Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Ulaji unaojali afya siyo tu huangazia aina ya virutubisho vinavyotumika, bali huzingatia pia mda sahihi wa ulaji wa vyakula.
Kwa kuwa usiku huwa ni muda wa kupumzika kwa watu wengi, mlo wa muda huu hupaswa kuendana na mfumo unaoongoza usingizi wa binadamu pamoja na kuruhusu mwili uweze kumeng’enya chakula husika kabla ya kwenda kupumzika.
Kwa kawaida, saa 2 hadi 3 kabla ya kwenda kitandani kulala hufaa sana kupata mlo wa usiku.

- Husaidia kutunza uzito sahihi wa mwili
- Huufanya mwili utumie vizuri nishati zake kabla ya kulala
- Hupunguza kutokea kwa changamoto mbalimbali zinazohusisha mfumo wa chakula, mfano kiungulia
- Husaidia kuboresha usingizi