Meseji (SMS) za dawa za Kiganga: Je, hawa ni matapeli? TCRA mko wapi? Namba wanatoa wapi?

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Wakuu ni kama Mara 3 hivi napokea meseji kwenye simu yangu inayoelezea masuala ya dawa za kiganga hasa mambo ya "Ndagu" na zindiko la biashara.

Meseji ya kwanza nliyowahi kutumiwa ilikua inasema hivi:-

"Mjukuu wa KISIRE naona biashara ya mabasi sasa inatosha umeshanunua mabasi mengi, sasa uje tena sumbawanga nikupe dawa ya kusafisha nyota na ya ndagu Mimi ni babu yako wa Sumbawanga"

Leo nimetumiwa hii:-

" Ile Dawa Ya Kusafisha nyota Yako Nazindiko Lamalizako Tayali Nimekamilisha Mjuku Wang Uje Uchukue Nashukulu Pia Kama Ndagu Imeaza Kufanya Kazi"

Je hawa ni matapeli!!? Kwa anaejua suala hili atuambie.

TCRA na Serikali wanatulindaje wananchi? Kwanini namba zimesajiliwa na watu wanaendelea kufanya uhalifu huu?

Sampuli za SMS na namba kadhaa zinazotumiwa:

9968BABD-E9DA-4BBD-9936-542A9D16CF81.jpeg

A7E4D653-DF61-4F44-832F-A8ADF6C68AC1.jpeg

9C27263A-BF0F-41B4-9AD6-C05EBF8139E1.jpeg

A0255471-3ABA-4FA2-9EE9-C93E56690AD5.jpeg

0C588EC8-89D8-4E21-BD22-2E08FCE0253B.jpeg

E3A05491-076F-4A92-BE8A-973E64FE4D86.jpeg


Naandika kwa uchungu, hasira na mshangao mkubwa juu hizi kampuni za simu za mikononi na mamlaka inayosimamia huduma hizi kushindwa kupambanana changamoto ndogo ya matapeli.

Binafsi sijatapeliwa ila nimeshuhudia na kukutana na matukio mengi ya kiutapeli juu watu mbalimbali. Binafsi naona kama ujinga na kukosa weledi wa viongozi wanaoongoza kampuni na mamlaka hii ya TCRA.

Matapeli wanatamba na kujisifu kabisa waziwazi juu ya uharifu wa kuwatapeli watu, kwa juhudi zangu nimeripoti matukio mengi juu ujinga huu na uvunjaji wa sheria ila kila kukicha matukio haya yanatamalaki. Prof. Mbarawa jana nimeona Dodoma ukizindua kitabu swali langu kwako ni kuwa UMESHINDWA KUDHIBITI UTAPELI HUU?

MH. RAIS TUNAOMBA ANGAZIA MAMLAKA HII YA TCRA.

Habari zenu wakuu...

Kumekua na utapeli mwingi sana mitandaoni siku hizi ya mitandao ya simu ambapo unatumiwa message ikianza na maelezo kama "Hiyo hela tuma kwenye number........ " ikiendelea na maelezo mengi ya kuashiria kwamba huyo mtu yupo kwenye shida na anauhitaji wa hiyo fedha na atakueleza kuwa hiyo hela uitume kwenye number flani au njia nyingine yeyote

Njia zipo nyingi sana ila huo ni mfano tuu

KWANINI NIMEHISI MATAPELI HAO HUWA WANASHIRIKIANA NA WAFANYAKAZI WA MITANDAO HIYO???

Nimefuatilia hizi message kwa ukaribu sana na nikagundua kwamba mara nyingi hizo messages huwa znaingia kipindi ambacho nimefanya miamala mingi ya fedha au nimetuma message kuhusu miamala flani kama "nikutumie shilling ngapi??" au nimepokea message inayotaka nitume fedha hapo ndipo huwa hizo message zinaingiaga.

Kwahiyo kwa akili yangu nimefikiria na kugundua kwamba wanaohusika na hii michongo ni wafanyakazi wa hiyo mitandao maana hao pekee ndio wanaoweza kuona messages zetu, calls zetu na transactions zetu.

Hayo ni mawazo yangu, unaweza pia ongezea na mawazo yako maana wanaotapeliwa ni wengi.

View attachment 794486View attachment 794487View attachment 794488View attachment 794489

Kama ilivyo kawaida, wezi ni watu wenye IQ kubwa sana. Huwa wanatumia mwanya kidogo sana kufanikisha mambo yao.

Hivi karibuni kumekua na taarifa za kusajiri line za simu kwa njia ya 'FINGER PRINT'. Wezi nao hawako nyuma. Wameamua kutumua mwanya huu kama fursa kwao.

Wanachokifanya.

Wanakufuata wakiwa na sare pamoja na vitambulisho vya kufanya kazi kwenye mtandao husika.

Wanajitambulisha na kukwambia wao wanahusika na kusajiri line zote kwa kutumia alama za vidole.

Ukikubali kupata hiyo Huduma, wanakuambia utume namba zako za siri za mpesa, Tigo pesa au airtel money kwenda 100. Hapo wanakua na uhakika wa ile Meseji kurudi ikiwa na hizo namba zako za siri.

Hapo ndipo wanapoingia kwenye acc yako na kuhamisha pesa yote kama unayo.

Tukio hili limempata jamaa mmoja karibu na ninapoishi.

Hivyo tuwe makini sana na utapeli wa aina hii.

Naandika kwa uchungu, hasira na mshangao mkubwa juu hizi kampuni za simu za mikononi na mamlaka inayosimamia huduma hizi kushindwa kupambanana changamoto ndogo ya matapeli.

Binafsi sijatapeliwa ila nimeshuhudia na kukutana na matukio mengi ya kiutapeli juu watu mbalimbali. Binafsi naona kama ujinga na kukosa weledi wa viongozi wanaoongoza kampuni na mamlaka hii ya TCRA.

Matapeli wanatamba na kujisifu kabisa waziwazi juu ya uharifu wa kuwatapeli watu, kwa juhudi zangu nimeripoti matukio mengi juu ujinga huu na uvunjaji wa sheria ila kila kukicha matukio haya yanatamalaki. Prof. Mbarawa jana nimeona Dodoma ukizindua kitabu swali langu kwako ni kuwa UMESHINDWA KUDHIBITI UTAPELI HUU?

MH. RAIS TUNAOMBA ANGAZIA MAMLAKA HII YA TCRA.

Habari zenu wanaJF.
Kuna hii tabia imeibuka ya watu kutumiwa meseji na watu wanaojifanya kuwa ni waganga kwa lengo la kutapeli watu, kuna jamaa yangu mmoja siku moja akanidokeza kuwa ni baadhi ya wafanyakazi wa mitandao wanahusika kutoa namba zetu ila mm sikutilia sana maanani majibu hayo. Ila sasa nimeamini maneno ya yule mdau.

Jumatatu ya wiki iliyopita nilienda kwenye ofisi moja za mtandao (sitotaja jina) kwa ajiri ya kusajili namba ya simu ila baada ya siku mbili kabla sijampa namba mtu yeyote namba hiyo ndo nikaona sms ya mtu anayejifanya mganga akinitaja jina mpaka mahari nilipo. Hizi sms zimekuwa ni kero sana tena nyingi zinatoka kwa watumiaji wa 062..... Maana unaweza kutuma sms wakati kuna mtu yuko kwenye ndoa yake na mwenza wake ndo aliyeshika simu kwa muda huo akadhani kuwa anataka kurogwa. TCRA ingilieni swala hili na kamateni hawa watu haraka sana maana imekuwa kero sana. Asnteni

Amani ya Mola iwe juu yenu wanajamvi,Ni siku nyingine tena ikiwa inaishia katika mwezi huu wa 5.
Niende moja kwa moja kwenye mada husika,Katika siku za hv karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la hawa MATAPELI ambao mm nadiriki kuwaita WASHAMBA TENA WASHAMBA KWELI,ambao wamekuwa wakibuni namba za watu na kuwaandikia UJUMBE MFUPI (SmS) watu mbalimbali ambao hawawajui na kuwaambia kuhusu matangazo ya Waganga wa jadi "Wanaotoa Pete za bahati,kupandishwa vyeo kazini,Kuwavuta wapenzi na takataka nyinginezo.Pia wamekuwa wakituma msg kwa watu mbalimbali wakijifanya kuwapa taarifa kuwa " Wasitume ile hela kwenye namba flani bali watume katika namba wanayopewa katika Ujumbe mfupi (SmS) hizo.

Kinachonishangaza sana Mara zote napopokea msg hizo zinatoka katika namba za mtandao wa HALOTEL na mara chache sana huwa za mitandao mingine sasa najiuliza hv Haloteli hawana taarifa kuwa matapeli wengi wanatusumbua kwa namba za mtandao wao kiasi kwamba tunakosa imani na mtandao huu hasa tukianza kuamini kuwa huenda usajili wa line za Halotel unafanyika kimagumashi??Au ni kuwa Halotel hawajapata malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na matapeli hawa na usumbufu wanaotusababishia????
Kibaya zaidi ni kuwa matapeli hawa wana namba nyingi sana kiasi kwamba ni nadra sana kupokea msg kwa namba ileile kwa mara zaidi ya moja hivyo maana yake ni kuwa wana lundo la line hizo kiasi kwamba huwezi wablock hata kidogo maana wakikutumia tena hutumia namna tofauti.

Mwisho ningeomba tushee mbinu ya kuweza kuwakomesha watu hawa maana usumbufu wao kwa kweli umekubuhu,mm binafsi huwa nikipokea SMS zao basi huwa napoteza just kama dakika 20 HV za kukaa chini na kuwajibu SMS yao kwa kuwashukuru na kuwaomba maelekezo zaidi juu ya kile walichoniambia ila Kuanzia ile namba iliyoniyumia mpaka namna za ndani ya SMS hiyo kila moja huwa naitumia SMS 600 hadi 1200 ndani ya muda mfupi ili tu kumjazia inbox yake na kuwapa karaha ya kila muda kupokea SMS zangu na kweli huwa nawasumbua kwa zoezi hili.

Mwisho ni muda sasa wa hii mitandaokulifanyia kazi na kuwakomesha Hawa wapumbavu ili tupate ahueni.
Wassalam, sincerely,
Bachelor Sugu.
Sina hakika kama hili linatokea kwa mitandao mingine pia, maana kwangu binafsi na watu wangu wa karibu niliowasikia yanatokea kwenye line zao za Vodacom Tanzania pekee. Ninatumia line zote za mitandao inayotoa huduma hapa bara lakini sijaona kwa mtandao mwingine zaidi ya Vodacom. Awali ilianza ule utapeli wa mtu anapiga simu anatoa maelezo meengi then anakuelekeza namba za kubonyeza ili upewe "bonus" yako na ukifuata process husika unatuma pesa kwenye namba yake na kutapeliwa.

Wengi waliibiwa na malalamiko yakawa mengi sana zama za utapeli huu. Binafsi niliwahi kupigiwa simu na mtu wa namna hii na bahati nilikuwa nimeshasikia aina hii ya utapeli. Nikapiga simu Vodacom huduma kwa wateja na baadaye kutuma namba ya tapeli huyu kwenye ukurasa wa wao rasmi kwenye facebook na wakakiri kupokea namba hiyo. Nilitegemea baada ya taarifa hiyo (pamoja na malalamiko ya wengine) Vodacom wangechukua hatua japo kwa kutoa tahadhari kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na ujumbe mfupi kama vile watutangaziavyo bidhaa na huduma zao mpya kupitia njia hizo lakini wakawa kimya tu.

Hivi karibuni umeibuka tena aina mpya ya utapeli na tayari malalamiko ni mengi zaidi miongoni mwa wateja wa Vodacom. Kwenye huu utapeli ulioibuka inaingia meseji ikikutaka "ile pesa" itumwe kwenye namba utakayopewa na jina lililotumika katika kusajili namba husika. Muhusika hutoa himizo kwa mlengwa kwamba pesa hiyo itumwe haraka maana kwa wakati huo mhusika yupo kwa wakala akisubiri kuitoa. Japo kuna ulazima wa kila mtu kuwa makini na miamala ya kifedha kwenye mitandao lakini zipo hali za dharura na wakati mwingine harakati za kuokoa uhai ambazo huweza fanya mtu asipate muda wa kufanya ufuatiliaji na kutapeliwa kirahisi.

Kutokana na haya na malalamiko mengi kuelekezwa kwa Vodacom (japo huenda mitandao yote inatokea) wateja tunapata wasiwasi na mtandao huu kuwa kuna ushirikiano baina ya waajiriwa wao wasio waaminifu (ambao ni wengi) na wahalifu hawa wanaoibuka kila uchao. Inaweza kuja hoja kuwa wanabuni namba lakini bado tutahoji tena tangu mambo haya yaanze kukithiri na sisi wateja kulalamika kwa namna mbalimbali kwa kampuni, zimechukuliwa hatua gani zinazoonekana kuonesha nia ya kampuni kupunguza kama sio kukomesha kabisa tatizo hili.

Wengi tunafahamu zipo sheria zinazo adress makosa kama haya lakini tunaamini pia kuwa utekelezwaji wa sheria hizi unategemea kwa asilimia kubwa ushirikiano mkubwa wa watoa huduma hawa wa huduma za simu pamoja na wateja wao.

Habari zaidi, soma=>ONYO LA POLISI: Ujumbe wa simu kutumiwa fedha, kuwasiliana na mganga ama kushinda bahati nasibu
 
Kumekuwa na utapeli ambao mtu hutuma sms kujifanya kumsifia mganga wake wa kienyeji akishukuru kupata mari au kwa wanawake akisifiwa kuweka ndoa vizur mwanzo niliaanza kupata sms mimi nikajuwa aiza nimtu alikuwa akikosea sasa sms izo zimeanza kuingia kwenye simu ya mke wangu zikiwa na ulagai wamaswara ya ndoa je nawewe umesha pata sms kama hizo
06203887b632fe5c944f5134700e7b59.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie washatuma sana mojawapo ni hii

Sent from Ili iweje
 

Attachments

  • Screenshot_20170726-183156.png
    Screenshot_20170726-183156.png
    18.9 KB · Views: 312
Hivi kuna watu huwa wanawaamini hawa matapeli kweli?

Sent from Ili iweje
 

Attachments

  • Screenshot_20170809-191204.png
    Screenshot_20170809-191204.png
    12.1 KB · Views: 242
  • Screenshot_20170809-191135.png
    Screenshot_20170809-191135.png
    12.1 KB · Views: 223
Namba si wanakisia tu, alimradi mtu ana salio au mesej za bure utaipata tu
 
Wanatuma sana..walinitumia kwa mara ya kwanza nikawa sijajua kama ni magumashi kwakua simu yangu huwa inaguswa na vjana hapa home nikaona ngoja nimpigie kujua ni nani alikua anawasiliana nae..nikaona anaongea kama msukuma hv nikamwambia mwaweja lolo
 
3dacc7f0d771159bc5ef4fee3a4b86da.jpg

Hawa kichwani hakuna kitu wanatapeli ivi Je wangekua na akili kama Chenge naamini wangeuza nchi kabisa wakatokomea Duniani uko.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom