Kusema ukweli kwa hili TCRA mnatuchanganya! Inaonesha hamjajipanga!
Usumbufu umekuwa mwingi mno!
Kuna majibu mepesi eti; kwa wamiliki wanaohitaji laini zaidi ya moja watatakiwa kusaini fom maaalum;
Swali!
HIZO SIMU ZIMENI TU TUJUE MOJA SIYO KUTISHANA KILA SIKU NA HAMZIMI
Usumbufu umekuwa mwingi mno!
- Tulisajili kwa majina mara ya kwanza mwaka 2002~2005, mkasema ni batili mkasema zoezi lirudiwe,
- Tukarudia tukasajili kwa vitambulisho vya kura 2007~2009, napo mkasema ni batili
- Mkasema tukamilishe usajili kwa kupiga picha mwaka 2012~2014 tukafanya hivyo lakini bado ikawa ni batili tena;
- Mwaka 2018~19 mkadai tusajili kwa vitambulisho vya NIDA kwa alama za vidole, tumefanya hivyo bado mnaona hiyo haitoshi!
- Mwaka 2020 wenye laini zaidi ya moja kwenye mtandao mmoja mlitangaza kwamba mtawazimia simu zao walizozisajili
- Bado baadhivya simu ukipiga zinataka kukamilisha usajili sasa ni USAJILI GANI, yaani UHAKIKI GANI tena mnautaka mtu afanye kama siyo kusumbuana?
Kuna majibu mepesi eti; kwa wamiliki wanaohitaji laini zaidi ya moja watatakiwa kusaini fom maaalum;
Swali!
- Kama electronic data za vidole hamziamini mtu amiliki laini zaidi ya moja, je hizo fomu maalum ndo zitaaminika?
- Hizo fomu zinawafikiaje wananchi huko vijijini?
- Kuna wafanya biashara ambao wana office zaidi ya moja ambazo zinahitaji namba za simu zaidi ya moja hilo hamjalifikilia?
- ufanisi na mazingila ya rushwa katika maombi maalum ya simkad mbili mnayajua?
HIZO SIMU ZIMENI TU TUJUE MOJA SIYO KUTISHANA KILA SIKU NA HAMZIMI