Tatizo la sukari ni kama biashara ya watu wachache walioweka vizingiti, tabia hii imeanza kitambo

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,611
8,739
Kuna kipindi ilishawahi Azam cola kushtakiwa kwa sababu kutumia neno Cola sababu wenye Cola waliona ni neno lao.

Hili jambo la sukari ni kama monopoly business ambayo haitaki mwengine kuanzisha kiwanda cha sukari. Ni kama familia fulani au watu fulani walijiwekea ili biashara hii ya sukari ibaki kuwa kwao.

Nikajaribu kuangalia mashine za kuchakata sukari nilishangaa sana, yaani kama sukari ingekuwa na ule wakukamua mafuta ya alizeti basi isingekuwa hivi.

Kama mtu anaweza kununua basi kumi za mabilioni wakati hiyo pesa inaweza kutengeneza kiwanda ambacho kinaweza kuhudumia mkoa mmoja tu sukari.

Ingie Alibaba mjionee mashine za uzalishaji sukari huku tukibeba miwa mingi kutengeneza juice ya miwa.
 
Back
Top Bottom