Tetesi: TCRA Wanaomiliki laini (simkadi) zaidi ya moja katika mtandao mmoja kupokonywa ifikapo June 2020

Kusema ukweli kwa hili TCRA mnatuchanganya! Inaonesha hamjajipanga!
Usumbufu umekuwa mwingi mno!
  • Tulisajili kwa majina mara ya kwanza, mkasema ni batili mkasema zoezi lirudiwe,
  • Tukarudia tukasajili kwa vitambulisho vya kura, napo mkasema ni batili
  • Mkasema tukamilishe usajili kwa kupiga picha mwaka juzi tukafanya hivyo lakini bado ikawa ni batili;
  • Mwaka jana mkadai tusajili kwa vitambulisho vya NIDA kwa alama za vidole, tumefanya hivyo bado mnaona hiyo haitoshi!
  • Mnataka mwaka huu wenye laini zaidi ya moja kwenye mtandao mmoja muwazimie simu zao walizozisajili
TCRA kwa hili sasa sio ungwana kabisa! Naona kama ni usumbufu mnaofanya wala siyo weledi!

Kuna majibu mepesi eti; kwa wamiliki wanaohitaji laini zaidi ya moja watatakiwa kusaini fom maaalum;
Swali!
  1. Kama electronic data za vidole hamziamini mtu amiliki laini zaidi ya moja, je hizo fomu maalum ndo zitaaminika?
  2. Hizo fomu zinawafikiaje wananchi huko vijijini?
  3. Kuna wafanya biashara ambao wana office zaidi ya moja ambazo zinahitaji namba za simu zaidi ya moja hilo hamjalifikilia?
  4. ufanisi na mazingila ya rushwa katika maombi maalum ya simkad mbili mnayajua?
TCRA mtatukosea sana
Unachosema ni kweli wanataka kuleta mianya ya RUSHWA TU, hakuna lolote jipya. Tuliwaeleza kuwa watu wana matumizi mbalimbali na hizo laini, kwa mfano mimi nina laini mbili za Airtel, moja ni purely for my Laptop, haitumiki kwa jambi linguine lolote, ipo fulltime kwenye modem sasa mnataka kuifunga ili IWEJE? Nije kuwaomba omba hapo ofisini ili iweje, wacheni hizo. Laini nyingine ni fulltime kwenye simu. Hii ni hali kwa watumiaji wengi, siyo lazima wote tutumie simu all the time kwa mambo ya mitandao, wengine we enjoy using our PC s and computers kwa mambo ya mtandao via other separate SIM CARDS. TCRA acheni mambo hayo!
 
Hata nagat
Mkuu bora umemwambie wewe, Watu wamekuwa walalamishi mpaka inakera, anyway wengine wanajitetea kwa uhalifu wao waendeleee na Simu ya Mke na Mchepuko kivyake. Kwa wale Wafanyabiashara Rasmi upo utaratibu wa Simu za Kibiashara unapata mpaaka Laini 50 ktk mtandao mmoja. Sasa kama biashara yako hulipi kodi kazi kwako.
Mwanaume unamiliki laini za Simu kila mtandao kwani wewe Dalaliiii! Hizi dalili mbaya
Hata magari yanatumika kufanya uhalifu lakini mtu mmoja anamiliki magari 4 au 6 au zaidi kwa nini asibanwe, yote ya nini?.
Suala la uhalifu halianzii kwenye laini nyingi. Mtu anaweza kuwa na laini 10 lakini kama hakuna ushahidi wa yeye kuhusika kwenye uhalifu utamtuhumu vipi?
 
wameweka pamba masikioni; kwanza hata hayo ya kusema ukitaka ya pili ukawaombe, mbona sheria haiko wazi juu ya Hilo?
 
Mkuu bora umemwambie wewe, Watu wamekuwa walalamishi mpaka inakera, anyway wengine wanajitetea kwa uhalifu wao waendeleee na Simu ya Mke na Mchepuko kivyake. Kwa wale Wafanyabiashara Rasmi upo utaratibu wa Simu za Kibiashara unapata mpaaka Laini 50 ktk mtandao mmoja. Sasa kama biashara yako hulipi kodi kazi kwako.
Mwanaume unamiliki laini za Simu kila mtandao kwani wewe Dalaliiii! Hizi dalili mbaya
Huna akili
 
Hata nagat

Hata magari yanatumika kufanya uhalifu lakini mtu mmoja anamiliki magari 4 au 6 au zaidi kwa nini asibanwe, yote ya nini?.
Suala la uhalifu halianzii kwenye laini nyingi. Mtu anaweza kuwa na laini 10 lakini kama hakuna ushahidi wa yeye kuhusika kwenye uhalifu utamtuhumu vipi?
Tatizo uvivu wa kufikiri na uvivu wa ubunifu, wanataka watu watumie line za makampuni yao ili mengine yashindwe kujiendesha, mbona kila siku tunatapeliwa lakini hakuna chochote wanachofanya zaidi ya kupiga makele tu!
 
WANATISHIA KUZIMA WALA HAWAZIMI siku zitapita tena watakuja kutishia
 
Back
Top Bottom