Tatizo la umeme: Awamu ya tano haiwezi kukwepa lawama labda tu kama madai hayana ukweli

By Zitto kupitia twitter:

Mradi wa 300MW Mtwara ulisimama. Mradi wa 350MW Kilwa ulisimama. Mradi wa nyongeza Kinyerezi 185MW ulisimama. Mradi wa Kinyerezi 3 and 4 umesimama. Utapata wapi Umeme kulisha nyongeza ya shughuli za Uchumi baada kufungua Nchi?

Miradi yote ya Umeme iliyokuwa kwenye power system master plan ilisimama kupeleka hela kwenye Stigler’s gorge ambayo wataalamu wote walituambia itachukua Miaka 7 kukamilika 100%.Lakini Kwa kuwa Sisi ni Watu wa kukubali uongo na propaganda tukaamini. Leo tunaambiwa delays tunawaka.

Siamini kuna hujuma. Ninaamini ni mambo ya kisera na madhara ya Miaka 5 unusu ya incompetence katika uendeshaji wa Uchumi. Tulidanganywa na tukaamini uongo huo. Sasa tunatumia uongo ule kuwapima wenye Mamlaka sasa. NCHI HAINA UMEME WA KUTOSHA. Hatujaongeza Hata 1MW kwa Miaka 5
Naomba Zito aje na cost benefit analysis ya matumizi ya Gas. Nani anamiliki gas, anatuuzia bei gani, gharama ya kuzalisha kWh 1 ni shs ngapi, na zaidi atueleze nani anamiliki mitambo ya kuzalisha umeme aliyoitaja. Kama si mitambo ya serikali, basi atueleze tanesco watalipa shs ngapi kwa kwh na wao watauza shs ngapi kwa mtumiaji/mteja. Na zaidi namwomba aeleze hapa jinsi songas inavyolipwa na Tanesco.
 
Magufuli aliwaambia Gas siyo yetu, kama Zito anadhani ni yetu atuambie ukweli.
 
Bora mara Mia tunge ingia makubaliano ya ujenz wa bandari na mabeberu kuliko wa China Una wajua wachina wewe watatujengea libandari lao watalitumia miaka 99 wakija kutuachia halifai tena kwa matumizi itabid serikal iingie galama za ujenz upya, alafu Wachina Wana njaa na wadokozi wa vitu vidogo vidogo tofauti na wazungu, Mim nimefanya kazi na Wachina nawajua vizur sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha story mingi, nimekuomba uthibitishe kauli zako kuhusu kutawaliwa miaka 99 kutokana na Bandari and Kikwete kupewa 10% ya gas!! Mbona unazunguka zunguka sana???
 
hahahah mkuu mbona mwendokasi inaendelea na sasa imefika asilimia 40? hebu punguzeni uongo bhana.....au wewe unaishi wapi ? umepita mawasiliano au umepita kariakoo na mbagala? au sio mradi wa mwendokasi ule? hahahaha
Inaendelea kwa plan/speed ile ile aliyoacha mtangulizi wake?
 
Mleta mada Ni upinzani kindaki ndaki

Sasa hivi Wana CCM tukiandika kitu Cha kukosoa Serikali humu. Upinzani unapinga nakutetea msimamo wa serikali .Hadi Raha .Mfano Ni huyu mleta mada

.CCM hoyeeee
 
Hao wanaomtupia lawama Magu ni wajinga pia, Magu ameshakufa, ni kuachana naye, tulio hai tusonge mbele, harudi tena! Na nyie mnaopambana kumtetea Marehemu as if yupo hai mnakosea pia, Mnapotaka kumgeuza Magu kuwa SI UNIT ya kutawala nchi hii mnakosea zaidi, hakuwa perfect!! Kinachoshangaza ni nyie wapambe kushupalia haya mambo, Sijawahi kumsikia Samia hata siku moja akimuongelea vibaya Magu, zaidi ya kummwagia sifa!! Siku Samia akiongea chochote kibaya kuhusu aliyekuwa bosi wake hapo mnaweza kuja juu na kutoa mapovu
Ukisoma tweet za makamba utagundua anamponda magu
 
Ukisoma tweet za makamba utagundua anamponda magu
Ni tafsiri yako tu Chief, Makamba hajawahi kumponda wala kumtukana Magu! Ile ishu yake na Magu alikuwa anajitahidi kulinda legacy ya Baba yake kutokana na matusi ya Musiba..Tuwekee Tweet moja hapa anayomponda Magu
 
By Zitto kupitia twitter:

Mradi wa 300MW Mtwara ulisimama. Mradi wa 350MW Kilwa ulisimama. Mradi wa nyongeza Kinyerezi 185MW ulisimama. Mradi wa Kinyerezi 3 and 4 umesimama. Utapata wapi Umeme kulisha nyongeza ya shughuli za Uchumi baada kufungua Nchi?

Miradi yote ya Umeme iliyokuwa kwenye power system master plan ilisimama kupeleka hela kwenye Stigler’s gorge ambayo wataalamu wote walituambia itachukua Miaka 7 kukamilika 100%.Lakini Kwa kuwa Sisi ni Watu wa kukubali uongo na propaganda tukaamini. Leo tunaambiwa delays tunawaka.

Siamini kuna hujuma. Ninaamini ni mambo ya kisera na madhara ya Miaka 5 unusu ya incompetence katika uendeshaji wa Uchumi. Tulidanganywa na tukaamini uongo huo. Sasa tunatumia uongo ule kuwapima wenye Mamlaka sasa. NCHI HAINA UMEME WA KUTOSHA. Hatujaongeza Hata 1MW kwa Miaka 5
huelewi tatizo, akili hazipo sawasawa kichwani.
 
View attachment 2015658

Zitto ni mtu ambae anatafuta information na kujenga premise uchwara anazotaka yeye.

TANESCO long term plan yao ya umeme inapatikana kwenye link hapo juu na kwenye pipeline kuna renewables, hydropower (stigler gorge is also mentioned), gas and coal. Hakuna priorities ya kipi kianze.

Yeye anachukua source moja na kujengea hoja kama makosa with very simple arguments, watu kama hao wakimpata mtu anaefahamu maswala ya energy kuwa expose limitations zao ni rahisi sana.

Ukiangalia tu ivyo vyanzo vyote vya gas gharama yake inafika $2.9 billion umeme ni megawatts 2500.

Bwawa la Nyerere gharama $2.9 billion umeme megawatts 2115.

Bwawa la Nyerere lina cheap unit costs.

More safe maana bomba la gas lina line moja tu hakuna back. Likichezewa nchi nzima aina umeme na tayari over 64% ya umeme wetu unatokana na Gas kuongeza tena hiyo sio hatua nzuri ya kumitigate energy security risks.

Ukishatengeneza vyanzo inabidi uajiri na kuna gharama za matunzo. Bwawa la Nyerere linaondoa operation costs za plant kama nne hivi za kujenga gas plants.

Vitu vingine ata kuandika shida, I tell you kule Twitter ni kikundi cha wapuuzi tu huwa wanaandika vitu ambavyo awajawahi kuvifanyia research na kuviandikia report katika maisha yao; yaani ni ujinga mtupu.
Wewe unaongelea gharama wakati shida ni maji ya kulijaza hilo bwawa kwa wakati wote ndiyo shida.Umeme wa maji ni lazima utegemee mito.Sasa kama mito yenyewe inajaa na kupwa na hivyo kupelekea bwawa kujaa na wakati mwingine kupungua ujazo hitajika,utasemaje ndiyo mkombozi pekee?.
 
Hivi nyie watu wakati huo mlikuwa mnaishi Tanzania au ndo ile ya kusifia kila kitu?

Hebu tuangalie kwa kwa haraka haraka tukianza na mdau kutoka Arusha...

View attachment 2015661
Fuatilia huo uzi uone watu walivyokuwa wanalalamika kuhusu umeme, tena February!!

Nyuzi nyingine....

1. Kuna mgao wa umeme wa kimya kimya December 05, 2020
2. Mgao mkali wa umeme Morogoro mjini - December 21, 2020
3. Wilaya ya Ubungo kuna mgao wa umeme? Mpaka sasa hakuna umeme March 01, 2021
4. TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini March 04, 2021

Hayo ni malalamiko yaliyotokea sehemu mbalimbali za nchi ndani ya miezi 3 TU!!!
Mkuu!Watu wa walishavurugwa na kuondokewa na .
 
Japo tuna ukame,lakini ukosefu wa umeme una mkono wa kisiasa na uzembe au hujuma.
Kama gas asilia inazalisha 60% ya umeme wa nchi nzima ni wazi miundo mbinu yake ikiwepo ma gas turbine ilitakiwa kuwa katika hali ya uhakika ready to run smoothly or standby mode muda wote.
Hawa wapuuzi inaonekana walikuwa wakizima mitambo ya gas wakati maji ya mabwawa yalipokuwa bwelele hawakuyafanyia planned maintenance, sasa wanakumbuka shuka asubuhi!
Lakini maji kwenye mabwawa yalipungua gradually kwanini TANESCO hawakufanya contigence plan hadi kiwango cha maji kwenye mabwawa kikawa kidogo?
Kuna wakati hizi taasisi za Umma kama TANESCO teuzi na maamuzi ya uendeshaji ni ya wanasiasa.
Kitu ambacho watu wengi hawajui black out ni uhaini yaani treason.
 
Acheni kuhamisha magoli.......awamu hii imeshafeli kwenye suala la umeme na maji. Watanzania sio wajinga.
Awamu hii ndiyo inamiezi 8 tu.Alafu unasema imefeli na wakati huohuo kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 10 ni mwaka huu joto limepanda kuliko miaka yote 10 iliyopita na huku mvua pia zikichelewa kuanza kunyesha.Sasa kwa nini maji yasipungue mabwawani?.Kususiwa na miradi ya gas kwa wivu na ubinafsi ndiyo sababu ya kukosa njia mbadala.
 
View attachment 2015658

Zitto ni mtu ambae anatafuta information na kujenga premise uchwara anazotaka yeye.

TANESCO long term plan yao ya umeme inapatikana kwenye link hapo juu na kwenye pipeline kuna renewables, hydropower (stigler gorge is also mentioned), gas and coal. Hakuna priorities ya kipi kianze.

Yeye anachukua source moja na kujengea hoja kama makosa with very simple arguments, watu kama hao wakimpata mtu anaefahamu maswala ya energy kuwa expose limitations zao ni rahisi sana.

Ukiangalia tu ivyo vyanzo vyote vya gas gharama yake inafika $2.9 billion umeme ni megawatts 2500.

Bwawa la Nyerere gharama $2.9 billion umeme megawatts 2115.

Bwawa la Nyerere lina cheap unit costs.

More safe maana bomba la gas lina line moja tu hakuna back. Likichezewa nchi nzima aina umeme na tayari over 64% ya umeme wetu unatokana na Gas kuongeza tena hiyo sio hatua nzuri ya kumitigate energy security risks.

Ukishatengeneza vyanzo inabidi uajiri na kuna gharama za matunzo. Bwawa la Nyerere linaondoa operation costs za plant kama nne hivi za kujenga gas plants.

Vitu vingine ata kuandika shida, I tell you kule Twitter ni kikundi cha wapuuzi tu huwa wanaandika vitu ambavyo awajawahi kuvifanyia research na kuviandikia report katika maisha yao; yaani ni ujinga mtupu.
Naomba uniambie sustainability ya hilo itakuaje maana hadi sasa kuna mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, hapo dsm tu mpaka sasa kuna mgao, mito haji hakuna!!

Je huu mradi wa bwawa hautakua kimeo baadae?
 
Naomba orodha ya shughuli za kiuchumi zilizofunguliwa kisha zikasababisha upungufu mkubwa wa umeme. Orodha hiyo iambatane na kiwango cha mahitaji ya umeme yasiyotiliwa mashaka kwa kila shughuli.

Karibu.
Hata wenzake wote hawawezi kukupa jibu. Wakati wa Nabii Walwa Njozi ungishatumiwa wasiojulikana.
 
Back
Top Bottom