KUKOSA USINGIZI (INSOMNIA/SLEEPLESS NIGHT)
Leo ninapenda tuongelee suala zima la kukosa usingizi.
Kwa kawaida mtumzima anatakiwa kulala masaa7-8 kwa usiku mzima. Lakini kuna watu hushindwa kulala kabisa au hulala kwa masaa machache sana kutokana na sababu mbalimbali.
KUKOSA USINGIZI(INSOMNIA) ni tatizo la kukosa usingizi japokuwa una fursa ya kuweza kulala. Tatizo hili linaweza kuwa ni la muda mfupi au ni la muda mrefu, yaani tatizo sugu ambapo mtu hushindwa kulala au kupata usingizi mzuri kwa miezi sita(6) au zaidi.
Tatizo hili husababishwa na mambo mbalimbali lakini zaidi nitazungumzia jinsi tatizo hili linayosababisha kwa kuwa na UPUNGUFU WA MELATONIN HORMONE.
Melatonini hormone ni vichocheo vinavyotengenezwa au kutolewa na pineal gland. Homoni hizi husaidia kuucontrol mzunguko wetu wa kawaida wa kulala na kuamka, hurekebisha saa ya mwili(biological clock) hivyo ukiwa na hormone hizi za kutosha utaweza kulala usingizi mzuri wala hautachukua muda mrefu sana kitandani pasipo kupata usingizi kama hauna shughuli maalumu ya kufanya.
Melatonini hormone hupunguzwa uzalishwaji wake kwa asilimia 10%-15% kila baada mtu akifikia umri wa miaka 35 na kuendelea.
SABABU ZINGINE ZINAZOSABABISHA KUKOSA USINGIZI
Sababu ziko nyingi sana zikiwemo;
1. Magonjwa hapa ni magonjwa mbalimbali kama Miguu kuwaka moto, pumu, shinikizo la damu, matatizo ya moyo, kipanda uso na kuwashwa au mzio.
3. Baadhi ya matibabu hii inahusisha matumizi ya baadhi ya dawa kali zenye kemikali
4. Upungufu wa hormone za kijinsia (estrogen).
5. Msongo wa mawazo.
6. Ugomvi na kelele.
7. Mazingira
8. Kuishi au kufanya kazi za usiku katika mazingira yenye mwanga kwa muda mrefu, hii huathiri sana.
ATHARI ZA KUKOSA USINGIZI
1. Uchovu wa mwili au kuhisi mwili hauna nguvu.
2. Kuwa na hasira au mkali bila sababu za msingi.
3. Maamuzi mabovu
4. Kupoteza kumbukumbu au kusahau sahau.
5. Kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi
6. Kupatwa na magonjwa ya shinikizo la damu au kisukari n.k
MATIBABU
· Badili mfumo wako wa maisha hapa ni katika ulaji wa vyakula pendelea kula zaidi vitu asilia kama mboga za majani na matunda na punguza vyakula au vinywaji vyenye caffein.
· Kunywa maji kwa wingi
· Tumia Asali mbichi vijiko viwili usiku
· Weka mazingira mazuri ya mtu kulala
· Tumia dawa zinazofanya uwe na hormone za melatonini katika kiwango sitahiki
KWA TIBA YA KUKOSA USINGIZI NA MAGONJWA MENGINE KAMA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, MATATIZO YA HORMON, VIDONDA VYA TUMBO, BAWASIRI, MATATIZO YA MIGUU KUWAKA MOTO, PRESSURE NA MENGINE MENGI;
PIGA/SMS/WHATSAP +255 (0) 714 206 306