King Cobra,nisaidie kujua hilo Neno la Mungu katika uzi huu ! Na je,naweza kupata nakala video ya kiti moto kama ulivyosema unayo? :israel:
KITI MOTO IPO TENA NI PART I &II
Kuhusu neno pia naweza kukusaidia ila kwa kuwa ni suala la imani neno lipo kila mahari ukimkuta mtumishi yoyote yule anayesimamia kweli kama Kakobe atakusaidia!!!!
Pia kama upo karibu na Pascal Manyalla atakusaidia mengi kwa kuwa ndiye aliyekuwa anaendesha kipindi cha KITI MOTO na alimhoji Kakobe Live lakini kufuatia majibu ya kakobe Serikali ilipiga marufuku mkanda ukafichwa;
Sisi tuliokuwepo tulirekodi yote kwa ajili ya ukombozi wa taifa hili.
Kwa Ufupi:
Serikali na vyombo vya dola walimwita Kakobe na kumuhoji Mambo kadha;
1. Kwa nini yeye akiwa Kiongozi wa dini anachanganya siasa na dini???
2.CCM walivumisha kwamba Kanisa la Kibweter Uganda ni la Kakobe???
3.Waziri Nyanda Mambo ya ndani alijenga fitina kuwa Kakobe anaiba dhahabu!!!
Waliokuwepo ni pamoja na Abslon Kibanda, Glory Tesha wa habari leo, Msafili Mtemela na wengine wengi utawaona humo:
Katika majibu ya Kakobe akasema juu ya Kibwetere Uganda kanisa lile ni tawi la Katoliki na wahusika walikuwa masister na ushahidi wa hilo Askof Pengo wa DSM alishatolea ufafanuzi na kuweka wazi . Sasa hilo likaonekana kuwa ni uzushi
Kwa kuwa vyombo uganda vilitoa uwazi juu ya ushiriki wa Masister katika uchafu ule na Kakobe akashinda hoja. Waandishi wakaelekezwa kufuatia suala hilo kupitia kwa wenzao uganda ii kuepuka Chuki
Hoja ya pili ni Wizi wa dhahabu ambao ulivumishwa na waziri wa mambo ya ndani kama ilivyo kwa Mwingulu kuvumisha ugaidi!!!
Kakobe alieleza kuwa Wanaovumisha ni polisi na watendaji wa serikali kwa masilahi ya kutafuta utawala ,akawataka polisi kutoa ushahidi hata kwa kupata mtu mmoja tu ambaye ametapeliwa na kuripoti:
Kakobe akasema kama mimi naiba dhahabu harafu polisi badala ya kunikamata munalalamika then jeshi la polisi ni dhaifu na hatuna vyombo vya dola nchni
Suala la kuchanganya dini na siasa:
Kakobe alijibu kuwa Serikali ina changanya siasa na dini na akatolea mfano:
1. Bunge linafunguliwa kwa sala wakati serikali haina dini!!!
2.Serikali inawapisha watendaji wake kwa miisngi ya dini wakati serikali hiyo hiyo haina dini
3. Mahakamani wanawaapisha watu kwa misingi ya dini wakati serikali haina dini
Kwa ufupi Kakobe aliitaka serikali kuacha kuchanganya siasa na dini ili kulinda katiba.
Baada ya hoja hizi na nyingine vyombo vya dola waliokuwepo pale walipiga marufuku mkanda huo .
KITI MOTO KILE ndicho kilichopelekea CCM kuruhusu Wachungaji kugombea na kupiga siasa hadi leo.
Mimi huwa nawashangaa sana watu wanao mbeza Kakobe kwa mchango wake katika jamii!!!