Simulizi: The Oath

Janie_Kelvin

Member
Jun 5, 2022
33
51
Sehemu ya kwanza
Katikati ya msitu mnene, giza zito likiwa limetanda kila kona ya msitu huo alionekana kijana akikimbia huku jasho likimtoka ni dhahiri alikuwa amekimbia kwa muda mrefu sana na alikuwa na hofu iliyopitiliza huku nyuma sauti tofauti tofauti zikimfuata kadri alivyokuwa akizidi kukimbia ili kujiokoa na jambo hilo.

“Harry! Harry! Haaaarry! Hahahahahahah” Sauti hiyo ilizidi kumsogelea huku vicheko tofauti vikichukua nafasi ya kumuogopesha zaidi na zaidi.

“Harry!! Harry! Harry!. Hapo alisimama kisha akafumba macho yake kisha akageuka nyuma taratibu na kuyafumbua macho yake tena.

“Ni ndoto mbaya? Harry!”

Harry alipofumbua macho alimuona mama yake ameketi pembeni yake huku akimtizama kwa umakini.

“Mama!”

“Nimekuita muda mrefu Harry inaonekana ulikuwa ukiota tena ndoto mbaya ona jasho linakutoka”

“Ni kweli mama it’s bad dream” Alimsimulia mama yake jinsi alivyoota ndoto hiyo mbaya huku bado akionesha hofu sana usoni.

“Pole! Muombe Mungu akuondolee ndoto mbaya mwanangu Sawaa?”

“Sawa mama”

“Sasa leo nafasi ipo ya kutosha kesho kanisani na unajua kabisa wiki ijayo it’s your 20th birthday so twende leo tukafanye shopping ya mahitaji yote nataka siku yako iwe ya kipekee sana”

“But mama……”

Kabla hajamaliza kuongea tayari alishamziba mdomo ili asiendelee kuongea.

“Najua Harry lakini look kwa miaka karibia mitano your daddy hakuwahi kusherehekea kuzaliwa kwako huoni hii ni nafasi nzuri kufurahi tukiwa pamoja na baba yako?”

“Nakuelewa unachomaanisha mama kwakuwa umependekeza hivyo I have to accept that”

“Yes! Good boy that’s why I love you, haya inuka kajiandae then twende”

“Okay mom”

Aliinuka na kuelekea bafuni ili ajiandae na hapo mama yake alimuacha ajiandae na yeye alishuka chini kuendelea na kazi nyingne alifanya kila kitu yeye mwenyewe hakuhitaji mdada wa kazi kumsaidia kwani kazi zake hazikumfanya kuwa bize kiasi cha kushindwa kufanya shughuli za nyumbani kama mama.

Maisha yao yalikuwa ya kifahari sana kutokana na kuwa na pesa, pesa kwao haikuwa tatizo kabisa waliweza kusafiri kwenda nchi yoyote waliyotaka.

Mr Maurice Hilary na Bi Hannah Mollel ndio wazazi halisi wa kijana Harry, mtoto wa kwanza na wa pekee kwenye familia hiyo, walimiliki kampuni za madini na mafuta pamoja na miradi midogo midogo mbalimbali nyumba za kifahari.

Miaka takribani kumi walikuwa nje ya nchi walizunguka nchi tofauti tofauti karibia saba tokea Harry ana miaka mitano hali hiyo iliwafanya kuwa na uzungu fulani kwenye maisha yao hivyo kwa upande mwingine waliishi kama wazungu.

Baada ya kurudi nchini ilipita miaka mitatu Harry alipendekeza apate chuo hapa Tanzania asome japo wazazi wake hawakupenda asome ndani ya nchi ila kwa sababu alikuwa mtoto wao wa pekee waliheshimu ombi lake kwa muda huo ndipo alipoanza masomo yake ya chuo kikuu akiwa kijana mdogo kabisa kutokana na kuwa kijana mwenye akili nyingi ya kuchanganua vitu tofauti.

Sasa zilikuwa zimebaki siku chache kuifikia siku ya kuzaliwa kwa kijana Harry alitarajia kutimiza miaka ishirini tokea kuzaliwa kwake, na walipanga kufanya tafrija ili kumpongeza mtoto wao wa pekee.

“Hubby! Bado unafikiria kuhusu ndoto uliyoota? Kwanini hutaki kuniambia nini umeota? Ila hata Harry ameota ndoto mbaya sana” Aliongea Bi Hannah akimwambia mume wake.

“No mke wangu sio ndoto mbaya hata hivyo siwazi kuhusu ndoto, nafikiria nimepata safari ya ghafla ya kikazi”

“Mmh lini?” Aliuliza kwa kuhamaki

“This time Hannah! But I want to spend much more time with my family, si unajua next week ni birthday ya Harry sitaki kumdisappoint”

“So what is your plan?”

“I want to send the representatives”

“But are you comfortable?”

“Yes love I’m very okay, na nina furaha sana kwasababu tutakuwa pamoja kwenye Harry’s 20th birthday”

Bi Hannah aliishia tu kutoa tabasamu na kuendelea kuandaa kifungua kinywa kisha waondoke.

“Am…. Nilisahau tutatumia ile BMW honey!”

“It’s okay hamna shida hata mkichukua yote mimi nitakodi taxi” Aliongea kiutani Mr Hilary na kumfanya mke wake acheke.

“Kitakuwa kituko cha siku hahahah magari matano yote tutajigawaje?”

“Hahahah……..Nahitaji kwenda kuweka mambo Sawa ili tuweze kuwa pamoja wiki ijayo”

“Sawaa hamna shida”

Muda huo ndio Harry alikuwa akishuka kutoka juu ili ajumuike na wazazi wake kupata kifungua kinywa, hakuwa sawa kama siku zote kutokana na mawazo aliyokuwa nayo juu ya ndoto aliyoota.

“Daddy!!! Good morning”

“Good morning my boy are you okay?”

“Yes Daddy I’m okay”

“Usiwaze sana kijana wangu hiyo ni ndoto tu japo sio nzuri just pray hard” Aliongea huku akimpiga Piga begani.

Wakati wakiendelea kupata kifungua kinywa simu ya Mr Maurice iliita naye alisita kidogo kuipokea baada ya kuona mke wake amehamishia umakini wote kwake.

“Excuse me!! Sitaki kuwakosesha breakfast” Aliinuka na kwenda pembeni kidogo ili aongee na simu.

“Eeh!! Ha..hallo!..”

“Najua! Najua lakini sio kwa vishindo hivyo jamani ingekuwa vyema kama tukienda taratibu Eeh mambo gani haya jamani”

“Sa..sawaaa Hamna shida nimeelewa vizuri kiongozi, Sawaa” Alisikika Mr Maurice akiongea na haikujulikana anaongea na nani kwenye hiyo simu.

Alivyomaliza aligeuka ili arejee mezani macho yake yalikutana na mke wake ambaye alikuwa amekishika kiuno chake.

“Hubby ni nani huyo mbona ni kama una wasiwasi sana?”

“Usijali mke wangu ni mambo tu ya kazi na unakumbuka nilikuambia ilihitajika nisafiri? Nilikuwa najaribu kuweka mambo Sawaa”

“Really?”

“Yes! Wife twende tukaendelee na chai unajua mtoto atajisikia vibaya” Alimshika mkono mke wake na kurudi tena mezani lakini hawakumkuta kabisa Harry, waliishia kuangalia na tu , wakati wakijiuliza Harry yuko wapi walimuona akishuka kutoka juu akiwa tayari kwa safari.

“Mom mimi niko tayari”

“Chai mwanangu…”

“Nimeshiba mama”

Mr Maurice alimgeukia mke wake na kumwangalia kama kumpa ishara fulani naye akaitikia kisha akapandisha juu kwenda kuchukua funguo pamoja na vitu vyake muhimu vidogovidogo vya muhimu kwaajili ya kuondoka navyo.

“Son!! Najua unawaza kuhusu ndoto ni Sawa ila usiwaze sana keep praying hard, usiruhusu ikutawale sana”

“Daddy I understand the situation, naelewa vizuri sio kama nawaza sana kuhusu ndoto ila siko tu poa kwa leo worry out King”

“It’s okay, we nenda na mama nilitamani sana tungeenda wote ila nina majukumu”

“Usijali baba”

Bi Hannah alikuwa akishuka kutoka juu taratibu huku akiwaangalia baba na mwana wakiwa wanaongea.

“Hubby ungependa kuongozana nasi?”

“Nilitamani iwe hivyo ila nina majukumu mke wangu, mkaniwakilishe tu usisahau kuninunulia ile suti niipendayo”

“Hahah…. Umekumbuka hiko tu yaani sawa, Son let’s go”

Harry alimfuata mama yake na wote wakaondoka muda huo, Mr Maurice aliichukua simu na kupiga namba aliyoijua yeye na punde tu ilipokelewa na aliinekana akiongea kwa hasira sana kisha akakata simu na kuondoka, alitoka ndani na kuingia kwenye gari kisha akapiga moto na kutokomea.

Bi Hannah na Harry licha ya kuwa mwendoni kwa dakika karibia ishirini lakini hakuna aliyetoa neno lolote kulikuwa na ukimya wa ajabu ndipo Bi Hannah alipoamua kuuvunja ukimya.

“Harry! What’s up Son mbona kinyonge?”

“That house…… that house sometimes is full of drama, nashindwa kuelewa nini shida”

“Harry!…”

“Please Mom just… just stay calm”
Bi Hannah aliishia tu kumtizama mwanaye bila kutoa neno na alielewa kitu ambacho Harry alimaanisha.

ITAENDELEA….
 
THE OATH

Sehemu ya pili

Katika maeneo ya Ubungo maji nyumba ya kawaida tu ambayo ilionekana ya kupangisha, ndani ya chumba kimoja ambacho muziki ulikuwa ukipiga kwa sauti ya juu kidogo.

“Roby! Inatosha nimechoka nataka nipumzike kwanza jamani”

“Subiri kidogo bhana namalizia tu sasa hivi”

“Ni muda sasa bwana mi nimechoka mwenzio”

“Fai subiri kidogo bhana”

Yalikuwa ni mabishano kati ya Robert au unaweza kumuita Roby na Faith ndani ya chumba hiko maana mtanange ulikuwa mzito kwa Faith, karibia masaa mawili walikuwa kitandani wakilicheza segere huku redio ikiwaburudisha na kuzuia sauti sizitoke mpaka nje.

Wakati Robert akizidi kumchezesha Faith gwaride simu yake ilianza kuita hapo alimuachia Faith baada ya kuona mtu aliyempigia kuwa wa muhimu.
“Oy Eddy! Niambie mwana”

“Oya ww mpuuzi uko wapi mbona adimu leo?”

“Nipo ghetto mwana kidogo”

“Shit!!! F**k you Roby nilijua tu hivi wewe una pepo gani? Umesahau leo tulikuwa na miadi gani”

“Oooh! Shit! Vipi Harry umeongea naye?”

“Ndio Sio muda mrefu nimeongea naye na yupo njiani anaelekea chuo.

“Nipe dakika sifuri tu nakujaaa” Alimgeukia Faith

“Babe vipi kuna nini?” Aliuliza Faith ambaye alikuwa ameketi kitandani bila nguo yoyote.

“Fai sitaweza kukaa na wewe leo sijui nitakukuta baadae natoka kidogo”

“Mbona ghafla jamani hauli?”

“Nitakula baadae mpenzi..Utachukua hela pale pika chochote unachokitaka au ukiona shida nunua hata chips ule usikae njaa mama”

“Sawaa nitapika”

Robert alivaa haraka na kutoka akimuacha Faith akihuzunika na kuhisi ahueni kwa wakati mmoja maana gwaride lilimtoa jasho kweli kweli.Hiyo ndio ilikuwa Roho ya kijana Robert au Roby akitoka mama yake na dada yake basi anayefuata ni mrembo Faith, Mungu hakumnyima kila kitu mrembo huyu alimtunuku sura nzuri ya kuvutia kila mwanaume rijali na umbo sio haba alibarikiwa kwa kiasi chake.

Baada ya Robert kuondoka Faith aliishia kuguna tu, akainuka na kuvaa kiblauzi chake pamoja na khanga kisha alitoka na kuufunga mlango safari ya sokoni ilianza.

******

Nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, Kibaha Maili moja katika eneo ambalo lilikuwa limejaa takataka za kila aina alionekana kichaa akizunguka zunguka ili ajitafutie chochote kitu ili apate kula na hayo ndio yalikuwa maisha yake ya kila siku kichaa huyu na hilo ndilo lilikuwa chimbo lake ambalo alikuwa akijipatia chakula chake muda wote aliohisi njaa.

Nita kadhaa kutoka pale alipo yule kichaa alionekana mwanaume mmoja akimwangalia kwa masikitiko makubwa sana, ilionekana alikuwa akimfahamu kichaa yule kindaki ndaki.

Wakati akiendelea kumuangalia kwa mbali alimuona kijana wa miaka karibia kumi na mitano alikuwa alimsogelea yule kichaa huku akiwa ameshika kitu mkononi na kumpatia yule kichaa.

“Yule kijana ni nani? Leo sio mara ya kwanza kumuona akiwa na Nana.Nakusikitikia sana Nana ila sio kosa lako najilaumu nimeshindwa kukusaidia mpaka yamekufika mazito kiasi hiki” Alibana pembeni ili aone yule mtoto alichokuwa akitaka kukifanya.

Jina lake aliitwa Nasphaty au jina alilozoeleka aliitwa Nana historia kamili haijajulikana na nini ambacho kilipelekea kuwa katika hali aliyonayo sasa ila ni muda alikuwa kwenye hali kama hiyo ni miaka kumi na mitano sasa na wengi walimfahamu kama kichaa licha ya kutokujua sababu iliyompelekea kuwa kichaa lakini hakuna aliyemjali.

Yule kijana alimpatia kichaa mkate pamoja na juisi na yule kichaa hakuwa na hiyana alipokea na kuanza kula kwa fujo ilionekana alikuwa na njaa sana, alipomaliza kula alimuaga na kuondoka eneo hilo na ndipo mbele alipokutana na mwanaume ambaye alikuwa akiwaangalia muda wote.

“Kijana….”

“Shikamoo”

“Marahaba!!! Naitwa Jamal vip wewe unaitwa nani?”

“Naitwa Enrico”

“Unajua leo sio mara ya kwanza kukuona na huyo mwanamke hapo Vipi una uhusiano gani na yeye? Ni ajabu kakukubali maana hakuna ambaye ana ujasiri hata wa kumsogelea ni mkali sana”

“Sina uhusiano wowote na yeye ni mwanamke niliyemzoea tu na kumuona kama mama yangu ni vile tu sikuwahi kulelewa na mama na ni kama historia yake na mama yangu zinafanana ila mama yangu alishafariki muda mrefu sana tokea nikiwa mdogo sijielewi”

“Pole sana Enrico, mimi huyu ni rafiki yangu mkubwa sana tokea muda mrefu yawezekana kabla hata wewe hujazaliwa na yupo hivi muda mrefu na sijui kipi kimepelekea akawa hivi lakini maisha yake ya nyuma nayafahamu sana”

“Anaitwa nani?”

“Anaitwa Nasphaty au Nana, nisikucheleweshe naona unatoka shuleni wahi nyumbani”

Waliaganana kila mmoja alishika njia yake lakini njia nzima kijana ambaye kwa sasa tulimjua kama Enrico alikuwa na mawazo njia nzima kuhusu yule kichaa alitamani sana aijue historia yake akawaza kupitia yule mwanaume aliyeitwa Jamal anaweza akaijua historia yake.

Mawazo yake yalimrudisha nyuma siku ambayo alikuwa akitoka shule kama kawaida yake, alikuwa akisoma shule ya sekondari Maili moja kidato cha pili.

Alikuwa mwenye mawazo sana sio kawaida kutokana na hali ya nyumbani kwao manyanyaso aliyokuwa akipitia kila siku kutoka kwa bibi yake na mama yake wa kambo ni mazito kwa mtoto kama huyo.

Hakuwa hata na hamu ya kurudi nyumbani hivyo aliamua kijibanza kwenye nyumba chakavu ambayo Ilikuwa haijamalizwa kujenga kwa muda mrefu hapakuwa mbali na lilipo lile eneo la takataka huku akilia kwa huzuni sana ndipo alipo kuja yule mwanamke kichaa aliyeitwa Nasphaty na kumkuta akilia kichaa Nasphaty alichukua kitambaa chake kikuu kuu na kumfuta Enrico machozi kama kumbembeleza asiendelee kulia, ilikuwa inaogofya lakini Enrico hakuogopa kwenye maisha yake ni bora akutane na huyo kichaa kuliko kukutana na bibi na mama yake wa kambo.Kwa kiasi fulani Enrico alijisikia faraja sana akauchukua begi lake la shule na kutoa vipande vya keki na juisi akampatia kichaa Nasphaty ili ale naye alivipokea na kuanza kuvila kwa fujo kama kawaida.

Zilipita siku kadhaa na Enrico alikuwa na kawaida ya kupita kumsalimia kichaa Nasphaty na kumpa chakula alikuwa akijibana shule ili tu hela ibaki amnunulie kichaa Nasphaty ale chochote alikuwa anamhurumia sana anavyotafuta mabaki ya vyakula pale jaani hata kama ni kichaa alistahili kula chakula kizuri hata hivyo alikuwa na moyo mzuri sana.

Kama kawaida ya Enrico siku nyingine tena alipita kumsalimia kichaa Nasphaty, Waliketi kwenye moja ya chumba katika ile nyumba chakavu na kichaa Nasphaty akila chakula chake alichopewa na Enrico.

“Najua hauwezi kunielewa lakini unanisikia” Aliongea Enrico kisha akameza mate kidogo na kuendelea

“Umekuwa sehemu ya maisha yangu, nakuona kama mama yangu wewe pekee ulionesha kunijali nilipokuwa na huzuni ulinifuta machozi”

“Sijawahi kulelewa na mama tokea nizaliwe na niliambiwa alipata ukichaa baada ya mimi kuzaliwa na akatoroka nyumbani huko aliishia kufa baada ya kugongwa na gari ni huzuni sana, tokea nilipozaliwa nimelelewa na baba, bibi na mama yangu wa kambo napitia magumu sana” Aliongea hivyo huku machozi yakimtoka naye kichaa Nasphaty alipoona Enrico analia aliacha kula na kumfuta machozi na kumbembeleza.

“Baba yangu anaitwa Buchard……….” Wakati akiendelea kuongea kichaa Nasphaty alishindwa kuendelea kula ilikuwa ni kama vile amepaliwa na kuanza kulia hapo hapo.

“Pole usilie, mama usilie” Alimbembeleza mpaka pale kichaa Nasphaty alipoacha kulia.

Alianza kuongea vitu tofauti na hivyo huku akicheka naye kichaa Nasphaty alipomuona Enrico akicheka na yeye alikuwa akicheka, ukiwaona unaweza kusema wote ni vichaa Enrico alijiona mwenye amani sana akiwa na kichaa huyo.

Hayo ndio aliyakumbuka Enrico mpaka ikatokea kumzoea huyo kichaa na sasa alikuwa ameshalifikia geti la nyumbani kwao, alipo lifungua alipigwa na butwaa kwa alichokiona hapo mabegi yake yote yalikuwa yapo nje alipoangaza vizuri ndipo alipomuona shangazi yake ambaye alizaliwa pamoja na baba yake.

Alifurahi sana aliposikia kuwa anaondoka na shangazi yake japo hakuishi mbali sana ni kama unapita mitaa miwili tu, kiumri hakuwa mkubwa sana ni kama miaka ishirini na saba tu na kipindi hiko alikuwa mjamzito hakuwa na mtu wa kumsaidia na kukaa naye maana mume wake alikuwa ni mtu wa kusafiri safiri kwa sababu ya kazi zake hivyo aliona Enrico atamfaa japo muda mwingi atakuwa yupo shuleni.

Hiyo haikuwa sababu kubwa kwake ila alitaka kumtoa Enrico kwenye manyanyaso ya mama yake wa kambo na mama yao ambaye ni bibi yake na pia apate muda zaidi wa kusoma kwa sababu kidato cha pili ni kidato cha mitihani hivyo alihitaji muda mwingi wa kujisomea na kupumzika, na yote hayo alifanya kwa sababu alimpenda Enrico vile vile alimpenda sana mama yake Enrico na pia ni ahadi aliyomuahidi mama yake Enrico nafasi hiyo aliitaka kwa muda mrefu sana ila aliikosa na leo ameipata ni lazima amtoe hapo maana kaka yake kuna muda ni kama vile hajali kuhusu mtoto huyo alijali zaidi watoto wa mke wake tu.

Shangazi mtu alimchukua Enrico mpaka kwake na alijisikia faraja sana kwani alitimiza ahadi yake kwa mama yake Enrico.

“Mtoto yuko wapi!! Nakuuliza wewe! Mmemchukua mdoli wangu mzuri mmepeleka wapi? Nitunzie mdoli wangu nakupa wewe hiyo kazi ukae na mtoto wangu” Hayo ni maneno ya mama yake Enrico alipokutana na shangazi mtu japo alikuwa kichaa lakini aliona alikuwa alimaanisha kitu, shangazi mtu aliyakumbuka vizuri maneno ya mama yake Enrico.

“HivI wifi alikuwa ni kichaa kweli au alikuwa anadanganya? Na kwanini adanganye sasa?

Masikini Mungu amlaze pema wifi yangu”

Wikendi ilipita na tayari Enrico alishaanza maisha yake kwa shangazi yake huyo, siju ya jumatatu alipokuwa akitoka shule kama ilivyo desturi yake alipita kwa kichaa Nasphaty lakini siku hii alionekana mwenye furaha sana kuliko siku zote, kichaa Nasphaty alifurahi pia alipomuona Enrico anafuraha, alimpatia soda ya kopo pamoja na chakula kilichofungwa na yeye alikuwa nacho kama hiko waliingia ndani na kuanza kula pamoja, ilikuwa ni pilau na nyama.

Walikula huku wakifurahia chakula walichokuwa wanakula.

Baada ya kumaliza kula walikunywa soda kisha Enrico alianzisha mazungumzo.

“Unajua kwanini nina furaha sana leo? Kwa sababu nimehama pale nyumbani nimehamia kwa Aunt Helma”

Enrico aliongea kana kwamba anaongea na mtu mwenye utimamu wa akili.

“Nimekumbuka kitu mama una jina zuri sana, sana.Nasphaty”

Alipoongea hivyo kichaa Nasphaty alionekana kushituka kidogo japo Enrico hakumuona na hapo machozi yalianza kumtoka.

“Enrico..”

Sauti hiyo ilimshitua Enrico ambaye alikuwa amejiinamia.

ITAENDELEA….
 
Wa andishi uchwara bhana akili zao wanazijuwa wenyewe wakishakuwa na stress za maisha ya kitaa basi ukurupuka uwazisha uzi alafu upotea mazima ebhana usirud tena Kwanza ujui chochote maisha bado yapo tafuta kazi nenda viwandan vya bakharesa utapata kazi ya kubeba viroba vya ngano kutwa buku 10 utaondokana na stress
 
Ni hobby Tu kama zilivyo hobby nyingne napenda tu stori in short sio kama sina cha kufanya na sijakuomba hela, wewe sio chochote wala lolote kwangu peleka makasiriko yako huko na stress zako za maisha.Sina stress wala nini Nafanya tu kama sehemu ya kurelax
So kama hujapenda kaa kimya
 
Lakini, mbona umejibu kama mtu mwenye stress?
 
Ni hobby Tu kama zilivyo hobby nyingne napenda tu stori in short sio kama sina cha kufanya na sijakuomba hela, wewe sio chochote wala lolote kwangu peleka makasiriko yako huko na stress zako za maisha.Sina stress wala nini Nafanya tu kama sehemu ya kurelax
So kama hujapenda kaa kimya
Dear ebu weka muendelezo story nzuri inasisimua
 
Sehemu ya kwanza
Katikati ya msitu mnene, giza zito likiwa limetanda kila kona ya msitu huo alionekana kijana akikimbia huku jasho likimtoka ni dhahiri alikuwa amekimbia kwa muda mrefu sana na alikuwa na hofu iliyopitiliza huku nyuma sauti tofauti tofauti zikimfuata kadri alivyokuwa akizidi kukimbia ili kujiokoa na jambo hilo.

“Harry! Harry! Haaaarry! Hahahahahahah” Sauti hiyo ilizidi kumsogelea huku vicheko tofauti vikichukua nafasi ya kumuogopesha zaidi na zaidi.

“Harry!! Harry! Harry!. Hapo alisimama kisha akafumba macho yake kisha akageuka nyuma taratibu na kuyafumbua macho yake tena.

“Ni ndoto mbaya? Harry!”

Harry alipofumbua macho alimuona mama yake ameketi pembeni yake huku akimtizama kwa umakini.

“Mama!”

“Nimekuita muda mrefu Harry inaonekana ulikuwa ukiota tena ndoto mbaya ona jasho linakutoka”

“Ni kweli mama it’s bad dream” Alimsimulia mama yake jinsi alivyoota ndoto hiyo mbaya huku bado akionesha hofu sana usoni.

“Pole! Muombe Mungu akuondolee ndoto mbaya mwanangu Sawaa?”

“Sawa mama”

“Sasa leo nafasi ipo ya kutosha kesho kanisani na unajua kabisa wiki ijayo it’s your 20th birthday so twende leo tukafanye shopping ya mahitaji yote nataka siku yako iwe ya kipekee sana”

“But mama……”

Kabla hajamaliza kuongea tayari alishamziba mdomo ili asiendelee kuongea.

“Najua Harry lakini look kwa miaka karibia mitano your daddy hakuwahi kusherehekea kuzaliwa kwako huoni hii ni nafasi nzuri kufurahi tukiwa pamoja na baba yako?”

“Nakuelewa unachomaanisha mama kwakuwa umependekeza hivyo I have to accept that”

“Yes! Good boy that’s why I love you, haya inuka kajiandae then twende”

“Okay mom”

Aliinuka na kuelekea bafuni ili ajiandae na hapo mama yake alimuacha ajiandae na yeye alishuka chini kuendelea na kazi nyingne alifanya kila kitu yeye mwenyewe hakuhitaji mdada wa kazi kumsaidia kwani kazi zake hazikumfanya kuwa bize kiasi cha kushindwa kufanya shughuli za nyumbani kama mama.

Maisha yao yalikuwa ya kifahari sana kutokana na kuwa na pesa, pesa kwao haikuwa tatizo kabisa waliweza kusafiri kwenda nchi yoyote waliyotaka.

Mr Maurice Hilary na Bi Hannah Mollel ndio wazazi halisi wa kijana Harry, mtoto wa kwanza na wa pekee kwenye familia hiyo, walimiliki kampuni za madini na mafuta pamoja na miradi midogo midogo mbalimbali nyumba za kifahari.

Miaka takribani kumi walikuwa nje ya nchi walizunguka nchi tofauti tofauti karibia saba tokea Harry ana miaka mitano hali hiyo iliwafanya kuwa na uzungu fulani kwenye maisha yao hivyo kwa upande mwingine waliishi kama wazungu.

Baada ya kurudi nchini ilipita miaka mitatu Harry alipendekeza apate chuo hapa Tanzania asome japo wazazi wake hawakupenda asome ndani ya nchi ila kwa sababu alikuwa mtoto wao wa pekee waliheshimu ombi lake kwa muda huo ndipo alipoanza masomo yake ya chuo kikuu akiwa kijana mdogo kabisa kutokana na kuwa kijana mwenye akili nyingi ya kuchanganua vitu tofauti.

Sasa zilikuwa zimebaki siku chache kuifikia siku ya kuzaliwa kwa kijana Harry alitarajia kutimiza miaka ishirini tokea kuzaliwa kwake, na walipanga kufanya tafrija ili kumpongeza mtoto wao wa pekee.

“Hubby! Bado unafikiria kuhusu ndoto uliyoota? Kwanini hutaki kuniambia nini umeota? Ila hata Harry ameota ndoto mbaya sana” Aliongea Bi Hannah akimwambia mume wake.

“No mke wangu sio ndoto mbaya hata hivyo siwazi kuhusu ndoto, nafikiria nimepata safari ya ghafla ya kikazi”

“Mmh lini?” Aliuliza kwa kuhamaki

“This time Hannah! But I want to spend much more time with my family, si unajua next week ni birthday ya Harry sitaki kumdisappoint”

“So what is your plan?”

“I want to send the representatives”

“But are you comfortable?”

“Yes love I’m very okay, na nina furaha sana kwasababu tutakuwa pamoja kwenye Harry’s 20th birthday”

Bi Hannah aliishia tu kutoa tabasamu na kuendelea kuandaa kifungua kinywa kisha waondoke.

“Am…. Nilisahau tutatumia ile BMW honey!”

“It’s okay hamna shida hata mkichukua yote mimi nitakodi taxi” Aliongea kiutani Mr Hilary na kumfanya mke wake acheke.

“Kitakuwa kituko cha siku hahahah magari matano yote tutajigawaje?”

“Hahahah……..Nahitaji kwenda kuweka mambo Sawa ili tuweze kuwa pamoja wiki ijayo”

“Sawaa hamna shida”

Muda huo ndio Harry alikuwa akishuka kutoka juu ili ajumuike na wazazi wake kupata kifungua kinywa, hakuwa sawa kama siku zote kutokana na mawazo aliyokuwa nayo juu ya ndoto aliyoota.

“Daddy!!! Good morning”

“Good morning my boy are you okay?”

“Yes Daddy I’m okay”

“Usiwaze sana kijana wangu hiyo ni ndoto tu japo sio nzuri just pray hard” Aliongea huku akimpiga Piga begani.

Wakati wakiendelea kupata kifungua kinywa simu ya Mr Maurice iliita naye alisita kidogo kuipokea baada ya kuona mke wake amehamishia umakini wote kwake.

“Excuse me!! Sitaki kuwakosesha breakfast” Aliinuka na kwenda pembeni kidogo ili aongee na simu.

“Eeh!! Ha..hallo!..”

“Najua! Najua lakini sio kwa vishindo hivyo jamani ingekuwa vyema kama tukienda taratibu Eeh mambo gani haya jamani”

“Sa..sawaaa Hamna shida nimeelewa vizuri kiongozi, Sawaa” Alisikika Mr Maurice akiongea na haikujulikana anaongea na nani kwenye hiyo simu.

Alivyomaliza aligeuka ili arejee mezani macho yake yalikutana na mke wake ambaye alikuwa amekishika kiuno chake.

“Hubby ni nani huyo mbona ni kama una wasiwasi sana?”

“Usijali mke wangu ni mambo tu ya kazi na unakumbuka nilikuambia ilihitajika nisafiri? Nilikuwa najaribu kuweka mambo Sawaa”

“Really?”

“Yes! Wife twende tukaendelee na chai unajua mtoto atajisikia vibaya” Alimshika mkono mke wake na kurudi tena mezani lakini hawakumkuta kabisa Harry, waliishia kuangalia na tu , wakati wakijiuliza Harry yuko wapi walimuona akishuka kutoka juu akiwa tayari kwa safari.

“Mom mimi niko tayari”

“Chai mwanangu…”

“Nimeshiba mama”

Mr Maurice alimgeukia mke wake na kumwangalia kama kumpa ishara fulani naye akaitikia kisha akapandisha juu kwenda kuchukua funguo pamoja na vitu vyake muhimu vidogovidogo vya muhimu kwaajili ya kuondoka navyo.

“Son!! Najua unawaza kuhusu ndoto ni Sawa ila usiwaze sana keep praying hard, usiruhusu ikutawale sana”

“Daddy I understand the situation, naelewa vizuri sio kama nawaza sana kuhusu ndoto ila siko tu poa kwa leo worry out King”

“It’s okay, we nenda na mama nilitamani sana tungeenda wote ila nina majukumu”

“Usijali baba”

Bi Hannah alikuwa akishuka kutoka juu taratibu huku akiwaangalia baba na mwana wakiwa wanaongea.

“Hubby ungependa kuongozana nasi?”

“Nilitamani iwe hivyo ila nina majukumu mke wangu, mkaniwakilishe tu usisahau kuninunulia ile suti niipendayo”

“Hahah…. Umekumbuka hiko tu yaani sawa, Son let’s go”

Harry alimfuata mama yake na wote wakaondoka muda huo, Mr Maurice aliichukua simu na kupiga namba aliyoijua yeye na punde tu ilipokelewa na aliinekana akiongea kwa hasira sana kisha akakata simu na kuondoka, alitoka ndani na kuingia kwenye gari kisha akapiga moto na kutokomea.

Bi Hannah na Harry licha ya kuwa mwendoni kwa dakika karibia ishirini lakini hakuna aliyetoa neno lolote kulikuwa na ukimya wa ajabu ndipo Bi Hannah alipoamua kuuvunja ukimya.

“Harry! What’s up Son mbona kinyonge?”

“That house…… that house sometimes is full of drama, nashindwa kuelewa nini shida”

“Harry!…”

“Please Mom just… just stay calm”
Bi Hannah aliishia tu kumtizama mwanaye bila kutoa neno na alielewa kitu ambacho Harry alimaanisha.

ITAENDELEA….
Good
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom