Tazama jua lilivyo surface yake kwa karibu

Tazama jua lilivyo surface yake kwa karibu

mkuu kumbuka kuwa galaxy ni mkusanyiko wa nyota milioni kadhaa na sayari za kila nyota, gases and other objects. Jua letu ni nyota. Na kutoka nyota hadi nyota nyingine kipimo chake ni spidi ya mwanga. sisi hapa tulipo tupo kwenye galaxy inaitwa milky way, kwahiyo unapoongelea joto nadhani katika galaxy ni kila nyota ina joto lake lakini nyota kama jua letu ni nyuzi 5500, na kila sayari joto lake linategemea umbali wake kutoka kwenye jua lake, zingine ni barafu tu kama pluto, majua mengine i hope ni zaidi ya au kidogo.
Ila jua letu linazeeka na kufa kwake ni kubasti. Mwisho wa maisha maana uhai wa viumbe hai na sola system yetu unategemea jua na activity zake.

Kufika kwenye galaxy nyingine nadhani bado sana, nadhani wanasayansi wamefaniki wa kupeleka chombo hadi sayari ya mwisho kwa jua letu, bado hata hatujafikisha chombo chetu kwenye sayari za jua lingine jirani. Ila camera ziko poweful kuona yote hayo yanayosemwa na wanasayansi, kilasiku kuna uvumbuzi wa mambo mapya.

Mwanga kutoka juani kutufikia hapa duniani inachukua dakika nane mfano jua lingezima gafla ingekuchua dakika nane kujua hakuna mwanga na kuanza kusikia baridi.
Pia ukumbuke kuwa mwaga unasafiri kwa spidi ya kilomita laki 3 kwa sekunde.

Kutoka jua letu mpaka jua lingine kwenye galaxy yetu, umbali wake unapimwa kwa spidi ya mwanga. kama ulivyoona mwanga unatufikia baada ya dakika 8 kutoaka jua letu, ila kwa jua lingine lilio karibu ya sola sysytem yetu mwanga wake unatufikia baada ya miaka 4!

Kuna nyota tunaziona angani usiku zingine zimesha kufa ila mwanga wake ulikua haujafika maana zingine mwanga wake unachukua miaka milioni kadhaa kutufikia...haya wakuu.
Tunahitaji sana watu kama nyie hapa Jamii forum. Majibu mazuri bila kudharau swali lolote la mtu. Hakika watu tupo tofauti.
 
Acha mbwembwe, kupata picha ya surface ya jua usiihusishe na dini hata kidogo, acha sayansi ifanye kazi zake.
Haya ndo walikua wanasema kabla ya ndege kutengenezwa, ati binadamu hatukuumbwa kupaa angani, leo hii kimya. Wewe unakuja na yako

Sawa mkuu,kwaiyo hao wana sayansi ndo wameunda ilo jua na mwezi wanavyovifanyia uchunguzi Mara kwa mara
 
Sawa mkuu,kwaiyo hao wana sayansi ndo wameunda ilo jua na mwezi wanavyovifanyia uchunguzi Mara kwa mara

Hehe mwanasayansi hajaumba jua wala mwezi lakini anajua kuvielezea vizuri sana jinsi vinavyotokea, tunajua vizuri jinsi jua linavyotengenezwa na hata ukitaka tunaweza kukutengenezea version ndogo kabisa laboratory.

Kukimbilia dini kwa kila phenomena ambayo huwezi kuielezea ni ignorance, curiosity ndicho kitu ambacho kimefanya leo hii unatumia internet, ingekua aliyegundua umeme angesema electrons hatuwezi kuzielezea tumwachie Mungu leo hii hata umeme tungekua hatuna.

Kwa hiyo somo la leo, kama una imani shika imani yako lakini isikugeuze kua mjinga au mtumwa, itumie tu kukufariji lakini sio kuondoa maswali
 
mwezi upo kilomita laki 3.8 kutoka hapa tulipo, jua lipo kilomita milioni 149.6, Kwenye mwezi joto ni nyuzi 100 mchana usiku ni baridi sana nyuzi negative 177 centigrade. joto kwenye jua inakisiwa ni nyuzi 5500. Kwenda kwenye mwezi unahitaji mavazi maalumu kujilinda na joto na kemikali zilizopo katika anga ya mwezi. Kwenda juani sidhani kama plan ipo ila kuna vifaa spesho vina zunguuka angani kulichunguza maendeleo yake. jua lina kadiriwa kuwa na umri wa miaka bilion 4.5 hata mwezi pia.
nakumbuka wakati nasoma tuliambiwa kila sayari ina mwezi wake'moon' mfano jupiter ina miezi zaidi ya tisa kama sikosei,je ni sahihi?
 
ni kweli jua kwa silimia zaidi ya 96 ni gesi ya hydrogen na helium, inakisiwa madini ambayo ni magumu tangible kama graphite, gold nk...ni asilimia 3 naa. Pia zipo gesi/hewa nyingine kadhaa kama oxygen ila ni chini ya asilimia 1
kama jua asilimia kubwa ni gesi,mbona haitawanyiki?
 
Mkuu Dabo, ardhi ya mwezi imegawanyika katika sehemu zifuatazo. vumbi kama majivu hivi /ashes lilitokana na milipuko ya volcano, mawe ya yaliyotokana milipuko volcano, mawe na vumbi linalotokana na kuangukiwa na vimwondo/ comets ambazo zinasababisha mashimo makubwa/ craters mojawapo linaweza kufikia upana wa kilomita elf 2 naa. Nadhani huwa unaviona vimwondo usiku, kunajiwe moja lipo mbozi lanamna hiyo au ukija coco beach wanapouza mihogo utaona yale mawe ukingoni utadhani chuma,

Kutokana na anga la dunia vimwondo vikiingia huwa vinaungua na kuyeyuka, ila mwezi hauna anga kwahiyo huwa vinaanguka kwenye arhi yake na kusababisha yale mashimo au craters kitaalamu. yapo maeneo yanayopata hicho kibano kwa sana na mengine hapana yapo smooth. pia volcano zimesababisha kuna milima na mabonde.

kwenye mwezi hakuna viumbe hai au bado havijagundulika ila wanahisi kuna maji na wanaendelea na uchunguzi..ila hakuna mazingira ya kuishi banaadamu.

Sura ya ardhi ya mwezini kwa karibu
Moon-Jan-2010-sharp-1024x680.jpg

moon_mare-imbrium-inc-sinus-iridum-mar15.jpg

moon_20150303_2039_20_sTycho1.jpg

10075965.jpg

Hapa ni kipindi wamarekani walipotembelea mwezini

10075965.jpg

DirectFromTheMoon1-tp_jpg_610x343_crop_upscale_q85.jpg

Tazama dunia inavyoonekana katika uso wa mwezi....its amzing!

earthrise_strip.jpg

bluemarble_apollo17_strip.jpg

ukiwa out of space hivi ndio unaiona dunia...sayari ya bluu
hivi ni kwa umbali gani unaweza kuiona dunia nzima ukiwa angani?
 
ASANTE. NA WANAVOSEMA BINADAMU AKILUSHA HATUA MOJA KWENYE MWENZI INAMPELEKA
UMBALI MREFU KULIKO KAWAIDA NI KWELI?
nikweli mkuu, nikupe mfano ukirusha kitu juu huwa kinarudi chini kwa spidi mfano embe invyo dondoka mtini, hiyo ni gravitation force....ila kule mwezini ukirusha kitu kitaelea kama vile unyoya unavyouona hapa duniani. kitendo hicho ndio kinasababisha ukitumia nguvu kupiga hatua unaweza pelekwa mbali kwasababu kule unaelea kama nyoya la kuku hapa duniani
 
Huwa napata shida watu wanapotumia science ku-prove mambo ya imani. Kama kusema, kwa kuwa jua lina joto kali sana na kuna Jehanam yenye joto kali sana, basi kwa kuwa Jehanam kuna viumbe wanaishi inawezekana kwenye jua nako kuna viumbe wanaishi. Au kusema; kwa kuwa Joshua aliomba na kusimamisha jua basi ni jua ndilo huzunguka dunia.

Mawazo finyu kama haya ndio yalimpa Galileo Galilei shida kubwa na kanisa Katoliki enzi za uhai wake na kumletea kifungo na matisho ya kuuawa toka kwa Papa Urban VIII na makadinali wengine enzi hizo.

Ikiwa sayansi itasupport imani au imani kusupport sayansi well and good, but this not the case all the time. Sababu ni moja tu kubwa! Huyo aliyeunda nature, hafungwi na kanuni za nature. Naturally binadamu hawezi kupaa mawinguni. Hebu nenda eneo la wazi na jaribu kujinyanyua kwenda juu!! Ni kanuni za nature; ila imani inasema Yesu alipaa mawinguni. Binadamu huwezi kutembea kwa miguu yako kawaida juu ya maji, ila kwenye imani kuna aliyetembea juu ya maji!! Ukisikiliza visa na Hadithi za kiimani za Mitume na Manabii ndio utachanganyikiwa kanisa.

Haijalishi jua lilisimama au dunia ilisimama, ila nuru ya jua ilibakia hadi Israel aliposhinda vita(hilo ndio la muhimu).

Bado science italeta mengi ya kushangaza. Wengine wataleta maswali kama; Is Black Hole black? How big is our black hole? Au, mwezi huzunguka dunia, dunia huzunguka jua, jua kwa mamilioni huzunguka black hole at the centre of the galaxy; sasa vipi kuhusu mizunguko wa galaxies zenyewe? Black hole yetu wenyewe(The Milky Way's Black hole) ni fumbo kubwa bado kwa wanasayansi wenyewe!!

Sayansi ipo na muhimu(in fact ni ya lazima) kwenye maisha ya mtu; ila iimarishe imani yako kwa Mungu.
 
kama jua asilimia kubwa ni gesi,mbona haitawanyiki?

Mkuu, wataalamu wanasema jua litatawanyika baada ya miaka bilioni 5, kumbuka kwamba lilizaliwa napia litakufa....
invyosemwa mwanzo wake ni mkusanyiko ulivyo kama uonavyo kimbunga kinavyoanzaga hapa duniani, na kadiri ile spidi ya kujizungusha inavyoendelea inasababisha liwe la duara....na katikati yake kuwepo kiini cha huo mduara ambacho ndio husababisha liendelee kuwepo.....kuna process inaitwa nuclear fusion ndio inayotoa au nikama inatengeneza chakula cha jua kuendelea kuwepo hadi leo....ila inakadiriwa baada ya miaka bilioni kadhaa litazeeka na kushindwa kujitengenezea hiyo energy ya ku survive hivyo kutawanyika na kubaki kitu kigumu kiduchu kama dunia....

I hope umepata kapicha

The_life_cycle_of_a_Sun-like_star_annotated-700x432.jpg
 
Hehe mwanasayansi hajaumba jua wala mwezi lakini anajua kuvielezea vizuri sana jinsi vinavyotokea, tunajua vizuri jinsi jua linavyotengenezwa na hata ukitaka tunaweza kukutengenezea version ndogo kabisa laboratory.

Kukimbilia dini kwa kila phenomena ambayo huwezi kuielezea ni ignorance, curiosity ndicho kitu ambacho kimefanya leo hii unatumia internet, ingekua aliyegundua umeme angesema electrons hatuwezi kuzielezea tumwachie Mungu leo hii hata umeme tungekua hatuna.

Kwa hiyo somo la leo, kama una imani shika imani yako lakini isikugeuze kua mjinga au mtumwa, itumie tu kukufariji lakini sio kuondoa maswali

Sawa kKa nimekuelewa, mi nataka nijue nani kaumba jua na mwezi,,na kisayansi nikwann jua na mwezi vinachomozea MASHARIKI NA KUZAMA MAGHARIB,? NINI KINASABABISHA JUA NA MWEZI VICHOMOZEE PANDE IZO ENYI WANASAYANSI NA ISIWE PANDE NYINGINE LABDA,,KWANN ISIWE KASKAZINI NA KUSINI,,,
 
Nakumbuka enzi hizo niko O-level. Physics tulikuwa tunafundishwa Three states of Matter. Sasa hivi.. it is no longer three states of matter..but FOUR -SOLID,LIQUID,GAS and PLASMA. Na hili jua ni PLASMA kama ilivyo radi.
images

State of matter - Wikipedia, the free encyclopedia

Mkuu, wataalamu wanasema jua litatawanyika baada ya miaka bilioni 5, kumbuka kwamba lilizaliwa napia litakufa....
invyosemwa mwanzo wake ni mkusanyiko ulivyo kama uonavyo kimbunga kinavyoanzaga hapa duniani, na kadiri ile spidi ya kujizungusha inavyoendelea inasababisha liwe la duara....na katikati yake kuwepo kiini cha huo mduara ambacho ndio husababisha liendelee kuwepo.....kuna process inaitwa nuclear fusion ndio inayotoa au nikama inatengeneza chakula cha jua kuendelea kuwepo hadi leo....ila inakadiriwa baada ya miaka bilioni kadhaa litazeeka na kushindwa kujitengenezea hiyo energy ya ku survive hivyo kutawanyika na kubaki kitu kigumu kiduchu kama dunia....

I hope umepata kapicha

The_life_cycle_of_a_Sun-like_star_annotated-700x432.jpg
 
Mkuu, wataalamu wanasema jua litatawanyika baada ya miaka bilioni 5, kumbuka kwamba lilizaliwa napia litakufa....
invyosemwa mwanzo wake ni mkusanyiko ulivyo kama uonavyo kimbunga kinavyoanzaga hapa duniani, na kadiri ile spidi ya kujizungusha inavyoendelea inasababisha liwe la duara....na katikati yake kuwepo kiini cha huo mduara ambacho ndio husababisha liendelee kuwepo.....kuna process inaitwa nuclear fusion ndio inayotoa au nikama inatengeneza chakula cha jua kuendelea kuwepo hadi leo....ila inakadiriwa baada ya miaka bilioni kadhaa litazeeka na kushindwa kujitengenezea hiyo energy ya ku survive hivyo kutawanyika na kubaki kitu kigumu kiduchu kama dunia....

I hope umepata kapicha

The_life_cycle_of_a_Sun-like_star_annotated-700x432.jpg
naomba endelea kunipa ujuzi:hiyo nguvu ya jua kupotea baada ya miaka kadhaa itahusisha majua yaliyoko sayari nyingine au hili yu la kwetu?halafu inasemekana karibu robo tatu ya dunia ni maji na wakati huohuo dunia huzunguka jua na kujizungusha,je hayo maji yanashikiliwa na nguvu gani bila kumwagika?msinicheke tafadhali nataka kujua
 
kila jua lina zaliwa na kufa kivyake mkuu, kila kitu duniani kinavutwa na gravitational force, pamoja na maji pia. ila yote haya ni kazi ya mungu.
 
Mkuu, Kwakweli mungu ni mwema.....ishu ni kwamba jua activities zake zina produce mambo hatari sana hata kueleza tu nikama kutishia watu...lakini ndio tuko hapa nawalikuwepo kabla yetu na watakuwepo baada yetu....

Kwa macho yetu tu sie tunaona mwanga ...lakini jua linatoa 1. sola flares,
faq3.jpg
(hapo kulia kwenye mng'ao)
milipuko yenye mng'ao mkubwa,

halafu kuna kitu kinaitwa 2. corona mass ejection,
faq4.jpg

hapa jua lina release gesi mchanganyiko na magnetic fields ( huo mliuko kwa juu ya disk)

halafu kuna kitu kinaitwa 3. prominence, surface ya jua ni plasma sasa hii ina paa kwenye anga la jua kama uonavyo wimbi la bahari liende miles kadhaa angani lakini still limeji attach baharini.....prominence inajiattach kwenye ardhi ya jua

kwa muda kadhaa na kupotea
faq5.jpg

halafu kuna upepo kama huku duniani huwa unavuma, juani unaitwa 4. high speed solar wind streams (kama hii artistic image)

faq21.jpg

nakingine ni 5. solar high energetic charged particles.

hayo yote above, yana athari zake yanapokuja kwetu duniani, vingine havifiki ila vipo vinavyofika kutegemea na nguvu na spidi ya mlipuko hahaha...nasema kama siogopi vile...inatisha mkuu. kuna ambayo tunayaona kwa macho yetu kuna vingine hatuvioni mpaka kwa vyombo maalumu...mfano ukipipigwa picha ya kawaida haiwezi ikaonyesha hadi mifupa au muscles zako mwilini kama ifanyavyo x-ray au ultrasound,

Kwahiyo kamera na vifaa maalumu vinawawezesha kuona hayo yote mpaka magnetic fields....

Dunia inajilinda na yote hayo, kwa njia ya atmosphere yake, na magnetic fields.....hizo particles zikija zingine zinaungua zikiingia tu kwenye anga letu, na hayo ma energy mengine yanazuiwa na magetic field za dunia. ambazo zinatoka kwenye ya ncha za dunia yani north na south poles... ingawa zingine zinafanikiwa kuingia.....
faq7.jpg
hizo line za blue ni magnetic field za dunia huzuia hicho kibano kutoka juani njano na other particles

Athari za jua ni exposure to radiation ina sababisha kansa, ni kama kupiga x-ray isivyoshauriwa labda kwa ulazima...hizo magnetic field zina affect radar, compass, etc, Waves zina affect radio waves, setellites, simu, tv, grid za umeme, (ni kama kitisho cha radi vile) ...yani karibu mambo yote yanay[totusaidia kuishi katika modern societies. cheki below ni artistic demo tu kunyesha vifaa vinavoweza kuathirika

465382main_SpWeather-orig_full.jpg

Tukija kwenye concern yako ya sasa na mabadiliko ya jua ni kwamba jua lina misimu miwili- maximum na minimum...kila average ya miaka 11. kwenye maximum hayo majanga juu yanaongezeka, kwenye minimum yanapungua sijafatlia kujua tupo msimu gani nitacheki later...

Kinachofanywa na wanasayansi kwasasa wanajitahidi kujua yote hayo ili wawe wanatutahadharisha ...ila wana confidence bado tupo safe kwasasa...kwamba hakuna balaa litakalo tumaliza kwasasa....rabsha zipo...ndio hayo unayasikia ya kutunza mazingira, carbon emission, green house etc......yote hayo ili tuwe safe...na wabishi wapo...

I guess nimechangia kiasi...thanks
i salute you,elimu hii hata darasani nadhani ilinipita,,,ahsante ndugu,naamini wengi tume na tuna nufaika na mada hii
 
Back
Top Bottom