Tetesi: TCRA Wanaomiliki laini (simkadi) zaidi ya moja katika mtandao mmoja kupokonywa ifikapo June 2020

Hawa TCRA wamekua wasanii wasanii tu mimi mpaka leo sijasajili na bado nipo hewani kama kawa (hawajafunga) dogo walimfungia line zake baada ya muda akaziweka hewani zinapiga kazi kama kawaida (kuweka vocha kupiga simu na kujibu msg vyote vinafanyika)

kimsingi naweza kusema ni wazee wa kuzua taharuki tu ili wapate kiki hamna kazi wanafanya kama tu wameshidwa kuwathibiti wale wazee wa "ile hela tuma kwenye namba hii" sasa wataweza nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo hapo sasa
 
Unaandika tetesi wakati kanuni ziko wazi tangia mwezi wa 2 tarehe 7! Na usipoteshe eti watapokonywa ila sema utapaswa kuchagua ni lain hipi uitumie na nyingine uziache na pia unaruhusiwa kuwa na lain zaid ya moja ndani ya mtandao mmoja isipokuwa lazima uireport utaitumia kwa matumizi ya modem tu na si vinginevyo.
Soma boss
IMG-20200309-WA0013.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa TCRA wamekua wasanii wasanii tu mimi mpaka leo sijasajili na bado nipo hewani kama kawa (hawajafunga) dogo walimfungia line zake baada ya muda akaziweka hewani zinapiga kazi kama kawaida (kuweka vocha kupiga simu na kujibu msg vyote vinafanyika)

kimsingi naweza kusema ni wazee wa kuzua taharuki tu ili wapate kiki hamna kazi wanafanya kama tu wameshidwa kuwathibiti wale wazee wa "ile hela tuma kwenye namba hii" sasa wataweza nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona hao kila siku wanatuma SMS zao juzi wamenitumia, yaani ingekuwa kama Google na Yahoo mnawagomea ili wazitafune hizo line

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahili Jambo Mpaka Wangoje
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Aseme, Yaani Watuachie Laini Tutumie Muhimu Usajili Ukamilike
 
Wanaongeza usumbufu tu, kuna maana gani ya kusajili laini kwa vidole kama wanashindwa kuzifatilia mpaka waje kupangia watu idadi ya laini.
Kuna watu wana magari zaidi ya 50 yamefungwa GPS trackers, kuna watu wana security cameras zaidi ya 10 zimewekwa simcard, kuna watu wana mifumo ya alarm systems inayotumia simcard.

Wanakaa wana assume kila mwenye laini nyingi ni wale wa TUMA ELA HUKU, hata hilo tatizo walishindwa kulidhibiti wakaja na gia ya kusajili upya matatizo ya kuwa na watu wasiona tija kwenye nyazifa za kuteuana.

Ifike hao viongozi wa taasisi waombe hizo nafasi na wafanyiwe vetting, sio hawa wa kuteuliwa wanamawazo ya miaka 50 iliyopita.

Hapo wameona wenyewe wamefanya bonge la ubunifu kumbe hovyo kabisa.
 
Mkuu bora umemwambie wewe, Watu wamekuwa walalamishi mpaka inakera, anyway wengine wanajitetea kwa uhalifu wao waendeleee na Simu ya Mke na Mchepuko kivyake. Kwa wale Wafanyabiashara Rasmi upo utaratibu wa Simu za Kibiashara unapata mpaaka Laini 50 ktk mtandao mmoja. Sasa kama biashara yako hulipi kodi kazi kwako.
Mwanaume unamiliki laini za Simu kila mtandao kwani wewe Dalaliiii! Hizi dalili mbaya
Cheki hili liboya linawaza mapenzi tu

Yaani hicho ndicho umewaza mkuu?
 
Vip nawewe ni Kizazi malalamiko! Tafuta pessa mkuuu malalamiko hayana tijja. Ukiwa na pessa Laini moja tu ya Simu inakutosha huna hajja ya Haloteli umpigie kwa Halo, Voda kwa Voda nk. Ukiwa njema UNATWANGA KOTE KOTE KWA LAINI MOJA hayo mambo ya kuwa na Laini Kibao ni Ishara za Uwoga wa Maisha.
Hizi ndizo akili za TCRA!

No wonder!
 
Kusema ukweli kwa hili TCRA mnatuchanganya! Inaonesha hamjajipanga!
Usumbufu umekuwa mwingi mno!
  • Tulisajili kwa majina mara ya kwanza, mkasema ni batili mkasema zoezi lirudiwe,
  • Tukarudia tukasajili kwa vitambulisho vya kura, napo mkasema ni batili
  • Mkasema tukamilishe usajili kwa kupiga picha mwaka juzi tukafanya hivyo lakini bado ikawa ni batili;
  • Mwaka jana mkadai tusajili kwa vitambulisho vya NIDA kwa alama za vidole, tumefanya hivyo bado mnaona hiyo haitoshi!
  • Mnataka mwaka huu wenye laini zaidi ya moja kwenye mtandao mmoja muwazimie simu zao walizozisajili
TCRA kwa hili sasa sio ungwana kabisa! Naona kama ni usumbufu mnaofanya wala siyo weledi!

Kuna majibu mepesi eti; kwa wamiliki wanaohitaji laini zaidi ya moja watatakiwa kusaini fom maaalum;
Swali!
  1. Kama electronic data za vidole hamziamini mtu amiliki laini apendavyo, je hizo fomu maalum ndo zitaaminika?
  2. Hizo fomu zinawafikiaje wananchi huko vijijini?
  3. Kuna wafanya biashara ambao wana office zaidi ya moja ambazo zinahitaji namba za simu zaidi ya moja hilo hamjalifikilia?
TCRA mtatukosea sana
Ni walewale zama hizo ni za kujimwambafai ubabeubabe tuwajue wao ni nani, kuna bwana yule alisema usipoweka pasiwedi kwenye simu yako faini shs5!!?!?! Nilijikuta nakuwa mtuhumiwa kwa kosa la kununua simu isiyo na pasiwedi. Mzazi amemnunulia mwanae simu ambaye hajatimiza miaka 18 hivyo hawezi kupata kitambulisho, mzazi kasajili laini kwa jina lake eti ni kosa! Awamu hii tinapenda sana kuwatia hatiani watu wema.
 
Kusema ukweli kwa hili TCRA mnatuchanganya! Inaonesha hamjajipanga!
Usumbufu umekuwa mwingi mno!
  • Tulisajili kwa majina mara ya kwanza, mkasema ni batili mkasema zoezi lirudiwe,
  • Tukarudia tukasajili kwa vitambulisho vya kura, napo mkasema ni batili
  • Mkasema tukamilishe usajili kwa kupiga picha mwaka juzi tukafanya hivyo lakini bado ikawa ni batili;
  • Mwaka jana mkadai tusajili kwa vitambulisho vya NIDA kwa alama za vidole, tumefanya hivyo bado mnaona hiyo haitoshi!
  • Mnataka mwaka huu wenye laini zaidi ya moja kwenye mtandao mmoja muwazimie simu zao walizozisajili
TCRA kwa hili sasa sio ungwana kabisa! Naona kama ni usumbufu mnaofanya wala siyo weledi!

Kuna majibu mepesi eti; kwa wamiliki wanaohitaji laini zaidi ya moja watatakiwa kusaini fom maaalum;
Swali!
  1. Kama electronic data za vidole hamziamini mtu amiliki laini apendavyo, je hizo fomu maalum ndo zitaaminika?
  2. Hizo fomu zinawafikiaje wananchi huko vijijini?
  3. Kuna wafanya biashara ambao wana office zaidi ya moja ambazo zinahitaji namba za simu zaidi ya moja hilo hamjalifikilia?
TCRA mtatukosea sana
binafsi naona system zao zipo week, mbona benki ukienda ukitaka kufungua akaunti nyingine ya aina moja ukiweka kidole inakataa, inaonesha bio ilishachukuliw siku nyingi na akaunti yako wanakupa kama ulikuwa umesahau. sasa kwanini wao wasiweke huo mfumo kwamba ukiweka bio ionekane kuna namba tayari iliwahi kusajiliwa.
 
Kwani form kitu, tutaijaza tu, muhimu hiyo form ijazwe online ili kuondolea watu usumbufu wa foleni
 
Back
Top Bottom