Nateswa na ugonjwa huu wa ajabu, msaada tafadhali

Hjalte

Member
Oct 20, 2023
25
100
Ndugu zangu naombeni ushauri,

Nina tatizo la ajabu linalonitesa kwa muda wa miaka mitatu sasa la mwili wangu kuwa na muwasho mithili ya pilipili hasa ninapolala tu.Ni maumivu makali ambayo yanaanzia katikati ya tumbo na kifua nakusambaa sehemu mbalimbali za mwili,mapajani,mikononi na sasa yanasambaa hadi usoni na kunifanya kila siku nisilale usiku.

Muwasho si wa kujikuna wala kuvimba ila ni WA ndani kwa ndani,kazi yake ni kuvuruga mwili tu na usingizi kupotea.

Nachoshangaa ni kwamba tatizo hili halitokei nikiwa nimeketi wala nikiwa nimesimama,natembea au kufanya chochote,bali nikilala tu na hasa napoanza kupata usingizi huanza kwa ukali!relief yangu ya kwanza huwa ni kuamka na kukaa,ambapo huchukua dakika moja yanapotea.

Nimeshafanya vipimo vingi kwenye Hospitali kubwa hapa Dar ikiwemo Saifei vya damu na Endoscopy, kilichogundulika kilikuwa inflammation bowels pekee (tatizo kwenye utumbo) ambalo sidhani kama ndio chanzo cha muwasho huu kama mtu unavyohisi muwasho wa pilipili halafu si mtumiaji.

Wadau hebu tushare experience ili na Mimi nifurahie usingizi, tatizo hili huja na kuondoka.
 
Unawashwa kama ule muwasho wa mtu anapotumia dawa ya chloroquine? Yaani unajisikia kama kuna vitu vinakuchoma choma mwili mzima na siyo kuwashwa ngozi hasa?. Yaani kama umemwagiwa upupu? Huenda tatizo ni hiyo inflamation kwenye bowel. Ngoja nirudi nikupe maelezo zaidi.
 
Chukua ndimu 10 kamua juisi yake changanya na sukari guru kisha wekamo asali nusu kikombe huo mchanganyiko uwe unakunywa kijiko kimoja kutwa mara tatu.

Maana kama hauna uvimbe kwenye uti wa mgongo itakua unasumbuliwa na mapepo au mizimu mibaya. Tumia hiyo dawa mkuu.
 
Kwa asilimia kubwa ni hiyo inflamation kwenye bowel japo utaona kama havina uhusiano. Nina kazi na nikimaliza nitakupa maelezo zaidi.
Bowel inflamation ndo isababishe maumivu usoni, mapajani na kifuani mkuu? Kumbuka kafanyiwa mpaka endoscope,
Pia hajalalamika kama anaharisha au kupata maumivu baada ya kula,
 
Unawashwa kama ule muwasho wa mtu anapotumia dawa ya chloroquine? Yaani unajisikia kama kuna vitu vinakuchoma choma mwili mzima na siyo kuwashwa ngozi hasa?. Yaani kama umemwagiwa upupu? Huenda tatizo ni hiyo inflamation kwenye bowel. Ngoja nirudi nikupe maelezo zaidi.
Hapana,si muwasho unaohitaji kujikuna,ni ule WA ndani kwa ndani,kama lingekuwa tumbo basi ni kama Ile vurugu ya vidonda vya tumbo Vikichachamaa
 
Bowel inflamation ndo isababishe maumivu usoni, mapajani na kifuani mkuu? Kumbuka kafanyiwa mpaka endoscope,
Pia hajalalamika kama anaharisha au kupata maumivu baada ya kula,
Mwili wa binadamu ni kitu complex sana. Nimesema hivyo kwa sababu kuna mtu wa wangu wa karibu sana alishapatwa na hilo tatizo. Huwezi amini hata macho muda mwingine anasema yalikuwa yanawasha kama amewekewa pilipili.
 
Bowel inflamation ndo isababishe maumivu usoni, mapajani na kifuani mkuu? Kumbuka kafanyiwa mpaka endoscope,
Pia hajalalamika kama anaharisha au kupata maumivu baada ya kula,
Siharishi,nakula vizuri,tatizo ni maumivu Tena nikilala tu,nikikaa nikitembea au hata nikiwa kitandani nimelala na kushika simu napitia pitia hayapo,tatizo ni pale naposhikwa na usingizi
 
Back
Top Bottom