Je, Wajua kumiliki laini ya simu zaidi ya moja ni kosa na adhabu ni kifungo zaidi ya mwaka mmoja jela?

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Huwa nawaambia kila siku kuwa jambo mpaka likukute ndo utajua kuwa lipo. Na nyote si mnajua kuwa kutokujua sheria sio kinga/hoja/udhuru. Hautafikishwa Mahakamani ukasema nilikuwa sijui, halipo hilo.

Kanuni ya 37 ya GN. No.60/2023 Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Kuhusu Usajili wa Laini za Simu inakataza mtu kumiliki laini ya simu zaidi ya moja kutoka mtandao mmoja kwa ajili ya matumizi ya kupiga, ujumbe na mtandao.

Kosa hili adhabu yake ni kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela au faini isiyopungua milioni tano au vyote kwa pamoja.

Kwa kipindi hiki tulichomo yawezekana kosa hili ni kati ya makosa yanayotendwa sana na wengi.

Kwa mujibu wa Sheria hii kampuni pekee ndo yenye uwezo wa kumiliki line za simu kufikia hadi 30. Mtu binafsi hata line mbili za mtandao mmoja ni kosa.

Hili sio kosa la madai ni jinai tuelewane hapa. Hili jambo ni serious. Wengi mnazo line hadi tano, ni basi tu siku yenu haijafika.

Nyongeza ya adhabu nilizotaja hapa juu, kanuni inasema pia ukikutwa na hatia utatakiwa kulipa Tsh 75,000/= kwa kila siku ambayo umemiliki hiyo Laini au kila siku ambayo umeitumia.

Kwahiyo upige hesabu kama umemiliki miaka 2 basi ni Tshs 75,000/= mara kila siku katika hiyo miaka 2. Sikwambiii kama unayo miaka 5 au zaidi.

Hii ni nyongeza ya zile adhabu za juu. Yaani baada ya kupewa zile adhabu za juu sasa unahesabiwa hizo siku ambazo umekaa nayo ili ulipe.

Incase mtu anakutafutia kosa hapa hawezi kukukosa.

Haya mambo yapo tukipata mda tuelezane tu kama hivi.

Andiko la Bashir Yakub, WAKILI. +255714047241
 
despicable-me-despicable-me-2-gru-despicable-me-wallpaper-preview.jpg
 
Acha kutisha watu kwann mitandao wanaruhusu uthibitishe if una laini zaid ya moja.....washitakiwe wana legalized hzo sim card to users...
 
Huwa nawaambia kila siku kuwa jambo mpaka likukute ndo utajua kuwa lipo. Na nyote si mnajua kuwa kutokujua sheria sio kinga/hoja/udhuru. Hautafikishwa Mahakamani ukasema nilikuwa sijui, halipo hilo.

Kanuni ya 37 ya GN. No.60/2023 Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Kuhusu Usajili wa Laini za Simu inakataza mtu kumiliki laini ya simu zaidi ya moja kutoka mtandao mmoja kwa ajili ya matumizi ya kupiga, ujumbe na mtandao.

Kosa hili adhabu yake ni kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela au faini isiyopungua milioni tano au vyote kwa pamoja.

Kwa kipindi hiki tulichomo yawezekana kosa hili ni kati ya makosa yanayotendwa sana na wengi.

Kwa mujibu wa Sheria hii kampuni pekee ndo yenye uwezo wa kumiliki line za simu kufikia hadi 30. Mtu binafsi hata line mbili za mtandao mmoja ni kosa.

Hili sio kosa la madai ni jinai tuelewane hapa. Hili jambo ni serious. Wengi mnazo line hadi tano, ni basi tu siku yenu haijafika.

Nyongeza ya adhabu nilizotaja hapa juu, kanuni inasema pia ukikutwa na hatia utatakiwa kulipa Tsh 75,000/= kwa kila siku ambayo umemiliki hiyo Laini au kila siku ambayo umeitumia.

Kwahiyo upige hesabu kama umemiliki miaka 2 basi ni Tshs 75,000/= mara kila siku katika hiyo miaka 2. Sikwambiii kama unayo miaka 5 au zaidi.

Hii ni nyongeza ya zile adhabu za juu. Yaani baada ya kupewa zile adhabu za juu sasa unahesabiwa hizo siku ambazo umekaa nayo ili ulipe.

Incase mtu anakutafutia kosa hapa hawezi kukukosa.

Haya mambo yapo tukipata mda tuelezane tu kama hivi.

Andiko la Bashir Yakub, WAKILI. +255714047241
Asante kwa angalizo, Msomi.
 
Back
Top Bottom