Stahiki za Familia katika Simu/Laini ya Marehemu

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Unajua kuwa ndugu au jamaa yako akifariki una uwezo wa kupata taarifa zake na miamala yake? Jibu la swali hili linapatikana katika kanuni mpya za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (CRA) za mwaka 2023?

Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za 2023 (Usajili wa laini za simu) sasa zimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo la kuwawezesha Watanzania wengi kuzisoma na kuzielewa kwa urahisi ili kupata urithi wa kidiiatili wa marehemu wao.

Chini ya kanuni hizi ni rahisi kwa watu binafsi kupata udhibiti wa taarifa za kidijitali za jamaa zao waliofariki na kuzitumia kwa manufaa ya familia.

"Kanuni hizo ziliundwa kwa kuzingatia umuhimu wa urithi wa kidijitali wa watumiaji wa simu za mkononi na haja ya kulinda taarifa zao muhimu," alisema Kaimu mkuu wa mawasiliano na uhusiano kwa umma wa TCRA, Rolf Kibaja alipozungumza na Mwananchi.

Kibaja alisema ili kanuni hizo zifanye kazi na wahusika wanufaike ni lazima wawakilishi walioidhinishwa na wana-familia kufuata taratibu za kisheria ili kuhifadhi urithi wa kiditali wa watu waliofariki. Alisema mtumiaji wa simu ya mkononi anapofariki dunia, namba yake ya simu hurudishwa kwa kampuni husika ya mtandao wa simu.

"Hata hivyo, namba hiyo inaweza tu kupangiwa mtu mwingine iwapo msimamizi wa mirathi atashindwa kuwasilisha nyaraka muhimu zinazomtambulisha kuwa mwakilishi aliyeidhinishwa wa mirathi ya marehemu," alisema.

Alisema kifungu hicho kinalenga kuhakikisha kuwa laini ya simu ya mtumiaji aliyefariki haiharibiwi, iwe chini ya uangalizi wa msimamizi au kupitia mipango mingine iliyopangwa. Hata hivyo, alisema kuwa ni vema kuhifadhi taarifa za mtumiaji halisi.

"Ni muhimu kutambua kwamba laini ya simu iliyohamishwa inabaki na taar-ifa zinazohusiana na mmiliki halisi, hi inajumuisha kumbukumbu za kifedha, data binafsi zilizosajiliwa kwa njia ya kibayometriki," alisema na kuongeza:
"Hata ushahidi wa uhalifu ikiwa mtumiaji aliyefariki alihusika kati-ka vitendo hivyo unaweza kupatika-na, kwa hiyo lengo la uhamisho liko kwenye matumizi ya laini ya simu, wakati umiliki na faragha ya taarifa ya mtumiaji wa awali huhifadhiwa vizuri" alisema

Alisema kanuni hizo pia zinashughulikia mchakato wa kubadilisha jina la mtumiaji ikiwa jina la mteja limesajiliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Kitaifa (Nida), mabadiliko yoyote ya jina lazima yaripotiwe ili kuhakiki-sha uhifadhi sahihi wa kumbukumbu," alisema.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, laini za simu za mkononi zinazohusiana na majina yaliyobadilishwa zitahitaji usajili mpya, unaojumuisha uthibitishaii wa kibayometriki kupitia utambuzi wa alama za vidole. Akizungumzia alivyopokea kanuni hizo, mkazi wa Dares Salaam, Sarah Johnson alisema kanuni zimemrahisishia kuhifadhi ipasavyo urithi wa kidijitali wa baba yake.

Sambamba na miongozo hiyo, alisema aliwasilisha nyaraka muhimu kama msimamizi wa mirathi ili kuhakikisha kuwa laini ya simu ya marehemu baba yake inabaki chini ya udhibiti wao na kuwaruhusu kusimamia mambo yake kwa ufanisi.

"Ilitutufariji kujua kwamba taarifa zake binafsi zililindwa na tungeweza kupata data muhimu na anwani zinazohusiana na namba yake ya simu.Ninashukuru kwa dhamira ya TCRA ya kuhifadhi urithi wa kidijitali wa watu waliofariki na uelewa wao wa hali nyeti ya mchakato huu," alisema.

Kwa mujibu wa Kibaja, kwa kuele: wa na kufuata miongozo, watumial! na familia zao wanaweza kuhakikisha kwamba taarifa zao muhimu zinaende-lea kuwa salama na kufikiwa ndani ya vigezo vya sheria.

"Ahadi ya TCRA ya kulinda haki na faragha za watu binafsi inaendelea hata zaidi ya maisha yao, ikitoa mfumo mpana wa usimamizi
Imeandikwa kwenye gazeti la Mwananchi
 
Laini ya simu ambayo imesajiliwa na kuthibitishwa haipaswi kuwa allocated kwa mtu mwingine yeyote yule.

Nashangaa sana eti unakuta namba yako ambayo hujaitumia kwa muda fulani amepewa mteja mwingine. Hii si sawa.

Naweza nisitumie laini sasa lakni baada ya muda fulani nikaanza kuitumia kwa sababu tofauti.

Hivyo TCRA wahakikishe huu ufedhuri unaachwa.
 
Back
Top Bottom