TCRA, Vodacom "Tusua Mapene" inawaibia watu

2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,700
4,616
Imekuwa ni kawaida ya makampuni ya simu kuanzisha promosheni au bahati nasibu na kuwatumia wateja wao sms za kuwataka waendelee kucheza michezo hiyo.

Kwa leo tuongelee kampuni ya Vodacom kupitia mchezo wao unaoitwa Tusua Mapene, ukitumia namba 15544. Huu mchezo umekuwa ukiwaibia wateja kwa kuwatumia SMS kila asubuni na jioni kwa SMS mbili zinazofuatana huku ukiambatana na makato ya tsh.300 pasipo ridhaa ya mtumiaji.

TCRA tunawaomba mfanye juu chini kuchunguza hii kadhia kwani huu ni unyonyaji mkubwa kwa wananchi.

Ikiwezekana msiishie hapo kwa Vodacom tu angalieni pia kampuni nyingine zinazojihusisha na promosheni kupitia simu maana wanatuma sms za promosheni hovyo na kuleta kero kwa wananchi.
 
Bora hiyo yako kuna siku utashinda tu.!

Vodacom wanatabia mbaya...
nikiongeza Salio kwa voda na ikatokea sijalitumia kwa kununua kifurushi,watatuma meseji kibao hadi Salio lote liishe...

Mbaya zaidi hayo 'mameseji' nilishayakataa hadi nikayaripoti vodashop

Yaani wamegeuka wakora kabisa.. tena meseji moja wanatuma zaidi ya mara3...ili tu wakombe salio
 
Ndicho kinacholalamikiwa, Makampuni yamekuwa na tabia hiyo hata kama hujashiriki promosheni zao kukata salio la mteja bila taarifa. Tunalalamika sana mpaka unajiuliza au TCRA nao wanachukua kamisheni?
 
  • Thanks
Reactions: sab
Ukweli mtupu huu ni ukiukwaji wa sheria zakimtandao , wapigwe faini
 
Kwel kabsa hawa majamaaa wamekuwa matapel Sana kama mtandao watigo wezi hatari Yani ukiacha credit Tu wanapita nayo shame on them
 
Kwel kabsa hawa majamaaa wamekuwa matapel Sana kama mtandao watigo wezi hatari Yani ukiacha credit Tu wanapita nayo shame on them
Hawa tupaze sauti zetu tu bila kuchoka wabadilike. Suala la kukata credit za mteja bila ridhaa yake ni wizi
 
Back
Top Bottom