Bashe, Isaidie saccos ya uwamigo ili ituokoe kwenye tatizo la sukari

tawakkul

Member
Oct 12, 2022
88
67
Habari wanaJF.
Hii makala ni kwa waziri wa kilimo ndg Hussein Bashe.

UWAMIGO SAVING AND CREDIT COOPERATIVE SOCIETY LIMITED yenye namba ya usajili PRI-MRG-KLS-DC-2023-5249, inapatikana kijiji cha Mbigiri wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
SACCOS hii ina wanachama zaidi ya mia nne(400) ambao kwa ujumla wao wana zaidi ya ekari zaidi ya elfu kumi wanazotarajia kulima miwa ya sukari.

Tofauti na SACCOS nyingine, SACCOS hii ni maalum kwa ajili ya zao la mkakati la kukabiliana na tatizo la sukari nchini mwetu.

SACCOS hii imeundwa na wakulima wanaokizunguka kiwanda(outgrower), kiwanda cha Mkulazi Holdings Ltd kilichopo Mbigiri.

kiwanda.jpg

Mkulazi Holdings Ltd, Kiwanda cha kuchakata miwa ya sukari.

Kwa nia na dhamira ya dhati waliyonayo wakulima hao, wamejaribu kujiwekea hakiba kwa lengo la kujikopesha ili waweze kulima miwa ya sukari.
Jitihada yao inakwemishwa na gharama kubwa ya uwandaaji mashamba kulingana na hakiba waliyojiwekea.

Kama waziri wa kilimo tena ni kilimo cha mkakati, ni vema ukitupia jicho lako kwenye hii UWAMIGO SACCOS kwa kuwasaidia wapate pesa ya kutosha ili waweze kukopeshana na kuanza kulima miwa.

Wamefanikiwa kuajiri Meneja na Muhasibu na wamejiwekea mfumo mzuri wa ukopeshaji.
Mfumo wao wa ukopeshaji ni kwamba mwanachama hapewi pesa bali anapewa huduma . Yaani , kama ana shamba la ekari let say tatu, wanachokifanya ni kumpatia huduma zote za shamba yaani kumlimia, kumpigia rija, kumpandia na kadharika na siyo kumpatia pesa taslim.

1706862024205.jpeg


Kama serikali, na kuzingatia hili ni zao la mkakati, WASAIDIENI WAKULIMA HAO WAPATE PESA ZA KUTOSHA ILI WAZALISHE MIWA YA KUTOSHA nasi tununue sukari kwa bei ya kawaida.
 
Kumbuka, ukiwasaidia wakulima hao utakuwa umetengeneza ajira nyingi sana kwa jamii masikini.
 
Ni upumbavu serikali awamu ya nne iliwekaga 1.2 BILIONI ULDUZUNGWA SACCOS karbu na kiwanda Hakuna hata mia imerudi Buladifakini.
 
Back
Top Bottom