Sikutaka kuchangia hapa na pia nimizima TBC na kuangalia stationa zingine, ila wewe umenifanya nichangie.
Kwanza naona mkutano wa ccm wala si wa ki serikali. Uwanja una sare za ccm ambao huenda mikutanoni kwa malipo na mujibu wa mila za ccm.
Ninathibitisha kwamba seriakli ya ccm haitafanya mkakati wowote wenye lengo halisi la kufuta ujinga Tanzania kwa sababu ujinga huo ndio mtaji wa umangimeza wa ccm.
Ninawasi wasi kama ccm itaendelea, tunakoelekea hakutakuwa na haja ya mahakama. Kesi zote zitahukumiwa kwenye mikutano ya hadhara kwa kura za ndiyo ama hapana.
Hainiingii akilini mwigulu kwenda kuzungumza habari ya deni la taifa kwenye mkutano uliojaa watu mbumbubu wasiojua masuala ya uchumi wala takwimu za maendeleo na matumizi ya fedha serikalini. Anaacha kuongea na wasomi wanaohoji kitaalamu ongezeko la deni la taifa kwa kuwianisha kiwango na ukusanyaji mapato na gharama investment zilizofanyika, anakimbilia kwa watu wasio na ufahamu ili awashindilie kwamba wamekopa kujenga UDOM na barabara bila takwimu. Upumbavu kweli kweli.
Habari za Katiba, kama ana justifications za msimamo wa chama chake, na kweli ni mwanamme, aseme kwenye forums za wasomi wanaoelewa pamoja na tume iliyotayarisha hiyo rasimu awakosoe kwamba wamekosea. Siyo kuwakimbia wasomi, na kwenda kuwarubuni watu wasio na utaalamu wa uandishi wa katiba ili apate moral support kwa kuwa mbumbumbu ni wengi.
Ninafikiri sasa wale Waombaji, ni muda sahihi wa kubadili maombi na namna ya kuyafanya. Hatuwezi kudumu katika utumwa wa ukoloni wa ccm wasiojali tena elimu wala maslahi ya wa Tanzania. Unafiki na hila , manipulation na uvunjaji wa sheria na haki za binadamu pasipo kuwa na chembe ya dhamira ya uwajibikaji wala kuleta mabadililko halisi kwa maisha ya MTanzania. Now it is more than enough!.
Watu wengi waliokuwepo kwenye mkutano huo wamebebwa kwa mabasi na wengi wamevalishwa matisheti, makanga, vikofia na nembo za CCM. Wengi ni wasiojitambua, lakini wapo wengi pia ambao wameenda kuwashangaa akina MWIGULU wakitoa mapofu yao ya kinafiki.