PostGE2025 Tatizo la Mtandao Tanzania kipindi cha Uchaguzi: Uchambuzi wangu wa kitaalamu na ushauri ili kukabiliana na janga hili

PostGE2025 Tatizo la Mtandao Tanzania kipindi cha Uchaguzi: Uchambuzi wangu wa kitaalamu na ushauri ili kukabiliana na janga hili

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

New Designer

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2025
Posts
390
Reaction score
633
Tanzania ilipitia kipindi ambapo internet haikuweza kufunguka vizuri, jambo lililochangia kuchanganyikiwa kwa watumiaji wengi.

Utafiti na uchambuzi wangu wa kitaalamu kabla na baada ya kufungwa na kurudishwa kwa mtandao nimebaini kwamba tatizo halikuhusiana na kuzimwa kabisa kwa mtandao, bali kupunguzwa kwa kasi (throttling).

Hii ni habari njema kwamba kunauwezekano wa watu kuendelea kutumia internet kwenye changamoto kama hii.

Kwanini mitandao nasema haikuzimwa kabisa ?

1 , Ushahidi kutoka kwenye minara, Simu zilikuwa zinaweza kupiga simu, kutuma SMS, na kuwasha data. Hii ni ishara dhahiri kwamba minara (tower) hazikuzimwa.

Ikiwa minara ingezimwa, hakuna mtu angeweza kupiga simu au kupata signal. Hali hii inaonyesha tatizo lilikuwa sehemu ya data tu.

2 , Tabia ya VPN wakati wa kupunguzwa kwa mtandao Baadhi ya VPN, kama DroidVPN, zilionekana ku-connect kupenya na mda mwengine zilikuwa zina connect lakini hakuna kitu kilichokuwa kinafunguka.

VPN zinapenya mara nyingine ni matokeo ya leak ndogo au kupitia sehemu ya throttle isiyo kamilifu. Hii haimaanishi kuwa internet ilizimwa kabisa, bali ni dalili ya throttling.


3. Matokeo baada ya mtandao kufunguliwa, Mara mtandao ulipoanza kufanya kazi kwa kawaida, data ilikuwa nzito kutokana na backlog ya traffic.

Baada ya masaa kadhaa, kasi ya mtandao ilirudi kwenye hali ya kawaida. hii inaonesha mtandao haukuzimwa kabisa bali ulipunguzwa kiwango cha chini


Ushauri

Hapa ninaushauri ambao naamini unaweza kuwasaidia kwenye changamoto kama hizi.

1, Download na uwe na vpn tofauti tofauti kwenye kifaa chako

Katika kipindi kama hiki, VPN tofauti tofauti zinaweza kusaidia kuepukana na tatizo la mtandao kushushwa. nashauri uwe na vpn angalau 10 na kuendelea na ziwe vpn strong na kubwa kubwa.

2, Kuwa na laini za mitandao tofauti tofauti

Laini tofauti za mitandao (SIM providers) zinaweza kusaidia kupunguza usumbufu na kuongeza uwezekano wa kupata traffic. wakati mitandao imeshushwa kuna baadhi ya laini zilikuwa zinapenya penya kwa baadhi ya watu ukiwa nazo tofauti unaweza kuwa unazi test.

3, kuwa na laini za nchi jirani kama kenya na angalau uwe karibu na mpakani ili kupata network kutoka kwenye nchi husika.


Hitimisho

Tatizo la kupungua kwa kasi ya internet ni tofauti na kuzimwa kwa minara. Simu zinaendelea kufanya kazi kikamilifu. Hali hii ni throttling ya kitaifa, si shutdown.

Ufahamu huu unasaidia watumiaji kuelewa kwa nini VPN zinaonekana ku-connect lakini data haifunguki.

Utafiti unaonyesha kwamba mbinu bora ni kujaribu VPN tofauti na laini tofauti za mitandao na hata laini za nchi jirani,

Asanteni sana!
 
Ccm majinga sana. Yanajihisi yanatumiliki kama mifugo yao
 
Back
Top Bottom