umenifurahisha kwa majibu haya uliyompa mwenzetu.
ila kuna jambo limenistua kidogo. mimi hupenda sana kuangalia discovery channel na madude yahusuyo anga na vyote vilivyomo. wanasayansi wamereport kuwa miaka ya hivi karibuni jua limekuwa linaonesha misbehaviour ya hali ya juu sasa wanahisi ni mabadiliko fulani katika entire sola system yaliyosababishwa au yamefikia wakati wake. na hii inaweza kuleta athari kubwa duniani na mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea sasa yaweza kuwa yamesababishwa na hilo swala.
sasa kwa jinsi jua lilivyo dude la kutisha nimekuwa najiuliza tabia hizi ngeni linalozifanya twaweza kupata madhara ambayo kwa kweli yanatisha. hivyo dunia si mahali salama sana ikiwa tu tupo katika hili limfumo la jua kwa ujumla wake.
ila mungu ni mwema sana.
Mkuu, Kwakweli mungu ni mwema.....ishu ni kwamba jua activities zake zina produce mambo hatari sana hata kueleza tu nikama kutishia watu...lakini ndio tuko hapa nawalikuwepo kabla yetu na watakuwepo baada yetu....
Kwa macho yetu tu sie tunaona mwanga ...lakini jua linatoa 1. sola flares,
(hapo kulia kwenye mng'ao)
milipuko yenye mng'ao mkubwa,
halafu kuna kitu kinaitwa 2. corona mass ejection,
hapa jua lina release gesi mchanganyiko na magnetic fields ( huo mliuko kwa juu ya disk)
halafu kuna kitu kinaitwa 3. prominence, surface ya jua ni plasma sasa hii ina paa kwenye anga la jua kama uonavyo wimbi la bahari liende miles kadhaa angani lakini still limeji attach baharini.....prominence inajiattach kwenye ardhi ya jua
kwa muda kadhaa na kupotea
halafu kuna upepo kama huku duniani huwa unavuma, juani unaitwa 4. high speed solar wind streams (kama hii artistic image)
nakingine ni 5. solar high energetic charged particles.
hayo yote above, yana athari zake yanapokuja kwetu duniani, vingine havifiki ila vipo vinavyofika kutegemea na nguvu na spidi ya mlipuko hahaha...nasema kama siogopi vile...inatisha mkuu. kuna ambayo tunayaona kwa macho yetu kuna vingine hatuvioni mpaka kwa vyombo maalumu...mfano ukipipigwa picha ya kawaida haiwezi ikaonyesha hadi mifupa au muscles zako mwilini kama ifanyavyo x-ray au ultrasound,
Kwahiyo kamera na vifaa maalumu vinawawezesha kuona hayo yote mpaka magnetic fields....
Dunia inajilinda na yote hayo, kwa njia ya atmosphere yake, na magnetic fields.....hizo particles zikija zingine zinaungua zikiingia tu kwenye anga letu, na hayo ma energy mengine yanazuiwa na magetic field za dunia. ambazo zinatoka kwenye ya ncha za dunia yani north na south poles... ingawa zingine zinafanikiwa kuingia.....
hizo line za blue ni magnetic field za dunia huzuia hicho kibano kutoka juani njano na other particles
Athari za jua ni exposure to radiation ina sababisha kansa, ni kama kupiga x-ray isivyoshauriwa labda kwa ulazima...hizo magnetic field zina affect radar, compass, etc, Waves zina affect radio waves, setellites, simu, tv, grid za umeme, (ni kama kitisho cha radi vile) ...yani karibu mambo yote yanay[totusaidia kuishi katika modern societies. cheki below ni artistic demo tu kunyesha vifaa vinavoweza kuathirika
Tukija kwenye concern yako ya sasa na mabadiliko ya jua ni kwamba jua lina misimu miwili- maximum na minimum...kila average ya miaka 11. kwenye maximum hayo majanga juu yanaongezeka, kwenye minimum yanapungua sijafatlia kujua tupo msimu gani nitacheki later...
Kinachofanywa na wanasayansi kwasasa wanajitahidi kujua yote hayo ili wawe wanatutahadharisha ...ila wana confidence bado tupo safe kwasasa...kwamba hakuna balaa litakalo tumaliza kwasasa....rabsha zipo...ndio hayo unayasikia ya kutunza mazingira, carbon emission, green house etc......yote hayo ili tuwe safe...na wabishi wapo...
I guess nimechangia kiasi...thanks