Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,809
- 6,081
Mods naomba msiunganishe uzi huu mana na nyie mmekuwa kama mnahusika na mitandao kila tukiweka uzi wa aina hii mnafuta au kaunganisha na nyuzi za miaka sita nyuma.
Kiukweli upande wangu imegeuka kuwa kero kuwa mtumiaji wa mitandao hii ya simu.
Si voda;airtel;Halotel ama Tigo yote hali ni moja.
Kwa usumbufu ninaopata nimelazimika kuweka simu yangu silent ila nikiigusa lazima nikutane na sms zaidi ya kumi kutoka kampuni za kuchezesha kamari.
Yani Boompesa;Instamoja;Biko;Bikosports;Tatumzuka;supatano;sportpesa;Sokabet;Mkekabet;15577(muito);PesaniMpesa; Tigoapp;vodataarifa; Matapeli; mganga kutoka sumbawanga; Polisi(japo hii ni muhimu kwa sasa ila mara mbili au moja kwa mwezi sio kila siku na kila dakika kadhaa);Tigobima.....
Yani imekuwa ni bandika bndua kiasi kwamba naona simu imegeuka kuwa kero kwangu japo ni muhimu katika kizazi cha sasa.
Hebu fikiria unangojea simu ya muhimu mara inakupigia hii namba 2259... Inakutangazia miito ya simu.
Ama unasubiri text ya muhimu (hasa watongozaji) unajua umejibiwa kumbe ni Biko...
Kiukweli naona upande wangu kuna haja ya mimi kufika mbele ya vyombo vya Sharia kuishitaki mitandao hii hasa kwa kugawa namba zangu bila ridhaa yangu kwa kampuni zote hizo na pia inaniondolea usalama wa matumizi ya simu yangu.
Kwa nini nimeandika?
Jana nilisajili laini ya simu yani natoka tu kwa wakala zinaingia sms kama tano hivi, tatu kutoka kwa matapeli na mbili za BIKO.
Nilijiuliza inawezekanaje hii kitu yani hata vocha sijaweka tayar wanaanza kutuma je wahusika ni wafanyakazi ama?
vodacom na mitandao mingine mnakila sababu ya kuwajibishwa hapa