TCRA angalieni sms za Biko, Tatu mzuka, Moja bet

TCRA angalieni sms za Biko, Tatu mzuka, Moja bet

Mimi ninavyojua hawawezi kukutumia meseji kama hujawahi cheza hata siku moja ukicheza wanajua wewe ni mteja kwahiyo wanakuhamasisha .
Kweli kabisa kama hujawahi kucheza huwezi kutumiwa msg
 
Hata kama uliwahi cheza lakin hakukuwa na sehemu ya vgezo na mashart kwamba tutatumiana message na pia unaweza cheza only tatumzuka lakn ukatumia message mpka na biko
 
Mimi ninavyojua hawawezi kukutumia meseji kama hujawahi cheza hata siku moja ukicheza wanajua wewe ni mteja kwahiyo wanakuhamasisha .
hiyo unavyojua ww na kujua kwako ww sio lazima iwe kweli,mm ninachokijua ni kwamba hawa wanaenda kwenye makampuni ya mitandao na kuwapa fungu ili wawatumie mesej wateja wao
 
Kwa mnaopokea mesage za TATU MZUKA NA BIKO na mnaona ni usumbufu Mnaonaje tujiunge tuwashtaki BIKO na TATU MZUKA kwa kusababisha usumbufu huo kwenye simu zetu, huu ni usumbufu mkubwa sana, kama promo wafanye kwenye mabango barabarani hawajatununulia simu wao, mwanasheria ajitokeze atupe mbinu za kwenda kuwashtaki ni kero sasa.
Nakuunga mkono mkuu. Kila wakati mtu unashika simu ukidhani kuna ujumbe wa maana kumbe ni hawa wapuuzi. Kwanini hizo msg hawatumiwi wale ambao wanacheza hizo kamari tuu? Yaani tunatumiwa wote wenye simu na line husika. aaargghhhhhhh
 
hiyo unavyojua ww na kujua kwako ww sio lazima iwe kweli,mm ninachokijua ni kwamba hawa wanaenda kwenye makampuni ya mitandao na kuwapa fungu ili wawatumie mesej wateja wao
Mimi sijawahi kucheza na nitatumiwa msg karibu 20 kila siku. Kosa langu hapo liko wapi jaman?
 
Na ule mtindo wa mtu unapigiwa af yanaanza matangazo gani cjuh..... Hv ukapata mwanasheria mzuri ukaenda kuwashtaki kwa kukypigia ukiwa na mkutano na wakubwa muda ambao hukutegemea kupokea simu yoyote ko wakafanya upoteze fedha kibao
Kwan wanasheria wao hawatumiwi hizo msg!
 
Wanakera sana hawa jamaa na sms zao. [emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Poleni sana wote.
Mm nimewahi kupiga simu huduma kwa wateja nikatoa malalamiko kuhusu hii kero ila nikajibiwa hovyo mpaka nikatamani kumtukana aliyekuwa ananijibu.
Kwa madai yake ni kuwa wao hawahusiki na hizo issue na nilipomsisitiza kuwa sijawahi kucheza na km anabisha aangalie rekodi zangu za miamala kama kuna hata moja imeenda kwenye kampuni ya kamari, sikupata mrejesho wa kuridhisha.
Nashukuru kwa sasa wameacha ila ni kero sana maana ilikuwa wananitumia ujumbe mpaka usiku mnene na wakati mwingine kupigiwa simu za hovyo za matangazo ya hadithi.
 
Rafiki, kesho ni siku yako kuitwa mvunja rekodi kwa kushinda Mil 150. Cheza utoke kimaisha huku TZ ikivuna Mil 200 za miradi ya jamii. Ukishinda TZ Inashinda
 
Back
Top Bottom