barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,405
- 29,811
Hawa jamaa HAWAWEZI kukutumia meseji kama haujawahi cheza bahati nasibu yao hata mara moja, kama ulicheza hata mara moja basi wewe ndo uliwapa "rasmi" ruhusa ya kukusumbua, nina uhakika kuna mahali sheria na masharti kuzingatiwa tuliingizwa kingi bila kujijua.Kwa mnaopokea mesage za TATU MZUKA NA BIKO na mnaona ni usumbufu Mnaonaje tujiunge tuwashtaki BIKO na TATU MZUKA kwa kusababisha usumbufu huo kwenye simu zetu, huu ni usumbufu mkubwa sana, kama promo wafanye kwenye mabango barabarani hawajatununulia simu wao, mwanasheria ajitokeze atupe mbinu za kwenda kuwashtaki ni kero sasa.
Mimi biko nilijaribu mara moja, mpaka leo ni usumbufu ila kabla ya hapo sikuwa nikipata meseji zao.
Ila labda kuna gepu mahali la 'kuwakamata'.