Kagera: Rais Samia atembelea Kiwanda cha Sukari Kagera, azindua mradi wa maji Kyaka - Bunazi, Missenyi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea na ziara yake Mkoani Kagera, hapa ni katika ziara yake kwenye Kiwanda cha Sukari Kagera, leo Alhamisi Juni 9, 2022

RAIS SAMIA ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA

Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani

Ni kweli Jeshi la Magereza linamiliki ardhi eneo hili. Na kama ambavyo umetupa maagizo wakati umenipa dhamana hii, na mara kwa mara umekuwa ukisisitiza, juu ya umuhimu wa vyombo vyetu kuweza kujiendesha kibiashara kupitia mashiika yake

Nakuhakikishia Mh. Rais kuwa kazi hii imeanza na ipo hatua nzuri kupitia Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi na Shrika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza.

Rais Samia Suluhu Hassan

Kilimo kinachangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda. Kilimo pia kinachangia asilimia 58 ya ajira na 27 ya pato la taifa na ndiyo maana serikali imefanya mageuzi makubwa kwenye Sekta ya Kilimo na Viwanda.

- Ushirikishaji Sekta Binafsi

Kwa miaka 50 ija, biashara itategemea sana Kilimo – na hasa mazao ya chakula. Hivyo, hatuna budi kuifanya nchi yetu kuwa mzalishaji mkubwa wa bidhaa za kilimo na kuwa moja ya nchi bora za kuuza nje bidhaa hizo.

Kwa muktadha huo, tufanye mageuzi ya kilimo ambayo yataendana sambamba na ukuzaji wa viwanda, hususan vile vinavyoendana na malighafi hizo.

Katika kutekeleza azma hii, Serikali itatekeleza sera yake ya Kiuchumi Shirikishi kwa kuishirikisha sekta binafsi kikamilifu kama mdau wake mkuu.

- Uwekezaji Mkubwa

Ndugu Wananchi, nimeshuhudia kazi kuba inayofanywa na ya kupigiwa mfano – kuanzaia uwezekano mkubwa uliofanywa katika mitambo ya kisasa na zana za kilimo inayotumia mitambo ya satellite kuweka sawa mashamba kwa utaalamu wa hali ya juu sana.

Nimeona mifumo ya umwagiliaji maji na utandazaji kwa zaidi ya milioni 4 pamoja na stesheni za kusukuma maji zenye pampu kubwa.

Nimeshuhudia pia uchakataji wa miwa kwa mashine na mitambo ya teknolojia ya kisasa. Kilichonifurahisha zaidi ni kwamba by-product inayobaki kwenye miwa inakwenda kuzalisha umeme kwa mtambo wa kisasa, umeme ambao unatumika kiwandani lakini huko huenda ukazidi na ukaingizwa kwenye gridi ya wananchi.

Hii ni mara yangu ya pili kufika Kagera Sugar. Mara ya kwanza nilikuja kama Waziri – Ofisi ya Makamu wa Rais nikimsindikiza bosi wangu, Makamu wa Rais. Lakini wakati ule sikuona mambo makubwa kama haya. Leo nimekuja kama Rais na nimeshuhudia makubwa.

- Sekta ya Miwa ipo vizuri

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alinidokeza kuwa katika Kilimo Sekta ya Sukari inaonesha mfano mzuri wa wa ukuaji mwaka hadi mwaka.

Nilikuwa napitia takwimu za uzalishaji wa miwa na miaka miwili iliyopita hatukufanya vizuri sana lakini taarifa niliyokuwa nikiisoma, inasema kuanzia mwaka 2020, hasa 2021 kwenda mbele, kutakuwa na ongezeko la kilimo cha miwa. Nafurahi kuwa ongezeko ili linaendana na utanuzi wa viwanda.

- Barabara ya Misenyi

Kwa upande wa barabara inayounganisha na Misenyi, TANROADS hili sina haja ya kulisisitiza sana. Ningependa mara nyingine nikija nikute hiyo barabara imekamilika.

- Taasisi za Fedha na Riba

Taasisi za fedha nawashukuru mepunguza riba kutoka mlipokuwa maka sasa ni asilimia 9. Jinsi mnavyoshuka kwa TSHS mkashuke kwa Dola pia. Uwekezaji huu ni wa Madola kuliko TSHS. Serikali kuu kupitia Benki Kuu tutaangalia namna ya kuiimarisha Sekta ya Kilimo.

Hivyo Mabwana Fedha, naomba mkainamishe vichwa muone nini mtafanya na sisi Serikali Kuu tutafanya.

- Yield per hactre

Suala lingine lililoongelewa hapa ni idadi ya viwanda vvilivyopo ni teknolojia tofauti. Suala kubwa tunaloliongelea hapa ni yield per hactre. Tunaweza kuchukuwa mashamba makubwa sana lakini kama hatutapandisha yield per hactre, bado tutataka ardhi kubwa na kubwa zaidi.

Nimemsikia Waziri akisema kiwanda fulani ni mfano mzuri wa kuigwa kwa yield per hactre. Si vibaya kubadilishana uzoefu. Si vibaya kubadilishana teknolojia mkaongeza uzalishaji, kwenu lakini pia kwa outgrowers – mkawafundisha huo utaalamu ili viwanda vikapate malighafi nyingi.

- Bilioni 20 za kilimo kumaliza uhaba wa mafuta

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetenga Tsh. Bilioni 20 za kuendeleza kilimo cha mashamba makubwa Nchini kwa lengo la kutengeneza mafuta mengi hadi kufikia kiwango cha kuuza nje ya nchi

Amesema""Tunawekeza uzalishaji wa ndani ili tujitosheleze, lazima tuwe na mashamba makubwa. Kagera ni moja ya mikoa ambayo tumeilenga katika mpango huo"

Rais anaongeza "Nchi yetu ni kubwa, tukitegemea kuagiza likitokea tatizo, yanatukuta haya yanayotokea kwa sasa. Naagiza Viongozi wa Mkoa (Kagera) kaangalieni maeneo kwa ajili ya kuendeleza mradi huo, tutapanda Alizeti na Michikichi kwa mbegu za kisasa."

Niwahakikishie Wawekezaji, Serikali itaendendelea kuwe mazingira mazuri kwa ajili ya uwekezaji.

RAIS SAMIA KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI KYAKA - BUNAZI WILAYANI MISSENYI

Mradi wa Kyaka – Bunazi ni Mradi wa Kisasa ukilinganishwa na miradi mingine ya miji mikuu ya baadi ya wilaya na hata miji mikuu ya baadhi ya mikoa.

- Umejengwa kwa Fedha za Ndani

Mradi huu tumeujenga kwa fedha za ndani kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na utanufaisha zaidi ya watu 67,470 wa kata ya Kyaka na Kasambya pamoja na vitongoji vyake ambapo watapata maji safi na ya kujitosheleza.

Niwape pongezi wote walioshiriki kutekeleza na kusiamamia mradi huu. Wizara ya Maji mmenifungua macho Mama yenu, na leo kwa mara nyingine tena mmenikosha.

- Mkopo wa Tshs Mil. 500

Ili twende na ile spirit ya Kazi Iendelee, nikupe maelekezo Waziri wa Maji na Katibu Mkuu. Naomba muwakopeshe, sisemi muwape bure, muwakopeshe Mamlaka za Maji za maeneo haya shilingi milioni 500 ili iwe ni nyenzo ya kuwaunga wananchi harakaharaka.

Nina hakika wananchi, pesa hizi zikitumika kuwaungia maji wananchi harakaharaka, wananchi siyo bure. Natoa pesa hii ili mamlaka ziweze kufanya kazi haraka. Lakini wale wanaoungiwa lazima walipe ili pesa irudi. Na ndiyo maana nimesema pesa ya mkopo.

- Tunzeni Miundombinu

Wenyeviti wa Bodi najua wamenisikia na watazisimamia ili zitumike vema.

Kama mlivyosikia, mradi huu umetumia fedha nyingi hivyo niendelee kuwasihi kutunza miundombinu. La pili, mlinde mazingira na mlinde Mto Kagera.

- Msibambike Wananchi Bili za Maji

Rais Samia Suluhu ametoa angalizo kwa wanaotoa bili za maji Nchini kutobambikia bili za maji kwa wateja wao.

“Wananchi walipe maji jinsi wanavyotumia, msiwabambikie bili kwa gharama za uendeshaji za ofisini kwenu,” amesema hayo akiwa katika ziara Mkoani Kagera, leo Juni 2022.

Aidha, kutokana na kukamilika kwa mradi wa maji uliopo Kyaka-Bunazi Wilayani Missenyi Mkoani Kagera ametoa maelekezo kwa Wizara ya Maji kutoa mkopo wa Tsh. Milioni 500 kwa mamlaka za maji karika eneo hilo ili wafanikishe zoezi la kuunganisha maji kwa wananchi kwa haraka.

RAIS SAMIA ATANGAZA MSAMAHA WA KODI KWA MADENI YA ZAIDI YA MIAKA MIWILI

Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka mamlaka zinazokusanya kodi kuachana na utaratibu wa kukusanya kodi kwa Wafanyabiashara ambao kwa zaidi ya miaka minne iliyopita walilipa kodi pungufu au hawakulipa kabisa.

Kauli hiyo imetolewa Juni 9, 2022 katika ziara yake Mkoani Kagera ambapo ameeleza wale ambao hawakulipa mwaka mmoja uliopita ndio wamulikwe na siyo wa miaka miwili na kuendelea.
 
Back
Top Bottom