DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 18,025
- 45,576
Kuna jambo katika nchi yetu lipo mtu akijiona mfupi au kuwa mlemavu anaamini yeye safari yake ya MAISHA haitokuwa na MAFANIKIO hii sio Kweli ni upotovu.
Katika MAISHA ili ufanikiwe unahitaji zaidi utimamu wa kiakili na kulivaa tumaini hata wakati Akili yako na Mwili vitakapokuwa havina Nguvu ya kusonga mbele.
Hivyo ikiwa wewe hauna mikono na Miguu au mfupi Sana hiyo isikupe hofu na kukatisha tamaa ,jitazame zaidi ndani yako na sio nje yako hakikisha unatumia MUDA wako katika kuishibisha Akili yako ili kuondoa mipaka katika MAISHA yako.
Huyu jamaa katika picha Hana mikono na Miguu ila anaishi MAISHA Makubwa na anawatia watu moyo na kuwafundisha namna gani waishi kwa furaha ,upendo na Amani.
Kama wasomi na wadau wa Jf tuna kila sababu ya kuhakikisha tunaibadilisha jamii na kuwafanya watu wote kuishi kwa usawa.
Kila mtu anaweza kutimiza ndoto zake Endapo akibadilisha mindest na kuamini MAISHA hayana mipaka
Kumbuka, mtu aliyepoteza matumaini anakuwa yupo hatarini kuzidiwa hata na mtu ambaye Hana mikono ,mikono na Miguu
Furaha
Amani ya moyo
UPENDO
Uthamani
Hivi vitu vipo ndani yako ikiwa utataka watu wakupe hivi vitu ndo pale mawazo hasi uzaliwa na kuona Dunia haipo upande wako anza Kujitazama ndani yako na ujipe thamani wewe Kama wewe,
Ukijitazama ndani utagundua una adhina kubwa Sana tofauti unavyojiona kwa nje.
Haya land kigamboni