Ni sahihi mkataba kati ya nchi na nchi (IGA) kusainiwa na Mkurugenzi wa Bandari?

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,229
12,954
Bado naendelea kujiuliza, Wanasheria wetu walilala au shinikizo la Rais lilikuwa kubwa kiasi hawakutana hata kufanya kazi kwa makini?

Nimepitia ule mkataba wa IGA kati yetu Tanzania na Serikali ya Dubai (kama wanavyodai) kiukweli sijaona sehemu yeyote Serikali ya Dubai hakuna mahala imesaini katika ile IGA, hata hapo walipotoa mamlaka kwa Mkurugenzi wa Bandari asaini, huyo aliyetoa hayo mamlaka hatambuliki ni nani na wala ana cheo gani katika Serikali yao.

Hivi najiuliza, Mkataba wa nchi na nchi inakuwaje unaenda kusainiwa na Mkurugenzi wa bandari? Hata kama issue inayoenda kufanyika ipo katika sekta yake, ila ninachojua, yeye labda sahihi zake zingeonekana katika HGA ila sio IGA.

Kiukweli TUJISAHIHISHE! Hapa tumeingia cha kike.

Screenshot_2023-07-10-22-03-23-68_f541918c7893c52dbd1ee5d319333948.jpg
Screenshot_2023-07-10-20-57-36-60_f541918c7893c52dbd1ee5d319333948.jpg
 
Shinikizo la Samia.lilikuwa kubwa ndio maana mpaka leo bado amewaacha kina Mbarawa ofisini, kama angekuwa hakubaliani nao angeshawaondoa kuonesha uzalendo wake kwetu watanganyika, lakini kuwaacha kunaonesha wazi ni Samia ndie engineer wa haya yote, na ndio maana anatoa majibu ya dharau kwamba ameziba masikio.
 
Back
Top Bottom