TCRA angalieni sms za Biko, Tatu mzuka, Moja bet

TCRA angalieni sms za Biko, Tatu mzuka, Moja bet

[emoji625] Tumerudi hewani Karibu Jamvini,bet na Biko Sports ujishindie mshiko na safari ya kushuhudia el classico,jamvi la leo lina deportivo vs las palmas na Girona vs Levante,ingia www.bikosports.co.tz

[emoji753] Chelsea vs Everton, Tottenham Vs West Ham United, Getafe Vs Alavase. Odds Tamu Kulikoni www.bikosports.co.tz
Cheza Tusepe Spain

TusepeSpain kuangalia Live El-Classico Desemba 20. Kila ubashiri unakupa nafasi 1 ya droo. LEO Sociedad-Espan(3usiku),Depor-Girona(4 usiku) www.bikosports.co.tz


KERO KERO KERO
These guys have been flooding my Inbox with these nonsence, its kinda emberassing too much
 
Mm huwa nashangaa pale mshindi wa biko anapopigiwa sim kuwa ameshinda milioni hamsini,hashtuki na furaha kama kalazimishwa.

Promo wanayopiga ni hatari.
Hahahaha wizi wa Waziwazi tu.... Keshapangwa zaman tu
 
Aiseeee
Nimechoka kila baada ya muda mfupi napata jumbe toka biko sport ikinikumbusha habari za betting
Huu ni usumbufu kwa watumiaji wa voda, najua hii itakuwa ni kero kwa wengi bila shaka, naomba njia naiepuka vipi

Halafu sijui wanatoa wapi idhini ya kuchukua namba zetu na kuanza kututumia ujumbe wa usumbufu muda wote
Wanapewa na kampuni husika ya simu
 
Jamani...Habarini!

Ni kweli ni kama nimejitakia ila sikujua kama itakuwa usumbufu hivi...
Niliwahi kushiriki mara mbili Biko na mara Tatu kwenye Tatu mzuka ila sikufanikiwa. Sasa toka hapo nikawa sihitaji tena kucheza hii michezo. Kwa sasa naona jumbe zao kama zimekuwa kero kwangu maana wananitumia sana nami sina haja nazo kwa sasa.

Je, nawezaje kujitoa ili nisipate hizo meseji zao?

maana sizihitaji kwa sasa, kwa anayejua namna ya kujitoa naomba aandike hapa anisaidie .
kwa asiyejua namna ya kujitoa naomba asiandike asome tu!
Asante.
 
Kama hutaki usumbufu wa hizo meseji zima simu.
 
Mnaonaje tujiunge tuwashtaki BIKO na TATU MZUKA kwakutuma mesage zenye usumbufu mkubwa sana, hatujawaomba watutumie mesage ya promo, mwanasheria ajitokeze atupe mbinu za kwenda kuwashtaki ni kero sasa
 
Kwa mnaopokea mesage za TATU MZUKA NA BIKO na mnaona ni usumbufu Mnaonaje tujiunge tuwashtaki BIKO na TATU MZUKA kwa kusababisha usumbufu huo kwenye simu zetu, huu ni usumbufu mkubwa sana, kama promo wafanye kwenye mabango barabarani hawajatununulia simu wao, mwanasheria ajitokeze atupe mbinu za kwenda kuwashtaki ni kero sasa.
 
Mnaonaje tujiunge tuwashtaki BIKO na TATU MZUKA kwakutuma mesage zenye usumbufu mkubwa sana, hatujawaomba watutumie mesage ya promo, mwanasheria ajitokeze atupe mbinu za kwenda kuwashtaki ni kero sasa
Ni kweli. Kama ni tatizo kwa wengi itahitaji liangaliwe kwa mapana zaidi.
 
yaan tuwapeleke tu kotini,ngoja nimtafute kibatala maana ndo kiboko yao hawa
 
Aisee KERO HIYO NI KUBWA MNO. Tatumzuka wananikera sana wananiandikia msg za kipuuzi eti "tunajua umekwama huna hela ya kodi, cheza leo upate milioni 6.... Hawa jamaa tutawablock vp? Au niende TCRA?
 
Na ule mtindo wa mtu unapigiwa af yanaanza matangazo gani cjuh..... Hv ukapata mwanasheria mzuri ukaenda kuwashtaki kwa kukypigia ukiwa na mkutano na wakubwa muda ambao hukutegemea kupokea simu yoyote ko wakafanya upoteze fedha kibao
 
Back
Top Bottom