TBC LIVE: Matangazo ya moja kwa moja ya CCM Mwanza

TBC LIVE: Matangazo ya moja kwa moja ya CCM Mwanza

Mwigulu ni kiongozi wa kutumainiwa, Akisimama kuongea hataki porojo, hotuba zake zinagusa maisha halisi ya mtanzania.

Tunawashukuru watu wa Mwanza kwa kumpa ushirikiano mkubwa!

Anatumainiea nawew msukule wake tu nadi
 
Dah! Yaani Mwigulu Amehutubia As If Ni Mpinzani Au Hayupo Serikalini Maana Mda Wote Analaumu Ubadhilifu Na Matumizi Mabaya Ya Ofisi,
Mimi Nafikiri Angesema Tumefanya Hili Na Hili Kukomesha Haya.
Yeye Mwenye Panga Analalamika Na Sisi Tufanyeje?
 
mwigulu ni kiongozi wa kutumainiwa, akisimama kuongea hataki porojo, hotuba zake zinagusa maisha halisi ya mtanzania.

Tunawashukuru watu wa mwanza kwa kumpa ushirikiano mkubwa!

ama kweli kupenda ugonjwa hata chongo utaita kengeza
 
Huu ukimya unanipa maswali,au wahudhuriaji ni wageni mjini walipigwa butwaa wameshangaa magorofa ya Mwanza au uchovu wa safari?
Maana kuna gari ya coca scania lori imepita punde Mkuyuni imebeba watu wamevaa nguo za Brazil!Mhhhh
 
mkuu hao wamesombwa kwa malori, hivo ni wageni hapo wanashangaa mabugando, kwikwii..
 
TBC wamejidhalilisha sana! Mara mia wangekuwa wanaonyesha ziara ya JK kule kusini labda ingewajenga kidogo...
 
wapendwa wakuu wana JF,
Naona ni wakati mwafaka sasa kwa vyama vya siasa hasa watani zangu CCM wanapompa mtu cheo wamempeleke hata semina ya wiki moja ya kujifunza How to make speech. Watu wengi wanafikiri kutoa hotuba hahitaji taaluma na ndilo kosa kubwa sana linalofanywa na vyama na wanasiasa. Kuhutubia kunahiaji mtu anaehutubia azingatie mambo muhimu baadhi kama yafuatayo;-
1.kuhakikisha watu anaowahutubia wanamuelewa kwa kutumia lugha rahisi na kuepuka mafumbo ambayo yatamfanya mtu atafakari badala ya kusikiliza.
2.kuzungumza kitu ambacho wanaomsikiliza wanakipenda na kukifurahia..Hili jambo ni mhimu sana na unaweza kulifanyia tathimini kwa kuangalia nyuso zao unapohutubia( SPOT DYGNOSISS)

3.Kujua matatizo halisi ya watu unaowahutubia na wanachotegemea kusikia kutoka kwako.
Naomba niishie hapo anayetaka taaluma nii kwa kirefu anipm. Nimeguswa kuandika haya yote kutokana na mkubwa mmoja leo hii kuwa anatoa hotuba yake ambayo imerushwa moja kwa moja na baadhi ya vyombo vya habari. Kwa kweli ilikuwa ni aibu kubwa sana leo. Mtu anafikia kuhamashisha kwa kusema TANZANIA HOYEE lakini hakuna jibu kwa anaohutubia na yeye anaendelea na topic hiyo....!!!! Lo aibu sana.
 
Umalaya wa kisiasa ni hatari sana... Misamaha ipi iliyofutwa? unafahamu kuwa mpaka sasa Mgodi wa Mwadui hawalipi hata sent moja mpaka 2018? unafahamu kuwa Wafanyakazi wa Tanzania wanatozwa kodi kubwa na baada ya hapo kila manunuzi wanayofanya wanaendelea kulipa kodi?... Wanamwanza si wajinga! Wanajua pumba na mchele....
Ukiona kobe kainama,ujue anatunga sheria.Wanamwanza wamekaa kimya wanatafakari majibu wanayo wenyewe,kama wanatubu vile?kama wanajuta vile?kama wanasikitika vile?kama yamewaingia vile?kama hotuba imewagusa vile? Kweli wako njiapanda maana waliipenda zaidi Chadema nayo ikamtema Zito kukiwa na hoja ya kikabila na ufisadi?CCM nayo tuhuma za ufisadi!
Wako Njiapanda,"kimya kingi kina mshindo mkubwa”
Kwa leo ......................hamna mwenye jibu!
KOBE AKIAMKA...........
-Ila jamaa lizalendo maana hata Bajeti yao aliwabana wabunge mpaka misamaha ikafutwa!
 
Wana jf
Kama mnavyofahamu leo mwigulu alikuwa na mkutano hapa jiji mwanza.
Cha kushangaza sikuona shamla shamla za vijana mtaani kama ilivyo kawaida kwa vijana wa mwanza kwani katika mikutano ya chadema hata inayroandaliwa na mbunge shamla shamla uoneka mapema.
Baada ya mvua kukata mida kama ya saa 11.30 hivi vijana wawi ( mmoja wa kiume mwingine wa kike) walionekana wakiwa wamevalia sare za ccm na ilionekana wamechoka dhahili walitokea mkutano.. Cha kushangaza wamekutana na zomea zomea mtaa wa liberty.. Wengi wakisema haoooo haooo wametoka magu kwa gari sasa wamerudi kwa mguu.. Mtaa mzima kila wakipita ni kuzomewa huku mjini sikuona kijani nyingine tofauti na hizo mbili nikajiuliza walio kuwa mkutanoni walitoka mwanza ipiii.!??
 
Tokalini Vampire muuaji akawa na maneno mazuri kwa wanaadamu? RIP Dr. Mvungi, Mbwambo na wengine wengi waliokatishwa maisha ...Hakika damu zao zitamsulubu hili gaidi lenye mhemko wa kutoa roho za raia wasiokuwa na hatia....
 
wapendwa wakuu wana JF,
Naona ni wakati mwafaka sasa kwa vyama vya siasa hasa watani zangu CCM wanapompa mtu cheo wamempeleke hata semina ya wiki moja ya kujifunza How to make speech. Watu wengi wanafikiri kutoa hotuba hahitaji taaluma na ndilo kosa kubwa sana linalofanywa na vyama na wanasiasa. Kuhutubia kunahiaji mtu anaehutubia azingatie mambo muhimu baadhi kama yafuatayo;-
1.kuhakikisha watu anaowahutubia wanamuelewa kwa kutumia lugha rahisi na kuepuka mafumbo ambayo yatamfanya mtu atafakari badala ya kusikiliza.
2.kuzungumza kitu ambacho wanaomsikiliza wanakipenda na kukifurahia..Hili jambo ni mhimu sana na unaweza kulifanyia tathimini kwa kuangalia nyuso zao unapohutubia( SPOT DYGNOSISS)

3.Kujua matatizo halisi ya watu unaowahutubia na wanachotegemea kusikia kutoka kwako.
Naomba niishie hapo anayetaka taaluma nii kwa kirefu anipm. Nimeguswa kuandika haya yote kutokana na mkubwa mmoja leo hii kuwa anatoa hotuba yake ambayo imerushwa moja kwa moja na baadhi ya vyombo vya habari. Kwa kweli ilikuwa ni aibu kubwa sana leo. Mtu anafikia kuhamashisha kwa kusema TANZANIA HOYEE lakini hakuna jibu kwa anaohutubia na yeye anaendelea na topic hiyo....!!!! Lo aibu sana.

kwi kwi kwi! mwigulu huyooooooooooooooo
 
Back
Top Bottom