Mugongo Mugongo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2006
- 223
- 8
Akinukuliwa na Hansard ya tarehe 16/07/2007, Mheshimiwa Kabwe Zitto alisema nanukuu kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na Mkataba mpya wa Mgodi Buzwagi ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi, amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli sivyo ambavyo vipo katika Mkataba ambao ameusaini mwisho wa kunukuu.
Sasa kama mheshimiwa ZITTO alimuita Karamagi muongo,lakini Zitto akashindwa kuprove kuwa KAramagi kweli ni Muongo hapo ni nani Muongo? Zitto au Karamagi? nani kalidanganya Bunge hapo?
Kama Zitto ametoa maelezo katika Bunge ambapo ikaja kudhihirika kwamba kumbe Zitto anachanganya mambo,sasa ni nani atakuwa ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi? Zitto au Karamagi? ni nani muongo hapo?
Na kama sasa imedhihiri kuwa Zitto ndiye muongo na si karamagi,kwa nini ZITTO ASICHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU ZA KULIDANGANYA BUNGE?
Huu ndio ugonjwa wetu mkubwa. Tunaangalia hili jambo kwa miwani ya kiitikadi. Mie nikiwa namba moja, by the way.