Ndugu wanaJF,
Nimesikitishwa na kushangazwa na habari iliyochapishwa na kupewa uzito mkubwa sana (lead story) na gazeti la The Citizen toleo la jumapili tarehe 07-04-2013 iliyo na kichwa kifuatacho:Katika habari hiyo mwandishi wake Bwana Mkinga Mkinga alidai kwamba Askofu Kakobe hajaonekana katika miezi sita iliyopita na kwamba kwa mara ya mwisho kuonekana kanisani Mwenge ilikuwa mwezi Januari mwaka huu. Na kwamba sasa hivi yuko Marekani ndiko alikohamia. Pamoja na madai mengine ya kuzushi mwandishi huyo ambaye kwa kweli ninao ujasiri wa naweza kumwita 'uchwara' anadai kuhudhuria ibada ya Pasaka tar 31-03-2013 na kukuta ikiongozwa na aliyemtaja kama Mchungaji Hezron (jina ambalo sijawahi hata kulisikia). Kwa FGBF Dar es Salaam tunaye mchungaji mmoja tu ambaye ni Mchungaji Zakaria Kabobe.
WanaJF kwa ufupi na watu wengine wapenda ukweli habari hizi ni za uzushi na uongo mtupu, na mimi kama mshirika wa kanisa la FGBF Dar es Salaam nasema hivi tangu Jumapili ya Agosti 15, mwaka 2010 alipokuwa Zambia kwa ajili kazi ya Mungu hatujawahi kumkosa kwenye ibada yoyote ya Jumapili. Kwa mfano, jumapili ya Pasaka tulikuwa na baba yetu Askofu Kakobe kama ilivyokuwa jumapili zote zilizotangulia.
Nilikuwa naliheshimu sana gazeti la The Citizen lakini kwa habari hii naanza kutilia shaka umakini wao. Natoa wito kwa Mtendaji Mkuu wa MCL Mzee Tido Mhando, Mhariri wake Mkuu Bwana Machumu na hata mwandishi wa habari hiyo ya kizushi Bwana Mkinga wawe makini vinginevyo wataliharibu gazeti