Tazama jua lilivyo surface yake kwa karibu

Tazama jua lilivyo surface yake kwa karibu

ni kweli mkuu ila hizi akili alizotupa ametupa uwezo kuchunguza ( ku explore) mazingira yanayotuzunguka bila kikwazo limit, kujua kwetu mazingira kumemuwezesha binaadamu kugundua mambo yanayosaidia maendeleo na teknologia kumfanya aendelee kusavaiv kizazi na kizazi mpaka mwisho wa dunia, tumeweza kujua misimu inavyoathiri maisha yetu na kujiboresha na mabadiko yake, mfano upimaji wa hali hewa mvua sunami kiangazi...kuboresha teknojia katika upatikanaji wa chakula kingi na jinsi ya kukihifadhi kutokana na ongezeko watu duniani, kugundua magonjwa yanayoathiri viumbe hai wote na matibabu yake, imagine hatua iliyofikiwa kupambana na ukimwi kwasasa ukilinganisha na miaka ya 80. Kwahiyo mkuu tunachunguza explore mazingira yetu mpaka level ya ulimwengu universe ili kuboresha maisha yetu kwa uwezo aliotupa mungu, hebu fikiria usingetoka chumbani kwako unapolala kila siku, ungekosa managapi?

Uko sawa, lakini Ametuwekea limit. Kuna mambo yatabaki kuwa siri Yake!
 
Mkuu vipi kwa upande wa galaxy ...?
kuna joto kiasi gani pande hizo..?
vipi pia , zinafikika...?

mkuu kumbuka kuwa galaxy ni mkusanyiko wa nyota milioni kadhaa na sayari za kila nyota, gases and other objects. Jua letu ni nyota. Na kutoka nyota hadi nyota nyingine kipimo chake ni spidi ya mwanga. sisi hapa tulipo tupo kwenye galaxy inaitwa milky way, kwahiyo unapoongelea joto nadhani katika galaxy ni kila nyota ina joto lake lakini nyota kama jua letu ni nyuzi 5500, na kila sayari joto lake linategemea umbali wake kutoka kwenye jua lake, zingine ni barafu tu kama pluto, majua mengine i hope ni zaidi ya au kidogo.
Ila jua letu linazeeka na kufa kwake ni kubasti. Mwisho wa maisha maana uhai wa viumbe hai na sola system yetu unategemea jua na activity zake.

Kufika kwenye galaxy nyingine nadhani bado sana, nadhani wanasayansi wamefaniki wa kupeleka chombo hadi sayari ya mwisho kwa jua letu, bado hata hatujafikisha chombo chetu kwenye sayari za jua lingine jirani. Ila camera ziko poweful kuona yote hayo yanayosemwa na wanasayansi, kilasiku kuna uvumbuzi wa mambo mapya.

Mwanga kutoka juani kutufikia hapa duniani inachukua dakika nane mfano jua lingezima gafla ingekuchua dakika nane kujua hakuna mwanga na kuanza kusikia baridi.
Pia ukumbuke kuwa mwaga unasafiri kwa spidi ya kilomita laki 3 kwa sekunde.

Kutoka jua letu mpaka jua lingine kwenye galaxy yetu, umbali wake unapimwa kwa spidi ya mwanga. kama ulivyoona mwanga unatufikia baada ya dakika 8 kutoaka jua letu, ila kwa jua lingine lilio karibu ya sola sysytem yetu mwanga wake unatufikia baada ya miaka 4!

Kuna nyota tunaziona angani usiku zingine zimesha kufa ila mwanga wake ulikua haujafika maana zingine mwanga wake unachukua miaka milioni kadhaa kutufikia...haya wakuu.
 
Ni moja ya ishara kubwa kwa wenye akili kwamba huyu muumbaji ana UTAALAMU wa UWEZO wa hali ya juu.Hakuna wa kufanana nae wala wa kumzidi.Ametukuka MWENYEZI MUNGU mbora katika uumbaji.
 
nature ya formation ya nyota na sayari ni kama unavyoona kimbunga kinavyoanzaga hapa kwetu ardhini, naamini umesha wahi kuona ule upepo unaendaga round and round na kufanya mzunguuko mkubwa sana kusababisha force kubwa inayoleta hata madhara kuezua manyumba nk. Ule mzunguuko kadri unavyo grow unasababisha kuvivuta vitu objects to its center , ile pull force inakua kubwa sana as mzunguuko unavyoongezeka, sasa hapa ni ardhini lakini kwenye space zile dusts na solid objects na gas zilizopo impact yake ni kubwa sana kiasi ule mzunguko unaweza kusabababisha kuzaliwa kwa nyota mpya na ku affect small obects zilizo karibu yake, kuizunguka ile nyota nakuwa sayari zake, hapa ni physics zaidi, lakini mzunguuko huu ni wakundelea...na ndio unaosababisha in the long run objects kuonekana duara....ila not necessarily ardhi zake kkuwa zipo smoothduara hapana, kuna mabonde na milima. Kuna mfano pia kwamba hata wacheza ice skate anapojizungusha kwa kasi na kukusanya mikono yake mwilini kasi huongezeka na huwa anaonekana wa duara. Tazama figure skating.

Asante mkuu . swali lingine since nizaliwe nilikuwa na tabia ya kuangalia angani usiku hasa mwezi. Mwanzo nilikuwa naona picha ya mama kama kabeba kuni kwenye mwezi usiku unapokuwaunang'aa lakini baada ya kuconcentrate nikawa naona picha kama ya kamnyama dizaini ya sungura. Ukitaka kuhakiki usiku angalia mwezi ukiwa full cycle. Kila siku hako kapicha hakatoki. Swali
Je ni miamba ya mwezini huonekana? Au ni picha ya sehemu ya dunia baada ya kuakisiwa na mwanga wa jua?
 
Mbona tunaambiwa kuna watu wanapanda hadi mwezini huko si linachoma sana???

Mwezi sio chanzo cha mwanga bali lenyewe huakisi mwanga kutoka kwenye jua na kutupa Duniani. Kuna sayari zingine zinazungukwa na miezi zaidi ya miwili....
 
mwezi upo kilomita laki 3.8 kutoka hapa tulipo, jua lipo kilomita milioni 149.6, Kwenye mwezi joto ni nyuzi 100 mchana usiku ni baridi sana nyuzi negative 177 centigrade. joto kwenye jua inakisiwa ni nyuzi 5500. Kwenda kwenye mwezi unahitaji mavazi maalumu kujilinda na joto na kemikali zilizopo katika anga ya mwezi. Kwenda juani sidhani kama plan ipo ila kuna vifaa spesho vina zunguuka angani kulichunguza maendeleo yake. jua lina kadiriwa kuwa na umri wa miaka bilion 4.5 hata mwezi pia.

Mugabe alisema wazibabwe wataenda Kwenye Jua akaulizwa utatumaje watu kule kwani kuna joto kali sana! akajibu wataenda usiku...
 
Ni moja ya ishara kubwa kwa wenye akili kwamba huyu muumbaji ana UTAALAMU wa UWEZO wa hali ya juu.Hakuna wa kufanana nae wala wa kumzidi.Ametukuka MWENYEZI MUNGU mbora katika uumbaji.

saana mkuu, hilo halipingiki
 
Mkuu Dabo, ardhi ya mwezi imegawanyika katika sehemu zifuatazo. vumbi kama majivu hivi /ashes lilitokana na milipuko ya volcano, mawe ya yaliyotokana milipuko volcano, mawe na vumbi linalotokana na kuangukiwa na vimwondo/ comets ambazo zinasababisha mashimo makubwa/ craters mojawapo linaweza kufikia upana wa kilomita elf 2 naa. Nadhani huwa unaviona vimwondo usiku, kunajiwe moja lipo mbozi lanamna hiyo au ukija coco beach wanapouza mihogo utaona yale mawe ukingoni utadhani chuma,

Kutokana na anga la dunia vimwondo vikiingia huwa vinaungua na kuyeyuka, ila mwezi hauna anga kwahiyo huwa vinaanguka kwenye arhi yake na kusababisha yale mashimo au craters kitaalamu. yapo maeneo yanayopata hicho kibano kwa sana na mengine hapana yapo smooth. pia volcano zimesababisha kuna milima na mabonde.

kwenye mwezi hakuna viumbe hai au bado havijagundulika ila wanahisi kuna maji na wanaendelea na uchunguzi..ila hakuna mazingira ya kuishi banaadamu.

Sura ya ardhi ya mwezini kwa karibu
Moon-Jan-2010-sharp-1024x680.jpg


moon_mare-imbrium-inc-sinus-iridum-mar15.jpg


moon_20150303_2039_20_sTycho1.jpg


10075965.jpg


Hapa ni kipindi wamarekani walipotembelea mwezini

10075965.jpg


DirectFromTheMoon1-tp_jpg_610x343_crop_upscale_q85.jpg


Tazama dunia inavyoonekana katika uso wa mwezi....its amzing!

earthrise_strip.jpg


bluemarble_apollo17_strip.jpg


ukiwa out of space hivi ndio unaiona dunia...sayari ya bluu
 
Mugabe alisema wazibabwe wataenda Kwenye Jua akaulizwa utatumaje watu kule kwani kuna joto kali sana! akajibu wataenda usiku...

hahahaha nice one
 
Hii ni Photoshop, haiwezekani background ya jua iwe usiku/giza/gallaxies. Na hakuna kamera ya hivyo. (im in the industry)
 
Mkuu mxyo16 mimi siku zote nashindwa kuamini kuwa dunia ni duara sasa ukiachilia mbali wale wanaoishi kaskazini jee hao wa kusini na pembeni wanaishije na kama wote wanapata jua la utosi inakuwaje wakati jua lipo stationary? Natanguliza shukrani
 
Last edited by a moderator:
unachotakiwa kufahamu ni kuwa pamoja na sayari dunia inajizungusha kwenye mhimili wake lakini pia wakati huo huo inalizunguka kwenye jua....hivyo kupata majira na nyakati...usiku na mchana etc..wengi wanazani kwamba wakiangalia anhani basi ukipaa kuna mwisho utagota..teh...teh
 
Hii ni Photoshop, haiwezekani background ya jua iwe usiku/giza/gallaxies. Na hakuna kamera ya hivyo. (im in the industry)

Sijakulewa kwakweli, lakini wanachofanya wanasayansi ni kutupa hali ya uhalisia wa mambo yalivyo pamoja na kutoa maelezo, taratibu na process wanazofanya, aim yao ni kutoa mwangaza/ elimu kwa jamii. ninaamini hizi picha walizitolea maelezo kutokana na swali/ wasiwasi ulilouliza hapo juu.....nao wakajibu wanapofanya huu utaratibu, wanatumia system inaitwa SDO-Solar Dynamics Observatory na hunasa picha za jua kama hivi chini-

solar%20flare%20in%20different%20wavelengths.jpg


Itakua umetutendea jambo la heri kutupa elimu zaidi, hiyo photoshop inavyofanya kazi katka hili la SDO....na ni vizuri umesema kuwa upo kwenye hii industry . Please tumegee....and BTW thanks for stepping in...
 
Mkuu mxyo16 mimi siku zote nashindwa kuamini kuwa dunia ni duara sasa ukiachilia mbali wale wanaoishi kaskazini jee hao wa kusini na pembeni wanaishije na kama wote wanapata jua la utosi inakuwaje wakati jua lipo stationary? Natanguliza shukrani[/QUO

Dah mkuu, ninachojua mimi ni kwamba sio misimu yote watu kona zote za dunia kaskazini, kusini, na katikati huwa wanapata jua la utosi. hapana. mfano kwa sasa hivi nchi za kaskazini jua wanaliona mda mchache sana na kwawatu wa kusini jua linakuwepo muda mrefu yani zaidi ya masaa 12 mpaka hata masaa 24 kusini kabisa au kaskazini kabisa,

Dunia sio perfect duara, ni spherical mfano wa yai.
 
Back
Top Bottom