Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

Habari zenu wakuu,

Mimi nina tatizo la kukosa usingizi tangu mwaka 2008, namaanisha sijawahi kulala kabisa na sasa naanza kupata tatizo nakuwa kama narukwa na akili.

Naombeni msaada wenu tafadhali.
kutopata usingizi husababisha kupatwa na ugonjwa wa wazimu (sio kukesha siku moja kwa wale wenye tabia ya kukosa usingizi siku zote). Kukesha kunaweza kumkondesha mtu na hudhurika ubongo.

yenye kuleta usingizi:

1. Miongoni mwa vinavyosababisha usingizi ni mafuta ya tango, hufaa sana kwa wale wenye usingizi mchache wajipake mafuta hayo kichwani.

2. Vilevile mafuta ya busanji ujipake kichwani busanji kwa lugha ya kiingereza inaitwa ( violet) yanasaidia kuleta usingizi, pia ukitia nyayo zako katika maji ya uvuguvugu .

3. Pia kunusa manemane na kunywa maji yaliorowekwa manemane.

4. Kunusa zafarani na Tunda la Tufaha (Apple) na pia maji ya zafarani ukayatia kichwani husaidia kuleta usingizi.

5. Kunywa maziwa yaliyochemshwa ukatia kidogo sukari huleta usingizi

6. Asali safi mbichi ya nyuki kunywa kabla kulala kwa saa huleta usingizi.

7. Tafuta dawa hii
(melatonin) - inatibu maradhi ya alzheimer's, kansa saratani, mfadhaiko, ukimwi, na kukosa usingizi

8. hatua nyingine ni kulala kwa wakati uleule sikuzote.
oga nusu saa hivi kabla ya kulala.

usinywe chai au kahawa au soda kama pepsi au cocacola kabla ya kulala.
usifanye mazoezi karibu ya wakati wa kulala bora ufanye mapema.
kunywa maziwa ya fukuto kiasi.

Jaribu kutumia hizo dawa mkuu kisha unipefeedback.@Mr lover lover

MziziMkavu ebu njoo huku kuna mdau ajapata usingizi tangia bush alipokanyaga bongo kwa mara ya kwanza. Ushauri plz.
Itabidi aende hospitali akapimwe akili yake itakuwa sio nzuri na akionekana anayo akili nzuri nawala hana maradhi basi atakuwa amefanyiwa mambo ya uchawi ili asiweze kupata Usingizi. Anaweza kunitafuta kwa njia ya Email Address yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com Au pia waweza kunitembelea Blog yangu bonyeza hapa.TUMIENI MAFUTA YA HABBAT SAWDA KWA KUTIBU MARADHI MBALI MBALI
 
Mkuu nimekuelewa vizuri sana. Mimi pia niliwahi kuwa na tatizo kama lako na nilidumu nalo kwa miezi minne na nusu, nilikuwa silali kabisa! Najua hutanii, and I can feel what your going through.
Mimi lilianza kama masikhara tu. Lakini baadae ndani ya hiyo miezi minne ilikuwa balaa..... Unaposema unahisi kupata kichaa ni kweli hiyo hali hata mimi ilinitokea, moja ya dalili zake ni kama kusikia sauti za watu wasioonekana au unaona vitu ambavyo havipo. Kifupi ni kuwa kama unaweweseka! Nilijaribu tiba mbalimbali zikiwepo baadhi ya alizotaja mzizi mkavu, zilinisaidia ila sio sana kwakuwa napata usingizi ila sio wakutosha.
 
Usemi ukweli kuwa Dawa zangu zimekusaidia tu? Ulikuwa hupati usingizi sasa unapata usingizi kwa dawa zangu si ushukuru tu Kwa Mungu umetumia dawa zangu zimekusaidia.
 
Usemi ukweli kuwa Dawa zangu zimekusaidia tu? Ulikuwa hupati usingizi sasa unapata usingizi kwa dawa zangu si ushukuru tu Kwa Mungu umetumia dawa zangu zimekusaidia.

Mzizi mkavu. Sina sababu ya kudanganya katika hili kwakuwa wakati nina tatizo hili nilikuwa hata sijajiunga na Jf, niliambiwa tu hiyo tiba na dada mmoja aliyekuwa banker. Na tiba yenyewe ni maziwa fresh moto, asali mbichi, kuoga maji ya uvuguvugu na kulala kwenye chumba kisafi chenye utulivu sana. Pia kuto kutumia kilevi cha aina yoyote!
 
Pole sana mimi nilishawahi kupata tatizo hilo kwa miezi michache lakini nilikonda sana sana na kichwa kilikuwa kinaniuma sana kama ni muislam nenda kwa ma sheikh wakusomee kisomo na kama ni mkristo nenda kwenye makanisa ya kiroho utapata msaada wa maombi ndugu yangu...
 
Sasa kama umeanza kurukwa na akili utakuwaje na uhakika na hii posti?
 
Pole ! Utapona ukiamini maombi kwa jina la Yesu;kama ilivyokuwa kwa bibi aliyeteseka miaka 25 na kutolewa pepo au majini
 
Bibi yetu baada kuombewa na mch.Kimwemwe wa kanisa la Kakobe pale Mpwapwa amepona tatizo la kukosa usingizi kwa miaka !.
 
kuna jamaa namfahamu hakulala miaka 3,alikuwa akijaribu kufumba macho jamaa refu linasimama mbele yake alipoombewa alianguka chini akapata usingizi hapo hapo amepona mpaka sasa yuko sumbawanga.jaribu kuombewa.

Hebu wasiliana na mleta mada PM msaidie number ya huyo rafikiyo wa sunbawanga.
 
Pole sana mimi nilishawahi kupata tatizo hilo kwa miezi michache lakini nilikonda sana sana na kichwa kilikuwa kinaniuma sana kama ni muislam nenda kwa ma sheikh wakusomee kisomo na kama ni mkristo nenda kwenye makanisa ya kiroho utapata msaada wa maombi ndugu yangu...

Nashukuru kwa ushauri wako blesses,nina ufanyia kazi.
 
Habari zenu wakuu,

Mimi nina tatizo la kukosa usingizi tangu mwaka 2008, namaanisha sijawahi kulala kabisa na sasa naanza kupata tatizo nakuwa kama narukwa na akili.

Naombeni msaada wenu tafadhali.

Mh hujawahi kulala aje? Yani hujawahi fumba macho kabisa au? Au ukilala unalala saa moja tu unaamka?
 
toka 2008 unakuja 2014 miaka almost sita baadaye kuoeta humu JF? hivi watu hua JF mmeiona daktari! nenda kwanza kwa dokta, ukimaliza ukakosa ndio uje humu sema ulipofikia na ulipoishia usaidiwe kama ni kuelekezwa pa kwenda au la.. watu wengi humu wanaambiwa dawa flani wanaenda wanatumia wanapata matatizo makubwa zaidi, dokta atachuuza ajue tatizo liko wapi, hizi description za juu juu kila mtu anakuja na solution yake huku hamna anayejua hali yako zaidi ya ku-guess tu.. Afya si kitu cha kuchezeachezea kwa comment za JF em kua
 
Habari zenu wakuu,

Mimi nina tatizo la kukosa usingizi tangu mwaka 2008, namaanisha sijawahi kulala kabisa na sasa naanza kupata tatizo nakuwa kama narukwa na akili.

Naombeni msaada wenu tafadhali.
Mbona hii kitu inafanana na ya dada mmoja toka Namibia, ambaye nilishawahi kutana naye Mbeya akiwa na shida kama hii kwa muda mrefu kiasi hicho. Au ndio wewe? Lakini nasikia yule dada sasa anapata usingizi...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom