Thamani ya kitu hutengenezwa katika akili ya mtu. Unaweza kumfanyia mtu mambo makubwa lakini akaona hayana thamani kwake

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
22,114
58,054
Katika MAISHA
thamani ya kitu inatengenezwa katika Akili ya mtu. Hivyo kabla ujamfanyia MTU Jambo lolote hakikisha analipa thamani katika Akili Yake .

Mfano Kuna watu wanahitaji tu MUDA wako na sio Jambo lolote ila pia Kuna wengine wanahitaji pesa zako hivyo inahitaji utulivu wa kifikra kujua hipi Sehemu sahihi ya kuwapa Thamani watu kupitia wewe.

Kuna watu utatumia PESA Ila utawakosa na Kuna watu kupitia PESA utawapata Ila thamani itajengeka katika Akili ya MTU.

Hivyo vitu unavyodharau na kuona havina maana ndo hivyo vimesababisha wengine wauane ,wasalitiane na kuwa maadui wakubwa.

Ishi kwa kuelewa thamani ya kitu au MTU hipo Katika Akili ya MTU na sio WATU.
 
Katika MAISHA
thamani ya kitu inatengenezwa katika Akili ya MTU , Hivyo kabla ujamfanyia MTU Jambo lolote hakikisha analipa thamani katika Akili Yake .

Mfano Kuna watu wanahitaji tu MUDA wako na sio Jambo lolote ila pia Kuna wengine wanahitaji pesa zako hivyo inahitaji utulivu wa kifikra kujua hipi Sehemu sahihi ya kuwapa Thamani watu kupitia wewe.

Kuna watu utatumia PESA Ila utawakosa na Kuna watu kupitia PESA utawapata Ila thamani itajengeka katika Akili ya MTU .

Hivyo vitu unavyodharau na kuona havina maana ndo hivyo vimesababisha wengine wauane ,wasalitiane na kuwa maadui wakubwa.

Ishi kwa kuelewa thamani ya kitu au MTU hipo Katika Akili ya MTU na sio WATU.
Nimetoka kapa licha ya kusoma mara mbili mbili. Kwa hiyo thamani ya nyumba yangu iko kwenye akili yangu na siyo kwenye gharama niliyotumia?

Swali: akili inatumia vigezo gani kupata thamani ya kitu bila kutumia gharama na muda wa kukipata hicho kitu?
 
😅😅
 
Robert Heriel Mtibeli anaweza fafanua hii thread vizuri
 
Nimetoka kapa licha ya kusoma mara mbili mbili. Kwa hiyo thamani ya nyumba yangu iko kwenye akili yangu na siyo kwenye gharama niliyotumia?

Swali: akili inatumia vigezo gani kupata thamani ya kitu bila kutumia gharama na muda wa kukipata hicho kitu?

Akili yako/yangu ndio inayoipa thamani nyumba yako.
Wakati wewe unaiona nyumba au Gari Fulani labda ni V8 ni la thamani lakini kuna wengine hiyo V8 sio chochote kwao.

Akili ndio huvipa vitu matumizi ili viwe na thamani.
Wakati Dhahabu NI jiwe kama nawe mengine lakini Akili imeipa Dhahabu matumizi ya anasa na hiyo kuifanya kuwa na thamani.

Akili ndio hutoa vipaombele vya mambo na vitu.

Hata hivyo kuna vitu ambavyo ni lazima ili Akili iweze kuishi. Vitu hivyo Akili huvipa thamani zaidi. Mfano Maji, chakula, hewa, vitu hivyo vinaisaidia Akili kuishi ndio maana MTU atafanya chochote kwaajili ya vitu hivyo na vingine ambavyo sijavitaja
 
Huenda unachanganya vitu viwili tofauti: Umuhimu na Thamani. Kwa mfano: Hewa ni muhimu lakini haina thamani.

Wachumi wanasema thamani ya kitu inaamuliwa na nguvu ya usambazaji na uhitaji

Je, kuna sehemu yoyote duniani kuna shida ya upatikanaji wa hewa hadi uhitaji uzidi usambazaji?

Akili inayotoa thamani ya kitu bila kutumia kanuni za uchumi itatufifisha.
 
Huenda unachanganya vitu viwili tofauti: Umuhimu na Thamani. Kwa mfano: Hewa ni muhimu lakini haina thamani.

Wachumi wanasema thamani ya kitu inaamuliwa na nguvu ya usambazaji na uhitaji

Je, kuna sehemu yoyote dunianiani kuna shida ya upatikanaji wa hewa hadi uhitaji uzidi usambazaji?

Akili inayotoa thamani ya kitu bila kutumia kanuni za uchumi ni ya kijima

😂😂
Embu acha masikhara Mkuu. Hewa haina thamani?
Nenda hospitalini kaulize wale wagonjwa wanaolazwa hospitalini na kuwekewa mifumo ya hewa ni shilingi ngapi?
Au kauulize ule mtungi WA hewa ya oksijeni ni bei gani.

Kitu chochote kinachoisaidia Akili kuishi kinathamani kubwa Sana.
Akili inaipa vitu thamani lakini vile vinavyoifanya Akili iishi navyo vinathamani zaidi
 
Uçhumi ni nini kwani?
 
Wewe hapo ulipo umewekewa mitungi mingapi ya hewa? Na kila mtungi umeulipia kiasi gani?
Angalizo: Gesi (siyo hewa i.e air) wanayopewa wagonjwa wenye changamoto ya kupumua inakuwa ya thamani kwa sababu ya uchakataji wake kuwa wa gharama, halafu mahitaji kuwa kidogo, hivyo kupelekea kuuzwa kwa bei kubwa.
Lakini hii hewa ya Mungu tunayovuta mimi na wewe haina thamani. Ni buuree
 
Kila kitu duniani Mungu alitoa Bure. Watu ndio wanauza na kuvipa thamani.

Kwa hiyo Kwa uelewa wako kipi ni cha thamani unachokijua?

Dhahabu, ni Bure.
Ardhi ni Bure.
Maji ni Bure
Kila kitu unachokiona Duniani kilitolewa Bure.
Thamani yake inatokana na Akili ya binadamu kutumika, kuongezea thamani kilichokuwa Bure.

Ndio hoja ya Mtoa mada ilipo.

Sasa nijibu, kipi unaona cha thamani?
 
Thamani ya kitu inatokana na Akili ya binadamu kutumika, kuongezea thamani kilichokuwa Bure.
Kwa maelezo yako hapo juu, ni ukweli ulio wazi kwamba akili inatumika kuongezea thamani kitu. Lakini value ya hicho kitu itategemea na gharama zilizotumika na muda.

PS: Robert Hariel na Dr. Haya Land ni mtu mmoja lakini majina tofauti.
 
Mkuu umeiva kwenye uchumi 😁😁😁
Hutaki elewa perspective nyingine

Ulichomaanisha kipo sawa kiuchumi kwa sababu value ya kitu huwezi kuipima pasipo monetary value yake ndio maana kuna vitu havipimwi kiuchumi katika GDP ila vinawekwa katika HDI.. Ila Mambo yasiwe mengi maana tulikota darasani kitambo 😁😁

Tukirudi kwenye social setting, watu hupima thamani ya mtu kutokana na umuhimu wake, iwe kipesa au kihali, lakini uzito wa unachokifanya kwa mtu mwingine, utategemea na emotional investment aliyonayo kwako na hivyo kuamua yeye kupata emotional impact flani. Mtu akikupenda kila utakalofanya ataliona la thamani na atalifurahia ila kama hakupendi, hata ufanye makubwa atayaona kawaida.. Nadhani mleta mada alilenga hapa
 
Back
Top Bottom