Tathmini yangu fupi kuhusu Baraza Jipya la Mawaziri

BETONY

Senior Member
Apr 4, 2012
139
250
Baada ya wanachi wa Tanzania kuchagua maendeleo ya kijani nchi nzima, kwa kuwapigia kura za kutosha wagombea wa CCM na kuufutilia mbali upinzani wa kupinga maendeleo ya nchi yetu. Wakati napitia matokea ya sehemu mbalimbali nikapata fikra pevu za kuangalia namna baraza la mawaziri litakavyokuwa. Hii ni tatmini yangu fupi kwa baraza jipya la mawaziri.

Waziri Mkuu
Kutakuwa na vita kubwa ya Uwaziri Mkuu, Kassim Majaaliwa amefanya kazi kubwa sana ya kuufuta upinzani, pia amechangia kiasi kukubwa cha kupata hizi kura za kishindo. Naona atakuwa na upinzani mkubwa wa Dr. Tulia, katika kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Mwanamama huyu amekuwa na taswira nzuri mbele ya Rais kwa kutekeleza yale ya kuwabana wapinzani wa kupinga maendeleo Bungeni. Kura yangu ya Uwaziri Mkuu naona ikimuangukia Dr. Tulia.

Waziri wa TAMISEMI
Selemani Jaffo ataendelea na wadhifa wake. Hakika ameitendea vyema hii Wizara toka akiwa naibu waziri na baadae kuwa Waziri kamili.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto.
Ummy Mwalimu ataendelea na wadhifa wake, amekuwa taswira sahihi ya namna ya kuendesha wizara nyeti.

Wizara ya Fedha
Doto Biteko atakuwa Waziri kamili wa wizara hii, ili kuendeleza yale mazuri aliyofanya wakati akiwa Waziri wa Madini

Wizara ya Uwekezaji
Anjela Kairuki naona akirudi kuwa Waziri wa Wizara hii baada ya kuteuliwa katika zile nafasi kumi za Rais

Wizara ya Viwanda
Mh Mpango atakuwa waziri wa wizara hii, ili litatikea ili kumpisha Doto Biteko katika wizara ya Fedha.

Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi
William Lukuvi ataendelea kuwa Waziri, japo naona kama karata anatakiwa kuzichanga vizuri

Wizari ya Utalii
Dr. Hamis Kingwangala ataendelea kuwa Waziri

Wizara ya Kilimo
Namuona Hussein Bashe akiwa Waziri kamili wa wizara hii ya kilimo

Wizara ya Michezo
Jokate Mwegelo atateuliwa kuwa Mbunge na baadae kupewa Wizara hii ya Michezo, Habari na Utamaduni. Hii inatokana na kazi yake nzuri na ya kutukuka akiwa kama Mkuu wa wilaya ya Kisarawe

Wizara ya Vijana,
Antony Mavunde ataendelea kuwa Waziri kamili wa wizara hii ya kuawasaidia vijana

Wizara ya Utumishi wa Umma
Jenista Mhagama atakuwa Waziri wa Wizara hii ili kuendelee kusimamia miongozo ya utumishi wa umma na kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma

Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Luago Mpina atakabidhiwa Wizara hii.

Wizara ya Nishati
Medard Kalemani ataendele kusambaza umeme vijijini kwa kasi kubwa baada ya kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa.

Spika wa Bunge
Kama Waziri mkuu atachagulia Kassim Majaliwa, naona kabisa Tulia atakuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge litahitajika kuwa na nguvu kwani naona kutakuwa na hoja nzito nzito zitakazotikisa Muungano wa Tanzania, ikiwa Zanzibar itakuwa chini ya ACT.

Wizara nyingine naomba muendele kupendekeza
 

Kimpyempye

Senior Member
Dec 11, 2018
150
250
Acha bangi. Tulia awe waziri mkuu mbele ya jemedari majaliwa? Top 3 haibadilìki.
Mpango habadilishwi, mbarawa na ujenzi, maji na mkumbo, uwekezaji kimei, nje kabudi, jafo hàpo hapo
Unaweza kuwa sahihi sana.Kabudi na Jaffo wabaki palepale. Mpango bora abadilishwe.
 

BETONY

Senior Member
Apr 4, 2012
139
250
Uongo mtupu
Muache Rais apange cabineti
Usianze kuchafulia watu na kubashiri
Uwe unasoma kichwa cha habari. Nimesema hii ni tamthimini yangu na sijamfunga yoyote kusema tofauti. Mh Rais yeye ndiyo atakayekuja kuitimisha haya yote kulingana na maono yake makuu.
 

BETONY

Senior Member
Apr 4, 2012
139
250
Acha bangi. Tulia awe waziri mkuu mbele ya jemedari majaliwa? Top 3 haibadilìki.
Mpango habadilishwi, mbarawa na ujenzi, maji na mkumbo, uwekezaji kimei, nje kabudi, jafo hàpo hapo
Jibu vizuri na usiwe mwepesi kutukana watu kama wapinzani wasiopenda maendeleo ya Nchi. Sijakufunga kutoa tathmini yako. Hiyo ni tathmini yangu waweza ikataa kulingana na hoja zako
 

BETONY

Senior Member
Apr 4, 2012
139
250
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mh Prof Palamagamba Kabudi ataendelea kuhudumu kama waziri

Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano
Naona kabisa Mh Charles Kimei akimtoa Eng Isack Kamwele

Wizara ya Sera na Uwezeshaji
Hapa namuona Mh Mrisho Gambo akiingia kuchukua nafasi

Wizara ya Maji
Naona kabisa Mh Prof Mbalawa makame akichukua kiti na kuendelea kusambaza maji

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Hii inategemea na matoke ya urais Zanzibar, Mh Dr Hussein Mwinyi au Mh Kassim Majaliwa kama asipoteuliwa Uwaziri Mkuu wanaweza kushika nadhifa hii. Kama nilivyosema hii mi wizara nyeti.

Wizara ya Mabo ya Ndani
Mh Alexander Mnyeti naona kabosa akichukua nafasi hii na kumtupa chini Mh Simbachawene
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,504
2,000
Tupige kazi ya kjijenga Tanzania tuachane na betting! Wenye kupanga nani awe nani katika serikali watafanya kazi hiyo. Kama ni mmoja wao usubiri mualikane kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Achana na mambo ya betting mleta mada.
 

BETONY

Senior Member
Apr 4, 2012
139
250
Tupige kazi ya kjijenga Tanzania tuachane na betting! Wenye kupanga nani awe nani katika serikali watafanya kazi hiyo. Kama ni mmoja wao usubiri mualikane kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Achana na mambo ya betting mlata mada.
Tathmini yangu, si ya kwako kiongozi. Hatukatazwi kuwa na ndoto na matumaini
 

cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
13,432
2,000
Kutuongezea mawaziri wakuu ni kuongeza mzigo wa kodi kwa wananchi kulipa mawaziri wakuu wastaafu, kassim majaliwa hyo nafasi inamfaa ana busara sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom