kitasa mlango ulikuwa wazi akafungua taratibu na kuingia huku bastola yake ikiwa mbele tayari kwa lolote.
Aliangaza macho huku na huku hakuona mtu, kilichomshtua zaidi hata yule mgonjwa aliyesikia kuwa Inspekta Aron anamlinda hakuwepo kitandani.
Big' alihisi pengine Inspekta Aron ameshtukia na kumuweka mtego, akaongea umakini. Akakagua chooni na bafuni lakini bado hakuona mtu. Kwa mara nyingine Big' akaona kabisa kuna kila dalili ya kumkosa Inspekta Aron. Aliuma meno kwa hasira huku akijipigapiga kichwani

"Kaenda wapi huyu mjingaaa" Big' alilalamika na kujitupa kitandani kwa hasira, akalala chali macho yake yakitazama paa la chumba hicho.
Akiwa bado amejilaza pale kitandani Big' aliwaza ni vipi ataweza kumpata Inspekta Aron ilikuwa ni lazima ahakikishe anamuua usiku huo hivyo ndivyo alivyomuahidi Osward.


Majira hayo hayo Godwin (sniper G') alikurupuka usingizini akachukua simu yake na kutazama saa ilikuwa ni saa sita kasoro usiku. Kulikuwa pia na ujumbe wa maandishi kutoka kwa Tino, akaufungua upesi na kuusoma.

,,,,,,,,,Vipi? Umeshamuua huyo mwanamke? Ukimaliza kazi niite upesi nije nikuchukue,,,,,,,,,
Baada ya Godwin kumaliza kuusoma ujumbe huo haraka akasogea karibu na bunduki yake ya masafa marefu, akaweka shabaha yake kuelekea chumba cha Annah kama kawaida. Bado pazia lilikuwa limefungwa lakini ile lenzi ya bunduki yake ilimuwezesha kuona kila kitu ndani.
Kulikuwa kimya kabisa wala hakuna mtu yeyote aliyemuona. Godwin akaamini kuwa wakati huo ni lazima Annah atakuwa amelala.

"Siwezi kusubiri hadi asubuhi, Tino hatanielewa kabisa" aliwaza Godwin huku akipiga mahesabu ya haraka haraka nini afanye, mwisho akapata wazo.
Godwin aliwaza apige risasi ya kwanza itakayopasua kioo na kumfanya Annah ashtuke, akijichanganya kuinuka basi hapo atapata wasaa mzuri wa kulenga shabaha na kumtwanga risasi ya kichwa.
Hivyo ndivyo alivyofanya Godwin, akafyatua risasi ya kwanza ambayo ilisafiri na kwenda kupiga kioo cha dirisha la chumba alichokuwa Annah kikapasuka, sasa akawa anasubiri matokeo kama Annah atashtuka na kuinuka pale kitandani au laa!


Big' aliyekuwa bado amelala kitandani ndani ya chumba alichokuwepo Annah awali alishtushwa na mlio wa kioo cha dirisha kikipasuka ghafula.
Big' alitoa macho kwa mshangao na kukurupuka pale kitandani kwa kasi akasimama na kuishika bastola yake vizuri, akawa anaangaza macho huku na huku, tayari alishahisi hali ya hatari.


Ni kweli kama alivyowaza Godwin ndivyo ilivyokuwa kwani sekunde chache baadae aliona mtu alikurupuka kwa kasi pale kitandani.

"Kwisha habari yako Annah" alisema Godwin huku akiweka shabaha yake vizuri na kuielekeza kwenye kichwa cha yule mtu aliyeamini kuwa ni Annah. Bahati mbaya kwake lenzi ya bunduki yake ilikuwa haiwezi kuonyesha sura ya mtu kutokana na kizuizi cha lile pazia dirishani, laiti kama angeweza kuona angegundua moja kwa moja kuwa yule ni mtu mwingine wala si Annah aliyemdhania.

Bila kupoteza muda Godwin alifyatua risasi iliyoenda moja kwa moja na kuzama kwenye kichwa cha Big' ikatokea upande wa pili. Big' alianguka chini kama gunia,akawa anarusha rusha miguu huku damu ikimtoka kwa wingi,ndani ya sekunde 30 akakata roho.

Haraka Godwin alijibu ujumbe wa Tino akamtaka aje amchukue, kisha haraka haraka akaifungua bunduki yake na kuipanga vizuri kwenye begi. Akaweka mazingira sawa kuhakikisha haachi ushahidi wowote baada ya hapo akatoka hadi nje ya Hoteli hiyo ambako alikuta tayari Tino ameshafika anamsubiri.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa, aliyeuwawa hakuwa ana bali Big' rafiki kipenzi wa Osward.


Saa saba usiku Inspekta Aron alikuwa macho akizunguuka zunguuka kuangalia usalama wa kile chumba kipya alichohamia Annah kwa sasa, wala hakujua kuhusu mauji yalitokea chumba kile cha kwanza, hakuna aliyejua.
Chumba hiki kipya kilikuwa upande wa pili kutoka vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU) ambako huko ndiko mama yake mzazi na Aron(Sultana) alikuwa amelezwa kwa zaidi ya miezi sita akiwa hajitambua.

Wakati inspekta Aron akizunguuka zunguuka alipata wazo akajisikia kunyoosha miguu hadi kule ICU alikolazwa mama yake akatamani kwenda kumuona, akafanya hivyo.
Alitembea taratibu huku akikumbuka mambo kadha wa kadha yaliyotokea siku hiyo, hapo akajikuta anatabasamu mara baada ya kumkumbuka Najma binti wa Waziri kuu, mwanamke aliyezoeana naye ndani ya mda mfupi sana bila kujali alikuwa na uadui mkubwa na baba mzazi wa binti huyo yaani Dokta Gondwe.
Inspekta Aron akiwa amekaribia kukifikia chumba cha mama yake mara alisikia mchakacho nyuma yake haraka akageuka kutazama lakini hakuona kitu hali ilikuwa shwari kabisa.
Ndani ya zile sekunde chache ambazo Aron aligeuka nyuma mara alionekana mtu aliyevaa mavazi meusi juu mpaka chini akitembea upesi kutokea ndani ya chumba cha mama yake Aron akafungua mlango taratibu akatoka na kuufunga kisha akapotea kama upepo.
Tukio lile lilifanyika ndani ya sekunde chache hii ilionyesha wazi kuwa mtu huyo alikuwa ni mtaalamu haswa, alitembea hata bila vishindo vya nyayo zake kusikia. Inspekta Aron alipotazama mbele tayari mtu huyo alishatoweka kitambo wala Aron hakuhisi chochote.
Inspekta Aron alisogea hadi mbele ya mlango wa chumba cha mama yake, akatazama ndani na kuhakikisha kila kitu kilikuwa sawa mama yake alikuwa amelala huku zile mashine za kumsaidia kupumua zikiendelea kufanya kazi kama kawaida. Aron aliondoka kurudi kwa Annah upesi ule mchakacho aliousikia mwanzo ulimfanya ahisi pengine kuna hatari lakini baada ya kufika alibaini hakuna hatari yoyote hali ilikuwa shwari kabisa

Dakika chache baadae ya Inspekta Aron kuondoka, yule mtu mwenye mavazi meusi alirudi tena akinyata taratibu akaingia ndani ya chumba alicholazwa mama Aron na kufungua mlango.
Alikuwa ni mwanaume mwembamba mrefu, sura yake ilikuwa ameificha kwa kufunika kitambaa cheusi na kuacha sehemu ya macho pekee, kichwani alivaa kofia nyeusi pia, kila kitu kwake kilikuwa cheusi. Alipiga hatua taratibu akasimama mbele ya kitanda cha mama Aron.
"Sultana ni mimi Shadow nimerudi" alisema yule mwanaume
Katika hali ya kushangaza mama Aron ambaye tunaamini alikuwa ni mgonjwa mahututi aliyelazwa akiwa hajitambua kwa zaidi ya miezi sita alionekana akiinuka huku akivitoa vile vifaa vya kupumulia na kuviweka pembeni, akainuka na kushusha miguu chini ya kitanda. Mama Aron alionekana ni mzima tena mzima mwenye afya tele.

"Shadow" mama Aron (sultana) aliita
"Naam Sultana" Shadow aliitika huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini kwa heshima
"Alikuwa ni nani huyo?" Aliuliza Sultana
"Alikuwa ni Inspekta Aron, mwanao"
"Aron? anafanya nini hapa hospitali usiku huu?"
"Nafikiri atakuwa anamlinda yule binti Annah niliyekwambia" alieleza Shadow
"Sasa kwa nini Dokta hajaniambia"
"Sijajua Sultana pengine na yeye hana taarifa kuwa Inspekta Aron yuko hapa" kimya kikatawala kwa sekunde kadhaa kisha Sultana akaongea.
"Enhe! nipe ripoti yangu haraka uondoke"
"Sultana, kesho ndio siku yetu ambayo pengine tunaweza kupata kitu tunachokitafuta kwa kipindi kirefu"
"Kweli? Unamaana gani shadow"
"Nimefuatilia nyendo zote za Tino, kesho ndio siku anakwenda kukabidhiana Vimelea vya V-COBOS na Waziri Dokta Gondwe"
"Hahahah!! sikutegemea kama itakuwa mapema hivi, kwani nini kimetokea?" Alisema Sultana huku akishuka kitandani, akasimama na kupiga hatua akasogea dirishani, akawa anaongea huku akitabasamu.

"Tino, Tino mwanangu hatimaye nitakwenda kuchukua vimelea vya V-COBOS kutoka kwenye mikono yako mwenyewe, huwezi kushindana na mimi wewe ni mwanangu nimewahi kuliona jua kabla yako. Najua umekuwa unatamani sana niamke ili uniulize maswali ambayo huna majibu yake kisha uniuwe kama ulivyomuua baba yako Jenerali Phillipo Kasebele. Unatumia pesa nyingi ili kuhakikisha napona na baadae nikwambie kile nachokijua kuhusu vimelea vya V-COBOS, huwezi Tino huwezi kushindana na mimi kijana wangu. Hii ni siri ambayo baba yako aliilinda kwa miaka mingi hata hao wazungu wa Dokta Gondwe kutoka Mexico hawajui chochote mpaka sasa, hahahah, mimi pekee ndiye nitakayeigeuza Dunia hii juu chini chini juu...." Sultana aliongea kwa kujiamini kisha akageuka kwa kasi kumtazama kijana wake mashuhuri, Shadow.
"Wanakutana wapi?"
"Habarini, watakuwa na boti"
"Sawa najua hakuna kitakacho kushinda hakikisha hivyo vimelea vya V-COBOS unavileta hapa sawa Shadow"
"Haina shida Sultana"
Alijibu Shadow kisha akaondoka, akimuacha Sultana ambaye alirudi na kupanda kitandani kisha akarudisha ile maski na vifaa vingine vinavyomsaidia kupumua kama awali.

JE NI NINI KILITOKEA? NI KWELI TINO ALIMUUA BABA YAKE? KWA NINI?
ILIKUAJE?
NI IPI MIPANGO YA SULTANA?
DOKTA GONDWE, RAIS MSTAAFU NA WALE WAZUNGU WATAFANYA NINI?
NINI KITATOKEA KWA ARON, OSWARD, NAJMA NA ANNAH?

TUMEMALIZA MSIMU WA KWANZA (SEASON 1) YA SIMULIZI HII KARIBU MSIMU WA PILI AMBAO TUNAKWENDA KUICHIMBA SIMULIZI HII KUJUA MBIVU NA MBICHI, NAAM HII NI MODERN WAR (vita ya kisasa).
 
THE MODERN WAR
(vita ya kisasa)
Sehemu ya...............16
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

16-(MAABARA YA ZMLST)
ILIPOISHIA (msimu wa kwanza)...
Sultana (Mama Aron) ambaye tuliamini ni mgonjwa mahututi aliyelazwa akiwa hajitambua kwa zaidi ya miezi sita mfurulizo anainuka kitandani akiwa ni mzima wa afya. Kumbe kwa kipindi chote alikuwa akiigiza kujifanya ni mgonjwa. Sultana anafanya mazungumzo na kijana wake wa siri anayemtumia siku zote anaitwa Shadow akimtaka ahakikishe anavileta vimelea vya V-COBOS mikononi mwake

Je, nini kitafuata?

TURUDI NYUMA MIAKA KUMI (10) ILIYOPITA.
MEXICO
Ndani ya nchi ya Mexico katikati ya mji maarufu wa Ciudad Juárez ndipo tunaikuta Maabara ya sayansi na teknolojia inayojulikana kwa jina la ZIVEMIC MEDICAL LABORATORY SCIENCE AND TECHNOLOGY - (ZMLST). Hii ilikuwa ni maabara kubwa na maarufu sana Duniani, kama ukitaja maabara za sayansi na teknolojia kumi bora ulimwenguni basi usinge acha kuitaja ZMLST.
ZMLST kama zilivyo maabara nyingine Duniani kote ilikuwa ikijihusisha sana na masuala ya utafiti wa magonjwa mapya yanayoibuka hasa haya ya mripuko, kuchunguza na kubaini chanzo, aina ya kimelea husika kama ni bakteria au kirusi kisha wanamaliza kwa kutengeneza kinga au dawa. Hivyo ndivyo namna maabara ya ZMLST ilivyofanya kazi.
Maabara hii ilikuwa ni kongwe kuliko maabara nyingine zote unazozifahamu lakini ukongwe wake haukuifanya ZMLST kuwa maabara bora kuliko nyingine.
Maabara nyingine kubwa zenye teknolojia ya kisasa zilikuwa zikiibuka kila iitwapo leo hali iliyopelekea ZMLST kuanza kupotea kwenye midomo ya watu, taratibu hata tenda zikaanza kupungua.
Kwa miaka mitatu mfurulizo ZMLST ikajikuta inaporomoka kwa kasi na kupoteza sifa yake kabisa, kila walipojaribu kuirudisha katika hadhi yake ya awali ilishindikana ushindani ulikuwa ni mkubwa mno.
Mwisho umaarufu wa ZMLST ukapotea na kubaki jina tu. Wanasayansi wakubwa ulimwenguni waliokuwa wakishikiriwa na maabara hii kama Dr Alain Aspeco, Prof David Baltimore, Allen Bard, Eng Timothy Berners na wengine wengi walianza kuchomoka mmoja baada ya mwingine wakihamia kampuni nyingine na baadae wakaisha wote, hali ikazidi kuwa tete


"Now it's time to use our weapon"(sasa ni wakati wa kutumia siraha yetu)
Hii ilikuwa ni kauli ya mkurugenzi mtendaji wa ZMLST Profesa Fernando Arturo ambaye pia ni mmoja kati ya waanzilishi wa ZMLST, alisema hivi akiwa amekaa kikao cha dharula na wafanyakizi waandamizi wa ZMLST. Mbele ya Profesa Fernando kulikuwa na begi dogo juu ya meza lililokuwa na muundo kama boksi hivi.
Profesa Fernando mwenye asili ya kituruki alifungua lile begi kuwaonyesha watu wake kitu kilichokuwa ndani. Wote walitazama na kushuhudia chupa mbili zilizohifadhiwa kwenye chemba mbili maalum ndani ya sanduku hilo. Chupa moja ikiwa na rangi ya kijani na nyingine ikiwa na rangi ya kijivu.

"Now it's time to show the whole world how powerful ZMLST is. We are going to spread these COBOS viruses in Africa and later around the World"( Ni muda wa kuionyesha Dunia ni jinsi gani ZMLST inanguvu, tunakwenda kusambaza hivi virusi vya COBOS Africa na baadae Dunia nzima)
Profesa Fernando aliongea kwa kumaanisha, akatulia kwa muda kisha akaendelea kuongea.

"We are the only ones who will be able to provide vaccine and cure against this deadly COBOS virus. This green bottle contains the COBOS virus and this gray bottle carries a cure/vacinne against it"( Ni sisi pekee ndio kutakaoweza kutengeneza chanjo na tiba dhidi ya kirusi hiki hatari cha COBOS. Hii chupa ya kijani imebeba virusi vya COBOS na hii chupa ya kijivu imebeba tiba/kinga yake)
Profesa Fernando alitulia tena kwa muda kuhakikisha kama maneno anayoyazungumza yanawaingia vizuri watu wake ambao wote walikuwa wakitikisa vichwa vyao wakionekana kwenda sambamba na kukubaliana na maelezo ya Profesa Fernando, akaendelea kuzungumza.
"Through this initiative we will not only make billions of money but we will also restore the dignity and status of our laboratory that was lost for many years. The important thing right now is to choose one country in Africa that will be our starting point. We will persuade some key leaders to join our initiative" (kupitia mpango huu si tu kutengeneza mabilioni ya pesa bali tutarudisha heshima na hadhi ya maabara yetu iliyopotea kwa miaka mingi. Kitu muhimu kwa sasa ni kuchagua nchi moja huko Africa ambayo itakuwa kama sehemu yetu ya kuanzia. Tutawashawishi baadhi ya viongozi muhimu waingie kwenye mpango wetu)
Alieleza Profesa Fernando.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa miezi michache baadae kila kitu kikawa kimekamilika Nchi husika Africa ikapatikana na baadhi ya viongozi muhimu wakaingizwa moja kwa moja kwenye mpango huu huku wakipewa kiwango kikubwa cha pesa na kuhakikishiwa usalama wao na ndugu zao kwani tiba na kinga ya virusi vya COBOS ilikuwepo.

Timu ya wazungu wanne(4) kutoka Mexico iliwasili nchini wakijifanya watalii ambao walipata mualiko rasmi hadi ikulu kwa Rais wa awamu hiyo Profesa Cosmas Kulolwa ambaye alikuwa ni mmoja kati ya viongozi waliopo kwenye mpango wa kuingizwa kwa virusi vya COBOS nchini. Viongozi wengine wa nchi walioshiriki alikuwepo Waziri wa afya Mheshimiwa dokta Isaack Gondwe, Mkemia mkuu wa serikali bwana Andiwelo Katabi, Mkuu wa masheji Jenerali Gwamaka Antony ambaye aliteuliwa na Rais wa awamu hiyo mara baada ya Marehemu Jenerali Phillipo Kasebele kustaafu (baba wa Tino na Aron).

Vimelea vya Virus-COBOS(V-COBOS) vikawa vimewasili rasmi nchini, kilichobaki ikawa inasubiriwa siku ambayo imepangwa kuviachia rasmi na kusababisha mripuko wa ugonjwa hatari ambao utasambaa kwa kasi na kuitikisa Dunia nzima.
ZMLST wakiwa katikati ya mpango huu hatari mara ukaibuka ugonjwa mwingine ukianzia China, ugonjwa huu ulikuwa ni mpya unaosababishwa na kirusi cha COVID-19 uliitwa KORONA. Hii ikawafanya ZMLST wasitishe zoezi la kukiachia kirusi cha COBOS mpaka pale maambukizi ya COVID-19 yatakapopungua au kuisha kabisa.
Zile chupa mbili yaani chupa ya kijani iliyobeba kimelea cha V-COBOS na ile ya kijani iliyobeba tiba na kinga ya V-COBOS zikahifadhiwa katika maabara kuu ya serikali kwa siri, na hii ikawa ni siri ya watu wachache.


Wakati mambo haya yakiendela Jenerali Phillipo Kasebele ambaye ni baba wa Inspekta Aron na Tino lakini pia mume wa Sultana alikuwa ni mmoja wa watu waliotakiwa kuwa kwenye mpango huu, lakini alikataa kata kata kuwa mshirika wao akisimamia kanuni misingi na kiapo alichokula kwa ajili ya Nchi yake na hii ndiyo sababu iliyomfanya Rais Cosmas Kulolwa kumtaka Jenerali Phillipo astaafu kwa lazima kabla ya muda wake kufika. Ikawa hivyo Jenerali Phillipo akastaafu na punde Rais akamteua mkuu wa majeshi mwingine Jenerali Gwamaka Antony.

Baada ya Jenerali Phillipo kustaafu hakutaka kuishia hapo na kuuacha mpango huo hatari wa kusambazwa kwa virusi vya COBOS kuendelea, alijipanga kuhakikisha anazuia taratibu zao zote.
Jenerali Phillipo alikuwa na kijana wake mashuhuri jasusi kutoka Kenya aliitwa Shadow.
Shadow alikuwa ni jasusi kweli kweli katika kazi zote alizokuwa akizifanya hakuwahi kushindwa hata mara moja.
Hakuna aliyewahi kuiona sura yake wala hakujulikana ni wapi anaishi hata Jenerali Phillipo wenyewe hakujua. Wakati wote shadow alikuwa anavaa mavazi meusi juu mpaka chini kuficha sura yake.
Kazi ya kwanza aliyopewa na Jenerali Phillipo ilikuwa ni kuiba vimelea vya V-COBOS kutoka maabara kuu ya serikali kazi iliyokuwa ngumu kwa Shadow pengine kuliko kazi nyingine zote alizowahi kuzifanya.
Siku zote Shadow aliamini 'kujaribu ukashindwa ni bora zaidi kuliko kushindwa kujaribu' hivyo aliifanya kazi hiyo na mwisho akafanikiwa kuiba chupa ya kijivu iliyokuwa na tiba dhidi ya V-COBOS lakini hakufanikiwa kuiba ile chupa ya kijani yenye virusi vya COBOS.

Ingawa haikuwa lengo la Jenerali Phillipo lakini kupata chupa ile ya kijivu ilikuwa ni hatua kubwa sana iliyowarudisha nyuma ZMLST ambao walikuja juu wakimtaka Rais Profesa Cosmas Kulolwa afanye kila analoliweza kuhakikisha chupa hiyo inarudi hali iliyoleta mkanganyiko mkubwa. Hadi anatoka madarakani Profesa Cosmas Kulolwa hakufanikiwa kujua ni wapi na ni nani aliyeiba chupa ile ya kijivu.
Mbaya zaidi ZMLST hawakuwa na uwezo wa kutengeneza tiba wala kinga nyingine ya virusi vya V-COBOS. Hii ilikuwa ni hazina yao iliyotuzwa kwa muda mrefu, hakuna aliyejua fomula ya kutengeneza au kuharibu V-COBOS na ili kufanikiwa ilihitaji utafiti mwingine ambao ungewachukua miaka zaidi ya kumi. Hii ndiyo sababu wakawa wanashinikiza iwe mvua iwe jua lazima chupa ile ya kijivu ipatikane.

Baada ya miaka mitatu kupita baadae wakaja kugundua kuwa Jenerali Phillipo Kasebele ndiye aliyehusika kuiba chupa ile ya kijani. Kukawa na vita kali baina ya mwanajeshi huyu mstaafu na viongozi wa serikali waliokuwa wakiijua siri.
Ilikuwa ni ngumu kwao kumshambulia moja kwa moja Jenerali Phillipo kwani waliogopa siri hii kujulikana hivyo wakawa wanawindana kimya kimya na mzee huyo ambaye kwa miaka hiyo mitatu alijipanga kikamilifu kuilinda chupa ile ya kijivu akishirikiana na mkewe Sultana.
Baada ya kuona wanashindwa kupambana naye wakaamua kutumia njia mbadala.

Siku moja Waziri wa afya Mheshimiwa Dokta Isaack Gondwe alifanikiwa kumlaghai Tino mtoto wa kwanza wa Jenerali Phillipo ambaye alishawishika kwa pesa kidogo akakubali kumsaliti baba yake. Tino hakuelezwa chochote kuhusu vimelea vya V-COBOS lakini kwa mikono yake alimuua baba yake bila mtu yeyote kujua hivyo ndivyo alivyokubaliana na Dokta Gondwe, kuanzia siku hiyo akawa ni kibaraka wake.
Licha ya kwamba Dokta Gondwe hakuweka wazi sababu za kumtaka Tino amuue baba yake mzazi lakini tayari Tino alikuwa anajua mchezo mzima kuhusu vimelea vya V-COBOS. Kuna wakati alikuwa akimsikia Baba na mama yake wakizungumzia suala hili nyeti kwa siri hivyo hata kabla ya kuungana na Dokta Gondwe tayari Tino alikuwa anajua karibu kila kitu kuhusu vimelea vya V-COBOS na hii ndio sababu alikubali kirahisi sana kumuua baba yake, kumbe naye alikuwa na mipango yake kichwani. Aliingia tamaa ya kuzitaka chupa zote mbili, ile ya kijani kutoka kwa Dokta Gondwe ile ya kijivu kutoka kwa mama yake.

Baada ya Jenerali Phillipo Kasebele kufariki siri ilipo chupa ya kijani ilibaki kwa mkewe Sultana pamoja na yule jasusi Shadow.
Sultana alielewa kila kitu kuhusu mwanae Tino kuwa ameshagundua siri ya vimelea vya V-COBOS na ndiye aliyemuua mume wake. Alijua wazi ipo siku Tino atambana na kutaka chupa ya kijivu pengine anaweza hata kujaribu mumuua kama alivyofanya kwa mumewe. Ili kujiepusha na hilo Sultana alitumia akili kubwa akatengeneza mpango kwa kujifanya mgonjwa akalazwa hospitali ya Mountenia kwa kipindi kirefu huku akifanya mambo yake kimya kimya.
Sultana naye alikuwa kinyume na matakwa ya marehemu mumewe aliyetaka kuzuia mpango huu hatari wa virusi vya COBOS. Baada ya kufariki Sultana aliingiwa na tamaa akatamani kuzipata chupa zote mbili ile ya kijani na hii ya kijivu aliyoachiwa na mumewe hivyo kipindi chote alichokuwa akijifanya mgonjwa alimtumia jasusi Shadow kufuatilia nyendo za Tino ili aweze kupata chupa ile ya kijani kutoka maabara kuu ya serikali.
Tamaa aliyokuwa nayo Sultana ndio hiyo hiyo aliyokuwa nayo mtoto wake. Tino alikuwa akizitaka chupa zote mbili ile ya kijani yenye vimelea vya V-COBOS na hii ndio sababu akajiweka karibu na Waziri wa afya Dokta Gondwe akiamini atamtumia kama njia ya kuvipata vimelea hivyo. Lakini pia Tino aliendelea kusimamia matibabu ya mama yake kwa nguvu zote huku akitumia pesa nyingi sana akiamini mama yake ndiye anaejua ilipo chupa ile ya kijivu hivyo lazima ahakikishe anapona.
HIVYO NDIVYO ILIVYOKUWA.


SASA TURUDI KWENYE STORI YETU...
Usiku wa saa nane hali iliendelea kuwa tulivu ndani ya hospitali ya Mountenia. Inspekta Aron alikuwa amekaa nje ya chumba kipya alichohamia Annah kwa sasa, wakati huo mama yake (Sultana) alikuwa katika hospitali hiyo hiyo ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi ICU akiyatafakari maelezo ya Shadow aliyemwambia kuwa kesho ndio siku ambayo Dokta Gondwe atakabidhi vimelea vya V-COBOS kwa Tino. Sultana akajikuta anatabasamu akiamini lengo lake linakwenda kutimia. Atamvamia Tino kirahisi na kumnyang'anya vimelea vya V-COBOS. Ilikuwa ni kama vile anamtegea mwanae, alisubiri aanze kisha yeye amalizie. Huu ndio ulikuwa mpango mzima wa Sultana.


Usiku huo pia ulikuwa ni mrefu kwa Tino ambaye alitamani masaa yaende kwa kasi ifike ule wakati ambao Dokta Gondwe aliahidi kutoa vimelea vya V-COBOS kutoka maabara kuu ya serikali kuvileta kwake. Tayari alishapanga kila kitu na kijana wake Bosco ambaye ndiye ataekuwa kwenye boti badala yake. Licha ya kwamba kulikuwa na kila dalili kuonyesha Dokta Gondwe anampango mwingine tofauti lakini Tino aliamini kupitia zile picha na video za ngono za Dokta Gondwe zitampa nafasi ya kuendelea kumthibiti.

"Acha ajichanganye na kuleta janja janja atajua hajui" aliwaza Tino

Hali ilikuwa hivyo hata kwa mheshimiwa Waziri wa afya Dokta Gondwe, hakuwa amepata hata chembe ya usingizi usiku huo bado alikuwa akiwaza kama mpango alioshauriwa na Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa utafanya kazi au laa!.

JE NINI KITAFUATA?
SASA TUMEELEWA KWA KINA KUHUSU VIMELEA HIVI VYA V-COBOS KUTOKA MEXICO...
JE NI NINI HATIMA YA MCHEZO HUU HATARI?
ITAENDELEA....
 
THE MODERN WAR
(vita ya kisasa)
Sehemu ya.............17
Mtunzi: saul david
WhatsApp: 0756862047

17-(USIKU WA CHATTING)
ILIPOISHIA...16
Sehemu iliyopita tulifanikiwa kujua chimbuko la virusi vya COBOS namna vilivyotoka Mexico mpaka vikaingia nchini. Namna marehemu Jenerali Phillipo Kasebele alivyopambana na baadae kuuwawa kikatili na mtoto wake wa kumzaa, Tino.
Simulizi yetu iliishia wakati Godwin amemuua Big' akidhani kuwa ni Annah asijue Annah alihamishiwa chumba kingine tofauti na sasa yuko chini ya uangalizi mkali wa Inspekta Aron mwenyewe.
Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA....
Ikiwa ni majira ya saa 8 usiku Inspekta Aron alikuwa amekaa kwenye moja ya viti vilivyokuwa nje ya chumba alicholazwa Annah ndani ya hospitali ya Mountenia. Alikuwa amechoka sana huku usingizi ukionekana kumuelemea lakini hakutaka kukubali kuyafumba macho yake hata sekunde moja. Kumlinda Annah ilikuwa ni kipaombele chake cha kwanza siku hiyo.
Akiwa anahangaika kupambana na usingizi huo kumbe kwa muda mrefu Annah alikuwa ameinuka kutoka kitandani akawa amesimama nyuma ya mlango wa kioo akimtazama Inspekta Aron namna alivyokuwa akihangaika pale nje kwa ajili yake.

Annah aliitumia nafasi hiyo kumkagua Inspekta Aron kwa muda mrefu sana, akajikuta anawaza mengi kumuhusu kaka huyo ambaye hakujua kama kuna mtu amesimama kwa muda mrefu anamtazama.

"Amechoka, anapambana kwa ajili ya usalama wangu, ameyaokoa maisha yangu na sasa yupo hapa ananilinda dhidi ya maadui" aliwaza Annah, mawazo yake yakampeleka mbali sana akakumbuka siku moja aliwahi kuambiwa maneno fulani na marehemu mama yake

"Mwanangu wewe bado ni msichana mdogo, usiyapaparikie mapenzi utaharibikiwa mapema. Unatakiwa utulie uchague mwanaume ambaye ni sahihi kwako, siku moja mimi na baba yako hatutokuwepo kila kitu tunachokifanya kwako sasa hivi kama kukupenda, kukujali na kukulinda atatakiwa kufanya huyo mwanaume ambaye utamchagua hivyo kuwa makini"
Sauti hii ya mama yake ilijirudia kichwani kwa Annah

"Mmeondoka mapema mama mmeondoka hata kabla sijamjua mtu atakayeyafanya hayo yote kwa ajili yangu" Alisema Annah machozi yakimlenga kwa mara nyingine.
Mara alishtuka kumuona Inspekta Aron liyekuwa ameanza kusinzia pale kwenye kiti alikurupuka ghafula baada ya kutaka kudondoka.

Inspekta Aron alifikicha macho yake yaliyojaa usingizi kisha akatazama huku na huku kuhakikisha usalama na hapo ndipo macho yake yalipogongana na macho ya Annah aliyekuwa kwenye mlango wa chumba chake anamtazama

Walitazamana kwa sekunde kadhaa kisha Annah akatazama pembeni kwa aibu za kike kike huku akitabasamu. Inspekta Aron naye alipata aibu kiasi baada ya kubaini kumbe alikuwa anasinzia mbele ya mrembo huyo.

"Wewe" Inspekta Aron aliita kwa sauti ya chini wakati huo Annah alikuwa akifungua mlango akatoka na kutembea taratibu hadi pale alipokuwa Inspekta Aron.
"Nambie afande"
"Mbona hujalala"
"Sijapata usingizi, nilitaka kutoka nje nitembee tembee kupunguza mawazo ndio nikakuona hapa"
"Aah! wewe mwanamke utembee uende wapi sasa usiku huu?"
"Kwani ni saa ngapi?" aliuliza annah huku akikaa kwenye kiti pembeni ya Inspekta Aron
"Ni saa tisa kasoro usiku"
"Mda hata hauendi jamani, sasa na wewe kwa nini haujalala?"
"Mimi nipo hapa, nakulinda"
"Ahahah unanilinda au unasinzia?" Alisema Annah, kwa mara ya kwanza Inspekta Aron akaliona tabasamu la mwanamke huyo aliyekuwa na huzuni kwa muda mrefu

"Angalau amecheka, mh! ni mrembo kumbe"Aliwaza Inspekta Aron
"Umesema?" Aliuliza Annah
"Nini kwani nimeongea?"
"Ndio kwamba nimesikia vibaya"
"Huenda, mbona mimi sijasema kitu" Alisema Inspekta Aron huku akimtazama Annah usoni wakatazamana tena kisha wakatabasamu kwa pamoja, lakini mara lile tabasamu likapotea ghafula kwenye uso wa Annah.

"Nini! Unawaza nini?" Aliuliza Aron
"Hamna niko sawa.. Aron, unaitwa Aron si ndio?"
"Yeah Aron Phillipo Kasebele"
Alijibu Aron kisha kukawa kimya tena, baadae Annah akavunja ukimya, akawa anazungumza kwa uchungu...
"Najaribu kuwaza tu ni jinsi gani maisha yangu yamebadilika ghafula, kweli hakuna aijuae kesho yake, ni siku chache tu nilikuwa naishi kwa furaha mimi na wazazi wangu wote wawili lakini kila kitu kikabadilika ghafula tangu siku ile ya Birthday yangu. Najuta kwa nini nilitaka tufanye ile part kwenye ule mgahawa, mwisho tukajikuta tunashuhudia mauaji ya kutisha. Yule Osward aliua mtu mbele ya macho yetu bila huruma akakimbia, baadae akaanza kuua watu walioshuhudia tukio lile mmoja baada ya mwingine, licha ya kukamatwa lakini bado watu wake wakaendelea kuua ili tu kufuta ushahidi, na hatimaye zamu yetu ikafika, wakamuua baba wakamuua na mama pia, mimi nikanusurika na sasa najua wananisaka kwa udi na uvumba kuhakikisha nakufa,najua ndio maana uko hapa Inspekta Aron, maisha yangu yamebadilika nimekuwa kama.....aaah jamani" Annah aliongea kwa uchungu akashindwa kumalizia sentensi yake, akaanza kulia kwa uchungu sana.

Inspekta Aron alijikuta anaanza umpya kumbembeleza Annah anyamaze, hakika maisha ya binti huyo yalikuwa ya kuumiza sana.
"Usijali Annah hiyo yote ni mipango ya mungu, kila kitu kitakuwa sawa hakuna baya litakalokukuta HAKUNA MTU ATAKAYEKUGUSA KABLA HAJANIGUSA MIMI" Aron aliongea kwa kumaanisha, maneno hayo yalikuwa ni faraja kubwa kwa Annah, akajikuta anamkumbatia Inspekta Aron kwa nguvu.

Walikumbatiana kwa zaidi ya dakika mbili, hapo Inspekta Aron akamtoa Annah taratibu huku akimpiga piga mgongoni

"Usiniachiee.." Alisema Annah kwa sauti iliyojaa mchoko. Inspekta Aron akamlaza kwenye kifua chake huku akiuzunguusha mkono wake nyuma ya mgongo wa Annah, akamshika vizuri.
Haukupita mda Annah akawa amepitiwa na usingizi akalala. Taratibu Inspekta Aron akamlaza kwenye miguu yake kisha akachukua shuka alilokujanalo akamfunika.

Inspekta Aron aliinamisha uso wake akawa anamtazama Annah kwa macho yenye huruma na upendo mwingi. Akawa anashikashika nywele ndefu za binti huyo na wakati mwingine akiugusa uso wake, alikuwa ni mrembo haswa.

Hapo Inspekta Aron aliikumbuka simu yake, akachukua kutoka mfukoni kisha akatazama saa, ilikuwa ni saa kumi kasoro usiku.
Inspekta Aron alifungua uwanja wa meseji kwenye simu yake akakuta kuna jumbe 14 ambazao hazijasomwa na zote kutoka kwa Najma mtoto wa Waziri Dokta Gondwe. Aron alifungua pia upande wa mtandao wa WhatsApp huko akakuta ametumiwa picha na yule rafiki yake ambaye ni askari magereza, zilikuwa ni picha zikimuonyesha Big na Osward wakati ule wakifanya mazungumzo pale gerezani.
Inspekta Aron alizitazama picha zile kwa makini kisha akausogeza karibu uso wa Big', alihisi ni kama mtu huyo alimuona mahali lakini hakukumbuka ni wapi, ni kweli Inspekta Aron alimuona Big' kwa mbali wakati ule akiwa amembeba Najma na kumuingiza kwenye gari lakini kwa bahati mbaya akawa hakumbuki.

***********
{TANGAZO:- Epuka matapeli simulizi hii imetungwa na SAUL DAVID simu 0756862047, Tafadhali usinunue kwa mtu mwingine tofauti }
******-*-
Inspekta Aron aliamua kuachana na picha hizo akiamini kabisa mchoko aliokuwanao ndio sababu hasa ya kumfanya asahau ni wapi alimuona Big' ambaye kwa sasa tunajua ni marehemu mwili wake ukiwa kwenye chumba ambacho Annah alikuwa amelazwa awali.
Inspekta Aron alirudi kwenye uwanja wa meseji akafungua na kuaanza kusoma zile jumbe 14 kutoka kwa Najma moja baada ya mwingine.

,,, Habari za mida,,,,,
,,,,,,Mambo,,,,,,,
,,,,,,Aron umelala?,,,,,,
,,,,,,Sorry naweza kupiga simu,,,,,,
,,,,,,,Aron Dokta wangu mguu umeanza kuuma sasa nafanyaje, nitumie dawa ipi kati ya hizi?,,,,,,
,,,,,,,Aron mwenzio naumia,,,,,,
,,,,,Sijapata usingizi hadi sasa,,,,,
,,,,,Hlw,,,,,,
,,,,,,,Aron,,,,,,
,,,,,,,Ee jaman huyo mkeo si akuache kidogo,,,,,,
,,,,,,Aron naumwa serious,,,,,,
,,,,,Hlw hadi sasa saa 7 sijapata usingizi Aron mguu unauma sana,,,,,
,,,,,,We mwanaume,,,,,,
,,,,,,,Mmh,,,,,,,

Inspekta Aron alijikuta anatabasamu mara baada ya kumalizia kuzisoma meseji hizo kutoka kwa pisi kali mtoto wa Waziri wa afya Dokta Gondwe.

,,,,,,,,,Pole, samahan nilikua bize kidogo si unajua hizi kazi zetu nitakupigia asubuh pumzika,,,,,,
Aron alijibu huku akimtazama Annah ambaye alikuwa akijigeuza kwenye miguu yake, akagundua shingo ilikuwa imeanza kukuuama baada ya kulala kwa muda mrefu kwenye miguu yake. Aron akaweka simu pembeni akavua koti lake kisha akamuinua Annah taratibu akaweka lile koti juu ya miguu yake kisha akamlaza tena.
Alipoichukua simu yake akakutana meseji mbili zilizoingia mfurulizo kutoka kwa Najma.

,,,,Eeh pole mwaya,,,,,,,
,,,,,Mguu unauma sana Aron au nimeumia sana?,,,,,,

"Duh hajalala huyu mwanamke" Alisema Inspekta Aron na hapo akajikuta anaanza kuchati na Najma. Ikawa ni mwendo wa meseji mfurulizo kila mmoja akionekana kufurahia kuchat na mwenzake. Wakati huo wote Annah alikuwa amelala kwenye miguu ya Inspekta Aron.

Hatimaye kukapambazuka ikafika asubuhi ya siku ambayo ilikuwa ikisubiwa kwa hamu, siku ambayo hakuna aliyejua itaisha vipi si Dokta Gondwe si Tino si Sultana wala si Shadow ilikuwa ni siku yenye kitendawili kizito ni nani atabaki na vimelea vya V-COBOS.

ITAENDELEA....
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya.............18
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
18-(Jasusi Shadow na Arone)
ILIPOISHIA....17
Hatimaye kukapambazuka ikafika asubuhi ya siku ambayo ilikuwa ikisubiwa kwa hamu, siku ambayo hakuna aliyejua itaisha vipi si Dokta Gondwe si Tino si Sultana wala si Shadow ilikuwa ni siku yenye kitendawili kizito ni nani atabaki na vimelea vya V-COBOS

SASA ENDELEA....
Ikiwa ni majira ya saa 12 alfajiri Inspekta Aron alimuinua Annah aliyekuwa amelala miguuni pake akambeba na kumuingiza chumbani kwake, akamlaza taratibu kitandani.
Inspekta Aron alisimama kwa sekunde kadhaa akimuangalia Annah ambaye alionekana bado amelala. Aron alitabasamu akamfunika vizuri kisha akaanza kuondoka.

"Unaenda wapi Aron" mara ilisikika sauti yenye uchovu mwingi kutoka kwa Annah, Inspekta Aron akashtuka na kugeuka
"Nilijua umelala?"
"Hamna niko macho usiku wote hata sijalala"
"Mmh!!"
"Ndiyo, sikuwahi kuwaza kama maaskari nao huwa wanachati kwa muda mwingi kama wewe leo, usiku kucha wewe na simu huo usingizi mimi ningepata wapi?" alisema Annah huku akifumbua macho yake kumtazama Inspekta Aron ambaye alitazama pembeni kwa aibu

"Aheheh unataka kusema mimi ndio nimesababisha usipate usingizi?"
"Ndio hivyo hata ungekuwa wewe ungelala?"
"Hahah haya bana samahani alikuwa ni mtu muhimu ndio maana" alijibu Aron huku akijichekesha
"Hata mimi naona alikuwa ni muhimu kweli kweli" Alisema Annah kauli iliyokuwa na wivu ndani yake.
"Ingia bafuni basi uoge nimwite daktari aje akuangalie kidonda" Alisema Aron wakati huo simu yake ikawa inaita mpigaji alikuwa ni Dokta Zyunga, akapokea.

"Inspekta Aron uko wapi?"
"Niko huku kwa Annah, vipi kuna shida Dokta?" Aliuliza Aron akihisi kuna jambo haliko sawa kutokana na namna Dokta Zyunga alivyozungumza
"Ndio hebu njoo mara moja"
"Nije wapi?"
"Huku juu chumba alichokuwa Annah mwanzoni"
"Sawa" Aron alikata simu kisha akatoka upesi bila hata kumuaga Annah.


Dakika mbili baadae Aron alifika mahali alipoitwa. Ndani alimkuta Dokta Zyunga na nesi mmoja wamesimama mbele yao kukiwa na mwili wa mtu umelala sakafuni huku damu nyingi ikiwa imetapakaa kuuzunguuka mwili huo

"Nini kinaendelea Dokta Zyunga?" Aliuliza Aron
"Mauaji?"
"Ni nani huyu amekufa, Oh! My God hii ni Risasi kutoka bunduki ya masafa marefu" alisema Aron mara baada ya kuliona jeraha la marehemu. Inspekta Aron akageuka na kutazama dirishani, kioo kilikuwa kimepasuka upande mmoja na upande mwingine kulikuwa na tundu risasi ilipopita
Inspekta Aron aliendelea kukagua kila mahali kwa macho yenye uzoefu wa kipelelezi hazikupita dakika tano tayari akawa anamajibu ya kila kitu.

"Nesi hebu tupishe mara moja tuzungumze, hakikisha hii pia inakuwa ni siri usimwambie mtu" Alisema Dokta Zyunga, yule nesi akatikisa kichwa kukubaliana na maelezo hayo kisha akatoka na kuwaacha Inspekta Aron na Dokta Zyunga ambao walianza kujadili tukio lile.

"Inspekta Aron mbona sielewi, nawaza hawa watakuwa ni watu wanaomtafuta Annah lakini kivipi huyu ameuwawa hapa?" Aliuliza Dokta Zyunga
"Namjua huyu mtu"
"Unamjua!! Kivipi? ni nani?"
"Alikuwa akinifuatilia mimi, ametumwa na Osward yule kijana mwenye kesi ya mauaji aliyepo gerezani mtoto wa mzee Matula" Alisema Aron huku akitoa simu yake akafungua na kumuonyesha Dokta Zyunga zile picha za Big' alizotumiwa na rafiki yake askari magereza.

"Hapo alikuwa akifanya mazungumzo na Osward akamtuma aje kuniua, alikuwa akinifuatilia tangu jana nilipotoka kule gerezani, wakati naingia kwenye gari nilimuona lakini sikumtilia maanani" alieleza Inspekta Aron kumbukumbu zake zikionekana kukaa sawa sasa

"Mmh! sasa nani kamuua na kwa nini?"
"Watu wanaotaka kumuua Annah ndio wamefanya haya mauaji, mdunguaji alikuwa ndani ya hiyo hoteli jirani hapo mbele, hakuweza kumuona muhusika anayempiga risasi kwa sababu ya haya mapazia hivyo wanaamini wamemuua Annah" Inspekta Aron alieleza akionyesha ni namna gani amebobea kwenye kazi yake ya upelelezi, alilielezea tukio zima kwa uharisia wake kama vile alikuwepo.

"Kwa hiyo tunafanyaje"
"Kila kitu kiendelee kuwa siri Dokta Zyunga hadi siku ya mahakamani itakapofika, kwa kuwa wanaamini wamemuua Annah basi na mimi nitawaaminisha hivyo ili waache kabisa kitufuatilia"
"Sawa vipi kuhusu huu mwili"
"Kautunze mochwari, Dokta Zyunga swali gani hilo unauliza? wewe ni mtu mkubwa hapa hospitalini unaogopa watakuhoji"
"Aah hapana ilaa...."
"Nini, au humwamini huyu nesi wako?"
"Hapana! hapana! huyu nesi hana shida, basi sawa nitafanya hivyo Inspekta ila kuwa makini hili swala ni zito, una maadui wengi sana Inspekta, narudia tena kuwa makini kwa kila hatua unayopiga"
"Usijali, kuwa makini pia mimi nikiwa hatarini hata watu wangu wanaonizunguuka wanakuwa hatari" Alieleza Inspekta Aron huku akiinama na kukagua mifuko ya nguo alizovaa Big' akakuta simu, akaichukua
"baadae narudi kwa Annah" alisema Inspekta Aron akapiga hatua na kuondoka.


"Sasa ni wakati wa kucheza kikubwa kaka Tino" Aliwaza Inspekta Aron akiwa anaingia ndani ya lifti, wakati huo akapishana na mtu mwingine akishuka kutoka kwenye lifti hiyo hiyo.
Walipopishana Inspekta Aron akageuka kumtazama tena mtu huyo. Alikuwa mwanaume aliyevaa mavazi meusi juu mpaka chini pia kichwani alivaa kofia aina ya kapero aliyoishusha chini kufunika sura yake, alitembea akiwa ameinama kiasi cha kumfanya Inspekta Aron asiione kabisa sura ya mwanaume huyo, hakuwa mwingine bali Shadow jasusi anayefanya kazi chini ya mama yake yaani Sultana.

"Hello kaka habari" Inspekta Aron alimsalimia, Shadow akavunga kama vile hajasikia akaendela kutembea
"Oi brother hebu simama kwanza..." Aron aliongea kwa mara ya pili tena kwa sauti kubwa zaidi ya mwanzo hapo Shadow akasimama lakini hakugeuka
Inspekta Aron alikuwa ni mtu makini sana zile sekunde chache alizopishana na Shadow zilitosha kuwasha taa nyekundu kwenye akili yake akajua moja kwa moja mtu aliyepishana naye hakuwa mtu wa kawaida.
Kwa bahati mbaya hakujua ile hatari aliyoinusa kwa mtu huyo ilikuwa ni mara mbili yake, Shadow alikuwa ni moto wa kuotea mbali, hata marehemu baba yake alikuwa akimpigia saluti.
Baada ya Shadow kusimama Inspekta Aron alihairisha kuingia kwenye lifti akaanza kupiga hatua taratibu kumsogelea
"Samahani ndugu mimi ni asifa wa polisi niko hapa kwa kazi maalumu tafadhali naweza kukutambua wewe ni nani" Aron aliongea kwa upole akiwa amebakiza hatua kadhaa kumfikia Shadow.

Shadow alitulia kimya bila kuzungumza chochote hakugeuka wala nini. Shadow alikuwa ni mtu mwenye maisha yenye misingi ya ajabu sana hakuwa akiruhusu mtu yeyote aione sura yake hata marehemu Jenerali Phillipo Kasebele hakuwahi kuiona sura yake licha ya kufanya kazi pamoja kwa zaidi ya miaka 10. Kitendo cha Inspekta Aron kutaka kumtambua lilikuwa ni jambo ambalo hawezi kukubali litokee, haraka alikili yake ilifanya kazi upesi akapata jibu nini cha kufanya

Inspekta Aron aliyekuwa anazidi kusogea karibu na Shadow alisita ghafula baada ya kuhisi mtu huyo alikuwa anataka kufanya jambo akachukua tahadhali


Upande wa pili nyumbani kwa wazari wa afya Mheshimiwa Dokta Isaack Gondwe aliamka asubuhi na mapema tofauti na ilivyokuwa kawaida yake, akajiandaa vizuri kisha akatoke nje ya nyumba yake, ratiba yake ya kwanza ilikuwa ni kwenda maabara kuu ya serikali vilipo hifadhiwa virusi vya COBOS

"Shikamoo Baba mbona mapema leo wapi?" Aliuliza Najma aliyekuwa akimwagilia maua nje ya nyumba yao
"Marhaba binti yangu, mguu wako unaendeleaje?"
"Safi ila usiku umeuma sana ila kwa sasa afadhali kidogo"
"Sawa leo nawahi ofisini nina kazi muhimu sana, baadae mwanangu" Dokta Gondwe aliongea kwa kifupi kisha akaingia kwenye gari lake, walinzi wakafuata na safari ikaanza

Najma alilisindikiza kwa macho gari la baba yake hadi lilipotoweka kwenye upeo wa macho yake. Najma alikumbuka yale maongezi nyeti aliyoyasikia usiku wakati baba yake akiongea kwenye simu na mtu ambaye hakumtambua, alihisi maongezi yale yalikuwa ni moja kati ya sababu ya baba yake kuamka mapema leo.
Baada ya kumaliza shughuli ya kumwagilia maua Najma alioga akapata kifungua kinywa kisha akakaa sebureni akiwa na kompyuta yake ndogo, akaifungua na kuwasha mtandao kisha akaandika maneno yafuatayo kwenye tovuti ya Google...

what's the V-COBOS...(nini maana ya V-COBOS)

Hili lilikuwa ni neno ambalo Najma alilisikia mara nyingi sana wakati ule baba yake anaongea na simu, sasa rasmi Najma akaanza kufuatilia nyendo za baba yake mzazi hasa baada ya Inspekta Aron kumwambia kuwa baba yake si mtu mzuri kama anavyofikiri hivyo Najma akawaza kulithibitisha hilo mwenyewe. Kwanza kabisa akataka kufuatilia kujua maana ya vimelea vya V-COBOS ambavyo baba yake alikuwa akivitaja mara nyingi wakati wa mazungumzo yale usiku


Upande wa pili Inspekta Aron aliendelea kusogea karibu na Shadow lakini mara alisita ghafula baada ya kuhisi Shadow anataka kufanya jambo ikabidi achukue tahadhari
Haraka Inspekta Aron alizunguusha mkono wake wa kuume nyuma ya kiuno chake akachomoa bastola akaikoki na kumnyoshea Shadow kichwani. Alifanya hivyo ndani ya sekunde chache tu kiasi cha kumfanya Shadow ahairishe kufanya kile alichokusudia kufanya.

"Tulia hivyo hivyo, weka mikono kichawani alafu geuka nyuma taratibu" Inspekta Aron alitoa amri
Shadow hakuwa mbishi, akatii kile alichoambiwa, akageuka nyuma taratibu lakini akiwa bado ameficha sura yake kwa kuinama chini.
"Inua uso wako juu tafadhali" alisema Inspekta Aron huku akichukua tahadhali zote muhimu, tayari nafsi yake ilimwambia aliyesimama mbele yake hakuwa mtu wa kawaida hata kidogo na huo ndio ulikuwa ukweli wenyewe.
Shadow alitulia kwa sekunde kadha kisha taratibu akawa anainua uso wake. Inspekta Aron alitoa macho kwa shauku kubwa ya kutaka kuitambua sura ya mwanaume huyo ambaye mapaka sasa alifanikiwa kuona kidevu, mdomo na pua yake tu.
Ghafula Shadow alifungua mdomo na kutema kitu fulani kidogo mfano wa sindano kilichoenda kwa kasi na kutua kwenye shingo ya Inspekta Aron.
Lilikuwa ni tukio la kufumba na kufumbua baada ya kufanya hivyo Shadow aligeuka na kuanza kuondoka, Inspekta Aron alipojaribu kuzungumza alishindwa alipojaribu kupiga hatua kumfuata alishindwa, kifua kilimbana ghafula na kujikuta anakosa pumzi, akaanza kupumua juu juu na bastola yake ikidondoka chini. Aliinama huku akiwa ameshikilia kifua chake na kuhema kwa taabu sana. Aron alidumu katika hali hiyo kwa zaidi ya dakika mbili baadae akaanza kupata nafuu.

Inspekta Aron alipeleka mkono wake shingoni akachomoa ile sindano ndogo iliyotoka kwenye mdomo wa Shadow. Kilikuwa kijisindano kidogo sana kilichomchubua Inspekta Aron shingoni wala hata damu haikutoka.

"Baba!" Inspekta Aron alijikuta analiita jina la baba yake wakati anaitazama ile sindano. Haikuwa mara yake ya kwanza kuiona aina ile ya siraha aliwahi kuiona pia kwa marehemu baba yake Jenerali Phillipo Kasebele. Inspekta Aron alijikuta akiyakumbuka maneno aliyowahi kuambiwa na marehemu baba yake siku anaiona siraha hiyo ya ajabu.

"Mwanangu Aron nitakufundisha namna ya kuirusha hii sindano kwa kuipuliza, ni siraha nzuri sana inaweza kukusaidia ukiwa kwenye shida. Hakuna mwingine anaeijua zaidi yangu, nililetewa na kijana wangu mmoja ni jasusi yupo kenya" Haya yalikuwa ni maneno ya marehemu baba yake ambaye alifariki hata kabla hajamfundisha matumizi ya siraha hiyo. Kwa mujibu wa maelezo ya baba yake alisema hakuna mwingine anaejua kuhusu siraha hiyo zaidi yake na huyo Jasusi kutoka kenya, hali hii ikamfanya Inspekta Aron kujiuliza maswali

"Au huyu bwana atakuwa ni huyo Jasusi wa baba kutoka kenya? Kafuata nini huku? Hapana sio yeye" Inspekta Aron alijiuliza na kujijibu mwenyewe na hapo akajikuta anamkumbuka Annah, alihofu huenda bado ni watu wanaotaka kumuua binti huyo, mbaya zaidi yule bwana alitokea sakafu ya chini ya hospitali hiyo kule kilipo chumba cha Annah.

Inspekta Aron alianza kukimbia akiteremka kwenye ngazi kwa kasi, wala hakukumbuka tena kupanda lifti. Kadri alivyokuwa akisogea ndivyo hofu yake ikazidi kuongezeka, imani yake ilimwambia huenda yule bwana akawa amemfanyia kitu kibaya Annah kama sio kumuua kabisa.
Akiwa kwenye kasi ile ile Inspekta Aron alifika na kunyonga kitasa cha mlango akaingia moja kwa moja ndani ya chumba cha Annah.

"Mamaa..." Annah aliyekuwa anajiandaa kwenda kuoga alipiga kelele kwa hofu iliyochanganyikana na mshangao mara baada ya Inspekta Aron kuingia ghafula bila kupiga hodi, mbaya zaidi Annah alikuwa amevua nguo zake zote akiwa amesalia na nguo za ndani pake yake.
Haraka alichukua taulo dogo lililokuwa kitandani akajifunika upande wa mbele kuanzia kwenye matiti hadi katikati ya mapaja yake sehemu kubwa ya mwili wake ikawa wazi.
Inspekta Aron alisimama akiwa amepigwa na butwaa huku akihema kwa nguvu, alitazamana na Annah aliyekuwa amejikunyata ukutani kwa aibu akijaribu kujisitili.

Je, nini KITAFUATA?
Aron ataweza kugundua lolote kuhusu jasusi Shadow aliyewahi kufanya kazi na marehemu baba yake?
Vipi kuhusu NAJMA aliyeanza kufuatilia kuhusu vimelea vya V-COBOS?
Ni nani ataibuka mshindi ndani ya bahari ya Hindi Ni Shadow au Tino? Ni Dokta Gondwe au Sultana?
ITAENDELEA....
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..........19
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

19-( D- DAY)
ILIPOISHIA...
Inspekta Aron alisimama akiwa amepigwa na butwaa huku akihema kwa nguvu, alitazamana na Annah aliyekuwa amejikunyata ukutani kwa aibu akijaribu kujisitili.

SASA ENDELEA...
"Samahani" alisema Aron huku akitazama pembeni kwa aibu hapo Annah alisogea kitandani akachukua ile nguo pajama la wagonjwa akavaa haraka haraka

"Kwa nini umeingia ghafula hivyo, ungenikuta niko uchi sijavaa ingekuwaje" Aliuliza Annah akionekana kukasirika kiasi
"Ndio maana nimesema samahani, jiandae tunaondoka"
"Tunaenda wapi Aron?"
"Sehemu salama zaidi"
"Sehemu samala wapi?"
"Jiandae tuondoke Annah acha kuuliza maswali utajua mbele ya safari" Inspekta Aron aliongea kwa msisitizo huku akichukua simu yake, akampigia Dokta Zyunga.
Tayari Inspekta Aron alionekana kupata hofu kutokana na mfuatano wa matukio yasiyoeleweka ndani ya hospitali hiyo. Kuanzia mda ule amekutana na Tino, likafuata tukio la kuuawa kwa Big' na sasa amekutana na mtu wa ajabu ambaye hajui ni kitu gani kimemleta ndani ya hospitali hiyo.
Kwa maana hiyo kulikuwa na kila sababu za Inspekta Aron kumtoa Annah katika hospitali ya Mountenia yenye usalama mdogo.

"Hallo Dokta" aliongea Aron baada ya Dokta Zyunga kupokea simu upande wa pili
"Ndiyo Inspekta, niko mochwari huku nauhifadhi mwili wa yule bwana"
"Sawa Dokta, ukitoka huko naomba uniandalie vifaa vyote muhimu kwa ajili ya huduma ya Annah nataka nimtoe hapa hospitali"
"Mh! kwa nini mbona ghafula?"
"Aah! Hapana hakuna shida, nataka nimpeleke sehemu salama zaidi" Inspekta Aron hakutaka kuweka wazi hukusu tukio la kukutana na jasusi Shadow
"Sawa Inspekta basi nipe dakika kumi"
"Sawa"



Ilikuwa ni katikati ya bahari ya hindi umbali wa kilometa 50 kutoka ufukweni ilionekana boti moja kubwa ya kifahari ikiwa imetia nanga huku upepo mwanana na mawimbi kiasi yakilipamba eneo hilo

Ndani ya boti hiyo wanaume wawili walioonekana kufanya maandalizi ya tukio maalum ambalo linakwenda kutokea muda mfupi ujao, hawa walikuwa ni Tino na kijana wake Bosco.

"Kila kitu kipo sawa sasa" Alisema Bosco
"Yes ni kweli lakini vipi kuhusu wewe uko tayari?" Aliuliza Tino
"Ndiyo, siwezi kukuangusha bosi"
"Najua huwezi ila unatakiwa ufanye zaidi ya uwezo wako, utakapokuwa unazungumza na Dokta Gondwe hakikisha unajiamini usionyeshe dalili zozote zitakazomfanya ahisi huenda wewe umetumwa na sio muhusika mkuu wa zile video na picha zake chafu"
"Sawa bosi nimeelewa"
"Vizuri kitu kingine cha muhimu, anaweza kuanza kukupa kauli za vitisho hata kujaribu kukuua lakini usijali mimi nitakuwa hapa kukulinda, Dokta Gondwe atakuja na mimi hapa na sio mtu mwingine hivyo usijali jiamini, nasisitiza tena jiamini"

Bosco akawa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akainua macho yake na kumtazama Tino, akauliza.

"Lakini bosi, kwa nini Dokta Gondwe amepanga kuja na vijana wake hapa wakati tulimpa sharti aje peke yake huoni kuwa lengo lake ni kuja kuua na sio kuleta virus vya COBOS?"
"Uko sahihi kuna mawili hapa, Dokta Gondwe amefanya kubeti kwanza atakuja na hivyo vimelea vya V-COBOS lakini atataka kuhakikisha kuwa video zake za ngono anazipata zote na hazipo sehemu nyingine yoyote, akihakikisha hilo basi atakuua na sio kukupa vimelea. Lakini kama utaonyesha hata kama atakuua bado video zake zitavuja basi anaweza kukupa hao vimelea ili kujilinda na mtaweka makubaliano, ndio maana nimekwambia unatakiwa kujiamini sana unapoongea na Dokta Gondwe lolote linaweza kutokea" alieleza Tino

Mwisho mipango yote ilikaa vizuri, Tino akapanda boti nyingine ndogo inayoendeshwa na mashine akarudi ufukweni akimuacha kijana wake Bosco ndani ya boti ile kubwa

Muda ulizidi kusogea na sasa Tino alikuwa ufukweni pamoja na vijana wengine wawili. Tayari ile boti aliyoagiza Dokta Gondwe ilikuwa imeandaliwa sasa walikuwa wakimsuburi Dokta Gondwe wenyewe.

Muda mfupi baadae taksi moja ilisimama hatua kadhaa kutoka pale alipokuwa Tino na wenzake, akashuka mzee mmoja alievaa koti kubwa jeusi miwani na kofia pana, mkono wake wa kulia alikuwa ameshikilia sanduku dogo mfano wa begi aina ya briefcase'. Huyu hakuwa mwingine bali Mheshimiwa Waziri wa afya Dokta Isaack Gondwe.

Baada ya taksi kuondoka Dokta Gondwe alianza kupiga hatua kusogea pale Tino na wenzake walipo. Kwa namna alivyokuwa amevaa usingedhani kuwa huyu ni waziri wa afya Dokta Gondwe alikuwa na muonekano wa tofauti sana haikuwa rahisi hata kwa vijana wake kumtambua kwa haraka hadi pale alipowakaribia.

Tino macho yake yote aliyaelekeza kwenye lile sanduku alilobeba Dokta Gondwe mapigo yake ya moyo yakabadikika na kuanza kwenda mbio. Kitu alichokisubiri kwa mda mrefu, kitu kilichopelekea akamuua baba yake mzazi, kitu kilichosababisha afanye kazi kwa kumtumikia Dokta Gondwe leo hii kipo karibu yake yaani vimelea vya V-COBOS.

"Vipi Tino ushaandaa kila kitu?" Aliuliza Dokta Gondwe huku akivua miwani yake
" Kila kitu kipo kama ulivyoagiza mkuu" Tino alijibu kwa unyenyekevu huku wakati wote akitazama lile sanduku mikononi mwa Dokta Gondwe

"Sawa, hii boti mbona ndogo mtajificha wapi?" Aliuliza Dokta Gondwe
"Iko vizuri bosi, kuna sehemu za kujificha kama buti hivi pendeni na katikati tutaingia humo na hatuwezi kuonekana" alieleza Tino
"Ok vizuri, kama nilivyowaeleza kuna mtu muhimu nakwenda kufanya naye maongezi huko tunapokwenda nikiwapa ile ishara yetu ya kila siku basi mtatoka na kuingia ndani ya ile boti kama nisipofanya hivyo basi mtulie humo humo msitoke" Alieleza dokta Gondwe,
"Sawa mkuu"Tino pamoja na wale vijana wawili waliitika kwa pamoja.

Sasa zilikuwa zimesalia dakika 16 kufikia ule wakati waliokubaliana kukutana baharini, Dokta Gondwe akawa anasubiri atumiwe uelekeo 'location' mahali alipo mtu ambaye wanakwenda kubadilishana virusi vya COBOS na video yake ya ngono.

Wakati wakiendelea kusubiri kwa mbali hatua kama 50 hivi kulikuwa na mlima mmoja mdogo sana usio na miti mingi. Nyuma ya mti mmoja mkubwa alionekana jasusi Shadow akiwatazama Dokta Gondwe na vijana wake kupitia Darubini. Shadow alikuwa hapo tangu kitambo akifuatilia kila kinachoendelea. Hakutaka kufanya makosa tena kama alivyowahi kufanya miaka kadhaa iliyopita akiwa na Marehemu Jenerali Phillipo Kasebele, ilikuwa ni lazima ahakikishe siku ya leo anarudi na vimelea vya V-COBOS kisha kuvikabidhi kwa Sultana. Anakumbuka miaka kadhaa aliyopita aliwahi kuagizwa kazi kama hiyo na mume wa Sultana marehemu Jenerali Phillipo Kasebele hakufanikiwa kwa asilimia zote, alifanikiwa kuiba chupa ya kijivu yenye dawa dhidi ya vimelea vya V-COBOS lakini si vimelea vyenyewe, leo kwa mara nyingine tena anakwenda kuirudia kazi hiyo akiwa chini ya Sultana.


Upande wa pili Inspekta Aron alikuwa ndani ya gari yake pamoja na Annah binti ambaye ni shahidi pekee aliyesalia katika kesi ya mauaji inayomkabili Osward. Aron alitakiwa kumlinda Annah kwa udi na uvumba kuhakikisha anakuwa salama dhidi ya maadui ambao walikuwa wakimuwinda kila kona.
Sasa alikuwa akimuhamisha tena kwa siri kutoka hospitali ya kimataifa ya Mountenia akawa anampeleka sehemu ambayo ni yeye pekee alikuwa akijua ni wapi.
Walienda kwa muda mrefu kiasi cha kutoka nje kabisa ya mji na baadae wakafuata barabara moja ya vumbi iliyokuwa ikielekea msituni.

"Aron tunaelekea wapi mbona mbali hivi?" Annah aliuliza baada ya ukimya wa muda mrefu
"Annah ukiona hivi ujue ni wazi kuwa wewe ni mtu wa muhimu sana, si kwangu tu bali kwa watu kibao ambao wanauwawa bila hatia kila kukicha" alieleza Inspekta Aron
"Unanichanganya Aron, najua mimi ni shahidi pekee niliyebaki lakini huku tunakoenda ni wapi?"
"Ni sehemu salama usijali kuna nyumba na kila kitu utakachohitaji"
"Mmh! nyumba gani porini huku?"
"Umesahau mimi ni nani eeh! kuna nyumba ya siri huku aliijenga marehemu baba yangu, huku ndiko alikokuwa akifanya mambo mengi ya siri ya kulisaidia taifa letu baada ya kustaafu"
"Kwa hiyo wewe ulikujua vipi?"
"Aliwahi kunileta siku moja, ni sehemu ya siri mno ambayo hakuna mtu anaejua zaidi yangu na baadhi ya watu aliofanyanao kazi"
"Unataka kusema baba yako alikuamini sana"
"Sana tena sana, lakini shida alikuwa haniambii chochote kuhusu mipango yake, alidai wakati ukifika nitajua kila kitu nitaanzia pale alipoishia alinambia siku moja hatima ya hii nchi na dunia nzima itakuwa mikononi mwangu" alieleza Inspekta Aron hapo Annah akaangua kicheko tena akacheka kwa sauti sana

"Sasa mbona unacheka?"
"Hahaha umenifurahisha, hivi umejisikia ulivyoongea kweli unasemaje hatima ya Dunia iwe mikononi mwako hahah"
"Aah! usicheke, baba yangu namuamini sana kila alichokuwa akikisema kilitokea, japo alifariki ghafula lakini bado naishi kwa kuyaamini maneno yake najua ipo siku yatatimia"
"Mmh! haya bana pengine kweli, wanajeshi huwa wanamambo mengi, punguza mwendo basi spidi kali sana Aron"


Upande wa pili zikiwa zimesalia dakika 5, mara simu ya Dokta Gondwe ilitoa mlio fulani haraka akaifungua na kuangalia.
"Katuma location huyu bwana" alisema Dokta Gondwe huku akitabasamu
"Tunafanyaje bosi" aliuliza mmoja wa wale vijana
"Ingieni kwenye boti jificheni, sio mbali kutoka hapa, kama dakika 5 tutakuwa tumefika alipo huyu mwanaharamu" Alisema Dokta Gondwe maneno yaliyoonekana kuuchoma moyo wa Tino moja kwa moja.

"Yaani umelala na mke wangu alafu unatuita wanaharamu" Tino aliwaza wakati huo yeye na wenzake wakiingia kwenye ile boti na kujificha
Bila kupoteza muda Dokta Gondwe akiwa na lile sanduku lake alipanda kwenye boti kisha akaiwasha taratibu akaanza safari kusogea mbele akifuata uelekeo wa ramani aliyotumiwa kwenye simu yake.

Wakati huo huo Jasusi Shadow alionekana akiteremka kwa kasi kutoka kwenye ule mlima akiwa na begi kubwa mgongoni, akafika ufukweni. Haraka alifungua begi lake akatoa mtungi wa gesi vifaa vya kuogelea na vifaa vingine vingi.
Dakika moja baadae tayari Shadow alikuwa amevaa kila kitu, mtungi wa gesi uliounganishwa moja kwa moja kwenye pua na mdomo wake pamoja na miwani maalumu ya kuogelea, alifanana kabisa na wale wazamiaji wa mamjini. Alipiga hatua kuingia ndani ya maji na baadae akazama na kupotea kabisa juu ya uso wa bahari.
ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(vita ya kisasa)
Sehemu ya..............20
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

20-(Kuilinda au kuiteketeza Dunia)
ILIPOISHIA...
Inspekta Aron anaamua kumuhamisha Annah kutoka hospitali ya kimataifa ya Mountenia kwenda msituni katika nyumba ambayo yalikuwa ni makazi ya siri ya baba yake Jenerali Phillipo enzi za uhai wake. Upande wa pili Dokta Gondwe yuko kwenye boti tayari kwenda kufanya mapatano na mtu anayeamini anazo video na picha zake za ngono, wakati huo pia Jasusi Shadow anawafuatilia kwa siri.

Nini kitafuata?

SASA ENDELEA....
"Aah! usicheke, baba yangu namuamini sana kila alichokuwa akikisema kilitokea, japo alifariki ghafula lakini bado naishi kwa kuyaamini maneno yake najua ipo siku yatatimia" Inspekta Aron aliongea tena kwa msisitizo ilibidi Annah ajilazimishe kukubaliana na kauli hiyo japo haikumuingia akilini kabisa

"Eti hatima ya Dunia nzima iwe mikononi mwako mbona ajabu sana hii" aliwaza Annah, wakati huo Inspekta Aron alinyonga usukani akakata kona upande wa kushoto wa barabara ile ya vumbi akaenda kwa mwenda wa taratibu kisha akasimamisha gari yake katika kichaka kimoja kikubwa

"Shuka tumefika" Alisema Inspekta Aron
"Mmh!!" Annah aliguna hali akiangaza macho huku na huku kuangalia mazingira ya eneo hilo, ilikuwa ni katikati ya msitu mnene
Walishuka na kuliacha gari wakaanza kutembea kwa miguu Aron akiwa ndiye kiongozi. Baada ya mwendo kama wa dakika kumi hivi hatimaye mbele yao waliliona jengo moja lenye muonekana chakavu kwa nje lakini ndani kulikuwa na kila kitu cha kumuwezesha mtu kuishi huko hata mwaka mzima.

Asilimia kubwa ya nyumba hii ilijengwa kwa miti ya mbao, ilikuwa na muundo kama ghorofa moja hivi yaani juu na chini. Kabla ya kuingia ndani Aron alikagua mazingira ya nje kujiridhisha na usalama wa eneo hilo baadae akaingia ndani akafanya hivyo hivyo. Wakati akifanya ukaguzi huo Inspekta Aron aligundua kitu cha tofauti

"Kuna mtu anaishi hapa, atakuwa ni nani huyo?" Inspekta Aron alijiuliza wakati akiendelea kuchunguza mazingira ya nyumba hiyo mwisho alirudi sebureni akamkuta Annah amajilaza kwenye kochi

"Mara ya mwisho kuja hapa ilikuwa ni lini afande?" Aliuliza Annah
"Tangu mwaka jana"
"Kwa hiyo hakuna mwingine anaejua kuhusu uwepo wa hii nyumba zaidi yako"
"Ndiyo ni mimi tu" Aron alidanganya akiuficha ukweli kuwa kuna kila dalili zinazoonyesha kuna mtu huwa anakuja au anaishi ndani ya nyumba hiyo, swali likabaki kichwani mwake, ni nani?
"Kwa hiyo Aron tutaishi huku hadi siku ya mahakamani ifike si ndiyo? au utakuwa unaondoka na kuniacha mwenyewe?" Aliuliza Annah swali ambalo lilikuwa ni muhimu sana kwa Aron, awali aliamini mazingira hayo yangemuweka Annah salama zaidi dhidi ya watu wanaotaka kumuua, aliamini ataweza kwenda kazini akamuacha Annah lakini kwa bahati mbaya bado aliona nyumba hiyo haiko salama pia

"Mbona hujibu?" Annah aliuliza huku akimtazama Inspekta Aron usoni
"Ah..ee tutaishi huku wote, siwezi kukuacha mwenyewe unakumbuka nilikuahidi nitakuwa na wewe kila wakati kukulinda" Alisema Aron maneno yaliyopenya moja kwa moja kwenye moyo wa Annah akajikuta anatabasamu na kumtazama Inspekta Aron kwa macho maregevu, taratibu Annah akaanza kujikuta anampenda Inspekta Aron.

BAHARI YA HINDI...
Baada ya mwendo wa dakika tano ndani ya maji hatimaye Dokta Gondwe alifika akasimamisha boti yake pembeni ya boti nyingine kubwa iliyokuwa imetia nanga katikati ya bahari. Kwa mujibu wa ramani aliyotumiwa hapo ndipo alipokuwa mtu anaetegemea kukutana naye.

Akiwa na lile sanduku Dokta Gondwe alishuka, akakanyaga ngazi za ile boti kubwa akaanza kupiga hatua taratibu hadi alipoufikia mlango fulani uliokuwa wazi akaingia ndani. Chumba cha kwanza kilikuwa kitupu lakini mbele yake kulikuwa mlango mwingine tena ulio wazi pia Dokta Gondwe akasonga mbele na kuzidi kuingia ndani ya vyumba vya boti hiyo yenye muundo wa kisasa.
Huku nyuma ndani ya ile boti ndogo aliyokujanayo Dokta Gondwe aliwaacha Tino na vijana wake wengine wawili wakiwa wamejificha kusubiri maelezo ya bosi wao. Katika mikono yao ya kushoto wote walivaa saa ambayo ni maalumu kwa ajili ya kutoa mlio wa kengere ya hatari mara tu Dokta Gondwe atakapo bonyeza kitufe kwenye saa yake ambayo imeunganishawa kitaalamu na saa hizo walizovaa vijana wake.

Baada ya kuvuka vyumba kadhaa hatimae Dokta Gondwe alifika kwenye chumba cha mwisho ambacho kilikuwa na meza nyembamba na ndefu sana, upande mmoja wa meza hiyo alimuona mtu aliyepigilia suti nadhifu yenye rangi ya ugoro akiwa amesimama na kumpa mgongo huku mikono yake ikiwa mfukoni, huyu hakuwa mwingine bali Bosco kijana aliyeaminiwa na kusimama badala ya Tino.

"Karibu kiti" Alisema Bosco huku akigeuka taratibu akavuta kiti na kukaa upande moja wa meza ile ndefu. Akiwa na tahadhali kubwa Dokta Gondwe naye alivuta kiti kilichokuwa upande wa pili wa meza ile akakaa.

"Sikuwa nategema kama nitakutana na kijana mdogo kama wewe" Dokta Gondwe aliongea kwa kujiamini
"Sidhani kama tuna mda wa kutosha hadi kupata nafasi ya kuzungumzia mambo ya umri, tuna robo saa tu kila kitu kiwe kimekwisha" Bosco aliongea kwa kujiamini vile vile
"Sawa, nimekuletea virusi vya COBOS kama ulivyotaka hivi hapa" Dokta Gondwe aliongea na kuliweka lile sanduku juu ya meza, akatulia kwa muda kisha akaendelea kuongea

"Kabla sijakukabidhi vimelea hivi nataka kujua kwanza utavifanyia nini?"
"Sijapanga bado" alijibu Bosco
"Unamaana gani?"
"Maana yangu ni hii kuna mawili, pengine nikailinda Dunia au nikaiteketeza Dunia"
"Una maana gani kusema utailinda au kuiteketeza Dunia?"
"Kuilinda Dunia maana yake nitavisambaratisha hivo virusi vipotee kabisa visiwepo tena Duniani, na kuiteketeza Dunia maana yake nitasambaza hivi virusi Duniani kote na watu wataumwa na kufa kama ilivyokuwa kwa virusi vya Corona" Bosco aliendelea kuongea kwa kujiamini sana.
"Kwa nini ufanye hivyo, huoni kama utaua watu wengi wasio na hatia wakiwemo ndugu na jamaa zako tena ndani ya nchi yako mwenyewe"
"Hayo maswali mimi ndio natakiwa kukuuliza wewe na viongozi wenzako mliokubali kuviingiza vimelea hivi nchini, je unaweza kunijibu mlikuwa mnawaza nini?" Aliuliza Bosco huku akimtazama dokta Gondwe usoni ambaye alibaki kimya
"Hahah jibu ni jepesi tu Dokta Gondwe, mlijiamini kwa sababu mlijua dawa ipo mtakunywa na kupona lakini wengine watakufa, basi mimi sina tofauti na ninyi kwa kuwa ninayo dawa dhidi ya virusi vya COBOS basi nitafanya chochote nachotaka" Bosco aliongea kwa kujiamini sana yaani ilikuwa ni zaidi ya vile aliivyotaka Tino.
Kauli hiyo ilimfanya Dokta Gondwe ameze fundo kubwa la mate, kusikia kuwa mtu aliyepo mbele yake anayo dawa dhidi ya virusi vya COBOS, dawa iliyoibiwa miaka michache iliyopita ilikuwa ni habari nyingine mpya kwake.
Hii ilikuwa ni moja kati ya mbinu waliyopanga kuitumia Bosco na Tino ili kumteka kiakili mheshimiwa Waziri Dokta Gondwe lakini ukweli ulikuwa ni kwamba wanaojua dawa ya virusi vya COBOS ilipo ni jasusi Shadow na Sultana pekee na hii ndiyo sababu Tino alikuwa akipigania uhai wa mama yake Sultana kwa udi na uvumba kuhakikisha anapona.

"Nikikupa hivi vimelea vya V-COBOS vipi kuhusu usalama wa picha na video zangu chafu?"
"Nitazifuta"
"Utazifuta, hivyo tu? mimi nitaaminije kama umezifuta?"
"Nitakupa video orijino kutoka kwenye kamera iliyokurekodi, najua unaelewa hata kama nitabaki na kopi itakuwa haina nguvu sana kama video orijino"
"Hayo ni mambo ya wataalamu wa kompyuta TI mimi najulia wapi alafu kwanini...." Alisema Dokta Gondwe lakini kabla hajamalizia kauli yake mara walisikia sauti ya kioo cha dirisha kikipasuliwa kutoka chumba jirani ikifuatiwa na kishindo

Bosco na Dokta Gondwe walitazamana kwa macho ya kuulizana kila mmoja akionyesha kusikia sauti hiyo lakini haelewi kinachoendelea mbaya zaidi watu hao wawili walikuwa hawaaminiani kabisa kila mmoja alikuwa anawaza mwenzake anaweza kumsaliti mda wowote.

Baada ya kutazamana kwa muda ghafula kila mmoja akachukua bastola yake na kumnyoshea mwenzake, ilikuwa ni kitendo cha haraka haraka kila mmoja akawa amemuwahi mwenzake kwa kumnyoshea bastola. Bosco aliitoa bastola yake chini ya meza usawa wa eneo alipokuwa amekaa, wakati Dokta Gondwe aliitoka kwenye mfuko wa juu wa koti lake

Sasa kila mmoja akawa anatazamana na mdomo wa bastola ya mwenzake

"Unataka kufanya nini mheshimiwa Waziri?" Aliuliza Bosco
"Nikuulize wewe unampango gani wa siri?"
"Sina mpango wowote"
"Hiyo sauti imetoka wapi na ni ya nani, uliniambia tutakuwa wawili tu?"
"Nikulize wewe umekuja na nani?"
"Niko mwenyewe, hii sauti imetoka ndani humu humu acha kujitoa ufahamu unaelewa kinachoendelea kijana" Dokta Gondwe aliongea huku akiishikilia bastola yake saawia.
Wakati huo si Bosco si Dokta Gondwe hakuna aliyekuwa akimuamini mwenzake hawakujua kuwa mzee wa kazi Jasusi Shadow alikuwa ameingia ndani ya boti hiyo naye akiwa anavitaka vimelea vya V-COBOS kama alivyoagizwa na Sultana. Tino na wale vijana wawili walienda kusubiri ndani ya ile boti ndogo, hawakujua chochote kinachoendelea..
Je, nani ataibuka mshindi kuondoka na sanduku?
Ni nani ambaye anaishi kwenye ile nyumba msituni walipo Annah na inspekta Aron kwa sasa?.
Vipi kuhusu Annah kuanza kumpenda Inspekta Aron?
Vipi kuhusu Najma?

ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya............21
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

21-(VITA BAHARINI)
ILIPOISHIA.....
Wakati huo si Bosco si Dokta Gondwe hakuna aliyekuwa akimuamini mwenzake hawakujua kuwa mzee wa kazi Jasusi Shadow alikuwa ameingia ndani ya boti hiyo naye akiwa anavitaka vimelea vya V-COBOS kama alivyoagizwa na Sultana. Tino na wale vijana wawili walienda kusubiri ndani ya ile boti ndogo, hawakujua chochote kinachoendelea..


SASA ENDELEA....
Bosco na Dokta Gondwe kila mmoja akiwa amemnyoshea mwenzake bastola mara walishtushwa na mtikisiko mkubwa ndani ya boti hiyo mtikisiko uliosababisha wote wawili kuanguka chini kwa pamoja. Boti iliyumba ikiwapeleka kulia na kisha kuwatupa upande wa kushoto. Walishindwa kustahimili kuendelea kushikilia siraha zao zikadondoka chini, kila mmoja akawa anajitahidi kujishikilia mahali ili asiumie kutokana na kuyumba yumba kwa boti ile wasielewe ni nini chanzo. Mara ghafula hali ikatulia kwa sekunde kadhaa kisha wakashangaa kuona boti inaanza kwenda mbele kwa kasi sana.
Mambo yakazidi kuwa mazito kwa upande wa Bosco na Dokta Gondwe kila mmoja akimuhisi mwenzake kuwa ndiye aliyekuwa kihusika na kila kinachoendelea wakati huo hawakujua kabisa habari za kuwepo kwa Jasusi Shadow ndani ya boti hiyo.
Hapo ndipo Dokta Gondwe alipokumbuka kubonyeza saa yake kuwashtua Tino na wenzake ambao walikuwa bado wamejificha kwenye ile boti ndogo wasielewe kinachoendelea.

Bosco na Dokta Gondwe walisimama tena wakawa wanatazamana, Bado kulikuwa na mtikisiko kiasi huku boti hiyo ikizidi kukata mawimbi kuelekea kusikojulikana. Hakuna aliyejua ni wapi siraha yake imedondokea. Katikati yao kulikuwa na lile sanduku lenye vimelea vya V-COBOS, wote walitupa macho mbele wakaliona sanduku lile likiwa limedondoka chini, mtihani ukawa ni nani kati yao ataliwahi.

Bosco alikimbia kulifuata sanduku Dokta Gondwe naye akakimbia kumuwahi kabla hajalifikia akamvaa na kwenda naye chini wakaanguka kama magunia, sasa ikawa ni mwendo wa piga nikupige vita kali ikaibuka kati ya Bosco na Dokta Gondwe.
Wakati hali hiyo ikiendelea mara ghafula kuna moshi mweupe ulitanda ndani ya kile chumba, kwa mbali Jasusi Shadow alionekana anaingia kwa kasi akafika na kulichukua lile sanduku lenye vimelea vya V-COBOS kisha akatoka. Badala ya kushirikiana kumzuia Dokta Gondwe na Bosco waliendelea kupigana huku kila mmoja akiwa amemjeruhi mwenzake vibaya.
Dokta Gondwe alikuwa akivuja damu puani wakati Bosco alikuwa akivuja damu mdomoni. Waliendelea kupigana kwa kuviziana kutokana na moshi mwingi uliotanda ndani ya chumba hicho.


Baada ya kengere ya hatari kulia katika saa ya Tino na wenzake, haraka walitoka kwenye maficho yao huku Tino akiwa ndio wa kwanza.

Wote walioshuhudia ile boti kubwa ikiondoka kwa kasi kuelekea upande wa mashariki

"Shiiit!! Nini kinaendelea?" Tino aliuliza kwa kustaajabu huku akiiwasha boti haraka, akashika usukani na kukata kona akaanza kuifukuzia ile boti yake kubwa.

Kuondoka kwa boti hiyo lilikuwa ni tukio ambalo lilimshangaza sana Tino, haikuwa kwenye mpango wake kabisa, alishindwa kuelewa ni nani hasa kafanya hivyo, je ni Bosco au Dokta Gondwe?
Aliendesha boti kwa kasi kujitahidi kuifikia ile boti kubwa ambayo nayo ilikuwa kwenye mwendo wa kasi ikikata mawimbi haswa.
Spidi aliyokuwanayo Tino ilifawafanya wenzake waanze kuogoapa kwani kuna wakati boti ilikuwa ikiruka juu mita kadhaa kutoka usawa wa maji na baadae kurudi chini kishakuendelea kukata mawimbi. Ilibidi wajishikilie kwa nguvu kwenye pembe za boti hiyo.
Akiwa amebakiza umbali wa mita chache kuifikia ile boti kubwa, mara mshare wa mafuta ulianza kuyumba yumba hii ilikuwa ni ishara tosha kuwa mafuta yalikuwa yanakaribia kuisha.
Tino alipiga hesabu za haraka haraka afanye nini kwani kulikuwa na kila dalili kuwa mafuta yataisha hata kabla hajaifikia ile boti kubwa.

"Shika endesha" Tino alimwambia mmoja kati ya vijana aliokuwanao
Bila kupinga yule kijana alipishana na Tino akashika usukani.
Tino alirudi nyuma akafungua sehemu fulani ndani ya ile boti akatoa begi moja kubwa lililokuwa limejaa vifaa vya kuogerea ikiwemo pia mtungi mdogo wa gesi unaoweza kumsaidia mtu kupumua kwa dakika kadhaa akiwa ndani ya maji.
Tino alivaa vile vifaa haraka haraka, wakati anamaliza tu kuvaa tayari boti iliisha mafuta ikazima na kusimama. Tino hakutaka kujiuliza mara mbili mbili haraka alijitosa majini na kuzama alipokuja kuibuka alikuwa karibu kabisa kuifikia ile boti kubwa, akazama tena na kuogerea kwa kutumia vile vifaa alivyovaa ambavyo vilimuwezasha kwenda kwa kasi akiwa ndani ya maji alipokuja kuibuka tena kwa mara ya pili tayari alishaifikia ile boti akapanda na kuanza kusogea taratibu akipandisha ngazi.
Wale vijana wawili walibaki kwenye ile boti ndogo wakielea elea juu ya maji, hawakujua wafanye nini kwani waliachwa umbali mrefu sana. Walichofanya walichukua miko na kuanza kupiga makasia kurudi nchi kavu.

Tino alipokanyaga ngazi ya mwisho kuingia kwenye boti mara mlango uliokuwa mbele yake ulifunguliwa. Kuna mtu alikuwa akitoka kwa kasi ambaye naye alisimama ghafula mara baada ya kukutana uso kwa uso na Tino, mtu huyu alikuwa ni jasusi Shadow.

Wote wawili walikuwa wamevaa vifaa vya kufanana, isipokuwa mtungi wa gesi wa Jasusi Shadow ulikuwa ni mkubwa kuliko wa Tino lakini kila kitu walifanana.

Shadow aliweza kugundua kuwa aliyepo mbele yake ni Tino mtoto wa kwanza wa bosi Sultana lakini Tino hakuwa akimjua mtu aliyesimama mbele yake licha ya hivyo hakuweza pia kuiona sura ya mtu huyo kutokana na ile maski ya kupitisha gesi aliyovaa usoni.
Tino alimtazama Shadow kuanzia juu hadi chini na hapo ndipo akaliona lile sanduku ambalo awali alimuona nalo Dokta Gondwe. Hapo ndipo Tino akagundua kuwa mtu huyo alikuwa na lengo la kuondoka na vimelea vya V-COBOS, lilikuwa ni jambo ambalo katu asingekubali kuona linatokea mbele ya macho yake, hakuwa tayari kumruhusu aondoke na sanduku lile. Lakini Tino hakujua mtu aliyesimama mbele yake ni nani na anauwezo kiasi gani.


Upande wa pili mtoto wa kishua Najma ama kwa lugha ya kisasa tungemwita Pisi kali toto la mheshimiwa Waziri wa afya Dokta Gondwe alionekana ndani ya gari akiwa katikati ya barabara kuelekea gereza alilohifadhiwa mumewe mtarajiwa Osward.
Bado akili ya Najma haikuwa sawa kabisa, alikuwa akiwaza kuhusu majibu aliyoyapata mtandaoni baada ya kutafuta maana ya vimelea vya COBOS ambavyo alimsikia baba yake akivitaja mara nyingi wakati akiongea na simu kwa siri.
Haya ndiyo majibu ambayo Najma aliyapata mtandaoni
,,,,,,,,,,,,,COBOS virus is a virus that was secretly invented by humans 25 years ago in Mexico. This secret was leaked and the practice was strongly opposed by all countries in the world and later banned by any country or laboratory involved in the manufacture of the virus. That was the last COBOS virus to be heard, there are rumors that the virus was taken and stored by the ZMLST international laboratory in Mexico. For over 25 years now the virus has never been heard anywhere in the world.,,,,,,

(virusi vya COBOS ni virusi vilivyotengenezwa na binadamu kwa siri miaka 25 iliyopita nchini mexico. siri hii ilivuja na kitendo hicho kikapingwa vikali na nchi zote ulimwenguni baadae ikapigwa marufuku kwa nchi au maabara yoyote ulimwenguni itakayojihusisha na utengenezwaji wa virusi. Huo ndio ukawa mwisho wa virusi vya COBOS kusikia, kuna tetesi kuwa virusi hivi vilichukuliwa na kujifadhiwa na maabara ya kimataifa ya ZMLST iliyopo Mexico. Ni zaidi ya miaka 25 sasa virusi hivi havijawahi kusikika mahali popote Dunia)

Haya ni majibu ambayo yalimfanya Najma kuendelea kufuatilia ukweli wa jambo hili. Kitu kikubwa kilichomfanya Najma kuzidi kumtilia mashaka baba yake ni zile safari ambazo baba yake alikuwa akizifanya mara kwa mara kwenda nchini Mexico, hata pale alipokuwa akikosa nafasi alikuwa akimuagiza kwa siri mkwe wake mtarajiwa Osward ambaye kwa sasa yupo gerezani akisubiri hukumu ya kesi ya mauaji inayomuandama.

"Hii inawezanaje? Baba yangu anawezaje kushiriki kwenye mambo kama haya? alafu kwa nini hawa wamexico wamchague yeye, hapana hakuna ukweli wowote hapa" Najma alikuwa akijiuliza na kujijibu mwenyewe, haikuwa rahisi kukubaliana na jambo hilo.

Najma alifika karibu na lile gereza alilopo Osward, gereza ambalo ni jana tu ametoka anaumia vibaya akasaidiwa na inspekta Aron.
Najma alifika gerezani hapo kwa lengo la kuongea na Osward akitaka kumuliza juu ya safari lizokuwa akienda Mexico badala ya baba yake, alikuwa akienda kufanya nini.
Najma aliyafanya yote hayo kimya kimya bila kumueleza Inspekta Aron chochote licha ya kwamba walikuwa na ukaribu mkubwa kwa sana na alikuwa akimkumbuka sana lakini hakumpigia wala kutuma ujumbe wa maandishi.


Upande mwingine msituni, Inspekta Aron na Annah walianza kuzoea mazingira huku Annah kimtazama Inspekta Aron kwa jicho la tofauti, tayari mwanaume huyo alianza kuuteka moyo wake taratibu.
Wakati wote jicho la Inspekta Aron lilikuwa makini kutazama kama kuna mtu atakuja kwenye nyumba hiyo ya siri iliyojengwa na marehemu baba yake, hakuwa amemwabia Annah chochote kuhusu hisia zake zilizomwambia kuwa ni lazima kuna mtu atakuja.

Upande wa pili mambo yalizidi kupamba moto, vita kali ilianza kati ya Tino ambaye hakutaka kumruhusu jasusi Shadow andoke na vimelea vya V-COBOS. Shadow naye hakutaka kukubali kushindwa kwa mara nyingine tena ilikuwa ni lazima ahakikishe anaondoka na sanduku hilo. Vita hiyo ilikuwa nje ya boti lakini ndani nako kulikuwa na vita kali kati ya Dokta Gondwe na Bosco kijana wa Tino. Dokta Gondwe hakutaka kumruhusu Bosco aende kwani aliamini huyu ndiye mwenye picha na video zake chafu za ngono lakini pili ni baada ya Bosco kusema kuwa anayo dawa(chupa ya kijivu) dhidi ya virusi vya V-COBOS.

Wakati haya yote yakiendela boti ilizidi kwenda kwa kasi ikikata mawimbi kuelekea kusiko julikana.

Je, nini kitafuata?

ITAENDELEA....
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom