The Citizen You Can't Be Serious!! Nyie ni Gazeti Makini!!

The Citizen You Can't Be Serious!! Nyie ni Gazeti Makini!!

Hivi siku Kakobe akiwa anumwa au ana udhuru wowote mnaongozwa na nani?

Askofu Kakobe hatakuwepo kwa jumapili kadhaa,tangu ya tarehe 16/juni/2013.Na askofu Nathan Meshack pichani kati ya kumi tisa ndiye anaongoza FGBF kwa sasa.Nenda jumapili kanisani Mwenge ukashuhudie. mwenyewe! askofu iringa 3.jpg
 
Kwanza Kakobe hajawahi kusema na wala haitwi mtume yeye ni mchungaji wa kanisa la FGBF Dar es Salaam na Askofu Mkuu wa Kanisa la FGBF, Tanzania. Pili Yesu alisema wataotenda miujiza kwa jina lake ni wale wamwaminio (Marko 16:15-18) kuhusu manabii wa uongo alisema watafanya ishara kubwa na kushusha moto kutoka mbinguni (ufunuo 13:12-14)
Yesu Kristo anasema "Mtawatambua mitume na manabii wa uongo kwa matunda yao kama wanazaa mazuri au mabaya[MATTHEW 3:8;7:16~23]
 
Ndg hii ni mfano tu, tunalishwa habari nyingi za uongo na hisia za mitaani tu, kwenye siasa ndo usiseme.
Kwa kuwa watu wanapenda kusikia wanachotaka kusikia magazeti yanatumia mwanya huo kutengeneza pesa.
Tatizo letu watz,tunapenda uongo ambao ni dhambi tosha ya kutupeleka katika adhabu ya milele pamoja na baba yao waongo ambaye ni Shetani na Ibilisi[JOHN 8:44].Na ukitaka kujua watz,wanapenda uongo,angalia jinsi wanavyoshabikia vichekesho katika Tv na kusoma habari za udaku ambazo ni dhambi[UFUNUO 22:12-15]
 
Duuh.. Hivi masihi maana yake ci mpakwa mafuta wa Bwana..? so kakobe.. mwingira na mzee wa upako ni wapakwa mafuta wa Bwana..? Wanaishi maisha ya fahari hawa wapakwa mafuta.. wanamiliki magari na majumba ya fahari.. Mh..
Anyway back kwa topic.. kama hicho unachosema ni ukweli unaweza/mnaweza kupeleka malalimiko yenu kwa baraza la habari mkiwa na ushahidi uliojitosheleza.. Najua magazeti wakati mwingine wana tabia ya ku-pre empt habari ili mtokeze na kupinga.. njia ambayo sio nzuri..
Askofu Kakobe alikwisha kueleza hadharani kuwa si tajiri kama maadui zake wanavyomzushia.Kumbuka katika kipindi chake cha somo"SHETANI BABA" kwenye Televisheni alionesha mpaka chumbani kwake na mali zote anazomiliki ambazo alizipata kabla kuwa pastor ! Kisha kuwaambia watanzania wataje kama ana mali nyingine lakini hakuna aliyejitokeza! Askofu Kakobe si fisadi kama unaowajuwa wewe duniani;kwani ametoa maisha kuwa kafara kama mitume wa kweli katika Biblia kama utakavyoona kwa macho yako ukipata neema ya uzima
 
Mimi nadhani wakati mwingine siyo vizuri kuwa too emmotional for nothing. Kama gazeti, hakuna kosa kuuliza mahali alipo any public figure, Kakobe akiwa mmoja wapo. Si sahihi pia kuleta emotions zitokanazo na imani binafasi kwa mtu badala ya kuwa na ile imani ya ukweli kwa Mungu. Napata picha kuwa ndugu mleta uzi unamuamini sana Kakobe kuliko hata Mungu wako na ndio maana umejitahidi kuhakikisha kuwa unamponda Bwana Mkinga na huku ukituonyesha waJF kuwa unafahamu The Citizen ni gazeti makini sana likiwa na uongozi thabiti wa Managing Editor Bakari Machumu aliye chini ya Managing Director wa Mwananchi Communications Limited, Tido Mhando. Sidhani kama emotions zako zinaweza kuondoa umakini wa gazeti mbele za wanaJF haswa wale wenye msimamo wa kumwamini Mungu aliyehai kuliko kumwamini mtu.

Mleta uzi unapaswa kukumbuka kuwa Kakobe ni binadamu kama wewe na kuwa naye yuko kama wengine wote so kumuamini kama yeye ni mtu asiye wakaida kunaweza kuathiri uwezo wako wakufikiri kwa kiasi kikubwa. Wote tunatambua kuwa Kakobe huyu huyu anakesi mahakamani akidaiwa na wale ambao katika kanisa lake mumewapa majina ya 'Wabaya wake' eti kwasababu wamehoji matumizi ya Kanisa mahakamani. Wote twajua kuwa kule mahakamani wale 'Wabaya Wake' wameambiwa kesi hiyo itawasumbuwa kwasababu eti kanisa limesajiriwa kama mali yake huyu Baba Yenu Askofu Kakobe (Kumbuka Yesu alikataa watumishi wake kuitwa Baba - Mathayo 23:1 mpaka mwisho) na hivyo kama ni kweli ametumia vibaya zile TSH14bilini basi ametumia pesa zitokanazo na his own investment. Je, huu ndio utukufu unataka kutuonyesha kuwa yeye hana dhambi? Na hata hiyo habari ya umeme wa Tanesco, ikumbukwe kuwa aliwahi kutuambia Watanzania kuwa ule umeme usingewaka baada ya Tanesco kulazimisha upite mbele ya kanisa lake. Mbona unawaka? Ni ule unabii wa kuwa Mrema angekua Rais wa Tanzania mwaka 1995, mbona haikuwa na sisi tunabaki kujifanya hatutaki kuona, kusikia wala kuambiwa kuwa mwaminini Mungu na siyo binadamu.

Kama unachosema wewe ni kweli, basi mpeleke Bwana Mkinga, Bakari Machumu au Tido Mhando kwa Kakobe. Kama kweli yupo nchini, basi aje kwenye ofisi za Mwananchi ili approve the newspaper wrong. Tuache propaganda ndugu zangu. Kama hayupo ni kweli hayupo. Binafsi nawapa hongera sana The Citizen kwani wangekuwa unprofessional, wangeweza hata kuandika mengine mengi ya mitaani yamhusuyo Kakobe. Wewe mwenyewe jiulize tu: Je, idadi ya wale tuliokuwa tukisali pale bado iko pale pale au wengine wameweza kupata kuokolewa na Mungu sasa amezifungua akili zao mpaka wamepata kuanza kufikri vizuri tena? Angalia idadi na utuletee uzi mwingine kwani ni dhahiri idadi imepungua sana na mumebaki wachache mnaod=subiri Mungu aje awaokoe kutokana na kifungo cha kutokusikia, kuona wala kutaka kuambiwa.

Wachungaji waliofungua kesi walidanganywa na adui na kudanganyika baada kupoteza wito wa utumishi wa Mungu kama Biblia inenavyo;maana wote nawafahamu!.Askofu Kakobe amekwisha toa maelezo kwamba hajawahi kusema Mrema atakuwa rais bali uzushi wa magazeti na maadui zake kama huo wa Citizen!Mwisho,inaelekea wewe unauliza vitu ambavyo vimekwishajibiwa na askofu Kakobe.
 
Askofu Kakobe alikwisha kueleza hadharani kuwa si tajiri kama maadui zake wanavyomzushia.Kumbuka katika kipindi chake cha somo"SHETANI BABA" kwenye Televisheni alionesha mpaka chumbani kwake na mali zote anazomiliki ambazo alizipata kabla kuwa pastor ! Kisha kuwaambia watanzania wataje kama ana mali nyingine lakini hakuna aliyejitokeza! Askofu Kakobe si fisadi kama unaowajuwa wewe duniani;kwani ametoa maisha kuwa kafara kama mitume wa kweli katika Biblia kama utakavyoona kwa macho yako ukipata neema ya uzima

Ungemjua unayemjibu usingemjibu!!!!
Sasa kwa kuwa umemjibu mimi nakupongeza kwa hekima yako!!!
 
Wachungaji waliofungua kesi walidanganywa na adui na kudanganyika baada kupoteza wito wa utumishi wa Mungu kama Biblia inenavyo;maana wote nawafahamu!.Askofu Kakobe amekwisha toa maelezo kwamba hajawahi kusema Mrema atakuwa rais bali uzushi wa magazeti na maadui zake kama huo wa Citizen!Mwisho,inaelekea wewe unauliza vitu ambavyo vimekwishajibiwa na askofu Kakobe.

Askofu Kakobe: Wanaosema nimekimbia nchi wazushi




Na Thobias Mwanakatwe



16th June 2013


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa






Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) la jijini Dar es Salaam, Zachary Kakobe, amesema watu wanaomzushia amekimbia nchi na kwenda kuishi nje wana ajenda ya siri na wanastahili kukemewa ili wasijezusha jambo kubwa litakaloweza kutikisa usalama wa nchi.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili jana jijini Dar es Salam, alisema yupo Dar es Salaam na tangu mwaka 2010 hajasafiri kwenda nje kama inavyoelezwa na baadhi ya watu kwamba amekimbia nchi.
“Uvumi huo ni wa wazushi ambao idadi yao inaelekea kuongezeka siku hizi.Wazushi hawa wamefikia hata kuwazushia watu kadhaa wakiwamo wasanii na wanasiasa kwamba wamekufa, wakati siyo kweli, sijui sababu za uzushi huu,” alisema Askofu Kakobe wakati akijibu maswali ya mwandishi kwa njia ya simu.
Alisema siku yoyote kabla ya Jumapili ya wiki hii atasafiri kwenda kufanya mkutano mkubwa wa injili jijini Toronto nchini Canada.
Kwa zaidi ya mwaka sasa kumekuwa na uvumi kwamba, Askofu Kakobe ameikimbia Tanzania na kwenda kuishi katika Jiji la Toronto, kufuatia mazingira magumu nchini katika kutangaza neno la Mungu.
Wanaozusha uvumi huo wamekuwa wakieleza sababu kadhaa zilizomfanya Askofu Kakobe kukimbia nchini kuwa ni kutokana na kukumbwa na mikasa kadhaa.
Miongoni mwa mambo yanayotajwa ni kwamba Mwaka 2007, Kakobe alikumbana na kikwazo cha kwanza baada ya serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, kufanya upanuzi wa Barabara ya Sam Nujoma kutoka Mwenge kwenda Ubungo.
Barabara hiyo ilisababisha sehemu ya maegesho ya magari nje ya kanisa lake lililopo Mwenge, jijini Dar es Salaam kumegwa. Maegesho hayo yalikuwa yakisaidia waumini wa kanisa hilo kuegesha magari yao wakati wakiwa kwenye ibada.
Mwaka 2010, kulitokea mzozo mkali kati ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo lilitaka kupitisha umeme wenye msongo mkubwa wa KV 132 mbele ya kanisa la Askofu Kakobe.
Askofu Kakobe alilipinga zoezi hilo akidai licha ya madhara kwa waumini wake, umeme huo mkubwa utasumbua mitambo ya Televisheni ya Holiness aliyowaonyesha waandishi wa habari ambayo aliifunga kanisani hapo kwa ajili ya kurushia matangazo ya kiroho.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Sinaga imani kbs na uponyaji wa Kakobe.Kuna kanguvu fulani anakotumiaga kutoka kwa Mungu mwingine tofauti na yule anayeaminiwa na kuabudiwa na wengi.

So what!!! una matatizo ya ubongo bila shaka,usipomwamini Kakobe,wakati tupo mamilioni toka kote
duniani tunamwamini unapunguza nini?!!!!!
 
kuwataja hao ndo naona kuwa sisahihi akini ndani ya imani kumeingia mazingaombwe kwa mfano kuwaombea wanafuni wafaulu bila kusoma, watu kupata kazi bila ujuzi, kujenga majumba bilakazi. kuna wachungaji wameacha ule msingi wa mafundisho ya Yesu kuwa "Tafuteni kwanza ufalme wa Mbingu na mengine mtayapata kwa ziada" wao husema njoo kwetu utapata kazi, utapona ukumwi, utaondokana na umasikini nk. kwa vile watu wana shida si watakuja? maana hayo pia ni mazingaonbwe. yesu alipowaponya watu hakuwatangaza hadharani. wao hununua vipindi kwenye tv kuonyesha uwezo wao! Yesu aliwakataza hata wale aliowaponya wasiseme lakini wao walisema. Kama unaponya watu watakutangaza huna haja ya kutafuta vipindi kwemye tv kujiuza. Yaani miujiza au mazingaombwe yamewekwa mbele ili kupata wafuasi. hilo lipo mana hata Yesu alisema wataoa pepo kwa jina langu lakini.. Sasa nawaonya enyi waumini kuweni makini na hawa manabii wa uwongo wanaoshindania mazingaombwe huku wakihalalisha utajiri wao na waumini wakiendele kukamuliwa kila kukicha ole wao!

Wewe ni Muinjilisti Mzuri.Basi tutajie Wachungaji, Mapadri, Maaskofu, Mitume, Walimu, au Manabii ambao wewe unawaona kuwa Wanahubiri neno la Mungu kwa Ukamilifu na Matendo Dhahiri ya Mungu yakadhihirika kwa Ukamilifu.Usije sema unamtaka Muhubiri anayesisitiza "Mungu anaponya" lakini uponyaji huuoni, au anayehubiri Injili isiyoambatana na Matendo, Ishara na Maajabu ya Mungu, ambayo hata YESU KRISTO mwenyewe wala MITUME WAKE hawakuwahi kujihangaisha kuhubiri Injili za namna hiyo!! Haya tutajie Mtumishi unayemwamini ili tumfuate huyo mkuu!
 
Bahati mbaya kabisa simwamini Kakobe pia! Namwona msanii tu kama wakina Lusekelo na wengine, hata Waganga wa kienyeji wanaombea na kutoa mapepo. Asante.

Tuambie unamwamini mtumishi yupi wa MUNGU, ukisema unamwamini Mungu tu pasipo kuwaamini watumishi wake, very sorry Mungu hatendi kazi pasipo mawakala wake anayewabebesha matendo, ishara na maajabu ili wathibike kuwa Yu Pamoja nao katika Kazi aliyowapa! Haya Tutajie Wewe Unamwamini Mtumishi Yupi wa Mungu?
 
Kinyamana, ukweli unao, ninachokiona kwako ni kujipa moyo. Nilikuwa napindisha sentensi sasa wacha ninyooshe. Kakobe si lolote na mbele ya Mungu ana ya kujibu. Mifano hai ninayo kama hii ligi unaitaka niko tayari. Hakuna aliyemuhukumu, magtendo yake yanaonyesha kwamba siyo.

Povu lote la nini ndugu!? tunakubali wewe "ndio lolote" na "kwa Mungu unalo la kujibu". Amina!
 
Naona waumini wake mmechachamaa kweli...

...naona wapinzani wake mmavuja povu sana! Kwani akiwepo au asipokuwepo, ninyi inawahusu nini na wala si waumini wake!!?? Anyway hii inaonesha ni namna gani huwa mnammiss ijapokuwa hawachungi ninyi!
 
Namzungumzia Mungu wa Isaka, Ibrahim na Yakobo..
Nawaambia tena nendeni mkatubu na Yesu atawasamehe..

Waende wakatubu wapi? Na utaaminije kama wametubu ilhali huwaamini kwa kila kitu? Hebu elekeza vizuri ukaeleweke!
 
BTW, hivi gumegume maana yake nini vile?

Naam kuu, "gumegume ni aina ya jiwe gumu sana" lakini Almasi ni ngumu zaidi kuliko gumegume. Neno gumegume pia Mungu amelitumia anapomwambia Nabii Ezekiel " Kama almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji chako" EZEKIEL 3:9. MYTAKE; Ni dhahiri katika Ulimwengu wa nyakati hizi chafu kabisa Mungu amewapa watumishi wake wa kweli Kama KAKOBE vipaji (vya nyuso) vigumu kuliko gumegume ili waweze kuingia katikati ya ngome za shetani (watu wasioamwamini Mungu Jehova) na kuzibomoa ngome hizo (YEREMIA 1:10) bila ya woga, aibu wala kukata tamaa ili kupanda Ufalme wa Mungu. Nakubali kama Kakobe ataridhia kuitwa mgumu zaidi ya gumegume katika utumishi wa Mungu.
 
He he......Kakobe katoroka.
Nini kilipelekea Mwandishi kusema hivyo na si huyo tu nimesikia habari hiyo kipindi cha nyuma

Kumbe umekimbilia kwenye thread za kidini?? Umemtosa mjomba wako Paul Kagame?? Haraka rudi kwenye international forum umnusuru mjomba!
 
Tuambie unamwamini mtumishi yupi wa MUNGU, ukisema unamwamini Mungu tu pasipo kuwaamini watumishi wake, very sorry Mungu hatendi kazi pasipo mawakala wake anayewabebesha matendo, ishara na maajabu ili wathibike kuwa Yu Pamoja nao katika Kazi aliyowapa! Haya Tutajie Wewe Unamwamini Mtumishi Yupi wa Mungu?

Hapo huwezi pata jibu ndugu kwa maana wengine mitume wanao waamini hata kukemea au kufukuza mapepo (majini) hawawezi! Mimi siyo mshirika wa kanisa la FGBF ila Kakobe ni mtumishi wa Mungu ninaye mwamini kwasababu hapindishi neno la Mungu. Pale kwenye lango kuu kanisani kwenye bango niliwahi kusoma: ---- UNAPENDA KUAMBIWA UKWELI UNAKARIBISHWA, KAMA HUPENDI HAPAKUFAI.
Mwaka 1998 nilisikia maneno mengi mabaya yakisemwa dhidi ya Kakobe ikiwamo kunyang'anya watu vito vya thamani, pete za dhahabu na pia eti kama hayupo wanaweka kaseti zake wakimaanisha eti yeye ndiye peke yake anasimama madhabahuni tu. Niliamua kufanya uchunguzi kwa kufanya ibada FGBF nikagundua yanayosemwa juu ya Kakobe na kanisa la FGBF ni uzushi mtupu. Hata sasa bado maneno hayo yanazungumzwa jambo la ajabu ni kwamba ukimuuliza mzungumzaji kuwa je aliyashuhudia hayo anayozungumza anakujibu 'hata yeye alisimuliwa'.
Ibilisi hatashuka laivu kuipinga injili, anatumia watu kwa mwavuli wa kushabikia dini zao ambazo haziokoi, zisizokemea uovu/dhambi. Ashukuriwe Mungu Yehova kwa kuwa Kakobe hafumbii macho uovu, NENDENI FGBF MFUNDISHWE KWELI YA NENO LA MUNGU YEHOVA.
 
Hapo huwezi pata jibu ndugu kwa maana wengine mitume wanao waamini hata kukemea au kufukuza mapepo (majini) hawawezi! Mimi siyo mshirika wa kanisa la FGBF ila Kakobe ni mtumishi wa Mungu ninaye mwamini kwasababu hapindishi neno la Mungu. Pale kwenye lango kuu kanisani kwenye bango niliwahi kusoma: ---- UNAPENDA KUAMBIWA UKWELI UNAKARIBISHWA, KAMA HUPENDI HAPAKUFAI.
Mwaka 1998 nilisikia maneno mengi mabaya yakisemwa dhidi ya Kakobe ikiwamo kunyang'anya watu vito vya thamani, pete za dhahabu na pia eti kama hayupo wanaweka kaseti zake wakimaanisha eti yeye ndiye peke yake anasimama madhabahuni tu. Niliamua kufanya uchunguzi kwa kufanya ibada FGBF nikagundua yanayosemwa juu ya Kakobe na kanisa la FGBF ni uzushi mtupu. Hata sasa bado maneno hayo yanazungumzwa jambo la ajabu ni kwamba ukimuuliza mzungumzaji kuwa je aliyashuhudia hayo anayozungumza anakujibu 'hata yeye alisimuliwa'.
Ibilisi hatashuka laivu kuipinga injili, anatumia watu kwa mwavuli wa kushabikia dini zao ambazo haziokoi, zisizokemea uovu/dhambi. Ashukuriwe Mungu Yehova kwa kuwa Kakobe hafumbii macho uovu, NENDENI FGBF MFUNDISHWE KWELI YA NENO LA MUNGU YEHOVA.

Msimamo wa Kakobe ni mwiba mkali kwa CCM na ni mtu asiyepindisha ukweli!!!
Ni Kiongozi pekee aliyepigania Viongozi wa dini kushiriki katika siasa na akashinda !!!
 
Ungemjua unayemjibu usingemjibu!!!!Sasa kwa kuwa umemjibu mimi nakupongeza kwa hekima yako!!!:canada:Kaseti zipo mitaani za video au dvd ya SOMO:"SHETANI BABA WA UONGO".Hili ndilo somo alilofundisha askofu Kakobe kwenye luninga kadhaa hapa nchini kuwa amejitoa kuwa maskini wa hiari kwa kazi ya Injili aliyotumwa ulimwenguni.
 
Back
Top Bottom