TCRA angalieni sms za Biko, Tatu mzuka, Moja bet

avalanche

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
227
250
Wadau,

Naomba kwa anayejua namna ya kusitisha hizi sms za BIKO maana zimekuwa kero nilicheza siku moja tu sijarudia tena lakini wao kila dakika wanakutumia txt. Mwenye kujua namna ya kuzisitisha msaada tafadhali.

-----

Jitu jeusi said,

Ningependa kuwakilisha kero inayo nikumba mimi pia hata watu wengi tu.

Haya makampuni ya michezo ya bahati nasibu kutuma SMS kila wakati pasipo option ya Usubscribe.

Mimi nimecheza mara moja tu, sasa kwann kila siku asubuhi, mchana, usiku mnanitumia SMS zenu..... kwani nimeji subsribe for news & updates?????.... hizi message zinaboa kweli kweli pia ni usumbufu kabisa.

Tena sikuhizi hadi wanakutaja jina kabisa.

OMBI KWA TCRA
Wekeni mikakati ambayo hawa makampuni waweke namba ya kutuma neno ONDOA ili waweze kujitoa na SMS za kinafiki

Pia kwanini wamtumia SMS pasipo makubaliano baina ya mteja?

Naimani maofisa wa TCRA mmeliona hili. Nawatakia utekelezaji mwema.

Nawasilisha tu maoni yangu.
 

Chifyono

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
924
1,000
Aiseeee
Nimechoka kila baada ya muda mfupi napata jumbe toka biko sport ikinikumbusha habari za betting
Huu ni usumbufu kwa watumiaji wa voda, najua hii itakuwa ni kero kwa wengi bila shaka, naomba njia naiepuka vipi

Halafu sijui wanatoa wapi idhini ya kuchukua namba zetu na kuanza kututumia ujumbe wa usumbufu muda wote
 

Kayoka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
1,890
2,000
Inakera sana kwa na sijui ni namna gani tutakuja!
Jumapili niliwapigia Vodacom kuwaeleza huu kero na ushenzi wa meseji kutoka kwa kampuni za kubashiri i.e BIKO, Tatu mzuka, mkekabet kuja kwa simu yangu nikaomba wanitoe kabisa na sitaki tena kutumiwa hizo jumbe, eti wakasema wao hawahusiki kwa chochote na kama kutoa niwapigie kampuni husika za kubashiri au niwapigie TCRA na kutoa malalamiko yangu.
 

City owl

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
1,976
2,000
Mwenyewe wanankera kinoma. Hii ni lawama ya moja kwa moja kwa mitandao ya simu Wanaouza uhuru na privacy yetu kwa faida zao binafsi.
 

zinginary

JF-Expert Member
Dec 18, 2015
2,412
2,000
Wazingua km hui

Je ulijua zawadi Kuu ya Tusua mapene imeongezeka?
Mwanzo ilikuwa 150,000,00 743539826. Leo ni 165,153,213 Tsh na inaongezeka kila siku.

Tena na hii


Mamilionea 7 kupatikana katika droo ya Leo!! Piga *150*00# kupata tiketi zaidi. Kila tiketi itaongeza kete zako kwenye droo ya Tsh. 165,153,213

Keroooooo kwelikweli
 

Wycliff_Lowassa

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
436
1,000

Mkuu Biko Wanakera Sio Siri Ila Assume Umeamka Asubuhi Unamkuta Sizonje amekutext kama Trump hapo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom