Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

Pole sana ndugu mwakibete ulitumia njia gani kulimaliza tatizo lako?

Mkuu, binafsi nilimlilia Mungu kwa imani yangu mpaka kikaeleweka kwa kumuona mbaya wangu. Na toka siku nilipomuona ndiyo ikawa mwisho wa matatizo yangu.

Asubuhi nilimtwanga na meseji moja ambayo mpk kesho hajawahi kujibu wala hata kuwasiliana nami.
 
pole sana kaka
bt niliwahi sikia case kama hizo bt nyingi zimekaaa ki spiritual..
try kuona wataalam na watumishi wa Mungu
 
kama kweli basi contact NASA au research institute yeyote ya marekani maana wewe ni mtu wa ajabu sana. Na utatengeneza hela ushaangae!
 
Ulisha kwenda Hospital? kama ndivyo unahitaji kuwaona masaikologist na watalaam wengine wa afya wakusaidie.Ukipenda ntafute ntakusaidi niwezavyo +255 689 417 472
 
Jamani wana JF we zangu Nina ugonjwa kila nikifika saa Tisa Usiku silali tena mpaka asubuhi.Je tatizo ni nini hasa

Cc Mzizimkavu
 
Saa 9 usiku? shukuru Mungu. kuna jirani yangu anasumbuliwa na huo ugonjwa ila yeye tangu alale Octoba mwaa jana hajawahi kupata usingizi tenaaa.
 
Tafuta chumvi ya mawe, ukishtuka kutoka usingizini chukua punje moja au mbili weka kwenye ulimi na uimung'unye taratiiiibu kama vile pipi, lazima ulale usingizi mzito. pia inashiria unapungukiwa maji mwilini, kunywa ya kutosha mpaka lita tatu na nusu kwa siku.
 
Mpenzi,
Salaam, ama baada ya salamu mimi ni mzima.
Dhumuni (Disco) la barua hii ni kutaka kukujulisha kuwa nimezama kwwenye lindi la mapenzi.
Nikinywa maji nakuona kwenye glasi, usingizi sipati, nakuota wewe malaika wangu.
Naomba unitunukie tunu ya mahaba na penzi lako maridhawa.
Wako mtiifu, mnyenyekevu, mvumilivu na mwaminifu penzi.
Cool Sumba.
Hizo zilikuwa enzi zetu zilee tukibonga vishtobe.
Akikukubali ugumu unakuja kwa kumpeleka kutoa jalamba.

Hawa dot com siku hizi hawajui hata kuandika barua za mapenzi sababu ya simu na mitandao ya kijamii. Zamani zile unaandika barua unajaza ukurasa kisha unaandika mpaka pembeni na maua unachora. Ule moyo unauchora halafu unapitisha mshare katikati. Kumtongoza msichana live ilikuwa kazi mpaka uandike barua au umtume rafiki yako au yake. Na ukimtongoza hakuangalii usoni. Siku hizi ndani ya dakika moja umemaliza na yuko tayari.
 
Hi Lutala. Mi mwenyewe mwanamke hapa. ao ulimaanisha nini hasa? niko tayari kwa kujaribu kitu chochote, kama nitapata usingizi. embu nifafanulie plz.

Fanya hivi kutibu tatizo lako:

Kabla ya kulala chukua glass moja ya maziwa changanya na asali vijiko viwili kisha kunywa mchanganyiko huo uje hapa utoe ushuhuda.
 
Ugonjwa huu unaambatana na tabia zifuatazo,

1. Kushindwa kupata usingizi KABISA
2. Kulala na usingizi kuisha usiku sana na kushindwa kulala tena
3. Kusinzia haraka baada kufika kitandani na usingizi kuisha
Haraka na kushindwa kupata usingizi tena.

UGONJWA HUU UNASABABISHA NA NINI?

1. MAZINGIRA MABAYA YA KULALA KAMA KELELE NYINGI,NA HARUFU KALI
2. UTUMIAJI WA MADAWA KAMA COCAINE,CAFEINE,NICOTINE,NA UNYWAJI WA POMBE ULIOPITILIZA
3. MAUMIVU MAKALI YA MWILI KAMA KIDONDA,KUVUNJIKA MIFUPA AU MISULI
4. UPUNGUFU AU ONGEZEKO LA HOMONI ZA UZAZI HASA KIPINDI CHA UZEE KWA WANAWAKE
5. MAGONJWA YA MOYO AMBAYO HUMFANYA MTU ASHINDWE KUPUMUA WAKATI WA KULALA.
6. MAGONJWA YA AKILI
7. MSONGO MZITO WA MAWAZO
8. UTUMIAJI OVYO WA DAWA ZA KULETA USINGIZI

MATIBABU YAKE
Matibabu yamegawanyika sehemu mbili
1. Matibabu yasiyotumia dawa
ni muhimu kuacha tabia zote ambazo ziko ndani ya uwezo wako zinazosababisha ukose usingizi.njia hii ni nzuri sana kuliko matumizi ya dawa ZA kuleta usingizi ambazo zinasababisha. Kuzitegemea zaidi bila hizo wewe haulali na kuleta madhara kiafya

ZINGATIA HAYA.
1. Usile chakula kingi wakati wa kwenda KULALA
2. Usinywe kahawa wakati wa kwenda kulala
3. Kitanda kitumike kama sehemu ya kulala na sio kuangalia video au kucheza gemu
4. Usiangalie video ZA kutisha wakati wa kwenda kulala.

TUMIA TIBA HII

Magonjwa yanayomfanya mtu ashindwe kulala yanatakiwa yapatiwe tiba kwanza.

Dawa ya kutibu tatizo la kutopata usingizi ipo imetengenezwa na mimea asilia,matunda,mbogamboga na mazao ya baharini,.inatibu kuanzia chanzo cha tatizo na inaondoa tatizo lako kabisa ndani ya mda mfupi tu.

Kama una swali maoni au mahitaji ya bidhaa hii, nitumie ujumbe mfupi wasap no 0717556768.
 
KUKOSA USINGIZI(INSOMNIA)

Hii ni hali inayodumu kwa muda ambapo mtu hushindwa kupata usingizi au kuwa na usingizi wa mang'amung'amu.
Kwa kawaida mtu mzima anatakiwa kupata usingizi kati ya masaa 7-8 wakati wa usiku.

Tatizo hili huenda sambamba na kutokuwepo kwa ufanisi wa tezi iitwayo pineal gland ambayo huwa na kazi kuu katika kutoa kichocheo kiitwacho melatonin.

Uwepo wa melatonin ambayo huzalishwa kwa wingi wakati wa usiku, huchangia kuleta usingizi.

Zifahamu dalili zake
1. Kushindwa kupata usingizi wakati wa usiku.
2. Kuamka wakati wa usiku bila sababu.
3. Kuamka mapema
4. Kutojisikia vizuri baada ya usingizi wa usiku.
5.Kuchoka wakati wa mchana
6. Kukosa kumbukumbu
7. Kuongezeka kwa makosa au ajali
8. Kuumwa kichwa
9. Kuwa na wasiwasi kuhusu usingizi.

Zifuatazo ni sababu za kukosa usingizi.
1. Msongo wa mawazo
2. Wasiwasi
3. Magonjwa, kama vile shinikizo la juu la damu, mapafu, Parkinson's disease.
4. Kubadili mazingira au muda wa kazi.
5. Tabia mbaya ya kulala, kama vile kutumia kitanda kwa shughuli zingine.
6. Kutumia vitu vyenye asili ya caffeine, nicotine pia chai.
7. Kula sana wakati wa usiku

Nani yuko hatarini kupata hili tatizo.
1. Wanawake, hasa wanaoelekea ukomo wa hedhi.
2. Wenye umri mkubwa
3. Zamu za usiku
4. Kusafiri umbali mrefu

Haya ni madhara ambayo mtu anaweza kuyapata pindi hali hii itakuwa sehemu ya maisha yake.
1. Kukosa ufanisi mzuri awapo kazini
2. Kukosa umaKini anapokuwa anaendesha vyombo vya usafi, hivyo kusababisha ajali
3. Kupata matatizo ya akili.
4. Uraibu.

Yapo mambo mengi ya kufanya ili kuepukana na tatizo hili.
Napenda kuishia hapo kwanza.
Juu ya ushauri unaweza tumia 0758986658
 
Tunatofautiana. Mimi nikipewa chakula cha moto sahani moja usiku, siwezi kumaliza kula bila kuhisi usingizi mkali tena sana!!
 
Wakuu wa Nchi.

Nina tatizo la kutopata usingizi naweza kukaaa kitandani anzia saa 5 usiku bila usingizi mpaka saa kumi alfajiri ndio napata usingizi kidogo tuu, na saa moja na nusu nahitaji kazini nakuwa nimechoka sana wakuu.

Kama kuna mtu anayejua dawa from phamacy au za Mbadala please msaada niko Arusha .

I hope to hear from you guys soon.
 
Habari.
Naomba kwa msaada wako unipe uniambie ni dawa gani ni nzuri kwa ajili ya usingizi maana nimetushatumia ambayo inaitwa Mellan lakini silali mda mrefu.

Kama unajua ambayo naweza kulala zaidi ya saa mbili na kuendelea bila kushtukashtuka naomba unihabarishe.

Nb
Dawa tu

Asante.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom