Mbinu za kuondoa tatizo la kutokupata usingizi wa kutosha

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Mwaka 2017, mtafiti wa mambo ya usingizi Dr. Tomath Roth aligundua kuwa tatizo la kukosa usingizi wa kutosha (Insomnia) linaweza kuathiri kiasi cha theluthi moja ya watu wote duniani katika muda fulani.

Ni kweli kuwa baadhi ya watu huwa hawapati kabisa usingizi?
Kutokana na kuugua tatizo la kukosa usingizi kwa zaidi ya miezi 6, Michael Corke alipatwa na changamoto nyingi za kimwili na kiakili, hatimaye alifariki. Hii ilikuwa ni mwaka 1993.

Mwaka 1964, Randy Gardner alikaa siku 11 na dakika 24 pasipo kusinzia. Wakati wa jaribio hili, ilifikia muda ubongo wake ukawa unalala huku macho yake yakionekana yamefunguliwa. Alipatwa pia na changamoto kubwa za akili, kiasi cha kukosa imani na kila mtu.

Hivyo, hakuna binadamu asiye lala, pia siyo sahihi kusema kuwa hulali. Namna nzuri ya kuelezea matatizo ya usingizi ni kusema unalala, lakini haulali vizuri (haupati usingizi wa kutosha) kama unavyotarajia.

Mathalani, kutokulala kwa siku nne mfululizo huku hauna dalili zozote za usingizi ni sawa na kisa cha mtu kutokula siku nne pasipo kuhisi kabisa njaa, huku akijigamba kuwa uzito wa mwili wake unaongezeka.

Wasiwasi, sonona, msongo wa mawazo, uchafu, mwanga, vyakula na vinywaji ni baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha tatizo la kukosa usingizi mzuri.

Jinsi ya kuondoa tatizo hili
Kama unasumbuliwa na tatizo la kukosa usingizi mzuri kulingana na mahitaji yako, fanya mambo haya kutatua shida hii.
  • Hakikisha chumba chako kina giza la kutosha. Vichocheo vya usingizi viitwavyo melatonin hufanya kazi vizuri kwenye maeneo ya giza.
  • Usitumie vifaa vya kieletroniki walau nusu saa kabla ya muda wa kulala mfano simu, kompyuta, TV n.k
  • Vaa vizuri nguo safi safi, chache na nyepesi. Hata kama kuna baridi kubwa kiasi gani, usivae nguo nzito. Badala yake, tumia shuka au blanketi nzito kujifunika.
  • Acha kuvata sigara karibu na muda wa kulala, au uwapo kitandani. Sigara huwa na kemikali za nicotine ambazo husisimua ubongo na kuondoa usingizi. Acha pia kutumia vyakula na vinywaji vyenye caffeine karibu na muda wa kulala. Hufanya kazi sawa na nicotine, na hupatikana kwa wingi kwenye energy drinks, chocolate, chai na kahawa
  • Tumia vyakula vyenye wingi wa madini ya magnesium kama maziwa na almonds. Ndizi mbivu, asali, chai ya chamomile na lavender huboresha pia usingizi.
  • Fanya mazoezi asubuhi au jioni, walau masaa 3 kabla ya kwenda kulala. Huuandaa mwili vizuri katika kupata usingizi.
  • Tunza ratiba ya kulala. Usingizi huongozwa na mifumo miwili ambayo hufanya kazi kwa pamoja. Kitaalamu huitwa homeostatic system na circadian system. Mifumo hii hufanya kazi kama saa, ikiwa na utaratibu wa kuamua nini kifanyike kwa wakati fulani. Mifumo hii ikifundishwa kuwa muda fulani huwa ni kulala, itakubali kufundishika. Kila mara ikifika muda husika mwili wenyewe utakuongoza kwenda kulala.
Chanzo: Why we sleep (Mathew Walker, PhD) na The Sleep Solution (W. Chris Winter, MD). Imenakiliwa kutoka Afyainfo
 
Asante kwa taarifa ila hiyo point ya tatu kwa watu wa dsm kipindi hiki cha joto ukijifunika hata shuka tu huo usingizi huwezi upata.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom