Tembo 170 kupigwa mnada Namibia

Alhamask

Member
Mar 17, 2010
22
3
Tembo 170 watapigwa mnada nchini Namibia kwa kile kilichobainishwa kuwa ni adha ya kuongezeka kwa ukame huku kukishuhudiwa ongezeko kubwa la tembo nchini humo.

Hii sio mara ya kwanza Namibia inauza wanyama kwa mnada, ambapo msimu wa kiangazi inaelezwa kuwa kunatokea mgogoro kati ya wanyama na binadamu ambao ndio unaifanya Namibia kuuza tembo hao 170 kwa mnada.

“Kwasababu ya ukame na kuongezeka kwa idadi ya tembo, na mgogoro kati ya tembo na binadamu, kumetambulika haja ya kupunguza idadi ya wanyama hao”- kwa mujibu wa tangazo lililowekwa katika gazeti la New Era linalomilikiwa na serikali....."

Tangazo hilo lililowekwa na wizara ya mazingira ni zabuni ya kutafuta kampuni inayofikia mahitaji yanayotakikana ikiwemo viwango vya kimataifa na kibali cha usafirishaji wa wanyama.

Mwaka jana, nchi hiyo iliidhinisha uuzaji wa karibu wanyama 1,000 ambao walikuwa katika hatari ya kufa kwasababu ya ukosefu wa chakula.

Aidha, wanyama waliokuwa wanauzwa ni pamoja na tembo, nyati, twiga na pala lengo likiwa ni kupatikana kwa dola milioni 1.1 kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira.

Star TV
 
Back
Top Bottom