Zaman nilikuona unachambua mambo fresh ila sku zinavoenda unaniangusha sana..
Shda ya chelsea sio beki, shida ni kukosekana kwa mastreka wa ukweli na wenye nguvi na weledi wa ushapu (quick technical skills)

Kama umeangalia vzur mipira yetu tunachelewa kutoa maamuz pale golin na hii ni kwa sabab hatuna vipaji vya wasaka magoli ,. Wengi pale ni waunganishaji ila si wamalizaji.

Pia msimu huu kuna kama ka-gundu flani kwenye timu yetu, runakosakosa sana hatuna bahat ya mpra.. Inaezekana mwaka huu ni tasa kwetu.. Conte akasafishe nyota kwa mwakani
Sema utakavyo lakini ukweli ni kwamba Uongozi wa Terry anakosekana pale nyuma, na hapo nieleweke kwa sababu simaanishi mabeki wetu ni wabovu. La hasha! Namaanisha UONGOZI wa Terry unakosekana pale nyuma. Terry akiwa uwanjani angeweza kumwambia Ludigar Fanya hivi, na maamuzi yale yakasaidia. Kumbuka Ludigar na Christensen hawana uzoefu wa kutosha. Sasa wanapokuwa na kiongozi inawajenga zaidi. Azpillicueta anajitahidi ila Terry is a miss. Kuhusu Lampard pia bado naamini pengo lake hakijazibwa. Fab hana kasi inayohitajika lakini pia unamuona umri ukizidi kusogea.

Kuhusu Drogba naona tunakubaliana kwamba striker ni tatizo kubwa kwetu. Maana pamoja na mambo yote Chelsea inatengeneza nafasi za kutosha. Finishing tu inaleta shida.
 
Sema utakavyo lakini ukweli ni kwamba Uongozi wa Terry anakosekana pale nyuma, na hapo nieleweke kwa sababu simaanishi mabeki wetu ni wabovu. La hasha! Namaanisha UONGOZI wa Terry unakosekana pale nyuma. Terry akiwa uwanjani angeweza kumwambia Ludigar Fanya hivi, na maamuzi yale yakasaidia. Kumbuka Ludigar na Christensen hawana uzoefu wa kutosha. Sasa wanapokuwa na kiongozi inawajenga zaidi. Azpillicueta anajitahidi ila Terry is a miss. Kuhusu Lampard pia bado naamini pengo lake hakijazibwa. Fab hana kasi inayohitajika lakini pia unamuona umri ukizidi kusogea.

Kuhusu Drogba naona tunakubaliana kwamba striker ni tatizo kubwa kwetu. Maana pamoja na mambo yote Chelsea inatengeneza nafasi za kutosha. Finishing tu inaleta shida.
Ukweli usiopingika ni kuwa Terry atakosekana kwa sababu hakuna na hatakuwepo wa kufanana na Terry ila tatizo la Chelsea sio mabeki ila ni haya yafuatayo
Mbele hatuna mshambuliaji wa kuwaweka busy mabeki wa timu pinzani kama enzi za Costa, Drogba na wengineo
Kiwango cha Fab kimeshuka sana sio kama 2014 -17
Hazard bado hajatulia, bado ana utoto sana siku akiamka vizuri anacheza lakini akiboreka hawezi kucheza kabisa, kupangwa false nine imemboa kiasi cha kutoonekana kabisa

Hawa wako poa kabisa - César Azpilicueta - Andreas Christensen - Antonio Rüdige
Wanahitaji tu kuzoea kwani hata Terry miaka ile ya 2001 alikuwa naye na silly mistakes mpaka alipozoea
 
MABOSI wa Paris Saint-Germain wameshakubaliana na hali halisi kwamba kocha wanayemsaka Luis Enrique atatimkia Chelsea mwishoni mwa msimu huu.
Mkurugenzi wa michezo wa PSG, Antero Henrique alikuwa na mpango wa kumvuta kocha huyo wa zamani wa Barcelona kwenye kikosi chake na kumpiga chini Unai Emery.
Lakini taarifa zinadai bosi huyo ameshaambiwa kila kitu kuwa Enrique amekubali dili la kwenda kuinoa Chelsea na kinachosubiriwa ni msimu tu umalizike akarithi mikoba ya Antonio Conte.
Kutokana na hilo, PSG sasa itakuwa na nafasi ya kumchukua Conte kama itahitaji huduma yake, huku taarifa za karibuni zikidai wababe hao wa Ufaransa wamekuwa wakipiga hesabu za kuinasa huduma ya Mtaliano huyo ili akawafanye kuwa bora zaidi na kushindana kwenye michuano mikubwa kama ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Haa haa aiseee ama kweli
Ukisema cha nn mwenzio anawaza
Atakipata lin Conte mwenyewe


Tim imemshinda uefa alaf
Psg wao ndo kwanza wanataka
Kubeba UEFA wakiwa na yy
 
Chelsea legend Didier Drogba Top 11 Chelsea Career Moments

Chelsea legend Didier Drogba reveals his top 11 Chelsea career moments. Which are you favourites? let us know in the comments below. Subscribe to Chelsea TV http://bit.ly/2ty8mXn
 
  • Thanks
Reactions: SIM
Nashauri muundo huu wa manager na makocha wasaidizi wa timu
  1. Jose Mounrinho: Manager
  2. John Terry: Defending coach
  3. Peter Cech: Goalkeeping coach.
  4. Frank Lampard : Midfield coach.
  5. Didier Drogba: Forward coach.
Ebu like kama unapenda huo muundo
 
Tetesi

Arsenal na Chelsea wanatarajiwa kushindana katika jaribio la kumsajili kipa wa Atletico Madrid na raia wa Slovenia Jan Oblak, 25. (Sunday Express)

Paris St-Germain wamefungua mazungumzo na wawakilishi wa Antonio Conte kuhusu raia huyo wa Itali Kuhamia katika mji mkuu wa Ufaransa kutoka Chelsea mwisho wa msimu huu. (Guardian)
 
INAELEKEA Arsenal na Chelsea zinaweza kuwa na makocha wapya kuanzia Juni mwaka huu kama ubuyu unaoendelea kuvuma Ulaya utakuwa na ukweli ndani yake.

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel ameripotiwa kuipiga chini ofa ya klabu ya Bayern Munich iliyokuwa inamtaka kwa udi na uvumba kwa ajili ya kuanza mazungumzo na Arsenal ambayo imeonyesha nia ya kumtaka.

Munich ilikuwa inamtaka kocha huyo Mjerumani kwa ajili ya kuwa mrithi wa kocha wake wa sasa, Jupp Heynckes lakini ofa zake zote zimekataliwa kwa kile kilichoelezwa Tuchel anataka kwenda kufundisha nje ya Ujerumani.

Huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho kwa kocha wa muda mrefu wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye amekuwa klabuni hapo tangu mwaka 1996 na gazeti maarufu la michezo la Ujerumani Bild limedai kocha huyo tayari yupo katika mazungumzo na Arsenal kwa ajili ya kuchukua kazi ya Wenger.

Vilevile inadaiwa hata Chelsea inavutika na mpango wa kumchukua kocha huyo mwenye umri wa miaka 44. Chelsea inatazamiwa kuachana na kocha wake, Antonio Conte mwishoni mwa msimu lakini inaonekana Arsenal ndio imekaribia zaidi kumnasa Tuchel.

Tuchel amekuwa hana kazi tangu Mei mwaka jana baada ya kuachana na Dortmund siku chache baada ya kuipa Kombe la Ujerumani na anajulikana vizuri kwa bosi mpya wa masuala ya utendaji wa timu ya Arsenal, Sven Mislintat aliyechukuliwa kutoka Dortmund.

Wawili hao walifanya kazi pamoja Dortmund, ingawa hawakuwa na uhusiano mzuri sana. Hata hivyo, kwa sasa wanaweza kufanya kazi tena pamoja wakati huu Mislintat akitazamiwa kukisuka upya kikosi cha Arsenal.

Wakati Wenger akiwa amekalia kuti kavu, Chelsea pia kunaweza kuwa na mabadiliko baada ya wawakilishi wa kocha wao, Antonio Conte kufanya mazungumzo na klabu ya PSG ambayo inatazamiwa kuachana na kocha wake, Unai Emery mwishoni mwa msimu.

Matajiri wa PSG hawatazamiwi kuongeza mkataba wa kocha huyo ambao unatazamiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu kutokana na kushindwa kuonyesha makali yake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya ambapo PSG ilitupwa nje na Real Madrid.

Na wakati huohuo Chelsea nayo haitazamiwi kubaki na Conte ambaye amekuwa na msimu mbovu mpaka sasa ikishika nafasi ya tano katika msimamo wa LIgi Kuu ya England licha ya kutwaa ubingwa msimu uliopita.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza, PSG imemfuata Conte na kuanza maongezi naye huku kukiwa na maendeleo makubwa katika dili hilo ambapo Conte, 48, atakuwa na ongezeko la Pauni 500,000 katika mshahara wake wa sasa.

PSG ina machaguo mengine mbalimbali klabuni hapo ikiwemo Jose Mourinho, Mauricio Pochettino, Diego Simeone na Max Allegri lakini Conte anaonekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kupatikana kuliko makocha wenzake.

Inadaiwa Conte anajisikia kuanza upya kwingine huku akiwa anavutiwa na mpango wa PSG kutumia pesa nyingi katika dirisha kubwa linalokuja kwa ajili ya kukisuka kikosi hicho ambacho kimekuwa na nia kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ulaya.

Conte amekerwa na jinsi ambavyo msimu wa Chelsea ulivyoenda ikiwa imebakia katika michuano ya FA tu huku ikiwa imetupwa katika michuano mbalimbali ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya na haina matumaini ya kutetea taji lake.

Kocha huyo pia amekuwa katika mapambano ya mara kwa mara katika vyumba vya kubadilishia nguo Stamford Bridge na inadaiwa baadhi ya wachezaji mastaa klabuni hapo hawatafurahia kama atakuwepo tena msimu ujao.

BAYERN Munich ina majanga, straika wake Robert Lewandowski amegoma kusaini akiitaka Real Madrid, huku kocha iliyekuwa ikimpigia hesabu kali, Thomas Tuchel kapiga chini ofa za klabu hiyo.

Lewandowski mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu lakini Tuchel, Kocha wa zamani Borussia Dortmund anawindwa kwa kiasi kuikubwa na vinara hao wa Bundesliga kuchukua nafasi ya Jupp Heynckes mwisho wa msimu. Heynckes, alirudishwa klabuni baada ya kutimuliwa kwa Carlo Ancelotti, mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu na Bayern italazimika sasa kusaka kwingine baada ya Tuchel kuwachomolea.

Tuchel alichukua nafasi ya Jurgen Klopp kikosini Borussia Dortmund na kutengeneza timu moja matata Ulaya kabla ya kunyakuliwa na Liverpool.

Kocha huyo anatakiwa na Chelsea na Arsena baada ya makocha wao kuonekana kuzingua.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anatajwa kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu Stamford Bridge baada ya kuvurugana na mabosi wa klabu huku Arsene Wenger, mkataba wake umesalia miezi 12 na utasitishwa endapo Arsenal na utaangaliwa endapo itatwaa ubingwa wa Europa na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tuchel ndiye aliyewapika wachezaji waliotua Arsenal dirisha la Januari, Pierre-Emerick Aubameyang na Henrikh Mkhitaryan walipokuwa Dortmund.

Habari zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa kocha huyo ameshatua Emirates na kilichobakia ni suala la muda tu, Wenger akusanye virago vyake ili achukue ukanda.
 
Tetesi

Kiungo wa kati Mbelgiji anayechezea Chelsea Eden Hazard amepuuzilia mbali wanaomfananisha na nyota wa Barcelona Lionel Messi. Mchezaji huyo wa miaka 27 amesema yeye huwa hafungi mabao mengi kiasi cha kufananishwa na nyota huyo wa Argentina. (Star)

Hazard amesema kwa sasa atapatia kipaumbele kuchezea timu yake ya taifa Kombe la Dunia badala ya mazungumzo kuhusu mkataba mpya Chelsea. (Guardian)

Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois amesema bado atakuwa Stamford Bridge msimu ujao hata kama hakutakuwa na maafikiano kuhusu mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa mlindalango huyo wa miaka 25 kutoka Ubelgiji unamalizika Juni 2019. (Sporza kupitia Telegraph)
 
Naomuona kijana wetu Rudiger ameanza mechi ya Ujerumani. Sipo upande wa German but all the best to him
IMG-20180327-WA0015.jpg
 
Morata yuko 100 percent fit, kasema anataka kuwa kwenye kikosi cha world cup, GO FOR IT MORATA
Jamani hata kama mchezaji wetu Morata goigoi hawezi hata shooting accurate, one 2 one na golikipa utacheka anaanguka ,mchezaji anachojua kwenda hewani na ku jiposition. Team ya taifa kuna Diego, ispas, Rodrigo hao sio watu wazuri atasubiri sana
 
Nimefurahia droo ya Liverpool vs Man City. Hii inaweza kuwa na advantage kwetu Chelsea.

Tar 31/3 Palace atakuwa nyumbani kumenyana na Liverpool. Lakini pia tar 3/4 Liverpool atakuwa na mechi kubwa dhidi ya Palace.

Hii ina maana gani?
Ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mkubwa Salah, Van Djik na keyplayer mwingine wakapumzishwa dhidi ya mechi ya Palace kwa ajili ya kukabili miamba isiyotikisika, Man City . Amini usiamini Liver ina first eleven nzuri ila nje ya hapo haina substitute. Hivyo kama watawapumzisha hao wachezaji itakuwa vigumu kuishinda Palace uwanja wao wa nyumbani. So matokeo ya Liver si zaidi ya droo kwenye hiyo mechi. Kama Liver ikidroo ina maana watakuwa wakitutangulia kwa point mbili tu na mkumbuke tuna mechi nao mwezi wa tano na watakuja Stanford bridge.

Chelsea ina kazi moja tu! Kushinda kila mechi iliyobaki. Otherwise tutakwenda kucheza yale mashindano ya Alhamisi maarufu kama Futuhi.

But let's be positive because there is a promising future for Chelsea.
Njoo uandike tena Ngonjera zako
 
Habari hizi sio nzuri!
Kane Mnyama leo anacheza!
Nadhani kesho Son ndiyo atabariki safari yenu ya Yuropa mwakani
Lkn mwakani Yuropa mnaweza fika mbali,huku CL kidogo bado team yenu sio nzuri
 
Back
Top Bottom