Tathmini yangu fupi kuhusu Baraza Jipya la Mawaziri

Kama kawaida yake Magufuli na mambo hadi sasa ameshaunda Baraza la Mawaziri kwa 0.03% anao Mawaziri watatu pekee.

Sijajua kigugumuzi kinatoka wapi wakati ameshakua mzoefu wa kuchagua, kuteua na kutumbua wakati katika ufunguzi wa Bunge tulimskia Mzee wa Amfifiro Mch. Josephat Gwajima kuwa mwaka huu Rais hatokuwa na kazi ya kuchagua mawaziri kwa vile tayari wananchi wameshampatia wabunge hivo ni kushika kalamu na kuandika jina.

Je, tutegemee Baraza lisilokuwa na Manaibu Waziri kama Zanzibar Je ni kweli kuna ukata wa kifedha ndo maana jamaa hajataka kubadilisha wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Mikoa?

Hata hivo huenda hawa wakaingia na kutoka katika Baraza lake hilo tunalolisubiria kuliona japo najua wengi ni Mawaziri remote control.

Prof. Kitila Mkumbo
Huyu huenda akachukua nafasi ya George Mkuchika

Humphrey Polepole
Huyu anaweza kuchukua nafasi ya Mwakyembe au Marehemu Balozi Mahiga au nafasi ya Mwinyi pale Wizara ya Ulinzi

Dr. Riziki Rashid
Huyu anaweza kuchukua nafasi ya Kigwangala pale mali asili au kuchukua nafasi ya Mama Kairuki pale Madini

Alexander Mnyeti
Uwezekano wa kuingia kwenye Baraza ni mkubwa anaweza kuchukua nafasi ya Simbachawene pale Mambo ya Ndani

Dr. Charles Kimei
Huenda akawa naibu waziri au waziri sekta ya viwanda na biashara au hata wizara ya kilimo

January Makamba uwezekano wa kupewa uwaziri upo huenda akachukua nafasi ya Mh. Mhagama pale sera uratibu na bunge

Hawa wanaweza kuachwa ama kurudi

1. Mwigulu Nchemba nafasi yake katika baraza hili uwezekano wa kurudi ni 10%

2. Mkuchika huenda akapumzishwa kutokana na umri wake au akabadilishwa wizara isiyokuwa na mikimiki mingi uwezekano wa kurudi ni 20%

3. Lukuvi huyu pia ana hatihati ya kuachwa huenda akapewa uenyekiti wa bunge 30%

4. Dr Angela Mabula huenda akachukua nafasi ya Lukuvi (60%)
Hawa wana uwezeakano wa kubaki ama kwa neema ama kwa tunguli si unajua Rais aliwaambia wakaroge kwanza.

Kigwangwala (20%)
Mhaga Mpina(40%)
Kamwele(50%)
Ndarichako(60%)
Ummy Mwalimu(80%)
Makame Mbarawa (75%)
Suleiman Jaffo (80%)

Vigezo vya kuingia na kubaki vinazingatia majina yao tu kisiasa (popularity) na sio uwezo (ability) wao katika utendaji kazi manake tulishuhudia 2015-2020 mtu uwezo anao ila anatumbuliwa kwa kutolewa kafara na kufurahisha majukwaa (audience) Week End hii huenda tukashuhudia baraza jipya la Mawaziri.

Kila la kheri mtakaochaguliwa lakini msiende kuwa Mawaziri remote.
 
kwa kweli Wizara hii inahitaji mtu mtulivu sana sana sana! maana jeshi linaweza kujiendesha lenyewe! hatutaki mtu wa matukio! tunataka MATURED person kama Simbachawene
Mwenye mamlaka ya kuongoza nchi atampa anaeona anaweza zaidi, aweza kuwa simbachawene au mwingine

Mungu ibariki Tanzania
 
Minashauri apewe Kibajaji, yule mb wa mtera ama apewe Musukuma yule mb wa geita.....😂😂
 
Waziri Mkuu
Kutakuwa na vita kubwa ya Uwaziri Mkuu, Kassim Majaaliwa amefanya kazi kubwa sana ya kuufuta upinzani, pia amechangia kiasi kukubwa cha kupata hizi kura za kishindo. Naona atakuwa na upinzani mkubwa wa Dr. Tulia, katika kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Mwanamama huyu amekuwa na taswira nzuri mbele ya Rais kwa kutekeleza yale ya kuwabana wapinzani wa kupinga maendeleo Bungeni. Kura yangu ya Uwaziri Mkuu naona ikimuangukia Dr. Tulia
Kwakuwa uteuzi umepita, njoo useme neno
 
Back
Top Bottom