Vodacom yaongoza kwa Wateja wanaotumia huduma za kifedha. Akaunti zaidi ya milioni 9.2 zasajiliwa kwa Januari-Septemba 2023

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Ripoti iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (#TCRA) imeonesha Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom inaongoza kwa Wateja waliojisali na huduma ya kutumia fedha kwenye simu

Usajili wa Wateja wanaotumia fedha kwenye simu umeongezeka kutoka akaunti Milioni 47.3 zilizokuwepo mwishoni mwa Juni 2023 hadi akaunti Milioni 51.4 kufikia mwisho wa Septemba 2023 ikiwa ni ongezeko la 8.7%

Ripoti hiyo ya Takwimu za hadi Septemba 2023, imerejelea idadi ya laini zote za simu zilizosajiliwa na zinatumika ambazo zina akaunti za fedha zilizotumika walau mara moja katika miezi mitatu
IMG_7891.jpeg


Aidha, jumla ya akaunti 9,248,902 zimejisajili kutumia huduma za fedha kupitia simu kwa mitandao mbalimbali nchini kuanzia Januari hadi Septemba 2023

Akaunti chache zaidi zimejisajili katika kipindi cha Machi hadi Aprili 2023 ikiwa ni Akaunti 586,873 huku akaunti nyingi zikisajiliwa katika kipindi cha mwezi Mei hadi Juni 2023, ikiwa ni akaunti 1,494,335

Akaunti zilizojiunga na Huduma za Fedha kwa Simu

Januari - 42,120,445
Februari - 43,172,914
Machi - 44,353,568
Aprili - 44,940,441
Mei - 45,781,325
Juni - 47,275,660
Julai - 48,673,694
Agosti - 50,007,613
Septemba - 51,369,347

Lakini pia idadi ya miamala imeongezeka kwa miaka mitatu iliyopita kutoka bilioni 3.4 kwa mwaka 2020 hadi bilioni 4.2 mnamo mwaka 2022

1698253582545.png

1698253685334.png
 
Back
Top Bottom