Tatizo si uislam

Tatizo si uislam

lakini mbona ni kimbilio la waislamu?..................hivi huamini kuwa uislamu unaruhusu ushirikina....hebu tembelea misikiti yote utakuna nje ya misikiti hasa siku za kumuabudu allah wao kuna waganga wa kienyeji.....hii sio story ni ukweli.........hii ndiyo dini ya allah

Jile79,

mwazilishi wa mada,CITYBOY ameleta mada nzuri sana leo.yenye nia ya kufahamisha wengi ambao wanashindwa kwa kutojua au kwa makusudi kuchanganya mambo,kuchanganya madawa.

kwako Jile79 dini zipo nyingi dunia,nyengine zina na matawi.
jaribu kuzisoma na kuzifahamu, usikurupuke tu na kutaka kuunganisha mabehewa ili treni ionekane refu.

Ukisema uislamu na uganga wa kienyeji ni kitu kimoja.
Ukisema ukatoliki na kuharibu vitoto vidogo ni kitu kimoja
ukisema ujews na kuuwa waarabu ndio dini yenyewe
ukisema ukristo na dhambi ya asili ndio dini yenyewe
ukisema uhindu na udhalilishaji ndio dini yenyewe.

Mifano hii yote ndio huko kuchanganya madawa. Na ndiyo hiyo ,mada imejaribu kuonesha ni vyema watu kutofautisha dini ya mtu na matendo yake.
Na wewe Jile79, umeibua mepya hata vumbi halijatulia...sasa maana yake nini?
Ungependa huu ugeuke mjadala wa dini? au malumbano ya kidini?

Vizuri uzisome, jipatie maarifa juu ya dini husika, ukiamua baadae kwa makusudi kuchanganya mambo itakuwa ni kwa kupenda tu.
 
Mtu mwenye dhana mbaya huwa ana maradhi ya wasiwasi na huwaogopa watu... uugua kwa dhana yake mbaya, mwili na roho yake huugua pia. Kisha usababisha aonekane mzee kabla ya wakati wake. Kwa sababu tabia hiyo isiyofaa huathiri vibaya mfumo mkuu wa fahamu na tezi za mwilini, na kusababisha ugonjwa wa utahahira wa kifikra kiasi cha kujenga chuki akilini mwake na kupelekea kujichukia yeye mwenyewe...!
Nyongeza:

Watu wa aina hiyo, huwa na roho mbaya na fikra zao nimbaya wakati wote kwa maana hawayawazi yaliyo mema bali maovu, Na katika kuwaza kwao maovu huwaona hata walio wema kwao kwamba ni waovu!! Na huwafikia hali wakajikatia tamaa na kunywa sumu (hili limethibitishwa - Watu wenye imani kama ya Jile ndio wanaoongozwa kwa kujiua)
 
Tanzania haina dini bali wananchi ndio wenye dini,hivyo katiba inawaruhusu wote kuabudu pasipo kuvunja sheria.Uislam uko wazi pia hivyo msiojua tuulizeni tuwafundishe.Uongozi katika Uislam unamaadili yake mfano kiongozi lazima awe mtusafi na akubalike kwa tabia njema na awe mwadilifu katika uongozi wake.Kiongozi awapendelee na kuwahurumia raia wake kwa kuwapa huduma yao inayostahili.Sasa anapopewa Muislam kungoza anatakiwa aongoze kwa kivuli cha Uislam na kwakua kama Tanzania haina dini basi Muislam huyu itabidi kwanza awe mnyenyekevu mbele za Mungu na pia atekekeleze sheria za nchi.Kama mtu anajina na hafuati ule mwelekeo wa Uislam kwa kutenda haki basi yuko mbali na Uislam pamoja na Mungu,kwa maana anaifuata na kuiabudu nafsi yake na matamanio yake binafsi.Hivyo MAFISADI na WEZI wahukumiwe kwa dhambi zao na usiandamwe Uislam kama wengi wafanyavyo hapa JF.Anayefanya dhambi hizo uislam hauko naye na tayali wamejitenga wenyewe kwa kuukanusha Uislam.Uislam siotatizo bali tatizo ni wao viongozi.Ingelikua ni sheria ya Uislam kwa kubainika kashfa kiongozi anang'atuliwa.Hivyo kama JK ana matatizo msimuhukumu kwa DINI yake bali muhukumuni yeye kama yeye na si UISLAM na Waislam.
Baadhi ya waislamu hawataki muislamu akosolewe, akikosolewa Dau au Kikwete basi hawachelewi kudai kuwa hawapendwi kwa sababu ni waislamu! Wakati huo wanasahau kuwa wakina EDWARD Lowassa na BENJAMIN Mkapa kila kukicha wanatupiwa madongo bila mtu kusema wanafanyiwa hivyo kwa sababu ni wakristu! Mbaya zaidi ni baadhi yenu hamchelewi kuhukumu ukristu ( hasa ukatoliki) kwa kila pungufu ya JULIUS Nyerere au BENJAMIN Mkapa. Ungesema tatizo si uislamu au kristu ningekuelewa. Lakini si kwa hili.

Amandla....
 
Tanzania haina dini bali wananchi ndio wenye dini,hivyo katiba inawaruhusu wote kuabudu pasipo kuvunja sheria.Uislam uko wazi pia hivyo msiojua tuulizeni tuwafundishe.Uongozi katika Uislam unamaadili yake mfano kiongozi lazima awe mtusafi na akubalike kwa tabia njema na awe mwadilifu katika uongozi wake.Kiongozi awapendelee na kuwahurumia raia wake kwa kuwapa huduma yao inayostahili.Sasa anapopewa Muislam kungoza anatakiwa aongoze kwa kivuli cha Uislam na kwakua kama Tanzania haina dini basi Muislam huyu itabidi kwanza awe mnyenyekevu mbele za Mungu na pia atekekeleze sheria za nchi.Kama mtu anajina na hafuati ule mwelekeo wa Uislam kwa kutenda haki basi yuko mbali na Uislam pamoja na Mungu,kwa maana anaifuata na kuiabudu nafsi yake na matamanio yake binafsi.Hivyo MAFISADI na WEZI wahukumiwe kwa dhambi zao na usiandamwe Uislam kama wengi wafanyavyo hapa JF.Anayefanya dhambi hizo uislam hauko naye na tayali wamejitenga wenyewe kwa kuukanusha Uislam.Uislam siotatizo bali tatizo ni wao viongozi.Ingelikua ni sheria ya Uislam kwa kubainika kashfa kiongozi anang'atuliwa.Hivyo kama JK ana matatizo msimuhukumu kwa DINI yake bali muhukumuni yeye kama yeye na si UISLAM na Waislam.

Tungekuwa na robo tu ya waislam wenye uelewa kama wako, tungeishi kwa amani bila misuguano na nchi ingeendelea kiuchumi. Tatizo la viongozi wetu ni wakristo au waislam wa jina tu. Hawaishi kulingana na mafundisho ya dini. Wanaishi kwa kufuata tamaa zao ambazo hazina kiwango.
 
Mada nzuri lakini baadhi ya watu wameshaanza kuaribu. Jile79 please kama hakuna ulazima wa wewe kuchangia mada hii tafadhali kaa kimya.
 
Mimi ninaona wanaosema JK ni mdini pengine hawajafanya homework ya kutosha kuhusu huyu mkuu.

Ninachokiona hapa ni kuwa amekuwa scapegoat tu wa CCM failings...hii ni kwa sababu yeye ni mkubwa na ukubwa ni jaa - so he will have to shoulder all the blame.

Mimi binafsi nishakuwemo kwenye coordination committees kadhaa za Kikristo ambazo zilihitaji participation ya JK kwenye shughuli mbalimbali za kanisa - kwa kweli ninakiri kwa ujasiri kabisa kuwa sikuweza ku-detect the slightest element ya hulka ya udini kwa JK.

Haya mambo ya kuongea udini-udini yameibuka sana tangu JK alivyoingia 2005.....
Why? To mention only a couple of reasons:
1) manifesto ya CCM kuongelea mahakama ya kadhi (hapa CCM walikuwa very insensitive - from historical point of view)
2) list of shame ya Dr Slaa iliyowaanika viongozi waandamizi wa CCM (list hiyo kuna Wakristo wengi tu)

Unaweza kusema sababu ya kwanza ni justified kama chanzo cha sentiments za udini kwenye awamu ya JK.
Ya pili ilitumika kuihanikiza ile ya kwanza very wrongly and unjustifiably.

Kwa hiyo pamoja na kwamba mimi binafsi JK hajani-impress kiutendaji kama rais, na kwamba nina nia ya dhati ya kuratibu impeachment process, nasema siyo fair kabisa kusema Uislam wa JK ndiyo umetusabishia madhira tunayopitia kwatika awamu hii.

JK akosolewe kwa utendaji wake dhaifu lakini si kwa vile ni Muislam.
Tukumbe kuwa hakuna dini (including Islam) inayomtaja Mungu wa Ibrahim, Isaka, Yakobo, etc inayobariki matendo haramu kama ufisadi, uwizi, uzandiki, uhuni, uchawi, etc!
 
religious leaders should be capable of realizing the manipulation of politicians. Tumeona hata jana, kwenye kuwaombea marehemu waliopigwa risasi hapa arusha na "polisi" kiongozi wa waislamu alijizuia kutoa maneno yoyote ya kukemea kilichotokea ili asiwaudhi viongozi wa nchi huu ni uoga na sidhani kama uislaumu unaruhusu uoga wa namna hii !!!!

huo uoga ni wake binafsi na si kwakua kiongozi wa dini ni waislamu. Mbona kuna viongozi wengi tu wa dini zingine wanawaogopa wakuu wa nchi jamani.
 
Mwanamageuko said:
inasemekana..... Tusimame katika ukweli mara zote. Udini Tanzania umeingia toka mwaka 1965 na ukathibitishwa rasmi miaka michache iliyofuatia. Wote wanaofahamu na wanaofuatilia siasa za tanzania wanaujua ukweli. Wala haukutokana na Mihadhara wala hizo kashfa unazozisema. Kwani maana ya kashfa ni nini? Ikiwa kupingana ndio kashfa basi jua ya kwamba walipowakisimama wahadhiri wa kikristo kwenye majukwaa (Padre Nkwera na wengineo - hiyo ni kabla ya 1986 unayoisema) na kuutaja UTATU, hiyo ni kashfa kubwa kwa UISLAMU, Je huo tuuite ulikuwa uchochezi wa kashfa za kidini. Mambo ya Mihadhara yanafanyika kote duniani na mwisho wa siku watu wanarudi kwenye masuala ya msingi. Nimepata kutoa mifano hapa na kufasiri maana ya NENO KAFIIR neno hili asili yake ni Kiarabu kwa kiswahili likiwa na MAANA "MPINGAJI" hivyo basi mathalan hata kisiasa, KAFIRI WA CHADEMA NI CCM na kinyume chake. Ukinijia ukaniambia Masiha ni Mungu au Mwana wa Mungu je ikiwa Imani yangu i kinyume na hivyo uone HUJANIKASHIFU!? ikiwa ndio maana ya Kashfa!!! Hivyo basi nami nikikwambia Imani yangu iko kinyume nawe IWEJE hapo iwe NIMEKUKASHIFU? Mihadhara ni hiyari ya mtu kwenda ama kusikiliza. Je tuseme TV ya AGAPE inawakashifu Waislamu? au Redio za Kiislamu zinawatusi WAKRISTO? Na laiti ikiwa hivyo ndivyo basi GAZETI LA AMKENI linaongoza kwa KUUKASHIFU Ukristo ikiwa kinyume na imani ya mmojawapo ni kashfa kwa mwingine!! haya hayakuanza leo ya kashfa za kidini kama ikiwa ndio maana halisi ya kashfa. Walikua wageni wakaziita DINI ZA KISHENZI, IMANI ZA KISHENZI kwa babu zetu, Nadhani huenda hizi zilikuwa sifa njema kwa baadhi ya watu!! HAZIKUWA KASHFA!!! Tunapojadili tusitazame tumeangukia wapi twende mbali zaidi ya hapo.

TUSIPENDE MAJIBU RAHISI KWENYE MASWALI MAGUMU.

UDINI NCHI HII UNASABABISHWA NA UBINAFSI, CHOYO, WANASIASA KUWATUMIA VIONGOZI WA DINI ZAO, WAUMINI WENZAO KWA MASLAHI YAO, SIASA MBOVU NA VIONGOZI KUTOWAJIBIKA IPASAVYO.

Mwanamageuko,

..hakuna tatizo kama kila mhusika atajiepusha na kuchukua vitabu vitakatifu vya dini ya mwenzake na kuanza kuvikosoa na kuvidhihaki.

..kama Nkwera anataka kuzungumzia utatu mtakatifu ni vema akatumia Biblia, akienda kukamata Msahafu wa Waislamu basi atakuwa amefanya makosa makubwa.

..namheshimu sana Marehemu Sheikh Mkuu Hemed Bin Jumaa Bin Hemed ambaye ktk mawaidha yake sikupata kumsikia akitumia kitabu tofauti na Koran tukufu.

..YES, HILI NI SWALI GUMU LAKINI JIBU LAKE NI RAHISI.

NB:

..hiyo mihadhara unayoitetea mbona hatusikii hata siku moja wamekwenda kuchukua vitabu vya Mabaniani, au Mabohora, badala yake wana-target Biblia na Koran.
 
Rafiki yangu Jokakuu,
Ikiwa hivyo ndivyo... basi itabidi na aya zingine ndani ya Quran ziondolewe kwa maana zinafanana na za kwenye Biblia!! Na ikiwa siku Sheikh anasoma aya hiyo nawe unapita Utajisikiaje? Hayo ya Mihadhara wala hayapaswi kuumiza kichwa kwani yalianza dahari ya miaka nchi hii, ila sema yameonekana kuwa wazi miaka hiyo uliyotaja lakini kwa nchi zote zinazotuzunguuka yapo miaka mingi. Mf. alikuwepo Mar. Ahmed Dedaat S.A. na akifanya mihadhara na Wataalamu wa Kikristo kwenye TV hapakuwa na ugomvi baina yao. Kushindanisha vitabu ni sayansi na hoja zinakubalika. Nimekupa mfano wa watu wa Jumba. Jehovah Witness mbona maandiko yao ukiyafuatilia ni kashfa tupu na huwasemi? Wameanza kuandika miaka ya sitini vijarida pinzani dhidi ya baadhi ya aya za biblia na maandiko mengine lakini hakuna shida. Ni vema sana mtu akiniambia tobo liliko kwenye kaptura yangu nikajistiri kuliko kukaa kimya nikaaibika. Binafsi tumelelewa nyumba moja na familia za kikristo na haya ya mihadhara yalikuwapo na hayakutugombanisha na mpaka leo tunajuana kama ndugu na tunatembeleana na hayakutuharibia heshima wala upendo. Ila ni wajinga wanaoyageuza kuwa chuki. Na chunguza sana utaujua mwanzo wake (nakupa home-work hiyo) Ukiona ni ngumu sana nitakukumbusha (waliotoka kwenye Ukristo kuja kwenye Uislamu - ndio chanzo)

Pia kuna jingine.. Biblia zilipelekwa kwenye Lodge na Guest houses, na kuwekwa kila chumba. hii pia iliwapa watu hamu ya kuisoma na kupata maarifa mengine. Waliyoyaona huko pia ilisababisha hayo. (maana ilikuwa kuwalazimisha kuzisoma - sasa lazima majibu yapatikane pia mtihani ukija!)

Nataraji tu pamoja mpaka hapo.

N.B:
Majawabu kwa vitabu vya dini zingine
fuatilia: http://www.peacetv.in/
 
Tanzania haina dini bali wananchi ndio wenye dini,hivyo katiba inawaruhusu wote kuabudu pasipo kuvunja sheria.Uislam uko wazi pia hivyo msiojua tuulizeni tuwafundishe.Uongozi katika Uislam unamaadili yake mfano kiongozi lazima awe mtusafi na akubalike kwa tabia njema na awe mwadilifu katika uongozi wake.Kiongozi awapendelee na kuwahurumia raia wake kwa kuwapa huduma yao inayostahili.Sasa anapopewa Muislam kungoza anatakiwa aongoze kwa kivuli cha Uislam na kwakua kama Tanzania haina dini basi Muislam huyu itabidi kwanza awe mnyenyekevu mbele za Mungu na pia atekekeleze sheria za nchi.Kama mtu anajina na hafuati ule mwelekeo wa Uislam kwa kutenda haki basi yuko mbali na Uislam pamoja na Mungu,kwa maana anaifuata na kuiabudu nafsi yake na matamanio yake binafsi.Hivyo MAFISADI na WEZI wahukumiwe kwa dhambi zao na usiandamwe Uislam kama wengi wafanyavyo hapa JF.Anayefanya dhambi hizo uislam hauko naye na tayali wamejitenga wenyewe kwa kuukanusha Uislam.Uislam siotatizo bali tatizo ni wao viongozi.Ingelikua ni sheria ya Uislam kwa kubainika kashfa kiongozi anang'atuliwa.Hivyo kama JK ana matatizo msimuhukumu kwa DINI yake bali muhukumuni yeye kama yeye na si UISLAM na Waislam.

Hapa umenena na kufafanua km Profesa, nadhani watu wote wa upande wako wangekuwa na mtizamo mpana km huu tusingelumbana kuhusu dini kabisaaa.
ila cha kushangaza, kuna wale masheikh wanaohubiri chuki za kidini hadharani, na walijitokeza kwa wingi enzi za mzee Ruksa.
Ungewapa somo hili likawaingia barabara tungeshukuru.
Nimefurahia uchambuzi wako ingawa huyo KJ ka udini ameanza kukaonyesha kwa sasa tu, jamaa PIA NI mgonga glass huwa anazuka mitaa mitaa ndani ya ka....:car:
 
Kuna mbinu nyingi za kutaka kuwafanya watu wasizungumzi matatizo ya kweli ya TAIFA hili ambalo ni UONGOZI mbovu usio adilifu na usiopenda kuwajibishwa.Haya mambo ya udini lengo lake ni kutaka kuwatenga watu na hasa viongozi wa kidini katika vita hii,Si kweli hata kidogo kwamba kiongozi ambaye ni Muislamu hapaswi kukosolewa na Wakristu au kiongozi Mkristu hapaswi kukosolewa na Waislam kwani uovu hauna dini na dini zote zinachukia uovu so Watanzania tusikubali kugawanywa na hatimaye kukosa sauti moja dhidi ya uovu.Cityboy u made my day.
 
Mwanamageuko said:
Rafiki yangu Jokakuu,
Ikiwa hivyo ndivyo... basi itabidi na aya zingine ndani ya Quran ziondolewe kwa maana zinafanana na za kwenye Biblia!! Na ikiwa siku Sheikh anasoma aya hiyo nawe unapita Utajisikiaje? Hayo ya Mihadhara wala hayapaswi kuumiza kichwa kwani yalianza dahari ya miaka nchi hii, ila sema yameonekana kuwa wazi miaka hiyo uliyotaja lakini kwa nchi zote zinazotuzunguuka yapo miaka mingi. Mf. alikuwepo Mar. Ahmed Dedaat S.A. na akifanya mihadhara na Wataalamu wa Kikristo kwenye TV hapakuwa na ugomvi baina yao. Kushindanisha vitabu ni sayansi na hoja zinakubalika. Nimekupa mfano wa watu wa Jumba. Jehovah Witness mbona maandiko yao ukiyafuatilia ni kashfa tupu na huwasemi? Wameanza kuandika miaka ya sitini vijarida pinzani dhidi ya baadhi ya aya za biblia na maandiko mengine lakini hakuna shida. Ni vema sana mtu akiniambia tobo liliko kwenye kaptura yangu nikajistiri kuliko kukaa kimya nikaaibika. Binafsi tumelelewa nyumba moja na familia za kikristo na haya ya mihadhara yalikuwapo na hayakutugombanisha na mpaka leo tunajuana kama ndugu na tunatembeleana na hayakutuharibia heshima wala upendo. Ila ni wajinga wanaoyageuza kuwa chuki. Na chunguza sana utaujua mwanzo wake (nakupa home-work hiyo) Ukiona ni ngumu sana nitakukumbusha (waliotoka kwenye Ukristo kuja kwenye Uislamu - ndio chanzo)

Pia kuna jingine.. Biblia zilipelekwa kwenye Lodge na Guest houses, na kuwekwa kila chumba. hii pia iliwapa watu hamu ya kuisoma na kupata maarifa mengine. Waliyoyaona huko pia ilisababisha hayo. (maana ilikuwa kuwalazimisha kuzisoma - sasa lazima majibu yapatikane pia mtihani ukija!)

Nataraji tu pamoja mpaka hapo.

N.B:
Majawabu kwa vitabu vya dini zingine
fuatilia: PeaceTV Official Website

Mwanamageuko,

..naelewa kwamba zipo aya fulani fulani za Kuran tukufu ambazo zinafanana fanana na maandiko ya kwenye Biblia.

..pamoja na hayo sioni sababu ya mtu kama Nkwera kutumia Kuran tukufu ku-prove his Christian point of view.

..pia sioni ulazima wa Digabula kutumia maandiko ya Biblia ku-prove his Muslim point of view.

..waumini wa kawaida hawana uelewa na uvumilivu wa kutokugeuza mihadhara ya kidini kuwa uhasama na uadui ndani ya jamii.

..masuala ya vitabu vitakatifu ni ya KIIMANI, usitarajie kwamba mjadala wake unaweza kuwa sawa na mjadala wa Science.

NB:

..ningekuwa na uwezo ningewakamata wahubiri wote wa mihadhara na kuwatupa gezaulole wakalime miraba.
 
Naona Mkuu unataka kutuchanganya. Mihadhara iliyoibuka miaka ya tisini ilikuwa tofauti na hiyo ya awali. Mihadhara hii si tu ilikuwa kwenye public space lakini vilitumika vipaza sauti ambavyo hata mtu ambae hakuwa amehudhulia alilazimika kusikikiliza yanayoendelea. Na yanayoendelea yaliegemea zaidi kukashifu dini nyingine na si kujaribu kuwavuta watu kwenye dini yao kwa kueleza mema yake. Wakristu nao walikuwa wanaendesha mikutano ya uamsho lakini wao hawakuwa wakikejeli dini nyingine bali walikuwa wanaonyesha ubora wa dini yao kwa vitendo kama uponyaji n.k. Matumizi ya vyombo kama redio na T.V. ku-proselytize ni tofauti maana muangaliaji au msikilizaji ana uwezo wa kuzima au kubadilisha stesheni kama anataka. Sijui huyo Ahed Dedaat alifanya wapi mihadhara na wakristu katika TV Tanzania wakati hicho chombo kimeingia hivi karibuni. Na hapa tunazungumzia sumu iliyoingia nchini kwetu na si huko kwengine.

Hivyo hivyo kwa Mashahidi wa Jehova. Haulazimiki kumkaribisha ndani au kupokea vipeperushi vyao. Mashahidi wa Jehovaa si wa kwanza kuikosoa dini ya kikristu na hawatakuwa wa mwisho. Ni haki ya kila mtu kuweza kumpinga mwenzie ili mradi upingaji huo hauingilii uhuru wa mwengine wa kutoa counter-pingamizi au kukataa kumsilikiliza. Naamini kuwa walimu wa madrassa tokea zamani walikuwa wanawafundisha wanafunzi wao kuwa Yesu si Mungu n.k. n.k. Hii ni sawa kabisa na hakuna anayeweza kuwakatalia. Lakini unapoitoa kwenye private space ya madrassa na kuitangaza kwa sauti kubwa kwenye public space unaingiza suala la provocation. Mashahidi wa Jehovah wanapingana na baadhi ya tafsiri za madhehebu mengine kwa kutumia maandishi na ni haki yao na wanakubaliwa kufanya hivyo. Wako wanaowapinga kwa kutumia media hizo hizo na hatujasikia mtu ambae amehukumiwa kifo kwa kupingana na mafundisho ya ukristu katika uhai wetu ( hayo yaliendelea wakati wa medieval huko ulaya). Wakati wenzetu Salmin Rushdie alipoonyesha mapungufu ya imani ya kiislamu kwa kutumia mfano wa maisha ya mtume Mohamed in a satirical way, mlimhukumu kifo. Na watu waliandamana nchini kwetu kukubaliana nayo bila hata kusoma kitabu husika! Hivi leo atokee padri mmoja arushe kwa sauti kubwa 24/7 kasoro anazoziona katika uislamu au maisha ya mtume wenu kama wanavyofanya hao unaowatetea dhisi ya ukristu na Yesu, nchi hii kweli itakalika? Tofauti kati ya dini zetu zilikuwepo lakini ni katika miaka ya tisini ndipo sumu ilipoingizwa.

Kudai kuwa kuweko kwa vijibiblia chumbani kwenye loji ni kukulazimisha kusoma ni upotoshaji mwingine. Kwanza wenye hizo gesti hawakulazimishwa kuweka biblia hizo na hakuna mahali ambapo panasema kuwa utapimwa kama umezisoma ( ingekuwa ni lazima basi lazima pangekuwa na utaratibu wa kuhakikisha kuwa umesoma, kamera chumbani, mtihani kabla ya ku-check out n.k.) Mtazamo kama huu ni kama ule wa kudai ati msichana amekulazimisha kumbaka kwa sababu amevaa nguo fupi! Upuuzi mtupu.

Lakini pale msikiti ulio jirani unapotumia vipaza sauti vyenye nguvu kuhubiri kuwa dini yako ni potovu n.k. unakuwa hauna jinsi bali kusikiliza au kuhama nyumba. Mbona miaka nenda rudi miskiti imekuwa ikiwahimiza waislamu kwenda kuswali kwa sauti ya juu na hapakuwa na matatizo?

Ni lazima mjiulize ni nini kilichotokea kupandisha hasira ya wakristu.
Itakuwa vizuri kama mtaweza kuwakosoa wale wachochezi miongoni mwenu badala ya kuwatetea kwa sababu tu ni sehemu ya umma.

Amandla....
 
Mwanamageuko,

..naelewa kwamba zipo aya fulani fulani za Kuran tukufu ambazo zinafanana fanana na maandiko ya kwenye Biblia.

..pamoja na hayo sioni sababu ya mtu kama Nkwera kutumia Kuran tukufu ku-prove his Christian point of view.

..pia sioni ulazima wa Digabula kutumia maandiko ya Biblia ku-prove his Muslim point of view.

..waumini wa kawaida hawana uelewa na uvumilivu wa kutokugeuza mihadhara ya kidini kuwa uhasama na uadui ndani ya jamii.

..masuala ya vitabu vitakatifu ni ya KIIMANI, usitarajie kwamba mjadala wake unaweza kuwa sawa na mjadala wa Science.

NB:

..ningekuwa na uwezo ningewakamata wahubiri wote wa mihadhara na kuwatupa gezaulole wakalime miraba.

Ni haki yangu kumkosoa mke wa jirani yangu ndani ya chumba changu lakini sina haki kwenda barabarani na kuchukua megafoni na kumkosoa. Bila shaka mwenye mke akinisikia hatafurahia hata kidogo hata kama ninachokisema kina ukweli kwa mtazamo WANGU. nDICHO HIKI WANACHOKIFANYA HAWA NDUGU ZETU. Wachambue Biblia kwenye Madrasa, kwenye kongamano zao n.k. lakini wasifanye hivyo kwenye hadhara kwa kutumia mikutano au/na vipaza sauti na kutegemea wakristu watakaa kimya tu.

Amandla....
 
Tanzania haina dini bali wananchi ndio wenye dini,hivyo katiba inawaruhusu wote kuabudu pasipo kuvunja sheria.Uislam uko wazi pia hivyo msiojua tuulizeni tuwafundishe.Uongozi katika Uislam unamaadili yake mfano kiongozi lazima awe mtusafi na akubalike kwa tabia njema na awe mwadilifu katika uongozi wake.Kiongozi awapendelee na kuwahurumia raia wake kwa kuwapa huduma yao inayostahili.Sasa anapopewa Muislam kungoza anatakiwa aongoze kwa kivuli cha Uislam na kwakua kama Tanzania haina dini basi Muislam huyu itabidi kwanza awe mnyenyekevu mbele za Mungu na pia atekekeleze sheria za nchi.Kama mtu anajina na hafuati ule mwelekeo wa Uislam kwa kutenda haki basi yuko mbali na Uislam pamoja na Mungu,kwa maana anaifuata na kuiabudu nafsi yake na matamanio yake binafsi.Hivyo MAFISADI na WEZI wahukumiwe kwa dhambi zao na usiandamwe Uislam kama wengi wafanyavyo hapa JF.Anayefanya dhambi hizo uislam hauko naye na tayali wamejitenga wenyewe kwa kuukanusha Uislam.Uislam siotatizo bali tatizo ni wao viongozi.Ingelikua ni sheria ya Uislam kwa kubainika kashfa kiongozi anang'atuliwa.Hivyo kama JK ana matatizo msimuhukumu kwa DINI yake bali muhukumuni yeye kama yeye na si UISLAM na Waislam.

Asante Mkuu...Tena ikumbukwe kuwa tatizo si dini yoyote..Tatizo lipo katika ndani ya nafsi ya mtu. Wote tuna tumejaaliwa utashi...unapofanya ubadhilifu ,usifadi n.k nafsi yako yakusuta..sema twafanya kiburi...
 
Tanzania haina dini bali wananchi ndio wenye dini,hivyo katiba inawaruhusu wote kuabudu pasipo kuvunja sheria.Uislam uko wazi pia hivyo msiojua tuulizeni tuwafundishe.Uongozi katika Uislam unamaadili yake mfano kiongozi lazima awe mtusafi na akubalike kwa tabia njema na awe mwadilifu katika uongozi wake.Kiongozi awapendelee na kuwahurumia raia wake kwa kuwapa huduma yao inayostahili.Sasa anapopewa Muislam kungoza anatakiwa aongoze kwa kivuli cha Uislam na kwakua kama Tanzania haina dini basi Muislam huyu itabidi kwanza awe mnyenyekevu mbele za Mungu na pia atekekeleze sheria za nchi.Kama mtu anajina na hafuati ule mwelekeo wa Uislam kwa kutenda haki basi yuko mbali na Uislam pamoja na Mungu,kwa maana anaifuata na kuiabudu nafsi yake na matamanio yake binafsi.Hivyo MAFISADI na WEZI wahukumiwe kwa dhambi zao na usiandamwe Uislam kama wengi wafanyavyo hapa JF.Anayefanya dhambi hizo uislam hauko naye na tayali wamejitenga wenyewe kwa kuukanusha Uislam.Uislam siotatizo bali tatizo ni wao viongozi.Ingelikua ni sheria ya Uislam kwa kubainika kashfa kiongozi anang'atuliwa.Hivyo kama JK ana matatizo msimuhukumu kwa DINI yake bali muhukumuni yeye kama yeye na si UISLAM na Waislam.

nasubiri conclusion yako binafsi bila kujali udini kama ulivyoainisha. Is JK fit to lead?
 
Post nzuri.
sasa inakuwaje watu walipomkataa kwenye sanduku la kura, kwa sababu ya uovu wake (wizi wa mali ya umma na kuwalinda wezi) yeye pamoja na wapambe wake (wengine humu JF); walikimbilia kuanzisha ajenda ya udini kwamba watu hawamtaki kwa sababu ni mwisilamu?

Divide and Rule ndugu yangu, imetumika chaguzi nyingi, kumbuka CUF walionekana ni Mujahaheeden mwaka 2005 umesahau.. hii ni mbinu wanayotumia kuficha uchafu wao na sasa wanaitumia sana, juzi Arusha walitaka kuzuia marehemu mmoja asipelekwe uwanjani kupewa heshima za mwisho lengo ni kupandikiza udini. Kwa bahati nzuri au mbaya kuna watu wengi wapumbavu wanapumbazwa na vihela vidogo wanaingia kwenye mtego wa hawa mafisadi kuifanya vita ya mafisadi ni ya kidini zaidi!

Lakini nadhani sasa wana nchi waelimishwe walitambue hili.

Cityboy thanks again for a very good and useful post!
 
Back
Top Bottom