Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
Kwa mujibu wa ripoti ya TCRA ya robo ya nne ya mwaka, hadi Desemba 2022 mitandao ya simu nchini ilikuwa imesajili jumla ya laini milioni 60.277.

Laini hizo ni sawa na ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa na zile milioni 58.1 waliokuwapo mwisho war obo ya tatu ya mwaka 2022 yaani Septemba.

Kati ya laini hizo, Vodacom ilikuwa na jumla ya laini milioni 18.18, Airtel 16.61 milioni, Tigo milioni 15.94, Halotel milioni 8.02 na TTCL ikiwa na laini 1.49 milioni huku Smile wakiwa na laini 15,547.

Hata hivyo, Februari 13, 2023, Serikali iliamua kuzifungia laini za simu zilizokuwa hazijahakikiwa ili kupunguza utapeli unaofanyika kwa njia ya simu.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye alinukuliwa akisema “Kumekuwa na utapeli mwingi kwa kutumia laini za simu, hatua ya awali ilikuwa ni usajili kwa alama za vidole na kila laini iliyokuwa imelengwa kusajiliwa ilisajiliwa,”

“Baadaye kampeni ya pamoja ya kuhakiki ilianzishwa na ilikubaliwa kuwa ambazo hazijahakikiwa zifungwe na 31 ilikuwa mwisho lakini tumeona tuongeze siku hadi Februari 13 mwaka huu”

Kwa kuongezea, Waziri Nape alisema kuwa lengo la uhakiki ni kuendelea kudhibiti utapeli unaofanywa kwa njia ya simu ambapo Februari 15, 2022 laini za simu 900,000 zisizo na uhakiki wa alama za vidole zilifungiwa.

Kuendelea kupokea jumbe za "Tuma kwa namba hii", "Umeshinda promosheni tupigie kwa namba..." au "Matangazo ya mjukuu wa babu" ina maana TCRA imeshindwa kudhibiti watu hawa?

Katika session iliyofanyika Club House Februari 24, 2023, Waziri Nape alipoulizwa kuhusu swala hili alisema kwamba watu wanapopokea jumbe hizo wanatakiwa kwenda kutoa taarifa polisi, polisi watenda TCRA NA TCRA watafanya tracking na mtu huyo atakamatwa.

Akiongeza kuwa changamoto iliyokuwepo mpaka kufikia maamuzi ya kufunga line ambazo hazijafanyiwa uhakiki wa usajili ni sababu mtu anayekamatwa line yake inakuwa imesajiliwa kwa taarifa za NIDA za mtu mwingine, kwa kuzufungia itasaidia kukamatwa kwa muhusika mwenye.

Akiendelea kusema kuwa changamoto iliyopo sasa, mtu akipokea jumbe hizo anaishia kunung'unika nyumbani kwakwe badala ya kwenda kuripoti polisi.
 
Sitetei utapeli ila utapeli kuisha ni Ngum sana mana unakuta mtu umeenda kusajili laini msajili anakuambia rudia kupiga dole gumba kama mara tano hivi kwa madai mashine mbovu kumbe anakufotolesha laini zingine kwa dole gumba lako na Wewe kubisha huwezi si ni msajili.

Sema Wamejitahidi Kudhibiti Kiaina
 
utapeli 2.jpg


Kuendelea kupokea jumbe Tuma kwa namba hii au matangazo ya mjukuu wa babu ina maanisha TCRA imeshindwa kudhibiti watu hawa?

utapeli.jpg


Januari 2023 TCRA ilitangaza kuzima huduma za mawasiliano ya laini zote ambazo hazijahakikiwa ambapo tarehe ya mwisho ilikuwa Februari 13, 2023, lengo likiwa ni kudhibiti matukio ya uhalifu ikiwemo utapeli wa "Ile hela tuma kwa namba hii," na Februari 15, 2022 laini za simu 900,000 zisizo na uhakiki wa alama za vidole zilifungiwa.

utapeli 1.jpg
 
Shida ni kwamba huwezi kumpeleka mtu mahakamani kwa kukutumia meseji ya hiyo pesa tuma namba flani, unadhibitisha vipi kama haukuwa sehemu unataka ufanyiwe delivery ya viatu na mnataka kulipana pesa..?
 
Back
Top Bottom